ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 16, 2019

KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YAKAGUA MAENDELEO YA MIRADI YA GESI ASILIA JIJINI DAR

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipokea taarifa za maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba (mwenye overall ya bluu) akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya PIC kazi ya kusambaza gesi asilia kwa wateja kwa matumizi ya majumbani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni.
Mhandisi Dora Ernest (alieshika mic ya TBC) akitoa maelezo ya huduma ya kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).
---
Kamati ya Bunge inayosimamia uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mhe. Dkt. Raphael Chengeni ilitembelea kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi na kujionea kazi za kitaalam zinazofanywa na wazawa katika kupokea gesi na kuisambaza kwa wateja mbalimbali wakiwemo wazalishaji umeme.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akitoa wasilisho juu ya mikakati ya TPDC katika kujiendesha kibiashara alisema “katika mwaka huu wa fedha tunategemea kuanza kutoa gawio Serikalini”. Mhandisi Musomba aliieleza Kamati ya PIC kwamba kwa sasa Shirika liko katika mageuzi makubwa ya kiutendaji nia ikiwa ni kuongeza ufanisi na hatimaye kutengeneza faida itakayoruhusu kutoa gawio kubwa Serikalini. 

Katika kipindi cha miaka mitatu TPDC imekuwa ikijeindesha kwa hasara kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mh. Dkt. Raphael Chengeni alisema “Sisi kama Kamati tumefurahishwa sana na mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika TPDC kwani hili lilikuwa moja ya Shirika ambalo linaonekana kuwa mzigo kwa Serikali kwa kushindwa kutoa gawio kwa Serikali”. 

Dk. Chengeni aliongeza kwamba kwa taarifa waliyopokea TPDC sasa wanaamini mambo yatakuwa mazuri katika Shirika hili ambalo linategemewa sana katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kuzingatia upekee wa bidhaa wanayozalisha, gesi asilia. Wajumbe wengine wa PIC pia walionekana kuridhishwa na utekelezaji wa miradi na mageuzi ambayo TPDC imeshaanza kuyafanya.

Katika ziara hiyo Wabunge walipata nafasi ya kutembelea eneo la Ubungo na kujionea wa mtambo wa kupunguza mgandamizo wa gesi kwa ajili ya kusambaza kwa wateja wa majumbani na viwandani. Pia walitembelea maeneo ya Mlimani City na kujionea zoezi la kuunganisha gesi kwa wateja wa majumbani na baadae kiwanda cha Coca-Cola maeneo ya Mikocheni ambao nao wanatarajiwa kuanza kutumia gesi baada ya kazi ya kuunganisha kukamilika.

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma inaangalia mambo matatu makubwa, kwanza gawio linalokwenda Serikalini, kupokea mtaji unaozidi na suala la mapato ghafi ambayo ni 15%, alieleza Mwenyekiti wa Kamati, Dk. Raphael Chegeni.

DAWASA YATUMIA WIKI YA MAJI DUNIANI KUTATUA KERO ZA MAJI KWA WANANCHI

Mtoa hudua katika wiki ya Maji Duniani toka Mamlaka ya majiSafi na MajiTaka (DAWASA) Tumaini Samwel akitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimishpo ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza leo Machi 16- 22, 2019 ambapo wananchi wanajitokeza kutoa matatizo yao pamoja na kupewa elimu juu ya matumizi sahihi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Watoa huduma katika wiki ya maji Clementina Mbogellah (Kushoto) na Neema Mbalamwezi wakitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika kuadhimisha wiki ya Maji Dunia iliyoanza Machi 16- 22, 2019.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa DAWASA, Evelasting Lyaro akitoa elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Burudani za amsha amsha wiki ya maji Duniani zikiendelea katika mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.
 Afisa Mwasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi akitoa elimu na vipeperushi wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka imeandaa utaratibu wa kusikiliza kero za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza jijini Dar es Salaam. DAWASA wameandaa dawati maalumu pamoja na wataalam ambao watatatua kero za wateja wa Maji kuanzia Machi 16- 22, 2019. Lengo ni kuwezesha wananchi kupata majibu ya kina ya changamoto mbali mbali zinazohusu huduma za majisafi na majitaka. Kauli mbiu: 'Hakuna atakayeachwa: Kuongeza kazi ya upatinaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi,"

ILIVYOKUWA UZINDUZI WA JUKWAA LA SITETEREKI JIJINI MWANZA.


VIDEO:- UTAMBULISHO WA JUKWAA LA VIJANA 'SITETEREKI' 
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Emily Kasagara (wa kwanza kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wakizindua jukwaa la mawasiliano ya afya liitwalo Sitetereki. Uzinduzi wa jukwaa hili lililo chini ya mradi wa USAid Tulonge Afya pamoja na Wizara ya Afya ulifanyika Machi 07, 2019 Jijini Mwanza kwa kujumuisha mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Dkt. Tumain Haonga alisema jukwaa la Sitetereki linawalenga zaidi vijana kuanzia miaka 15 hadi 24 katika kutekeleza afua mbalimbali za afya ili kupambana na vifo vitokanavyo na uzazi.

Afua hizo zitasaidia kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000 kwa mwaka hadi kufikia vifo 292 ifikapo mwaka 2020.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Emily Kasagara akisisitiza jambo baada ya uzinduzi wa jukwaa la Sitetereki kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa uliofanyika Jijini Mwanza.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi/ wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Mgeni rami, viongozi mbalimbali na wanahabari Jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi/ wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Kumbukumbu na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi/ wadau kutoka taasisi mbalimbali.
Kumbukumbu kupitia zuria jekundu la Sitetereki pia zilikuwepo.
Washiriki wa warsha ya uzinduzi wa jukwaa la Sitetereki kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Washiriki wa warsha hiyo.
 Waganga wakuu wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoka mikoa ya Mara, Kagera, Geita, Mwanza na Kigoma wakiwa katika meza kuu ya washiriki wa warsha ya uzinduzi wa jukwaa la Sitetereki.

 Mabalozi wa jukwaa la Sitetereki.
Washiriki wa warsha ya uzinduzi wa jukwaa la Sitetereki kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Baada ya uzinduzi huo, wadau walijadiliana namna ya kutekeleza afua mbalimbali katika kupambana na changamoto za uzazi na baada ya majadiliano, ukafuatia wasaa wa maakuli.
Baada ya uzinduzi huo, wadau walijadiliana namna ya kutekeleza afua mbalimbali katika kupambana na changamoto za uzazi na baada ya majadiliano, ukafuatia wasaa wa maakuli.

BREAKING NEWS: WENYEVITI 7 CHADEMA WATIMKIA CCM.


Wenyeviti Saba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  ( CHADEMA )
Wilayani Arumeru mkoani Arusha wamejiunga na Chama cha Mapinduzi CCM mapema jana katika ziara ya kikazi ya Mkuu wa wilaya hiyo Ndugu Jerry Cornel Muro katika Kata ya Maji ya Chai , Wenyeviti wameamua kujiuzulu baada ya hapo juzi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Ndugu. Joshua Nassary kuvuliwa ubunge na Spika wa Bunge la Tanzania baada ya kutokuhudhuria vikao vitatu vya bunge mfululizo 


Dc Muro akiwa ameambatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Meru Mwalimu Kanuthi wamewapokea wenyeviti hao walioleza kuwa wameamua kujiunga na CCM ili kumuuunga mkono Rais John Pombe Magufuli Kwa utendaji Kazi wake Sambamba na kumpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo kwa kazi anazozifanya na namna anavyotatua migogoro ya wananchi  

Mwenyeviti waliopokelewa ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ngurdoto Ndugu Mosses Ayo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Maji ya Chai Ndugu Mase David Mbise pamoja na hapo amewapokea wenyeviti wa vitongoji vitano ambavyo ni Ndugu Perfect Philemon Mwenyekiti wa kitongoji cha Bondeni,Laurant Kessy Kitongoji cha Mburueshi, Elisante Akyoo Kitongoji cha KCenter Mwenyekiti wa kijiji cha Seneto Ndugu Christopher Mbise  pamoja na Ndugu Amani Kitali Mwenyekiti kitongoji cha Kimandafu

WAKUU WA IDARA ZA ARDHI WATAKAOKALIA HATI ZA ARDHI OFISINI SASA KUKIONA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mji wa Mtukula wilayani Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Mtukula wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kyaka wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya majalada ya ardhi aliyoyakuta katika ofisi ya halmashauri ya Misenyi mkoa wa Kagera wakati akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis Mwila na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Elia Kamyanda na kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Ardhi Misenyi Emanuel Samson.

Na Allawi Kaboyo, MISENYI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema kuanzia sasa Mkuu wa Idara ya Ardhi atakayekutwa amekaa na hati ya ardhi kwa muda mrefu   bila kuipeleka ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda kwa ajili ya kukamilisha taratibu za utolewaji hati hiyo basi Mkuu huyo ataondolewa katika nafasi yake.
Dkt Mabula alisema hayo jana tarehe 15 Machi 2019 alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi.
Kauli hiyo ya Dkt Mabula inafuatia kukuta baadhi ya hati katika halmashauri ya wilaya ya Misenyi zikiwa kwenye masijala ya ardhi tangu mwaka 2017 bila kupelekwa ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.
Alisema, baadhi ya halmashauri alizozitembelea wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia sekta ya ardhi amebaini wakuu wengi wa idara ya ardhi wakiwa na hati kwenye ofisi zao kwa muda mrefu bila kufanya jitihada zozote za kuhakikisha hati hizo zinaenda ofisi ya Kamishna kwa ajili ya kukamilishwa ili wahusika wapatiwe hati.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, ucheleweshaji utoaji hati miliki za viwanja na mashamba siyo tu unawakera wananchi bali unaikosesha serikali mapato ya kodi ya ardhi kwa kuwa wananchi wanakuwa hawajamilikishwa ardhi kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Mabula ametoa onyo kali kwa Mkuu wa idara ya ardhi halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kwa kukaa na hati kwa zaidi ya miaka miwili kwenye ofisi yake bila kuwasilisha  hati hizo ofisi ya Kamishna Msaidizi Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukamilishwa na hatimaye kukabidhiwa kwa wahusika  kwa haraka na wakati.
Katika hatua nyingine Dkt Mabula amewataka wananchi wa miji ya Kyaka na Mtukula katika wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera kuchangamkia zoezi la urasimishaji makazi holela ambalo limeonekana kusuasua katika miji hiyo.
Akizungumza na wakazi wa Kyaka na Mtukula kwa nyakati tofauti Dkt Mabula alisema kuwa, haridhishwi kabisa na namna kasi ya urasimishaji inavyoendelea katika miji hiyo ambapo takwimu zinaonesha wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo ni ndogo ukilinganisha na wakazi wa miji hiyo.
Dkt Mabula ametolea mfano wa Mji wa Mtukula katika kitongoji cha Katede kuwa, pamoja na eneo hilo kuwa na Kaya 842 zenye wakazi zaidi ya 3000 lakini ni watu 13 tu waliolipia fedha za kurasimishiwa maeneo yao na watu hao wamechangia jumla ya shilingi milioni moja na laki nane.
Aidha, Naibu Waziri Mabula amewataka wananchi wa miji ya Kyaka na Mtukula kutofanya maendelezo katika eneo lolote ambalo hawajajua mipango yake ili kuepuka kubomolewa na kupoteza haki zao kwa kujenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa ambapo ameitaka halmashauri ya wilaya ya Misenyi kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kuwa na miji iliyopangika.

Friday, March 15, 2019

SAKATA LA MAJI NA KUHARA ARUSHA MWENYEKITI APC AZUNGUMZA HAYA.


Jana Waandishi wa Habari Arusha waliandamana hadi Makao Makuu ya Polisi kwa kile walichokidai kuachiliwa kwa mwandishi Basil Elias anayeshikiliwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kusambaza taarifa za ugonjwa wa kuhara kwa wakazi wa Arusha kunakodaiwa kutokana na matumizi ya maji

Mwandishi huyo alinashikiliwa na jeshi la polisi tangu majira ya saa 18:00 jioni ya Jumatano, chanzo Cha kukamatwa kwake Bado hakija fahamika.

Akafikishwa kituo kikuu cha Polisi na kutakiwa aandike maelezo kutokana na kosa alilo kamatiwa(Bado hakija wekwa wazi) ambapo kwa mujibu wa taarifa zisizo Rasmi ni agizo kutoka juu,kufuatia taharuki ya baadhi ya Maeneo jijini Arusha kukubwa na ugonjwa wa homa ya matumbo (Kuhara).

Japo taarifa hizo zilikanushwa na mamlaka ya maji Safi na usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA).

Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu amezungungumza nasi kuhusu sakata hilo.....

RC MONGELA ARIDHISHWA NA MAANDALIZI KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAWASILIANO

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. John Mongela, imefanya ziara rasmi katika ukumbi wa BOT kukagua maandalizi ya kikao kazi cha Maofisa Mawasilino Serikali kinachotarajiwa kufungulia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa, Jijini humo.
Akitoa tathmini yake mara baada ya ukaguzi wa ukumbi wa mkutano huo, Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na mandalizi yanayoratibiwa kwa pamoja na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Uongozi wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.
 “Mnakwenda vizuri, naona kila kitu kipo vizuri na kwa maandalizi haya ni imani yangu kuwa mkutano huu utaenda vizuri na msisite kutufahamisha endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote”.
Mapokezi ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, yaliongozwa na Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo ambaye pia ndiye msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abasi na viongozi wa chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini TAGCO.
Kikao hicho ni cha siku tano kinachotarajiwa kuanza siku ya Jumatatu, Machi 18 hadi Ijumaa 22, mwaka huu kinachotarajiwa kuwakutanisha zaidi ya Maofisa Mawasiliano 300 kutoka Wizara, Mashirika ya Umma, Taasisi za Serikali, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa.

Thursday, March 14, 2019

NEC WATHIBITISHA JOSHUA NASSARI (CHADEMA) KUVULIWA UBUNGE.


Tume ya Uchaguzi (NEC) imethibitisha kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kuvuliwa ubunge kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

DC KASESELA : MARUFUKU WANAUME KUWAKATAZA WANAWAKE KUMILIKI ARDHI

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali wakati wa maazimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyikia katika kata ya ulanda mkoani Iringa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi mbalimbali akiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA) ambao ndio wamesaidia kutoa hati miliki kwa wanawake na kupunguza migogoro wilaya ya Iringa
Baadhi ya wadau wakiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA)
 Wadu wakiwa kwenye banda la mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA)

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WANAWAKE mkoani Iringa wametakiwa kuanza kumiliki ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo na badala yake waachane na tamaduni kandamizi za kuwaachia wanaume; katika umiliki wa mali.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela katika kilele cha maadhimisho ya wanawake yaliyofanyika katika kijiji cha ibangamoyo kata ya ulanda wilaya ya Iringa alisema kuwa wanawake waaze kumiliki ardhi ili kujiinua kiuchumi kwa kuwa wanawake ndio walezi wa familia tofauti na wanaume wanaokuwa na makazi tofauti tofauti.

Kasesela aliwataka wanaume kuwapa haki wanawake kumiliki ardhi kwa kuwa wanahaki hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi hivyo mwanaume atakayemkataza mwanamke kumiliki ardhi atachukuliwa hatua za kisheria.

“Nasema nileteeni wanaume wote wanaowazuia wanawake kumiliki ardhi tutamtafutia sehemu ya kuishi kwa kuwa atakuwa anakiuka katiba ya nchi yetu hivyo ni lazima sheria ifuate mkondo wake” alisema

Akitembelea banda la mradi wa urasilmishaji ardhi vijijini (LTA), Kasesela alisema kuwa mradi huo umekuwa mkombozi kwa wanawake kumiliki ardhi kutokana na kutoa elimu kwa wanaume na kufanikisha wanawake kupatiwa hati miliki za kimila ambazo ndio limekuwa suluhisho la migogoro ya ardhi vijijini.

Aidha Mtaalam wa mawasiliano na uenezi wa mradi wa urasimishaji ardhi vijiji (LTA), Jackline Mhegi alisema kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasisitiza kuwa binadamu wote ni sawa na huzaliwa  huru hivyo basi wanatakiwa kupata ulinzi sawa na sheria za nchi ikiwepo kumiliki ardhi.

“Kwa mujibu wa ibara ya 24(I) inasema kila mtu anahaki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi kwa mali yake aliyokuwanayo kwa mujibu wa sheria,hivyo mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi kama mojawapo ya mali na kupata ulinzi wa mali kulingana na katiba ya nchi” alisema Mhegi

Mhegi alisema, sera ya taifa ya ardhi ya mwaka 1995 inaeleza kuwa “ni haki ya kila mwanamke kupata,kumiliki,kutumia na kuuza au kugawa ardhi  kwa kuwa hata mwanaume ana haki hiyo” Sheria ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999,Kwa mujibu wa kifungu cha 3 (2) cha Sheria ya ardhi Na.5 ya Vijiji ya mwaka 1999 inasema “Haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na kuuza au kuigawa ardhi ifahamike kuwa ni sawa na haki ya mwanamume yeyote kwa viwango vilevile na masharti yaleyale”

“Sheria hizi zimeondoa ubaguzi dhidi ya mwanamke. Mwanamke anaehitaji ardhi atafuata taratibu zinazohusika na hapaswi kunyimwa ardhi kwa sababu tu yeye ni mwanamke, Sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2002, Sheria ya marekebisho ya utatuzi wa migogoro namba 2 ya mwaka 2004, Sheria ya ndoa ya mwaka 1971”alisema Mhegi

Mhegi alimalizia kwa kusema, Wanawake ni watumiaji wakuu wa ardhi hivyo vyombo vinavyohusika na masuala ya usimamizi na utawala wa ardhi vihakikishe kuwa wanawake na wanaume wanashirikishwa ipasavyo katika masuala yahusuyo ardhi ili kuleta usawa wa kijinsia katika usimamizi na umiliki wa ardhi utakao changia maendeleo endelevu kutoka na rasilimali ardhi kiuzalishaji, Hivyo wanawake wahakikishe wanatumia nafasi walizonanzo kwa kushiriki na kutoa mawazo yao kwa lengo la kuboresha maslahi ya familia zao na taifa kwa ujumla.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Stella Mosha, alisema ni wakati sasa kwa wanawake kutambua ya kwamba wana haki ya kumilki ardhi sawa kama wanavyomiliki wanaume kwa njia mbalimbali zikiwemo wao binafsi, wao Pamoja na waume au ndugu zao.

“Pia jamii inakumbushwa kuachana na mila na desturi kandamizi katika zinazo wazuia wanawake kuto miliki ardhi kwa sababu wakati umebadilika wanawake na wanaume wanatakiwa kushirikiana ili kuweza kuinua uchumi wa familia na baadae taifa kwa ujumla” alisema mosha

Mosha aliesma,Mradi uliweza kutoa elimu ya juu ya haki ya wanawake kupitia mikutano ya hadhara kwa kila kijiji kwa wanawake pekee na baadae kuwaunganisha na wanaume ili kuwa na majadiliano ya pamoja.

“Mradi ulitoa mafunzo juu ya Sera na Sheria za ardhi zinazoelezea haki ya wanawake kumiliki rasilimali ardhi” alisema mosha

Mosha alimalizia kwa kusema,mradi uliwajengea uwezo wanawake kuingia katika vyombo mbalimbali vinavyosimamia masuala ya usimamizi wa ardhi ngazi ya kijiji, kama vile: kamati ya Mpango bora wa Matumizi ya ardhi, Kamati ya Uhakiki wa maslahi ya ardhi, Baraza la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya kijiji.

IJANA WA UMRI CHINI YA MIAKA 25 HATARINI KUAMBUKIZWA VVUxMWANZA

 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emil Kasigara akizindua rasmi Jukwaa la “SITETELEKI” litakalozungumzi maswala ya Afya hususani Vijana chini ya mika 25 ili waweze kujitambua na kuwa na tabia chanya. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.

 Mtaalamu wa maswala ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Gerald Kihwele akiwakilisha maada ya “SITETELEKI” kwa wadau wa Afya(hawapo pichani) litakalozungumzia maswala ya Afya kwa Vijana chini ya miaka 25 mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa hilouliofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
 Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza
 Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Mwanza
Wadau wa Afya kutoka sekta tofauti wakisiliza maada mara baada ya uzinduzi wa Jukwaa la “SITETELEKI” litakazungumzia maswala ya Afya haswa kwa Vijana chini ya miaka 25 uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini MwanzaUWEZEKANO wa Vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kushindwa kutimiza ndoto zao za maisha ni mkubwa endapo hawatapata elimu sahihi ya afya ya uzazi na maambukizi ya Ukimwi (VVU) itakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi kwa mstakabali wa maisha yao.

Kundi hilo liko kwenye hatari hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto za ongezeko la maambukizi mapya ya VVU na mimba za utotoni kwa sababu ya uelewa mdogo (elimu) na upungufu wa huduma rafiki za afya ya uzazi na VVU kwa vijana.

Akizindua Jukwaa la Vijana ( SITETEREKI  Najifunza Kila Hatua ) kaimu Katibu Tawala wa msaidizi Mkoa wa Mwanza Emily Kasigara alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya wakishirikiana na Mradi wa USAIDI Tulonge Afya i 360 imeanzisha jukwaa hilo  la vijana ili kuwajengea uwezo katika masuala ya afya ya uzazi na Ukimwi, wajitambue na kubadilisha tabia zao.

Alisema serikali, jamii na wadau wana kazi kubwa ya kuwaelimisha vijana kujitambua , wakijitambua na kujali afya zao kutakuwa na matokeo chanya kwao na watafanya maamuzi sahihi, hawatachezea afya zao na kuwahimiza waende vituo vya huduma za uzazi na kupima afya. “Jukwaa la SITETEREKI Najifunza kila hatua  litakuwa kimbilio la vijana kufikia maisha wanayoyahitaji kwani ni eneo muhimu ambalo ni nguvu kazi na taifa la kesho, watapata mahali pa kutoa dukuduku zao na watajengewa uwezo.

Lengo la serikali wafikiwe ili wasijiingize kwenye changamoto 
zinazowaharibu na kuhatarisha maisha yao ya baadaye,”alisema Kasigara.

Alisema serikali imeanzisha jukwaa hilo litakalowawezesha kuwa na maisha bora baada ya kujengewa uwezo  na kujitambuawatatimiza azma ya serikali ya Tanzania ya uchumi wa kati wa viwanda kwani familia ikiwa duni kiafya haitakuwa na mchangokwenye uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Afya ya Uzazi Wizara ya Afya  Dk. Gerald Kihwele alisema licha vijana kuwa tegemeo kiuchumi wanakabiliwa na changamoto nyingi ambapo vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24 sawa na asilimia 40 wana maambukizi ya VVU, kati ya hao asilimia 70 ni wasichana na ndio wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi mapya.

Alisema ni asilimia  41 tu ya vijana wa kiume wanaozingatia njia za afya ya uzazi na wanatumia kinga kwa usahihi wakati wakujamiiana huku wasichana wanaopata huduma hizo wakiwa ni asilimia 37 na ndio wenye changamoto kubwa hivyo wakijengewa uwezo watajitambua na kusimama kwenye misimimo thabiti.

  Dk. Kihwele alieleza kuwa serikali inafanya jitihada kubwa za kuweka mazingira bora ya huduma ya afya ya uzazi kwa vijana na kuwafanya wawe sehemu ya mipango yake, hivyo lazima kuwe na huduma za viwango vya  kuwavutia na kuchochea fikrazao waende kwenye maeneo ya kutolea huduma.“Upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana badosi za kuridhisha ni asilimia 30 hivyo hatuwezi kuwavutia vijana waende kupata huduma hizo ambapo  serikali zifikie asilimia 80 na ipo haja mitizamo ya watoa huduma ivutie na kuhamasisha vijana wazichangamkie,”alisema Dk. Kihwele. 

Naye Mshauri Mwandamizi wa SBCC Shahada Kinyanga alisema vijana hupewa  taarifa zisizo sahihi na wanakosa motisha ya kufikia malengo yao kimaisha  hivyo jukwaa la SITETEREKI  litajibu changamoto zao na kuibua hisia za kufikia matarajio na mahitaji yao,litawaongezea ukweli kabla yakujiingiza kwenye uhusiano  na kufanya uamuzi sahihi.“Tunalenga maeneo yatakayonyesha mafaikio makubwa  katika kuboresha afya za vijana wa Kitanzania wa umri wa miaka 15 hadi 24hasa huduma za afya ya uzazi kabla ya ujauzito,upimaji wa VVU na tohara ya hiari kwa wanaume.

Baadaye tutahusisha vipaumbele vya jamii na kimaisha kwani takwimu zinaonyesha VVU na mimba za utotoni husababisha afya duni na vifo kwa vijana,” Kinyanga.Alisema jukwaa hilo ambalo lipo  chini ya Wizara ya Afya,ndani ya mradi wa  miaka mitano wa USAID Tulonge Afya wanalenga kuwafikia vijana 22,800 kwa mwezi kwa kuwatumia wahamasishaji 520  katika Kanda ya Ziwa  na Magharibi na kati ya wahamasishaji hao 270 ni wasichana. 

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI MWAKYEMBE MKOANI SINGIDA KUJIONEA MAENEO YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia eneo lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani  eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma moja ya kaburi la wakoloni wa Kijerumani  eneo la Kilima Tindewakati  akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia handaki lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani  eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa viongozi na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida wakati alipotembelea pango lilotumiwa na mashujaa wakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.


Pix 05: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia handaki lilotumiwa na wakoloni wa Kijerumani  eneo la Kilima Tindewakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Pix 06: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa viongozi na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakati alipotembelea njia iliyotumiwa na wakoloni kusafirisha watumwa eneo la Rungwa wakati wa ukoloni akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Singida kwa ajili ya kutembelea maeneo ya historia ya ukombozi wa Bara la Afrika ikiwa ni mikakati ya kuhamasisha viongozi na wananchi kutunza, kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo kwa matumizi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Pix 07: Sehemu ya njia njia iliyotumiwa na wakoloni kusafirisha watumwa eneo la Rungwa Mkoani Singida wakati wa ukoloni.
Picha na WHUSM -Singida