ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 6, 2022

POLISI WAFANYA MAZOEZI NA MAMBA UKEREWE.

 NA ALBERT G. SENGO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA imetenga bajeti kwaajili ya kutoa mafunzo kwa askari wasaidizi wa ulinzi maeneo ya Bandari. - Ramadhan Ng'anzi ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza. - Mrisho S. Mrisho ni msimamizi wa huduma za ulinzi wa bandari. wamekuwa mashuhuda wa hitimisho la mafunzo hayo yaliyofanyika jijini hapa.

RUTO AWATAKA WAPIGA KURA KUAMKA MAPEMA KWENDA KUMMALIZA MPINZANI WAKE UCHAGUZI MKUU KENYA.

Naibu Rais William Ruto amewataka wafuasi wake kurauka kumpigia kura katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 Ruto ametaniana na wafuasi wake Narok akiwaambia kuwa warauke saa tisa asubuhi badala ya saa kumi walivyomwambia Ruto pia amemtupia vijembe Raila Odinga akisema kuwa tayari wilibaro imetengwa ya kumsafirisha nyumbani.

Akihutubia wafuasi wake katika mkutano wa kisiasa katika Kaunti ya Narok mnamo Jumamosi, Agosti 6, Ruto alitaniana na umati kuhusu wakati wa kuamka kwa shughuli hiyo. 

Katika mazungumzo yao, umati ulimwambia Ruto kuwa utaamka saa kumi asubuhi ili kwenda kupiga kura lakini kiongozi huyo wa chama cha UDA akasema kuwa kwa kuamka saa tisa watakuwa wamechelewa. 

 Ruto aliendelea kuulizana na umati: "Ati saa ngapi? Saa kumi? Mimi naona muamke saa tisa. Mimi naona saa kumi mnaanza kuchelewa. Sindio?" Kwa mujibu wa Ruto, iwapo wafuasi wake wataamka mapema na kumpigia kura, watahakikisha kuwa anambwaga mpinzani wake mkuu Raila Odinga mapema. 

Ruto ametupia vijembe Raila ambaye ni mgombea wa Azimio akisema kuwa tayari mikakati ipo ya kuhakikisha anaastafu kabisa kutoka kwa siasa. 

Tumekubali ni saa tisa? Ndio tumalize hii kura. Kabla ya mzee wa kitendawili hajaamka kura imekwisha. Mnanisikia jameni? Na tayari tumemtayarishia wilibaro. Si mmeona wilibaro?" Ruto alisema. 

WATUMISHI WA SERIKALI TANGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA NYONGEZA YA MSHAHARA,WASEMA AMEUPIGA MWINGI

 

Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja

 

Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja

Mtumushi wa Jiji la Tanga kada ya Elimu  Mwanaidi Mashaka


Na Oscar Assenga,Tanga.

WATUMISHI wa Serikali Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 23 ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo ambalo miaka ya nyuma halikufanyika na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Tanga jambo ambalo amelifanya kwao ni kubwa mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.

Akizungumza mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka alisema wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo limefanyika.

“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii”Alisema

Naye kwa upande wake mtumishi mwengine Waziri Ally ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Elimu ya Msingi alisema wana mpongeza Rais kwa mengi aliyoyafanya kwa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23 imewagusa moja kwa moja wao kama watumishi.

Alisema asilimia 23 sio ndogo wanaweza kufanya jambo kubwa kama watumishi na wana morali wa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza malengo yaliyotarajiwa yanafikiwa.

“Kwa kweli ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara na ongezeko la watumishi sasa tumekuwa wengi na tunafanya kazi bila kuwepo kwa mzigo mkubwa”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake Stella Siang’a ambaye ni mtumishi wa Jiji Kada ya Elimu alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewafanyia mengi mno jambo la kwanza ni kuongeza wafanyakazi miaka mingi watu walikuwa hawajaajiriwa walikuwa mitaani iliyokwenda sambamba na ongezeko la mishahara ambalo litawawezesha kufanikisha majukumu yao.

Halikadhalika mtumishi mwengine Kasim Bashiru Lyimo kutoka Idara ya Elimu Sekondari alisema kwamba wanampongeza Rais Samia ameupiga mwingi kwa mambo mazuri aliyoyafanya kwa kuweza kuwaongezea asilimia 23 ya mshahara.

“Hili jambo sisi tumelifurahia sana na tupo pamoja na Rais na tuna hari ya kufanya kazi na atakapokuwepo mama na sisi tutakuwepo kuhakikisha tunamuunga mkono”Alisema

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Joshua Kiula alisema wana mpongeza Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuifungua nchi na inakwenda na imetulia .

Alisema pia amefanikiwa kufungua biashara zilikuwa zimefungwa na kurudisha na kuhuisha mahusiani na mataifa mengine ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha madaraja.

“Kwa kweli Rais Samia ameupiga mwingi kubwa ni kupandisha madaraja ambayo ni haki ya Msingi ya wafanyakazi na nyongeza ya mishahara jambo hilo ni nzuri na limewapa faraja kubwa kwetu”Alisema

Hata hivyo alisema nyongeza hiyo hawakuitegemea kama wataipata walidhani walipopandisha huo ndio ungekuwa mwisho lakini akaje na jambo lingine kwao la kuwaongezea asilimia 23 wamelipokea kwa moyo mkunjufu.

Thursday, August 4, 2022

USIKU WA VITASA | Hizi hapa 'show' za Mandonga na Shaban Kaoneka - 30/07/2022

 Tazama mambo yalivyokuwa wakati bondia Karim Mandonga 'mtu kazi' akimenyana Shaban Kaoneka kwenye #UsikuWaKisasi dimbani Majimaji Songea.

NANE NANE MWANZA 2022 TAYARI PAMENOGA

 Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) yalianza rasmi Mwezi Agosti mwaka 1994 na yamekuwa yakiadhimishwa Kitaifa kwenye Kanda Nane (8) kama ifuatavyo: –

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, uwanja vya John Mwakangale, Uyole, Jjijini Mbeya; Kanda ya Kaskazini, uwanja wa Themi, Jijini Arusha;

Kanda ya Mashariki, uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Manispaa ya Morogoro; Kanda ya Ziwa, uwanja wa Nyamhongolo, Jijini Mwanza;

Kanda ya Kati, Uwanja wa Nzuguni katika Jiji la Dodoma; Kanda ya Magharibi, Mkoani Tabora katika uwanja wa Ipuli;

Kanda ya Ziwa Mashariki, Mkoa wa Simiyu katika uwanja wa Nyakabindi na mwisho ni Kanda ya Kusini, Mkoani Lindi katika uwanja vya Ngongo.

Ikiwa leo ni siku ya pili tu lakini tayari wajasiliamali, mashirika na taasisi mbalimbali binafsi na zile za Serikali tayari wamekwisha simika mabanda yao kwenye viwanja hivi kwaajili ya kushiriki maonesho haya. Moja kati ya vivutio vikubwa hambavyo huwavuta watu hata wakahudhuria kwa wingi ni masuala ya misosi na zile chomachoma, askwambie mtu zipo za kutosha nazo zikipatikana kwa bei rahisi kuliko hata zile bei zetu za kitaa. Hatua chache Napata nafasi ya kuzungumza na wadau wa banda la masuala nyeti ya fedha … Nazungumzia Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza….

Wednesday, August 3, 2022

MALIMA AKABIDHIWA OFISI RASMI.

 

🖐🏾Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkuu mpya wa Mkoa Mwanza, Adam Malima.


Akizungumza kwenye makabidhiano hayo yaliyofanyika leo Agosti 03, 2022, Mhandisi Gabriel amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha kuanzia Juni 11, 2021 hadi Agosti 01, 2022.


Pia ametumia nafasi hiyo kuwaasa watumishi mkoani kutoa ushirikiano kwa Malima, kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutojihusisha na rushwa pamoja na kumuombea Rais Samia ili Taifa lizidi kwenda mbele zaidi kimaendeleo.


"Lipendeni Taifa lenu la Tanzania kwani watumishi mmepewa dhamana katika nafasi mbalimbali hivyo mnapaswa kutumia akili zenu na elimu mliyonayo ili kuweza kulitendea haki Taifa, ukiendekeza rushwa unalisaliti Taifa lako" amesema Mhandisi Gabriel.


Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima ameahidi kushirikiana vyema na watumishi mkoani Mwanza ili kuendeleza utendaji kazi wenye tija kimaendeleo.


Amesema Mwanza ni Mkoa wa kimkakati kiuzalishaji na biashara hivyo atashirikiana na wafanyakazi na wafanyabiashara katika sekta za umma na binafsi ili kupata mawazo yao yatakayokuza maendeleo ya Mkoa.

.

.

#DriveMix

@mcsuzuki_

@gsengoTv

WAZIRI AWEZO ARIDHISHWA NA UJENZI WA BWAWA MAJI IRINGA

Waziri wa maji Juma Aweso akiwa na viongozi wa wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa wakipewa maelezo ya namna ambavyo bwawa hilo litakavyo jengwa.
Waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza waziri wa maji Juma Aweso akiwa mkuu wa wilaya na viongozi wengine wilaya ya Iringa wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika kata ya Masaka Mkoani Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

WAZIRI wa maji Juma Aweso amewapongeza uongozi wa wilaya ya Iringa kwa kusimamia vizuri ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika bodi ya maji bonde la Rufiji kwa kuwa litafanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa kata ya Masaka.

 

Akiwa katika ziara ya kiazi mkoa wa Iringa waziri Aweso alisema kuwa ameridhishwa na ujenzi wa mradi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kwa kuwa mmoja ya miradi mingi mikubwa ambayo itakuja kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo.

 

Aweso alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeigiza wizara ya maji kuhakikisha inachimba mabwawa ya kila wilaya ili kutatua changamoto hiyo na kuongeza njia za kukuza uchumi wa maeneo husika.

 

Alisema kuwa kukamilika kwa bwawa hilo kutaisaidia kuleta maendeleo ya miradi mingine ya maji kutokana na usimamizi mzuri ambao unafanywa na uongozi wa wilaya na mkoa kwa ujumla kwenye maendeleo ya miradi ya kijamii.

 

Alisema mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua utagharimu kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni 900,982,000/= ambazo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amezileta  kutatua changamoto hizo kwa wananchi wa kata ya Masaka.

 

Akijibu maombi ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa na diwani wa Masaka Methew Nganyagwa alisema kuwa wanayafanyia kazi maombi yao na tayari suala la kuchimba bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Magubike lipo kwenye mpango wa fedha za mwaka huu na ombi la matank ya maji wataletewa mapema iwezekavyo.

 

Awali akisoma taarifa ya mradi kwa waziri,msimamizi wa mradi huo Eng Geofrey Simkonda alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni mkakati wa uendelezaji,utumiaji,uhifadhi na usimamizi wa vyanzo vya maji katika bonde la Rufiji.

 

Alisema kuwa lengo la ujenzi wa mradi huo wa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua ni kuvunia maji na kurahisiha upatikanaji wa maji kwa wananchi hususani wenye uhaba wa rasilimali za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kibinadamu.

 

Eng Simkonda alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Iringa,kata ya Masaka inayojumuisha Vijiji vya Makota, Sadan na Kaning'ombe watanufaika na mradi huo.

 

Alisema kuwa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua la Masaka lina kimo cha mita 14,urefu mita 260 na litakuwa na ujazo wa mita 439,803 na ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwaka 2022 hadi sasa mradi umefikia asilimia 50.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya mradi huo ambao kwa kiasi kikubwa utatua kero za wananchi pamoja na kuleta maendeleo kwa wananchi.

 

Alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji ya mvua katika Kijiji cha Sadan kutachochea maendeleo ya wananchi kiuchumi kwa shughuli ambazo zitakuwa zinafanywa katika eneo hilo.

 

Naye diwani wa kata ya Masaka Methew Nganyagwa alisema kuwa mradi huo utawanufaisha zaidi ya wananchi 7000 kwa shughuli mbalimbali za wananchi ambazo watakuwa wanazifanya kwenye mradi huo wa bwawa.

 

Nganyagwa alisema kukamilika kwa bwawa hilo licha ya kuondisha changamoto ya miaka mingi ya ukosefu wa maji Safi na salama, pia kutafungua na kuchochea fursa ya ukuaji wa kiuchumi kupitia fursa ya Kilimo cha umwagiliaji, Uhakika wa maji kwa ajili ya mifugo  pamoja na shughuli za uvuvi na biashara ya samaki katika Vijiji vinavyozunguka kata hiyo.

 

Nganyagwa akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa kata ya Masaka alisema  Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kwa vitendo dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani kwa kuwakumbuka wakina mama na wananchi masikini waliopo vijijini kwa kuwasogezea miradi mbalimbali hivyo ahadi ya wananchi ni kuendelea kumuunga mkono na kumuombea ili kufanikisha malengo ya maendeleo kupitia Serikali yake ya awamu ya sita.

Tuesday, August 2, 2022

Sababu 4 za kwa nini wanaume huumia zaidi kwenye mapenzi

 


Mapenzi ni kitu cha ajabu sana, watu kutoka koo, makabila, mataifa na wenye rangi tofauti hujikuta katika dimbwi zito. Hujikuta katika wakati ambao kila mmoja haoni kitu kingine cha thamani zaidi ya mpenzi wake. Huu ni wakati ambao si tu kuwa neno usaliti linakuwa halipo bali wapenzi hawahisi hata kama kuna maisha bila ya yule wampendaye.

Usaliti ni jambo lenye maumivu yasiyovumilika hasa ikiwa ni jambo ambalo halikutarajiwa. Mtu hahisi kama itatokea mpaka inapotokea. Mwishoni mwa wiki hii kumeenea picha za mwanaume aliyejikatisha uhai kisa mapenzi. Hii ikanikumbusha utafiti usio rasmi nilio ahi kufanya juu ya kwanini wanaume huumizwa zaidi na usaliti kuliko wanawake.

Sababu 4 za kwa nini wanaume huumia zaidi kwenye mapenzi

1. Wanaume si wepesi kusema yaliyowasibu.
Ukisikiliza vyombo vya habari au kusoma magazeti ni rahisi kukuta story ya mwanamke anayelalama baada ya mpenzi, mchumba au mume au mume kutoka na mwanamke mwingine. Lakini ni nadra sana kukuta mwanaume akilalama! Si kwa kuwa hawaumizwi au hawana majeraha, bali ni sababu kwa wanaume inaonekana kama kujidhalilisha kusema hivyo.

Hawatamani hata rafiki zao. Huishia kuumia peke yao, huishia kuhuzunika peke yao hiyo hupelekea kujenga majeraha makubwa moyoni. Kuendelea kufuga hasira ambazo saa nyingine hupelekea wao kufanya maamuzi ya ajabu na yenye kustaajabisha kwa jamii.

2. Mwanaume hupenda kuendelea kuwa na nguvu juu ya jambo fulani siku zote
Ndiyo, kwa mwanaume kuwa na watu wanaomtii, wenye kumheshimu na kumsikiliza ni jambo linalompa faraja na kumfanya ajivunie. Mwanaume anapokuwa na mwanamke hupenda kuona huyo mwanamke akimnyenyekea, akimtii na kumsikiliza, Kwa taarifa yako mwanaume hapendi hata yule mwanamke asiyempenda awe wa kwanza kusema imetosha,au awe na mwanaume mwingine, inapotokea hayo humfanya mwanaume ajione amepungikiwa kitu, humfanya ahisi yeye si bora tena hapo ndipo tatizo linapoanzia.

3. Wanaume wana tabia ya kumuamini sana mwanamke wanayekuwa naye
Moja kati ya kazi ngumu kwa mwanamme ni kumfanya amwamini mtu mwingine kwa kiwango kikubwa, Inaweza kuchukua miaka mpaka kufikia hatua ya kumuamini mtu mwingine hasa mwanamke. Lakini inapotokea akafanya hivyo huamini jumla. Hatua ya kumuamini sana mwenza wake huleta madhara makubwa mbele ya safari.

Tofauti na mwanamke ambaye siku zote anakuwa anawasha taa ya tahadhari na kujua inawezekana saa yoyote mpenzi wake atachepuka na inapotokea kweli mshtuko wake hauwezi kuwa sawa na mwanaume ambaye humwamini sana mwenza wake. Mwanamke anaweza kuzama kimapenzi au hata kuolewa na mwanaume asiye mwamini ni ngumu kwa mwanaume kufanya hivyo.

4. Sio rahisi kwa mwanaume kuhamisha upendo
Katika ulimwengu wanaume ndiyo wanaongoza kwa kuwa wasaliti kuna msemo unasema ‘every guy cheats’, ukweli tusioujua ni kuwa pamoja na kuwa wanaume hucheat zaidi kuliko wanawake ila wanafanya hivyo kwa sababu ya tamaa ya miili na nafsi zao hubaki kwa wenza wao wa kudumu

Si rahisi kwa mwanaume kumuacha mwanamke anayempenda na kuhamishia mapenzi hayo kwa mwanamke mwingine. Mwanamke anapokuwa mpweke Nna akatokea mtu ambaye akamtolea ule upweke anakuwa ameuwin moyo wake.

Usaliti umetokea ameamua alivyoamua, huo sio mwisho wa maisha kuna sababu nyingi za wewe kuendelea kuishi na kufurahia maisha. Pengine haya yanaweza kusaidia kukuamsha tena na kuona maisha yapo na hakuna sababu ya wewe kuumia.

NANE NANE MWANZA 2022 FASTA PAMEANZA KUNOGA

 Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) yalianza rasmi Mwezi Agosti mwaka 1994 na yamekuwa yakiadhimishwa Kitaifa kwenye Kanda Nane (8) kama ifuatavyo: –

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, uwanja vya John Mwakangale, Uyole, Jjijini Mbeya; Kanda ya Kaskazini, uwanja wa Themi, Jijini Arusha; Kanda ya Mashariki, uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Manispaa ya Morogoro; Kanda ya Ziwa, uwanja wa Nyamhongolo, Jijini Mwanza; Kanda ya Kati, Uwanja wa Nzuguni katika Jiji la Dodoma; Kanda ya Magharibi, Mkoani Tabora katika uwanja wa Ipuli; Kanda ya Ziwa Mashariki, Mkoa wa Simiyu katika uwanja wa Nyakabindi na mwisho ni Kanda ya Kusini, Mkoani Lindi katika uwanja vya Ngongo.

Ikiwa leo ni siku ya pili tu lakini tayari wajasiliamali, mashirika na taasisi mbalimbali binafsi na zile za Serikali tayari wamekwisha simika mabanda yao kwenye viwanja hivi kwaajili ya kushiriki maonesho haya. Moja kati ya vivutio vikubwa hambavyo huwavuta watu hata wakahudhuria kwa wingi ni masuala ya misosi na zile chomachoma, askwambie mtu zipo za kutosha nazo zikipatikana kwa bei rahisi kuliko hata zile bei zetu za kitaa. Hatua chache Napata nafasi ya kuzungumza na wadau wa banda la masuala nyeti ya fedha … Nazungumzia Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza….