ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 8, 2017

MAJAMBAZI SITA WANAODAIWA NI MTANDAO WA KIBITI WAPATIKANA JIJINI MWANZA WAKIWA WAMEJIFICHA NDANI YA NYUMBA YA UDONGO.

NA ZEPHANIA MANDIA, GSENGO BLOG. TAREHE 8.7.2017

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limeanza kuvunja mtandao wa majambazi wanaofanya matukio ya uhalifu nchini, yakiwemo  mauaji yanayoendelea wilayani Kibiti mkoani Pwani, baada ya kuua majambazi sita kati ya wanane kwenye majibizano makali ya risasi na majambazi hao.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, majambazi wawili kati ya hao walifanikiwa kukimbia, hukuJeshi hilo likifanikiwa kukamata silaha za kivita, mavazi ya kijeshi, bunduki za kienyeji, magazine, risasi pamoja na nyenzo mbalimbali za kufanyia uhalifu.


Katika majibizano hayo ya alfajiri yaliyodumu takribani saa mbili, katika eneo la Fumagila kata ya Kishili wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, majambazi hao walikuwa wamejificha ndani ya nyumba ndongo ya udongo, wakipanga mikakati ya kufanya uhalifu.


Wakiwa kwenye mjadala huo ghafla jeshi hilo liliizingira nyumba hiyo, na walipogundua kuwa wapo chini ya ulinzi, kila jambazi akabeba silaha nzito kama njia ya kujihami, ingawa jitihada zao hazikuzaa matunda kwa kuwa walishawaiwa, ingawa majambazi wawili walikimbia.


Majambazi wawili kati ya sita waliouwawa waligundulika kuwa ni wanachama wa mtandao wa uhalifu wilayani Kibiti mkoani Pwani, akiwemo mkazi wa kata ya Kishili ambaye hivi karibuni, aliwakimbia askari wa Jeshi hilo akiwa nyumbani na nyumba yake kuchomwa moto na Wananchi wenye hasira.


Eneo la Fumagila wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, ambalo limezungukwa na mapango ya mawe limekuwa likitumika kama maficho ya majambazi, ambapo miezi kadhaa iliyopita Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuuwa majambazi wengine kwa majibizano ya risasi wakiwa Pangoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.