ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 25, 2012

ZAO LA NDIZI KUTOWEKA MKOANI KAGERA?

Maradhi kwa mmea aina ya migomba wilayani Muleba mkoani Kagera yanayofahamika kama 'mnyauko' yameibuka kwa kasi na kuathiri zao hilo. Dalili za awali ndizi hata kama ni changa huonekana kama mbivu nayo majani taratibu hukauka na kukatika.

Hatua ya pili ndizi hukauka na kuwa kavu kama kuni nayo majani hukauka kabisa...

Ni dizaini flani kama virusi kwa mmea wa mgomba kwani ni vijidudu visivyoonekana kama tuonavyo wadudu wengine kama viwavi, papasi nk. na ni ugonjwa unaoambukiza mmea baada ya mmea.

Sehemu zenye udongo mzuri wenye rutuba ndiko hasa huathirika na maradhi haya...Wito kwa serikali kupeleka wataalamu wake haraka katika maeneo yaliyoathirika zaidi vijiji vya Iyunga Kishanda mkoa wa Kagera kwani zao hilo maarufu lenye kushika eneo kubwa la uchumi wa watu wa mkoa huo kuna kila dalili linaweza kutoweka kabisa na kubaki historia kwani baadhi ya wakulima wameanza kubadili kilimo kwa kufyeka zao la ndizi na kuelekea kwenye ukulima wa mazao ya maharagwe na karanga wakikwepa maradhi hayo ya migomba.


Chunguza mjomba utabaini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.