ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 2, 2016

KAMA UNATAKA MAPENZI YASIKUUMIZE BASI HII HAPA SIRI.

Dr. Paul Nelson kutoka Mwanza Tanzania.
Kwa nini itokee kwangu? ... usiwe mjinga wewe mtoto, yani ujiuwe sababu gani mwanaume kwani ulizaliwa nae? Yaani pamoja na kumsomesha na kumgharamia maisha yote hii leo amenitosa? Ni moja kati ya kauli ambazo si ngeni toka kwa waachwao au kukutana na kimbunga cha mapenzi.

Nazo taarifa za watu kujiua kisa wivu wa mapenzi zimekuwa si ngeni tena huku zikijitokeza kila kukicha kwa kila taarifa 5 za kujiua basi 4 ni wivu wa mapenzi.

Kwanini watu uchukua maamuzi magumu ya kushangaza ambayo kadri siku zinavyosonga pamoja na elimu inayotolewa na wananchi mmoja mmoja na makatazo ya Serikali (kujichukulia sheria mkononi) lakini bado idadi ya wahanga wa kuumizwa na mapenzi inaongezeka .......Ushike wapi ili mapenzi yasikuumize? Jeh ni kipi cha kuthamii katika mapenzi? BOFYA PLAY KUMSIKILIZA 


KOCHA JOSEPH OMOG AHAIDI MAKUBWA SIMBA. YANGA NA TFF HAPATOSHI.


 Kocha Joseph Omog  awahidi viongozi na mashabiki wa  klabu ya Simba kuisaidia klabu yao kutwaa kombe la ligi kuu soka Tanzania bara; 

 Klabu ya Yanga yaeleza kushangwa na hujuma zinazofanya na shirikisho la soka nchini TFF kwa kuitaka CAF kufuta mchezo wao dhidi ya TP Mazembe uliofanyika tarehe 28.06.2016 jijini Dar es Salaam; 

MSIMU WA WACHEZI KUVUNA NDIYO HUU.

KLABU ya Liverpool imekamilisha rasmi usajili wa Sadio Mane aliyetua Anfield kwa kitita cha paundi milioni 34 kutoka Southampton. 

Nyota huyo anajiunga kwa mkataba wa muda mrefu na usajili wa tatu kwa Liverpool kiangazi hiki baada ya kuwa tayari wamewanasa kipa wa kimataifa wa Ujerumani Loris Karius na beki wa Cameroon Joel Matip.

 Ada ya uhamisho wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 24, inadaiwa inaweza kupanda na kufikia paundi milioni 36 hivyo kupita ile ya paundi milioni 35 aliyosajiliwa Andy Carroll mwaka 2011 na kuwa mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo. Mane amefunga mabao 21 katika mechi 67 za Ligi Kuu alizoichezea Southampton baada ya kujiunga nao kwa kitita cha paundi milioni 10 akitokea Salzburg mwaka 2014.

Henrikh Mkhitaryan, 27, atakamilisha uhamisho kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United weekend hii.

Mchezaji huyo kutoka Armenia atagharimu takriban pauni milioni 26 (Daily Mail), Manchester City wapo tayari kulipa hadi pauni milioni 50 kumsajili beki John Stones, 22, kabla ya kuanza kwa mechi za kabla ya msimu (Telegraph), Crystal Palace wamekubali kulipa pauni milioni 12.5 kumsajili beki wa West Ham James Tomkins, 27 (Daily Mail), mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanafikiria kumsajili beki wa kati wa Arsenal, 30, ambaye mkataba wake Emirates unamalizika mwaka 2019 (Evening Standard),

Everton wamekubali kumsajili kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel, 27, kutoka Zenith St Petersburg na watamlipa mchezaji huyo zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki (Squawka), Stoke City wametoa dau la pauni milioni 16 kutaka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, na wako tayari kumlipa pauni 70,000 kwa wiki (Mirror).

Burnley wanataka kumfanya beki Michael Keane, 23, kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo ili kuzuia kusajiliwa na Leicester City (Mirror), mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 32, anauzwa na klabu yake ya Fernabahce (Evening Standard), mshambuliaji wa Manchester United Ashley Fletcher, 20, amekataa mkataba mpya na atafanya vipimo West Ham (Manchester Evening News).

PIX ZA BIRTHDAY YA MWANANGU MWENYEWE CUTHBERT

Tarehe 27 juni tullimpa hongera ya kuzaliwa Cuthbert Albert G. Sengo
Tabasamu la msimu.
Surprise inapohusishwa.....Dah
Avator ......
Familia.
Brothers.
Baba na mwana.

SASA NI VITA KATI YA CHRISTIANO RONALDO DHIDI YA GARETH BALE.

TIMU ya soka ya Wales iliweka rekodi nzuri usiku wa Jumamosi katika historia ya soka nchini humo walipotoka nyuma na kuishinda Ubelgiji katika michuano ya Euro 2016 na hivyobasi kujikatia tiketi ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika mchuano mkubwa.

Radja Nainggolan aliiweka kifua mbele Ubelgiji mjini Lille kupitia mkwaju mkali alioupiga umbali wa miguu 25 lakini nahodha wa Wales Ashley Williams alifunga bao la kichwa kupitia kona na kusawazisha katika kipindi cha kwanza cha mechi.
Lakini mashabiki wa Wales walifurahishwa zaidi na bao lililofungwa na Hal Robson Kanu ,ambaye ni mshambuliaji bila klabu,na kufanya mambo kuwa 2-1.
Na baada ya presha kali kutoka kwa washambuliaji wa Ubelgiji ,Wales walikifunga kidomodomo cha wapinzani wao kupitia kichwa kilichofungwa na mchezaji wa ziada Sam Vokes na hivyobasi kutinga nusu fainali dhidi ya Ureno huku wachezaji nyota wa Real Madrid Gareth Bale na Christiano Ronaldo wakijipata katika pande pinzani.

RUFANI YA SHEIKH PONDA YAKWAMA MAHAKAMA KUU

RUFANI ya Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kumwachia huru Sheikh Ponda Issa Ponda, dhidi ya kosa la kushawishi wakazi wa mkoa huo kufanya kosa, ilikwama kuendelea jana na kuahirishwa kwa wiki tatu baada ya mawakili wa utetezi kuomba muda wa kujadili na mteja wao.

Jana kesi hiyo ilitajwa na Jaji Edson Mkasimongwa katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Malangwe Mchungahela alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza.

Hata hivyo, mawakili wa utetezi, Abubakar Mohammed na Juma Nassoro, kwa nyakati tofauti waliomba mahakama kuwapa muda wa kuzungumza na Sheikh Ponda, kama wataendelea kutoa huduma kwake ama la.

Nassoro alidai kuwa makubaliano yao ya awali ya kumtetea katika mahakama ya chini yalishamalizika, na hakuna maelekezo yoyote ili kuweza kumuwakilisha mahakamani hapo. Jaji Mkasimongwa alisema kesi hiyo itasikilizwa Julai 23.

Katika rufani hiyo, upande wa Jamhuri uliwasilisha hoja nne ikiwemo, mahakama ya chini ilikosea kwa kutokuzingatia uzito wa ushahidi wa kielektroniki katika kutoka uamuzi wake.

Sababu ya pili na ya tatu, Jamhuri inadai, Hakimu wa Mary Moyo alikosea aliposema hati ya mashtaka ilikuwa na mapungufu ya kisheria na Sheikh Ponda hakuwa na nia ya kushawishi umma wa mkoa huo kufanya kosa siku ya tukio.

Sababu ya mwisho ya Jamhuri katika kupinga kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda ni kwamba hakimu alikosea kusema kuwa ilishindwa kuthibitisha kosa bila kuacha shaka.

PPF YAIBUKA KIDEDEA KUNDI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NA MAKAMPUNI YA BIMA MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016

Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wapili kulia) akiwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, (wakwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya msindi wa kwanza kundi la  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makampuni ya Bima, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele (wakwanza kulia) akiungana na wafanyakazi enzake kusherehekea tuzo ambayo Mfuko umepata wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Afisa wa PPF anayeshughulikia huduma kwa Wanachama Mohammed Siaga,akionyesha tuzo hiyo
Wafanyakazi wa PPF wakishangilia ushindi huo mbele ya banda lao.
Wafanyakazi wa PPF wakishangilia ushindi huo mbele ya banda lao.

MADC WAPYA MKOANI TANGA WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA UMAKINI MKUBWA

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza kwenye halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Othumani Shijja.

Mkuu wa wilaya mpya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella leo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanaisha Rajabu akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martne Shigella 
Add caption
Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdallah Issa akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo.
Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Robert Gabriel akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella anayeshuhudia kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said.


Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Steven Ngonyani alimaarfu Professa Maji Marefu kulia akimtambulisha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM)Stanslaus Mabula wakati wa Halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya leo

Mkuu wa wilaya Mpya wa Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe kulia akitete jambo na Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga,William Mngazija mara baada ya kuapishwa

Mkuu wa Mkoa wa Tanga katikati akiwa picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga leo mara baada ya kuwaapisha
picha kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Friday, July 1, 2016

UGAIDI WACHANGIA YANGA KUAMUA KUBADILI KAMBI YA UTURUKI.

Tukio la shambulio la kigaidi kwenye Uwanja wa Ndege wa Ataturk mjini Istanbul, Uturuki limebadili mipango ya Yanga kwenda kuweka kambi nchini huko kubadilika na badala yake inajipanga kwenda Pemba.


Yanga ilikuwa Antalya, Uturuki ilipoweka kambi kujiandaa na michezo yake miwili ya Kombe la Shirikisho, ikaahidi kurejea Uturuki baada ya mechi dhidi ya TP Mazembe, Jumanne ya wiki hii lakini sasa imebadili uamuzi.

"Timu itaondoka kesho (leo) kuelekea Pemba kwa ajili ya kambi ya muda kujiandaa na mechi na Medeama ambayo ni muhimu kwetu kupata ushindi ili hesabu ziende sawa.

"Sisi tulichopanga ni kushinda michezo yote iliyobaki ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya MO Bejaia na Medeama.

"Maamuzi hayo ya kambi ya Pemba yametokana na tukio kubwa la kigaidi lililofanywa huko Uturuki, hivyo kiusalama tumeona ni vema tukabaki nchini," alisema mtoa taarifa wetu.


Alipotafutwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro kuzungumzia hilo alisema: "Kambi yetu tutaitangaza wakati wowote wapi tutakapokwenda, hivyo subirieni kwanza tutawajulisha.”

TAARIFA KWA UMMA


ThisTAARIFA KWA UMMA
Kufuatia kutimiza agizo la uzimaji wa simu bandia, kutokana na agizo elekezi la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inapenda kuwajulisha wateja wake walio nunua simu orijino kutoka kwa watoa huduma ndani ya maduka yetu ya Airtel, endapo baadhi ya wateja simu zao zitazima kutokana na agizo hilo. Airtel inawatangazia wateja wote watakaoathirika na zoezi hili kutembelea maduka yetu nchi nzima kwaajili ya kuhudumiwa/kurekebishiwa simu zao wakiwa na simu husika pamoja na risiti za manunuzi ya simu hizo.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na zoezi hili.
Imetolewa na Idara ya mawasiliano Airtel Tanzania
Mwisho
Jackson Mmbando
Airtel Tanzania | Public Relations Manager

PENUEL CONFERENCE 2016PENUEL Maana yake ni mahala pa Kukutana na Mungu uso kwa uso na nafsi yako ikabaki salama, hii ni kulingana na Mwanzo 32:30 kwa kile kilicho mtokea Yakobo,Kongamano la Penuel linamahanisha mahala pa kukutana na Mungu kupitia Neno lake linalo hubiriwa na watumishi wake mbalimbali kulingana na maelekezo juu ya watu wa Mungu!

Katika Kongamano hili la PENUEL 2016 litajumuisha wanenaji kutoka nje ya Tanzania na ndani ikiwemo Arusha,Afrika Kusini,Mbeya, DRC, Kenya, Cameroon n.k

Mwenyeji wa PENUEL 2016 Apostle Onesmo Ndegi na Lilian Ndegi. Pia wanenaji wengine kutoka Tanzania ni Askofu Emmanuel Tumwidike kutoka Mbeya na Bishop Olam Mustapha kutoka Arusha. Kutoka Kenya ni Bishop Tengu Yoka na kutoka Africa Kusini ni Dr.Apostle Peter Muteba pia kutoka Cameroon tunaye Bishop Angela Acha-Morfaw na Apostle Israel Abam kutoka Nigeria.

Mahali ni Living Water Centre Kawe, Dar es salaam, Tanzania Uzinduzi wa Kongamano ilikuwa ni leo siku ya Jumanne kuanzia saa 8:00 mchana,siku zinazofuata ni kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.Karibu Ukutane na Mungu kupitia Neno kupitia watumishi wake! Barikiwa!

Theme: Transformation Romans 12:2


 Source:gospelhabari.blogspot.com

PBZ YAADHIMISHA MIAKA 50 YA PBZ KWA iFTAR MAALUM KWA WATEJA WAKE NA WAFANYAKAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir na Mgeni Rasmin Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Ali Khamis, wakijumuika na Wananchi na Wafanyakazi wa PBZ katika futari ilioandaliwa kuadhimisha Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa PBZ mwaka 1966 2016.iliofanyika katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar, 
Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wastaaf wa PBZ wakijumuika katika futari Maalum ya kusherehekea Miaka 50 ya PBZ wakipata futari katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Wafanyakazi wa PBZ wakipata futari katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO July 1, 2016


Takukuru na TRA wataja mwizi EFD, Wabunge watatu wa CHADEMA wafungiwa, Lissu atoa kauli nzito, Afya ya Meya Dar yateteleka. Pata undani wa dondoo hizi hapa.

Milya, Sugu na Kubenea matatani, UKAWA wamaliza bunge kwa msiba, Hoja ya waziri mkuu yachomekewa Lugumi. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.

Thursday, June 30, 2016

sss

ssss

BILA KUBORESHA SHERIKA YA USIMAMIZI WA MAZINGIRA VITA DHIDI YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NI NDOTO.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini (ADLG), Mr. Jimmy Luhende,  akitoa darasa katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo Jijini Mwanza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali toka Taasisi, mashirika na vikundi vya ujasiliamali Kanda ya Ziwa.
 Jamal Baruti ambae ni Mratibu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Kanda ya Ziwa, akiwasilisha mada juu ya tathmini ya athari za mazingira zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini.
Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini. 

 Katika mjada ulio wasilishwa, wadau wameishauri serikali kupia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEC, kuboresha sheria ya usimamizi wa mazingira ili kuweza kuwafanyia tathmini za uchafunzi wa mazingira wachimbaji wadogo kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakichangia uchafunzi wa mazingira nchini. 
Kwa umakini na kumbukumbu daftarini, wadau wa mazingira wakichukuwa pointi.
Kwa mujibu wa wachangiaji, Tathimini ya uchafuzi wa mazingira imekuwa ikifanyika kwa wachimbaji wakubwa wa madini kabla na baada ya uchimbaji lakini wachimbaji wadogo wamekuwa hawaguswi na tathmini hiyo kutokana na kutojumuishwa katika tathimini hiyo kwa mjibu wa sheria ya mazingira.Ni vyema sasa wachimbaji wadogo wadogo wakashirikishwa ipasavyo ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira katika shughuli zao.
Kasi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea inaweza kurudi nyuma miaka mitano ijayo,iwapo hatua thabiti hazitachukuliwa kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira.
Ripoti ya 2011 kuhusu uendelevu na usawa ilieleza kuwa, uendelevu wa mazingira unaweza kufikiwa kwa njia ya haki na yenye matokeo mema iwapo masuala ya afya, elimu, kipato, na tofauti za jinsia kuchukuliwa hatua za kimataifa kuhusu uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira.

Uharibifu wa mazingira unatishia uhai wa viumbe duniani kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli mbalimbali za wanadamu ikiwemo ukataji miti na uchomaji moto misitu ya asili.

Msisitizo mkubwa umekuwa ukifanywa na wadau wa mazingira kwa kuhakikisha mikataba na sheria zinawekwa ili kulinda, mazingira na viumbe adimu wasitoweke.
Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizobarikiwa kuwa na misitu ya asili na mito mikubwa isiyokauka maji kwa kipindi cha mwaka mzima.

Mbali na vivutio hivyo,kumekuwa na uelewa mdogo wa masuala ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji miongoni mwa jamii.

Ukosefu wa elimu kwa jamii ya Watanzania umesababisha wananchi kushindwa kutambua umuhimu wa kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji vilivyowazunguka katika maeneo yao.
Wadau wa habari ambao vile vile ni Bloggers wa Mwanza, kutoka kushoto Gsengo, Atley Kuni na Kijukuu cha Bibi.
Mchanganuo toka katika jedwali la Makampuni na kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na mapitio ya sheria ya mazingira.
Wadau wa mazingira wamekusanyika hapa