ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 8, 2017

MAJAMBAZI SITA WANAODAIWA NI MTANDAO WA KIBITI WAPATIKANA JIJINI MWANZA WAKIWA WAMEJIFICHA NDANI YA NYUMBA YA UDONGO.

NA ZEPHANIA MANDIA, GSENGO BLOG. TAREHE 8.7.2017

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeanza kuvunja mtandao wa majambazi wanaofanya matukio ya uhalifu nchini, yakiwemo  mauaji yanayoendelea wilayani Kibiti mkoani Pwani, baada ya kuua majambazi sita kati ya wanane kwenye majibizano makali ya risasi na majambazi hao.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, majambazi wawili kati ya hao walifanikiwa kukimbia, hukuJeshi hilo likifanikiwa kukamata silaha za kivita, mavazi ya kijeshi, bunduki za kienyeji, magazine, risasi pamoja na nyenzo mbalimbali za kufanyia uhalifu.


Katika majibizano hayo ya alfajiri yaliyodumu takribani saa mbili, katika eneo la Fumagila kata ya Kishili wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, majambazi hao walikuwa wamejificha ndani ya nyumba ndongo ya udongo, wakipanga mikakati ya kufanya uhalifu.


Wakiwa kwenye mjadala huo ghafla jeshi hilo liliizingira nyumba hiyo, na walipogundua kuwa wapo chini ya ulinzi, kila jambazi akabeba silaha nzito kama njia ya kujihami, ingawa jitihada zao hazikuzaa matunda kwa kuwa walishawaiwa, ingawa majambazi wawili walikimbia.


Majambazi wawili kati ya sita waliouwawa waligundulika kuwa ni wanachama wa mtandao wa uhalifu wilayani Kibiti mkoani Pwani, akiwemo mkazi wa kata ya Kishili ambaye hivi karibuni, aliwakimbia askari wa Jeshi hilo akiwa nyumbani na nyumba yake kuchomwa moto na Wananchi wenye hasira.


Eneo la Fumagila wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, ambalo limezungukwa na mapango ya mawe limekuwa likitumika kama maficho ya majambazi, ambapo miezi kadhaa iliyopita Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuuwa majambazi wengine kwa majibizano ya risasi wakiwa Pangoni.

MICHEZO MBALIMBALI YAENDELEA GYMKHANA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA KLABU HIYO.


 Kapteni wa Mchezo wa Snooker wa Klabu ya Gymkhana, Shaizad Bhanji akishiriki katika mashindano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Washiriki wa mchezo wa Tennis Inga Njau/Jitendra Singh/ Kunal Vadgama/Sanjay Chokshi wakishiriki katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo inayoendelea katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mchezo wa Tennis Inga Njau/Jitendra Singh/ Kunal Vadgama/Sanjay Chokshi wakishiriki katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo inayoendelea katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mchezo wa Tennis Inga Njau/Jitendra Singh/ Kunal Vadgama/Sanjay Chokshi wakishiriki katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo inayoendelea katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam.
 Washiriki wa mchezo wa Tennis Inga Njau/Jitendra Singh/ Kunal Vadgama/Sanjay Chokshi wakishiriki katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo inayoendelea katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Klabu ya Gymkhana, Walter Chipeta (kulia) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa klabu ya Gymkhana  Ali Mmandi (mwenye jezi ya kijani) baada ya timu yake kuibuka kidedea katika michuano ya kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya klabu hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jana jijini Dar es salaam.

MWENGINE AUWAWA KIBITI USIKU WA KUMKIA LEO.Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yake saa 6 usiku, kisha kufanya mauaji hayo.

Alisema kabla ya kufanya mauaji hayo walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha kumpiga risasi mbili mume wake.

Mganga wa Kituo cha Afya Kibiti Dk Sadock Bandiko amesema Ndikaye amepigwa risasi mbili mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAFURIKA KATIKA BANDA LA UBER NA KUJIUNGA NA HUDUMA

Wafanyakazi kampuni ya Uber Godfrey Mabula na Ibrahimu Kunguya wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika katika banda kujua jinsi Program ya Uber inayorahisisha usafiri  wa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu pia wateja wote waliopakua Program hiyo walipata punguzo la kiasi cha 8200Tsh  kwa safari yao ya kwanza.Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Mfanyakazi wa Uber Ibrahim Kunguya akimsaidia mteja jinsi ya kutumia Program ya uber ambayo imekuwa msaada  kwa wakazi wa jiji la Dar kusaidia kurahisisha usafiri kwa njia ya kiteknolojia ,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar Es Salaam.

Balozi wa Uber akimsaidia mteja jinsi ya kupakua na kutumia program ya Uber katika banda lao katiika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar es salaam.Wateja waliofika katika banda la uber wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Uber Jinsi ya kupakua na kutumia Progamu ya Uber ambayo inarahisisha usafiri na kwa gharama nafuu,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakipata maelekezo jini ya kujiunga na programu ya Uber katika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar Es salaam.

Bango linaloonyesha jinis ya kuipata program ya  Uber katika APP store na Google play na kutumia kutumia usafiri kwa bei nafuu na kwa kisasa zaidi .Balozi wa Uber akitoa maelekezo kwa  mteja aliyefika katika banda lao ambapo pia wateja walijipatia punguzo la kiasi cha 8200 Tsh mara baada ya kupakua na kutumia program ya uber katika kuagiza usafiri kwa bei nafuu na kwa teknolojia ya kisasa mapema jana katika maonesho ya saba saba.

Huduma zikiendelea kutolewa katika banda la Uber mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

MAONESHO YA SABASABA 2017;FINCA MICROFINANCE BANK WANG'ARA KATIKA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUHUDUMIA WATEJA

Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank  Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.


Wakala wa Finca Express Grace Kimaro akiwa anamsajili mteja mpya wa Finca kwa kutumia Tablet katika banda lao mapema jana katika maonesho ya sabasaba.Jijini Dar es salaam.

Mfanyakazi wa FINCA Microfinance Bank Beatrice kimaro akimpiga picha katika kumsajili mteja mpya wa FINCA kwa kutumia mfumo wa kisasa ambao hutumia Tablet mapema jana katika maonesho ya sabasaba ,Jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank  Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.


Wafanyakazi wa Finca Microfinance Bank wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda la FINCA kufungua akaunti Mapema jana katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wateja waliofika katika banda la Finca Microfinance Bank wakipata maelezo jinsi ya kufungua akaunti na huduma za mikop zinazotolewa na Benki,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

BALOZI DK.PINDI CHANA NA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI WA LAPF WATEMMBELEA BANDA LA LAPF MAONYESHO YA SABASABA

Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akisalimiana na  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam,mapema jana.

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya LAPF Prof. Faustine  Bee (katikati aliyeshika tuzo ya ushindi wa Lapf )akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa LAPF Bw.James Mlowe   pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati alipotembelea  banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF katika viwanja vya Sabasaba mapema jana .


Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa mtumishi wa LAPF Simboninsia Ndosi  alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe mapema jana
Wanachama wapya wa LAPF wakielekezwa kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika viwanja vya sabasaba mapema jana.

Mtumishi wa LAPF  akimsajili  mmoja wa wanachama wa  LAPF alietembelea banda hilo.

Wateja wakiwa wanasubiri kupata kadi zao za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika maonesho ya sabasaba.
Maafisa wa LAPF wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye banda la LAPF na kujiunga na uanachama kwenye mfuko katika maonesho ya SabaSaba mapema jana.