Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika
lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika
lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la
Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu
tatu mia moja ( 95,503,100)
Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la
Rural Development Organization (RDO) Tanzania na
umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu
tatu mia moja ( 95,503,100)
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua
mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea
maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo
ulifadhiliwa na shirika
lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania
ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza amelipongeza shirika lisilo la kiserikali la Rural Development
Organization (RDO) Tanzania kwa kufanikisha kupatikana kwa maji katika baadhi
ya vijiji vya wilaya ya Kilolo na Mufindi ambayo itakuwa njia moja wapo ya
kuchochea maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kuzindua
mradi wa maji katika kijiji cha Nandala’ Masenza alisema kuwa amefurahishwa na
mfumo ambao unatumiwa na shirika hilo kwa kutoa huduma ya maji kwa kushirikiana
na wananchi wa maeneo husika.
“Mradi wowote ule ukiwa na
ushirikiano mkubwa na wananchi mara nyingi wananchi wanautunza mradi huo kwa
kuudhamini na kuulinda,hivyo nawapongeza RDO kwa kufanya maamuzi sahihi ya
kubuni mradi huo pamoja na wananchi” alisema Masenza
Masenza alisema kuwa mradi huo
wa maji utatoa huduma kwa wananchi wengi na taasisi binafsi nyingi hivyo
wananchi wanatakiwa kuutunza na kuudhamini ili udumu kwa muda mrefu na kuondoa
tatizo la maji ambalo limekuwa kero ya muda mrefu.
Nimesikia kwenye risala yenu
kuwa mradi huu utahudumia kata zifuatazo Ifwagi,Mdabulo,Ihanu,Luhunga,Mtitu na
Kising’a na vijiji vitakavyopata huduma hiyo ni
Igonongo,Ludilo,Kidete,Ikanga,Nandala,Ibwanzi,Isipii,Mkonge,Lulanzi,Luhindo,Barabara
mbili na Isele hivyo ukiangala utagundua kuwa mradi huu ni mkubwa na upaswi
kupuuzwa kwa maendeleo kwa wananchi wa maeneo ambayo mradi huo umepita.
“Jamani wananchi ambao mmepata
bahati ya kupitiwa na mradio huu mkubwa wa maji mnapaswa kuulinda na kuudhamini
kwa kuwa ni mmoja ya mradi mkubwa ambao unapunguza adha ya upatikanaji wa maji
ambayo hapo awali ilikuwa kero kubwa” alisema Masenza
Kwa upande mkurugenzi mtendaji
wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO)
Tanzania Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umegharibukiasi cha shilingi
milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100) ambao ndani
yake kuna pesa zilizochangwa na wananchi kwa ajili ya kusaidia kupata huduma ya
maji.
“Sisi kama RDO ambao ndio
wafadhili namba moja wa mradio huu wa maji tumechangia kiasi cha shilingi
milioni themenini na sita,laki nane ishirini na moja elfu (86,821,000) na
wananchi walichanga kiasi cha shilingi milioni nane,laki sita themenini na
mbili na mia moja (8,682,100)” alisema Filipatali
Filipatali alisema kuwa mradi huo wa maji utazaliza ujazo wa lita 776 kwa vijiji vyote ambazo vinatumia huduma hiyo
ya maji na pia wananchi watakao pata huduma hiyo ni 10,874 kwa vijiji vyote
vilivyopitiwa na mradi huo na jumla ya taasisi 18 nazo zitanufaika na huduma
hiyo.
“Mkuu wa mkoa sasa ukiangalia
kwa ujumla ndio utagundua kuwa ni mradi ambao utakuwa unakomba wananchi wengi
waliokuwa wanapata tabu juu ya kupata maji hivyo naomba pia nisisitize wananchi
kuutunza na kuchangia kwa malipo kidogo kwa ajili ya ukarabati wa mashine na
mitambo mingie inayosukuma maji hayo ili isihalibike” alisema Filipatali
Filipatali alisema kuwa mradi
huo unakabiliwa na changamoto zifuatazo baadhi ya watumiaji maji kutochangia,
viongozi kutotimiza majukumu yao kama kutohudhuria mikutano ya mapato na
matumizi,watumiaji maji kutotilia mkazo elimu wanayopewa na wataalamu wa
maji,siasa kuingia mfumo mzima wa mradi huu na baadhi ya serikali za vijiji
kuchukulia mapato ya miradi ya maji kama sehemu ya mapato ya serikali kitu ambacho sio kweli mfano kjiji cha Lidilo
“Hizi changamoto zimekuwa kero
sana kwenye miradi ambayo imekuwa inatekelezwa kwenye maeneo husika hivyo
niwaombe viongozi wa kiasa wawe wa kwanza kutoa elimu juu ya miradi ambayo
inafaida na kutatua changamoto za wananchi kwenye maeneo yao” Filipatali