ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 1, 2011

FIESTA MUSOMA USIKU HUU NDO HAYA...!!!

Adam Mchomvu aka Baba Jonii, ni Fiesta 2011 ndani ya uwanja wa Karume Musoma mjini, watu wamejitokeza vya kutosha, swagga zimetyuniwa vya kutosha wazawa na wageni wamependeza ile kinowma yaani safiii.


Ngosha The Swagga Don amepiga show ya ukweli si kitoto..

Sajna wa Iveta

Kwa afya zetu.com sekta ilikamilika.

Ni nani huyu aliyebahatika kucheza na mwanadada Dayna?

Kutoka mkoani morogoro naikiwa ni mara yake ya kwanza kupiga show kwa wakazi wa Mara msanii Linex, alipata shangwe za kutosha kiasi cha kuurudia mara mbili wimbo wake wenye kibwagizo 'Kama ningeweza kuzirudisha siku nyuma..'

Si hip hop pekee bali hata Dansi za kiafrika Sheta anazimudu kinomanoma.

SWALI: "Oyaaaah! mbona wajisachi hivyo?"
JIBU: "Sasa we-weeee, unataka nikusachi wewe..?"


Kutoka shoto Dj Abuu, Dj Haruna, Dj Mully B na Dj White.

Chege na Temba na makamuzi ya kufufuka mtu!!

Siyo chini ya ulinzi bali ni Burudani tu mwakwetu! Hapa wazeeyah.. walikuwa wakicheza mapanga ya Wanaume TMK.

Hey out there!!

Mavijana ya kazi Lusajo, Jurnior na Pacha .

Roma alizioga shangwe...!!

Usafiri tegemeo usiku huu...

Mwanadada Mwasiti na vipaji vya ku-dance...

Tuite- Mwasiti Dance la Musoma.

MUSOMA HAINA MAJOTRO' MUSOMA MMETISHAAAAAaaaaaaa!!!!

BATA LA USIKU KUELEKEA FIESTA MUSOMA!


Ni shindano la kucheza Aladji' ndani ya Club House ndani ya msimu wa Dhahabu na Fiesta 2011 musoma mjini ambapo zawadi za kutosha zilimwagwa kwa akina dada.

Mtamboni kasimama Dj. Abuu.

Baadae wakachambuliwa na kubaki wachache.. Ushindi unasakwa..watuwamejipanga ile kinyama.

Mzuka Ulishapanda hatimaye zawadi nyingi tena nzito nzito zilitolewa kwa akina dada haswa kwa washindi wa kurudi mangoma.

Baada ya sekta ya kwanza kukamilika.. Ilikuwazamu ya baba jonii kuchanwa na kijana huyu kihipopU'....

Nae baba jonii ilipofika zamu yake poteza Mbaya.

Thursday, June 30, 2011

NAILETA KWENU FIESTA FOOTBALL


Ni katika maandalizi ya fiesta Musoma ndipo nakutana na mjasiliamali huyu anayetumia kipaji chake kujipatia riziki, aliyesafiri toka Rock City nyumbani anakoishini ya mji huu, binti huyu anauwezo kuutawala mpira wa miguu kupitia danadana kwa jinsi anavyotaka.

MUSOMA KUMEKUCHA BANA.....!!

Mmechisho!

Kutoka shoto ni mwana hip hop toka A.Town JCB mzee wa ukisikia Paaah! ambaye tayari keshatua Musoma kwaajili ya Fiesta akiwa na Baba Jonii na washikaji hapa wakidariz pande za Tembo beach jioni ya leo.

KIKAZI ZAIDI ni Mully B, Mblogishaji maarufu Kajuna Son na Lusajo wakihakikisha taarifa za Serengeti Fiesta 2011 Musoma zinasambaa kote Dunia.

Msonge bar iliyopo mkabala na Mativilla Garden, barabara ya Kennedy mjini Musoma, Panachomwa kuku hapa na michemsho ndo usiseme...

Mezani na wana Musoma... Kutoka shoto Abbas Chamba, Sanjey, Hamit, Anwar, Jaggler, G. sengo, Zuberi wa Serengeti na Mdau kiongozi Musoma Dick Nyongo

HAINA MAJOTROoo SERENGETI FIESTA MUSOMA NI KESHO IJUMAA KARUME STADIUM HAKUNA KUJIPE-PE-A COZ HAINA MAJOTRO'

Mpango mzima kesho haina kujipe-pea chako getini buku tatu tu!!!!

"Ni majira ya saa tano na nusu leo alhamisi kipindi hewani ni Extra Vaganza Show kupitia Victoria fm Musoma nami naitwa 'Cares One' Mpango mzima jidondoshe kesho pale Karume stadium tusherehekeee msimu wa Dhahabu pamoko!!"

Radio washirika, nami siwakanipa time sasa ...Bassss!!'

Kitaani leo asubuhi..na Mundeba bar Musoma.

Wednesday, June 29, 2011

PICHA YA LEO....!!!

JAMAA WALIPANGA NINI KUTUPIA KITU CHA RED AU NDO TUSEME INSHU ZA MSIMBAZI? Ni Fid Q na Profesa Jay ndani ya Fiesta Mwanza.... Pale back. What Next.

MUSOMA KWELI HAINA MAJOTROooooo!!!

Tumepata fursa ya kuitembelea Victoria Fm 90.6 na kugawa mizawadi ya msimu wa dhahabu ambayo pia kupitia redio hiyo yalikuwa yakimwagwa! siunajuwa tena' toka shoto Dj Lima, Adam mchomvu na Hosti wa kipindi husika (Ladha kamili) presenta John Mponeja.

Zamani mtu mzima nshatinga pande za Mara.

Kibao elekezi..

Kumuona babu''

Adam mchomvu akisema na wakazi wa maeneo ya stendi ya zamani iliyokatikati ya mji wa Musoma mkoani Mara, ambapo mizawadi ya msimu husika ilitolewa.

Sahihi zikiangukwa Eneo la Nyakato kwa saa nane, madereva wa pikipiki walizawadiwa mafuta kwaajili ya vyombo vyao vya usafiri, wengine wakitunukishwa tiket kuhudhuria Fiesta Musoma ijumaa hii tarehe 1july2011.

Sahihi kitabu cha dhahabu zilimwagwa vya kutosha na wakazi wa Musoma.
Makaribisho ndani ya mji wa Musoma tumekutana pia na mwenyeji wetu Dj Abuu na Musoma' ambaye ile vile alihudhuria Fiesta ya Kwanza Mwanza akitupa ushirikiano kiwango kikuu!!

Tuesday, June 28, 2011

VINJARI ZA MSIMU WA DHAHABU JIJI LA SANGARA

"Kwa faida ya wale wasio na kawaida ya kumgeuza samaki kutokana na mila zao walizojiwekea agiza samaki mbili namna hii, kisha kula ile pande iliyo juu ya samaki w0te - Of coz utakuwa umekula samaki kamili,BASSSi!" Says Adam Mchomvu aka Baba Jonii

Nguli wa muziki wa Ragga na Dancehall Shaggy ameondoka leo jijini Mwanza majira ya saa 6 kuelekea Dar es salaam ambapo atapanda pipa jingine kurudi kwao.

Awali alitembelea vivutio vya utalii vilivyoko jijini Mwanza kama vile Bismark Rock, sehemu za biashara kuu ya zao la samaki, hifadhi ya makumbusho ya tamaduni za wasukuma iliyopo Bujora na halikadhalika sehemu zote za vivutio mwambao wa ziwa victoria.

Amesifia mazingira mazuri ya jiji la Mwanza, makaribisho aliyopata toka kwa waandaaji Prime Times Promotion na mashabiki wa Mwanza.

Mie na best female vocalist wa bendi ya Shaggy aitwaye Aisha

CEO wa blogu hii na Shaggy

CHILUBA AZIKWA

Aliyekuwa Rais wa Zambia Frederick Chiluba amezikwa kwenye mji mkuu, Lusaka, kufuatia kifo chake wiki moja iliyopita. Mamia ya waombolezaji, walioongozwa na Rais Rupiah Banda, walihudhuria mazishi hayo.

Bw Chiluba alifariki dunia nyumbani kwake mwishoni mwa juma- sababu ya kifo chake hakijtangazwa kwa umma mpaka sasa. Aliiongoza Zambia kwenye demokrasia kwa kuanzisha vyama vingi mwaka 1991, lakini urais wake uligubikwa na madai ya rushwa

Amezikwa pembeni mwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Levy Mwanawasa, katika makaburi maalum kwa ajili ya Marais. Bw Mwanawasa, aliyemrithi Bw Chiluba, alifariki dunia mwaka 2008.

Maelfu ya watu walishuhudia mazishi ya Bw Chiluba kupitia televisheni ya taifa na kwenye skrini kubwa ziliozwekwa nchini kote.

Viongozi wakuu kutoka nchi za kigeni waliohudhuria mazishi hayo ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jospeh Kabila na waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KUPITIA BIA YA BALIMI EXTRA LAGER-KAGERA.

Mgeni Rasmi Mh. Ndyamukama Katibu Tawala (W) Bukoba akihutubia Mashindano ya Ngoma za Asili yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Balimi Extra lager, kushoto ni Andrew Mbwambo Meneja Mauzo na Erick Mwayela, Meneja Matukio kanda ya ziwa.

Mshindi wa kwanza Mashindano ya Ngoma za Asili kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba akishapokea fedha taslim laki tano(500,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Ndyamukama, hapa anasalimiana na Andrew Mbwambo Meneja Mauzo Kampuni ya Bia. Mshindi wa pili ni Rugu toka Karagwe walijipatia laki Nne(400,000/=), wa tatu ni Kabale toka Manispaa ya Bukoba walijipatia laki tatu(300,000/=).

Kundi la Rugowoile kutoka manispaa ya Bukoba wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wa kwanza.

Kundi la Rumanyika kutoka Karagwe wakionyesha umahiri wao wa ngoma za asili.

Haya ndio mambo yalivyokua katika viwanja vya Kaitaba katika kumsaka mshindi wa mashindano ya ngoma za asili kupitia kinywaji cha Balimi Extra lager.

Makundi mbalimbali yakionyesha umahiri wao.

Shughuli bado inaendelea ...