|
Marehemu Neema (kushoto) enzi za uhai wake alipotembelewa na Albert G.
Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza
kwa ajili ya kuchukuwa taarifa za kuomba msaada. |
Mtoto Neema George (16) amefariki dunia leo asubuhi majira ya saa moja huko wilayani Sengerema ambako ndiko wazazi wake wanaishi.
Mtoto huyu aliyetajwa kuwa na matundu matatu kwenye moyo (kwa mujibu wa vipimo) hivi karibuni akiwa na wazazi wake walijitokeza katika blogu hii na kuomba wasamaria wema kujitokeza kumchangia
fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
Taarifa za kiuchunguzi zinasema kuwa moyo wa marehemu Neema ulifikia hali ya kushindwa kutambua na kutofautisha kati ya damu safi na damu chafu na kama inavyojulikana kuwa kazi ya moyo ni kusukuma damu safi kwenda sehemu mbalimbali za mwili, pia damu chafu kuifanya ikasafishwe kwenye kibofu, ini na mapafu basi zoezi lote hili lilikuwa limefeli kwenye moyo wa mtoto huyo.
Marehemu Neema anatarajiwa kuzikwa kesho wilayani Sengerema.
Japo imeshindikana kunusuru maisha ya mwanae, baba wa marehemu aitwaye George
Lenatus Mugunga amewashukuru wasamaria wema waliojitokeza kumsaidia.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.