Saturday, September 24, 2011
huzuni
Friday, September 23, 2011
SIASA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kwamba licha ya madai kuwa chama hicho kimepoteza mvuto mbele ya jamii lakini takwimu zinaonyesha watashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga mkoani Tabora.Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema kwamba wanaodai kuwa Chama hicho kimepoteza mvuto wanatumia hoja za jumla badala ya takwimu. Amesema kwamba utafiti mdogo alioufanya katika mikoa 12 kwa kuangalia matokeo ya chaguzi ndogo za serikali za mitaa zilizofanyika kati ya mwaka 2009 hadi 2011, unaonyesha kuwa CCM bado ina mvuto mbele ya jamii na ana uhakika wanashinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge huko Igunga.
Mikoa ambayo amefanya utafiti ni pamoja na Mara, Pwani, Dar es salaam, Shinyanga, Mbeya, Manyara, Singida, Morogoro, Mtwara, Arusha, Tabora na Tanga pia katika mikoa hiyo kwa kipindi cha kati ya mwaka 2009 na 2011 zimefanyika jumla ya chaguzi ndogo za viongozi wa vijiji 84, mitaa 22 na vitongoji 248.
Kwa mujibu wa Nape, kati ya viti 84 vya wenyeviti wa vijiji, CCM kimefanikiwa kunyakua viti 83 sawa na asilimia 98.8, kati ya mitaa 22, CCM kimeshinda viti 17 sawa na asilimia 77.3 na kati ya vitongoji 248, CCM kimeshinda vitongoji 186 sawa na asilimia 75.
Akizungumzia kuhusu ukali wa maisha Mh. Nape anasema suala hilo linahusiana na uchumi wa dunia na si kwa nchi ya Tanzania.
Akizungumzia hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuachia nyadhifa zake za ubunge na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) akidai kuchoshwa na siasa uchwara lakini akarejea tena katika ulingo wa siasa kumnadi mgombea wa chama hicho Dk. Peter Kafumu, Nape amejitetea kwa kutoa mfano kwa kusema kuwa hata kanisani mtu akifanya kosa kuna adhabu maalum zilizo wekwa kama vile kutokushiriki meza ya bwana na kadhalika lakini siyo kwamba mtu huyo atakatazwa kuingia kanisani, ataingia kanisani kwa minajili ya kulishwa neno kuendana na utaratibu.
Amebainisha kubainisha kwamba Chama Cha Mapinduzi kinao mtaji wa wanachama ambapo katika kura za maoni kuwapata wagombea katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mgombea wa CCM alichaguliwa na wanachama 588 ilhali mgombea wa CHADEMA alichaguliwa wanachama 63.
Kupitia takwimu hizo Nape amejigamba kwa kusema kuwa CCM ina msingi mzuri iliyoujenga wa kushinda katika uchaguzi huo mdogo wa ubunge katika Jimbo la Igunga licha ya fitna zinazojitokeza kila kukicha toka kwa wapinzani wake, hivyo watu wasishangae siku chama hicho kitakapotangazwa kuwa mshindi.
Friday, September 23, 2011
HABARI
KAMPUNI ya uuzaji wa mafuta ya BP imesalimu amri kwa Serikali, hivyo kuamua kuondoa mahakamani shauri la kupinga kufungiwa kwake na badala yake kurejea katika meza ya mazungumzo, hivyo kupewa masharti manne inayopaswa kuyatekeleza kabla ya kurejeshewa leseni kuendelea na biashara hiyo.
Masharti hayo yanatokana na kampuni hiyo kukaidi agizo la Serikali la kushusha bei ya mafuta iliyotolewa Agosti mwaka huu, na badala yake kufunga vituo vyake vyote, hali iliyochangia uhaba mkubwa wa mafuta nchini. Hatua hiyo ilisababisha Serikali kutoa amri ya kufunguliwa kwa vituo hivyo katika muda wa saa 24, amri ambayo BP iliendelea kuikaidi, hivyo kupokwa leseni yake.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, BP ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizokuwa zikisambaza mafuta nchini, lakini baada ya kushushwa kwa bei ya bidhaa hiyo kampuni hiyo iligoma, badala yake ikakimbilia mahakamani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Masebu alisema kutokana na hasara waliyopata, BP wamelazimika kufuta kesi na kutaka kuingia kwenye kikao cha majadiliano kilichohitimisha malumbano yaliyokuwapo kwa kuwapa masharti manne kabla ya kuwarudishia leseni.
Chanzo cha mvutano
Mvutano baina ya Serikali na BP ulianza Agosti 3, mwaka huu baada ya Ewura kupitia kwa Masebu ilipotangaza kushusha bei ya mafuta mjini Dodoma ambapo petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa sawa na asilimia 9.17.
Katika tangazo hilo, dizeli ilishuka kwa Sh173.49 sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa yalishuka bei kwa Sh181.37, sawa na asilimia 8.70. Masebu alisema kushuka kwa bei hizo kulitokana na kukamilika kwa mchakato wa kuandaa kanuni mpya ya ukokotoaji wa bei za bidhaa za mafuta hasa kutokana na maagizo ya Serikali na pia, kubadilika kwa viwango vya kodi katika bidhaa za mafuta.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, kodi za mafuta ya taa ziliongezwa na pia kupunguzwa kwa kodi za mafuta ya dizeli na tozo za mamlaka mbalimbali zimetazamwa na kupunguzwa.
CHANZO www.mwananchi.co.tz
Thursday, September 22, 2011
MICHEZO
Wednesday, September 21, 2011
MICHEZO
Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena leo kwa michezo mbalimbali mmojawapo ukipigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo timu za Simba ya Dar es salaam na Toto toka jijini hapa zimegawana pointi mara baada ya kutoka sare ya 3-3.
Mchezo ulianza kwa kasi ya ajabu pasi za nguvu, wachezaji wa timu zote wakionana mithili ya game za soka barani Uropa na haikuchukuwa muda ilikuwa ni dakika ya 8 tu kipindi cha kwanza mchezaji Felix Sunzu aliwanyanyuwa mashabiki wa timu ya wekundu wamsimbazi kwa kupachika bao la kuongoza.
Toto wakicheza nyumbani wakiwa na kibri cha kuwa na mashabiki lukuki huku wakionana walifanikiwa kuichanganya ngome ya simba kwa samba la hatari likiongozwa na vifaa vipya walivyosajili mwaka huu hali iliyopelekea ngome yake kupoteza mwelekeo hivyo kusababisha madhambi na Toto kuzawadiwa penati, bila ajizi mshambuliaji wa kimataifa aliyesajiliwa na timu hiyo Darlington Enyina aliutumbukiza kimiyani mpira huo kuandika bao la kusawazisha ikiwa ni dakika ya 15 ya mchezo.
Toto ilijipatia bao la pili dakika ya 26 kupitia Mohamed Sudi , Simba ikasawazisha dakika ya 59 mfungaji akiwa Felix Sunzu.
Bao la tatu la Toto lilipatikana katika dakika ya 65 kupitia Iddi Mudy nao Simba kusawazisha tena bao hilo dakika tatu baadaye kwa mkwaju wa kiufundi wake mshambuliaji mahiri wa wanamsimbazi Patrick Mafisango.
Mchezo uligeuka kuwa wa upande mmoja kwa Simba kulisakama kama nyuki lango la Wanakishamapanda waliopoteza uelekeo mara baada ya moja kati ya kifaa chake Filemon mwendafile kulimwa kadi nyekundu akimkanyaga mgongoni tena kwa maksudi mchezaji wa Simba Kago.
Hadi mwisho ngoma droo Simba 3, Toto 3.
Sunday, September 18, 2011
huzuni