Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja
Mtumushi wa Jiji la Tanga kada ya Elimu Mwanaidi Mashaka |
Na Oscar Assenga,Tanga.
WATUMISHI wa Serikali Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 23 ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo ambalo miaka ya nyuma halikufanyika na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Tanga jambo ambalo amelifanya kwao ni kubwa mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.
Akizungumza mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka alisema wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo limefanyika.
“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii”Alisema
Naye kwa upande wake mtumishi mwengine Waziri Ally ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Elimu ya Msingi alisema wana mpongeza Rais kwa mengi aliyoyafanya kwa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23 imewagusa moja kwa moja wao kama watumishi.
Alisema asilimia 23 sio ndogo wanaweza kufanya jambo kubwa kama watumishi na wana morali wa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza malengo yaliyotarajiwa yanafikiwa.
“Kwa kweli ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara na ongezeko la watumishi sasa tumekuwa wengi na tunafanya kazi bila kuwepo kwa mzigo mkubwa”Alisema
Hata hivyo kwa upande wake Stella Siang’a ambaye ni mtumishi wa Jiji Kada ya Elimu alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewafanyia mengi mno jambo la kwanza ni kuongeza wafanyakazi miaka mingi watu walikuwa hawajaajiriwa walikuwa mitaani iliyokwenda sambamba na ongezeko la mishahara ambalo litawawezesha kufanikisha majukumu yao.
Halikadhalika mtumishi mwengine Kasim Bashiru Lyimo kutoka Idara ya Elimu Sekondari alisema kwamba wanampongeza Rais Samia ameupiga mwingi kwa mambo mazuri aliyoyafanya kwa kuweza kuwaongezea asilimia 23 ya mshahara.
“Hili jambo sisi tumelifurahia sana na tupo pamoja na Rais na tuna hari ya kufanya kazi na atakapokuwepo mama na sisi tutakuwepo kuhakikisha tunamuunga mkono”Alisema
Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Joshua Kiula alisema wana mpongeza Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuifungua nchi na inakwenda na imetulia .
Alisema pia amefanikiwa kufungua biashara zilikuwa zimefungwa na kurudisha na kuhuisha mahusiani na mataifa mengine ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha madaraja.
“Kwa kweli Rais Samia ameupiga mwingi kubwa ni kupandisha madaraja ambayo ni haki ya Msingi ya wafanyakazi na nyongeza ya mishahara jambo hilo ni nzuri na limewapa faraja kubwa kwetu”Alisema
Hata hivyo alisema nyongeza hiyo hawakuitegemea kama wataipata walidhani walipopandisha huo ndio ungekuwa mwisho lakini akaje na jambo lingine kwao la kuwaongezea asilimia 23 wamelipokea kwa moyo mkunjufu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.