ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 28, 2012

TANZANIA YETU KUBWA

Watoto hawa walikuwa wakitega samaki kwa kutumia ndoano hatimaye wamenasa kuku maji.

Mie katika kijiji cha wavuvi wilayani Nyamikoma Magu mkoani Mwanza.

Michezo ya watoto ufukweni.

Pozi la kurejea toka shambani baba jembe mkononi mama kuni kichwani na mbwa mlinzi.

Wavuvi bado hawajatia utii nyavu zisizo ruhusiwa.

Usafishaji nyavu na uanikaji.

Nyavu anikoni.

Enzi za NCU Bandari hii ilikuwa bize kwa kusafirisha pamba nchi mbalimbali afrika mashariki lakini hii leo eneo hili limegeuka sehemu ya kuanikia dagaa.

Style ya kuanika dagaa.

Thursday, January 26, 2012

UHAMISHO ASKALI KITENGO CHA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA MWANZA WAFANYWA KUWANUFAISHA WAHUJUMU?...?

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mwanza wamelalamikia uhamisho wa askali mpelelezi kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya jijini hapa, Benson Kalokola na kumuomba mkuu wa jeshi la Pilisi nchini (IGP) Said Mwema kubatilisha uhamisho huo vinginevyo wataandamana.Afande Kalokola (L) akitunukiwa zawadi ya utumishi bora na mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikilo katika hafla iliyofanyika hivi karibuni ndani ya ukumbi wa ofisi za jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa chati Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow katikati akishuhudia tukio hilo.
Askali huyo amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti uingizwaji na uuzwaji holela wa dawa hizo jijini hapa na kwamba kitendo cha kumhamisha kimelenga kuruhusu biashara hiyo haramu kushamiri.

Kalokola ambaye hivi karibuni akiwa na askali wenzake tisa, aliongoza mapambano ya kujibizana kwa risasi na majambazi matano kisha kuyaua wakati yalipotaka kupora katikati ya jiji.Kikosi kazi cha kupambana na madawa ya kulevya toka jeshi la polisi mkoa wa Mwanza na nishani zao.

Kama hiyo haitoshi Afande Kalokola ndiye aliyefanikisha zoezi la kutokomeza mauaji ya walinzi waliokuwa wakiuawa kila kukicha miezi kadhaa iliyopita katika mitaa ya jiji la Mwanza na kukatwakatwa kwa mapanga vipande vipande, hatimaye kumnasa mganga wa jadi aliyekuwa akiagiza damu za walinzi hao kwaajili ya kufanya zindiko kwa sehemu za wavuvi na machimbo ya madini.

Uhamisho huo wa kumtoa mpiganaji' huyo jijini Mwanza na kumpeleka mkoani Manyara unatajwa na wengi wachambuzi wa mambo kuwa ni zengwe na shinikizo kutoka kwa matajiri wanaojihusisha na biashara mbalimbali haramu anaowaumbua au pengine kukamata mizigo yao haramu.


CHA AJABU; mara baada ya taarifa za uhamisho kusikika baadhi ya askali wa beria za kukagua mizigo inayoingia na kutoka jijini Mwanza wameonekana kupiga shangwe juu ya uhamisho huo.

BACELONA 2 REAL MADRID 2

Ngoma ya wakali wa Hispania Real Madrid na Barcelona USIKU WA LEO' imeisha kwa droo ya 2-2, dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliisha kwa Baca kuongoza 2-0, real walirudisha kupitia C. Ronaldo na Benzema.

Real imewabidi kumaliza mchezo wakiwa pungufu mara baada ya Ramos kupigwa red card ya utata.

AAAAAH LIVAaaaaaaaaa!!!!!

Kocha Kenny Dalglish ameweza kukonga nyoyo za mashabiki walio na kiu cha muda mrefu baada ya kikosi chake cha Liverpool kuikamilisha safari yao ya kwanza kuelekea Wembley tangu miaka 16 iliyopita.

The 2-2 home draw with Manchester City saw the Reds through to the Carling Cup final 3-2 on aggregate, with Cardiff City of the Championship now the only obstacle to them securing a first trophy since the 2006 FA Cup.

However, that success over West Ham six years ago, and the League Cup wins over Birmingham in 2001 and Manchester United in 2003, were all garnered at the Millennium Stadium, with Liverpool not having played at the new Wembley stadium before – they last played in the old ground when losing the 1996 FA Cup final to Manchester United.

Wednesday, January 25, 2012

LUGHA GONGANA.

Mtumbi umeandikwa hivi nanukuu:- REMBU MIHAYO MV LENDA TUGEME NKEONE KAZI BILA MAJUNGU HAYIEDI. NO2

ZAO LA NDIZI KUTOWEKA MKOANI KAGERA?

Maradhi kwa mmea aina ya migomba wilayani Muleba mkoani Kagera yanayofahamika kama 'mnyauko' yameibuka kwa kasi na kuathiri zao hilo. Dalili za awali ndizi hata kama ni changa huonekana kama mbivu nayo majani taratibu hukauka na kukatika.

Hatua ya pili ndizi hukauka na kuwa kavu kama kuni nayo majani hukauka kabisa...

Ni dizaini flani kama virusi kwa mmea wa mgomba kwani ni vijidudu visivyoonekana kama tuonavyo wadudu wengine kama viwavi, papasi nk. na ni ugonjwa unaoambukiza mmea baada ya mmea.

Sehemu zenye udongo mzuri wenye rutuba ndiko hasa huathirika na maradhi haya...Wito kwa serikali kupeleka wataalamu wake haraka katika maeneo yaliyoathirika zaidi vijiji vya Iyunga Kishanda mkoa wa Kagera kwani zao hilo maarufu lenye kushika eneo kubwa la uchumi wa watu wa mkoa huo kuna kila dalili linaweza kutoweka kabisa na kubaki historia kwani baadhi ya wakulima wameanza kubadili kilimo kwa kufyeka zao la ndizi na kuelekea kwenye ukulima wa mazao ya maharagwe na karanga wakikwepa maradhi hayo ya migomba.


Chunguza mjomba utabaini.

KARIBU KATIKA TAMASHA LA INJILI VIWANJA VYA COCA COLA IGOMA MWANZA JUMAPILI HII

Moja ya matamasha yaliyopata kufanyika viwanja vya Coca cola.
KWAYA MBALIMBALI ZA MWANZA KUHUDUMU LINI: JUMAPILI 29/01/2012

KIINGILIO: WAKUBWA SH. 1,000/=

WATOTO 500/=

TAMASAHA HII NI KWA WATU WOTE

!!!!!!....USIKOSE.....!!!!

NYOTE MNAKARIBISHWA

IDHAA YA REDIO JAPANI KUSIKIKA LIVE FEBRUARI MOSI 2012 KUPITIA TBC FM

Kuanzia Feb mosi mwaka huu, matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya Redio Japani yatasikika moja kwa moja kupitia TBC FM Dar es salaam baada ya mkataba rasmi kutiwa saini mwishoni mwa wiki iliyopita Jumamosi tarehe 21/1...jijini Dar es salaam. Ilikuwa hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa TBC Bw.Clement Mshana aliyetia saini kwa niaba ya TBC na Mwakilishi wa NHK World Bi Yuko Asano akiwa na ujumbe wake wa watu watano kutoka Japani. Waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na balozi wa Japani Nchini Tanzania Mh. Okada , Mkurugenzi wa habari maelezo Bw. Raphael Hokororo aliyesoma hotuba kwa niaba ya waziri wa Habari, utamaduni na Michezo mh. Emannuel Nchimbi, na wadau wengine wakiwemo wasikilizaji wa radio japani kutoka katika nchi za Kenya, Uganda na wa nyumbani Tanzania. Mwingine ni makamu wa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC na wafanyakazi wa TBC waliotoa support sana.. tafadhali fuatilia habari hizi kwa njia ya picha.

Shughli watu...

Shughuli haikuwa ndogo...mbali na viongozi Meza kuu.. mkuu wa TBC FM Bw. Othmn Iddi aliongea katika hafla hiyo,

Ilifana...

Mmoja wa wasikilizaji wa Redio Japani Generoza Ndunguru (Picha ya chini)mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, akiongea katika hafla hiyo...

Picha ya pamoja.
CHANZO MIRINDIMO

Tuesday, January 24, 2012

MWANZA KWANZA WAFANYA ONYESHO MAALUM STONE CLUB KUMUENZI MSANII MWENZAO MO-CHELA

Afisa Utumishi wa Kampuni ya Sahara Media Group Raphael Shilatu ambaye alikubali kuwa mlezi wa Mwanza Kwanza hapa akitoa Speach, pembeni ni Mwenyekiti wa Mwanza kwanza Philbert kabago ambaye ni myangazaji wa Passion Fm.

Baba mdogo wa marehemu (L) akiwa na baba mkubwa wa marehemu (R) wakitoa shukurani kwa tukio hilo.

Member wa 'Swagga Maker' hili ni kundi ambalo marehemu Mo-Chella alilitumikia enzi za uhai wake hapa ni katika dakika moja ya ukimya.

Kutoka kushoto ni Sisar Madini, Mox Wanted, G.Ricko, na Shebby.

The area A'

Dj Ally B. akitoa mchango kwenye box la mchango wa ziada ambao ulijumuishwa na pato lililopatikana mlangoni nalo linatazamiwa kuwasilishwa kwa mama mzazi siku ya Ijumaa huko Ukerewe.

The area B'

Mkali anayekuja kwa kasi bongo flevani Sajna akishow love kwenye tukio hilo la kumbukumbu.

Dogo Baraka (L) akiwa na T.Nock wakikamua songi jipyaaaa.

Ezden The Roca wa Kiss Fm 'oN zE wILz zA sTeel.

Sissar madini akiimba kwa hisia wimbo maalum.

The area C' aka Centre.

Dj. Ally Coco n Dj.Abuu wa Metro Disco Musoma wakipata flash....

Monday, January 23, 2012

TANI 40 ZA DAGAA ZAKAMATWA ZIKISAFIRISHWA KWA NJIA YA MAGENDO KUELEKEA NCHINI KENYA, WENYE MALI WAKUTWA NA VIBALI FEKI.

Gari aina ya roli mali ya Grace Enterprises ya Nairobi nchini Kenya yenye namba za usajili KBJ 409 W na tela lake lenye namba za usajili ZC 9486 limekamatwa likisafirisha kwa magendo mzigo wa dagaa unaokadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 40 ukitoka katika bohari ya kuhifadhia kijiji cha Nyamikoma wilayani Magu mkoani Mwanza njiani kuelekea nchini Kenya kwaajili ya biashara.

Afisa wa polisi akichukuwa maelezo toka kwa mmiliki wa roli hilo Godfrey Mwangi mara baada ya dereva kulitelekeza gari hilo na kutoweka kusiko julikana.

lameck Mongi Afisa Mfawidhi usimamizi Uthibiti na Doria wa Uvuvi mkoa wa Mwanza "Ndani ya nyaraka zilizogushiwa zinaonyesha gari lina mzigo wa tani 20 lakini mara baada ya ukaguzi tumegundua ni zaidi ya tani 40"

Kutokana na rasilimali ya uvuvi serikali ya Tanzania inajipatia mrabaha kupitia kodi za usafirishaji zao la samaki wakavu na wabichi hivyo utoroshaji wa bidhaa hizo unapofnyika unaikosesha serikali mapato.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya shilingi bilioni 3.7 zimekusanywa na serikali kupitia zao la samaki kwa mkoa wa Mwanza pekee.


Dalali wa serikali Henry Susuma "Mzigo kama huu ni wa kuharibika hivyo mara baada ya mzigo kukamatwa tu mahakama hutoa oda ya kuuzwa na pesa kupelekwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi, taratibu zimekwisha fanyika kujua thamani ya mzigo kinachofuata ni mali kupigwa mnada"

Juma Makongoro mkuu wa doria udhibiti uvuvi haramu Mkoa wa Mwanza."Kitengo changu kimejipanga vizuri kuhakikisha kuwa mbinu zote za wahalifu zinadhibitiwa lakini yote yanafanikiwa kwa msaada wa wananchi walio wazalendo wa taifa hili"

Wavuvi wakianika dagaa katika fukwe za kijiji cha Nyamikoma mkoani Mwanza.

Bohari za kuhifadhia dagaa eneo la Nyamikoma wilayani Magu mkoani Mwanza, awali bohari hizi zilitumika kuhifadhia zao la pamba lakini mara baada ya zao hilo kushuka zimegeuzwa matumizi.

JK, SLAA WATETA IKULU/SLAA AFUNGUKA KUHUSU TAFSIRI ILEE....!!

RAIS Jakaya Kikwete amekutana na uongozi wa Chadema Ikulu Jijini Dar es Salaam, akiwemo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya. Kwa mujibu wa taarifa kupitia gazeti la Mwananchi, mkutano huo ulifanyika jumamosi ya tarehe 21jan 2012 kuanzia saa 10:30 jioni na kuendelea hadi usiku, lakini walifanya mapumziko mafupi saa tatu usiku.Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam usiku wa tarehe 21jan 2012 katika muendelezo wa mazungumzo ya mchakato wa Katiba mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe na katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Said Alfi. Picha na IKULU
Ujumbe wa Chadema uliokuwa wa watu wanane, ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Wengine waliofuatana naye pamoja na Dk Slaa ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, John Mnyika, Said Arfi, John Mrema, Profesa Mwesiga Baregu na Profesa Abdallah Safari. Hadi tunakwenda mitamboni kikao hicho kilikuwa kinaendelea.

Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Slaa kukutana na Rais Kikwete tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2010, ambao Dk Slaa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 akiwa nyuma ya Rais Kikwete aliyepata kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17, Dk Slaa hakuwahi kukutana na mkuu huyo wa nchi ana kwa ana.

Katika hafla ya kutangazwa matokeo ya urais iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, Dk Slaa hakuhudhuria tofauti na ilivyokuwa kwa waliokuwa wagombea wenzake wote.

Dk Slaa, ambaye alikataa kuyatambua matokeo hayo, tangu wakati huo hawakuwahi kukutana rasmi na Rais Kikwete huku uvumi ukizagaa kwamba kwamba mwanasiasa huyo amekuwa akijaribu kukwepa asikutane ana kwa ana na Rais Kikwete kwenye mazingira yoyote.

Katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema yaliyofanyika katika Kijiji cha Lipangalala, hivi karibuni Dk Slaa alidaiwa kumkwepa Rais Kikwete, kwa kutokwenda kukaa kwenye nafasi aliyoandaliwa jirani na kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Ilidfaiwa kuwa nyumba kulikofanyika shughuli za awali za mazishi, waandalizi waliandaa majukwaa mawili, moja maalumu kwa ajili ya wabunge huku jingine likiwa ni maalumu kwa ajili ya viongozi wakuu ambalo alikaa Mbowe, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe.

Mbali ya kukaa viongozi hao, kulikuwa na nafasi ambayo ilikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya Rais. Mbali ya nafasi hiyo, pia kulikuwa na kiti ambacho ilitegemewa kwamba Dk Slaa angekalia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Chadema alidaiwa kukikwepa na kwenda kujichanganya katika jukwaa la wabunge na kiti hicho kubaki bila ya kukaliwa na mtu.

Hata hivyo Dk Slaa alikanusha uvumi huo na kudai kwamba asingeweza kwenda kukaa jukwaa alilokaa Rais Kikwete kwani yeye si kiongozi wa serikali hivyo kwa mujibu wa itifaki, asingeweza kumfuata Rais Kikwete na kwenda kumsalimia alipoketi.

Hii ni mara ya pili kwa ujumbe wa Chadema kukutana na Rais Kikwete Ikulu kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.

CHANZO: MWANANCHI