ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 20, 2018

DIAMOND PLATNUMZ : RWANDA NI NYUMBANI KWETU PIA ( Exclusive Interview ) RTV



Naseeb Abdul Juma, popularly known by his stage name Diamond Platnumz, is a Tanzanian bongo flava recording artist and dancer from Tanzania.

MKURUGENZI WA MAJI MUSOMA ATUMBULIWA.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe , ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Musoma, Gantala Said (pichani kushoto) ambaye anachunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha kwenye Mradi wa Maji Bunda na akizivunja Bodi za Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira za Mikoa ya Arusha na Mara (Musoma) baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wao siyo mzuri.

Kamwele amefikia uamuzi huo leo baada kubaini kuwa kumekuwepo na uzembe wa utekelezaji wa miradi ya serikali ya maji kwa baadhi ya watendaji katika idara hizo.

“Kufuatia ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majliwa mkoani Mara, imebainika kuwa kumekuwepo na matatizo ya huyo Mkurugenzi Gantala ambaye Waziri Mkuu ameagiza Mkurugenzi huyu watendaji wengine wachunguzwe na TAKUKURU.

“Hivyo kuanzia leo Januari 20, 2017 ninatengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Mji wa Musoma, Gantala Said na nafasi yake itakaimiwa na Eng. Robert Petro Mponya wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUASA), ninamuagiza aisaidie Musoma ili waweze kufanya kazi inayotakiwa,” alisema Kamwele.

Friday, January 19, 2018

WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI KIRUMBA MWANZA WAWEKA MGOMO

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMAKI LA KIMATAIFA LA KIRUMBA MWALONI LILILOPO WILAYANI ILEMELA MKOANI MWANZA WAMEGOMA KUFANYA BIASHARA SOKONI HAPO KWA MADAI YA KUTOZWA USHURU WA NJE YA NCHI (ROYALITY EXPORT) PINDI WANAPOTAKA KUSAFIRISHA KWENDA  MIKOA ILIYOPO PEMBEZONI  MWA NCHI HUKU WAKIWA NA VIBALI VYA KUSAFIRISHA KWA MIKOA YA NDANI YA NCHI 

UGONJWA WA KIPINDUPINDU WAZIDI KUSHIKA KASI RUKWA.

Ugonjwa  wa kipindupindu ulioibuka mwezi Novemba mwaka jana katika tarafa ya Mtowisa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, umeendelea kushika kasi baada ya wagonjwa kuongezeka kutoka 170 wiki iliyopita na kufikia 207 katika kipindi cha siku tano.

Hayo yamebainika katika ziara ya mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Leonard Wangabo katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa wa kipindupindu na kubaini kuwa baadhi ya wavuvi walioondolewa katika kambi za uvuvi zilizofungwa wamekaidi na kurejea katika kambi hizo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na Diwani wa kata ya Nankanga wamewashauri wananchi kuacha kukaidi maelekezo ya serikali ili kutokomeza ugonjwa wa kipindu pindu

NEW ZEALAND: WAZIRI MKUU AFUNGUKA KUWA NA UJAUZITO


Waziri mkuu wa New Zealand mwenye umri wa miaka 37 Jacinda Ardern amefichua kwamba yeye ni mjamzito.

Bi Ardern alisema kwamba yeye na mpenzi wake Clarker Gayford walikuwa wakitarajia mwana wao mwezi Juni ambapo baadaye atachukua likizo ya wiki sita.

''Na tulidhani kwamba mwaka 2017 ni mwaka mkuu'', aliandika katika mtandao wake wa Instagram.

Bi Ardern mwenye umri wa miaka 37 alikuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo nchini New Zealand tangu 1856 akiungwa mkono wakati alipotangaza kuhusu hali yake mpya siku ya Ijumaa.

Chama cha leba cha Bi Ardern kilikuwa cha pili katika uchaguzi wa mwezi Septemba ambapo hakuna chama kilichofanikiwa kupata wingi wa kura.

Aliunda serikali kupitia usaidizi wa Winston Peters ambaye ni kiongozi wa chama kidogo cha New Zealand.

''Nitakapokuwa ugenini Bwana Peters atakuwa kaimu waziri mkuu, akifanya kazi na ofisi yangu mbali na kuwasiliana nami'', alisema bi Ardern katika taarifa ilioripotiwa na gazeti la New Zealand Herald siku ya Ijumaa.

''Nitawasiliana na kupatikana katika kipindi hicho cha wiki sita wakati nitakapohitajika''.

Bi Ardern alisema kuwa aligundua kwamba ni mjamzito siku sita kabla ya kujua kwamba atakuwa waziri mkuu , na lilikuwa swala la kushangaza.

''Mimi sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi mbili.Sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi huku nikihudumia mwanangu, kuna wanawake wengi ambao wamekuwa katika hali kama hii awali'', alisema.

''Bwana Gayford atakuwa baba ambaye atakuwa akisalia nyumbani'', aliongezea.

Mawaziri 2 wakuu wa zamani nchini humo walikuwa watu wa kwanza kutoa pongezi zao.

Thursday, January 18, 2018

POLE SINGIDA UNITED KWA KUMALIZA MCHEZO KABLA YA DAKIKA 90


Singida united iliingia na plan ambayo sio sahihi kwa Mchezo wa leo..huwezi kucheza na simba yenye viungo zaidi ya wa3 kati kati kisha uweke soft players na wachezaji waliotoka majeruhi..

Huwa nawasifu sana Azam kwa nidhamu bora sana ya ukabaji na kuwasumbua wachezaji wa simba kiasi cha kuwafanya wasicheze mpira unaotakiwa..........

Singida waliwaachia simba wacheze na waliamini wao pia wanaweza kucheza..Walisahau falsafa ya asili ya Simba na namna ya kucheza mpira...beki zao zimekatika sana leo na walishindwa kabisa kudhibiti mikiki ya simba.....

Singida lazima wawe wanaangalia approach nzuri ya kucheza game kubwa na hasa kwenye uwanja mkubwa na aina ya timu kubwa kama simba......

Ni kipigo "Heavy" lakini naamini kitawapa somo kubwa katika mechi zinazokuja na watafanya vizuri ikiwa watabadilika na watakuwa na approach nzuri dhidi ya game kubwa na timu kubwa kama Simba.

Hongeren Simba
Juma Ayo Mtalaam

POLE SINGIDA UNITED KWA KUMALIZA MCHEZO KABLA YA DAKIKA 90

MHE BITEKO AMUAGIZA KAMISHNA WA MADINI KANDA YA KUSINI KUANZISHA OFISI YA MADINI WILAYANI RUANGWA

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua mgodi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya maeneo ya uzalishaji madini ya dhababu kwenye kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Lindi

Kamishna msaidizi wa madini kanda ya kusini Ndg Mayigi Makorobela ameagizwa kuanzisha haraka ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo kupeleka wataalamu ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo ikiwemo elimu ya usalama kazini.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ametoa agizo hilo leo tarehe 18 Januari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

Alisema kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo ambapo alibaini kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali wa ofisi kwani wanalazimika kutumia zaidi ya kilomita 45 kuzifikia ofisi za madini zilizopo Wilayani Nachingwea.

Alisema kuwa Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa anawapenda wachimbaji wadogo nchini ambao hata hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alibainisha kukusudia kuwanufanisha watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo madini.

"Mhe Rais Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi kunufaika na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi iliporuhusu uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania badala yake madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine ambayo baadaye tunayapigia magoti kuyaomba msaada" Alikaririwa Mhe Biteko huku akipigiwa makofi na wananchi waliohudhuria katika mkutano huo

Mhe Biteko alisema kuwa lengo la kuanzisha ofisi ya madini katika Wilayani hiyo ya Ruangwa ni kuwarahisishia wachimbaji kuwa na jukumu moja la kuchimba na kuuza rasilimali wanazozipata kwani watakuwa sehemu ya kuchagiza maendeleo sambamba na kuinufaisha serikali kutokana na ulipaji kodi.

Aliwasihi wachimbaji hao kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwani tangu ameingia madarakani katika kipindi kifupi ameimarisha nidhamu mpya kwa kila mtanzania na usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameipongeza kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) ambayo ni kampuni ya wazawa kwa kufanya kazi kwa kufuata vyema sheria na taratibu za uchimbaji.

Alisema kuwa kampuni zingine zinapaswa kujifunza kwa kampuni hiyo ya GEMS kutokana kulipa kodi mbalimbali kwa uwazi na ushiriki wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya, Maji, sekta ya elimu sambamba na michezo.

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA NDEGE MWANZA.

 Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini Dar es Salaam.

Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.

Amesema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.

“Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia  na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema Mayongela.

Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka,  taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.

“Haijulikani mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama uwanjani hapo.

 “Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia katika njia ya kurukia ndege,” amesema.

Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA VIONGOZI KUJADILI MASUALA YA JESHI LA MAGEREZA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya Jeshi la Magereza baada ya kukutana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dk . Juma Malewa.Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira (kushoto) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa(kulia), wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo, Dk. Mwigulu Nchemba walipokutana kujadili masuala  ya jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu Projest Rwegasira, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa (kulia), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya jeshi hilo.Kikao hicho kimefanyika leo ofisi ya wizara,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wednesday, January 17, 2018

RAYVANY AFUNGUKA SIRI YA TUZO YAKE YOU TUBE


Kadri siku zinavyo songa ndivyo Rayvany kutoka WCB anavyozidi kutusua anga za kimataifa. 

Ukiachana na matokeo mazuri ya jisongi lake Makulusa kuendelea kufanya uzuri, sasa ni zamu ya video zake zinazopatikana kupitia channel yake ya YouTube kupata tuzo.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram ametupia picha yake akionesha tuzo aliyopewa. Jeh nini siri ya yote hayo tambaa na Natty E pamoja naye BabaJuti wa 'HIT ZONE'

MAHAKAMA YA UFARANSA YAWAACHIA HURU ASKARI WALIOWANAJISI WATOTO BANGUI.

Mahakama ya Ufaransa yawaachia huru askari waliowanajisi watoto Bangui
Mahakama moja nchini Ufaransa imetangaza kuhitimisha faili la tuhuma za askari wa nchi hiyo waliowanajisi watoto wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa madai ya kutokuwepo ushahidi wa kutosha.
Jumanne ya jana mahakama ya Ufaransa ilidai kwamba, hakuna nyaraka wala ushahidi wa kutosha kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili askari wake walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya mwamvuli wa kikosi cha Sangaris kwa kuhusika na kuwabaka na kuwadhalilisha kijinsia watoto wadogo wa taifa hilo.

Askari wa Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2015 askari kadhaa wa Ufaransa walituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo baada ya watoto kadhaa kutoa ushahidi kwamba walikumbwa na udhalilishaji wa askari hao. Kwa mujibu wa watoto hao, askari wa Ufaransa walikuwa wakiwarubuni watoto wadogo wa jinsia tofauti kwa kuwapa mkate au bisikuti na kisha kuwafanyia ukatili huo.


Watoto wadogo wa nchi hiyo hawako salama kutokana na askari wa Ufaransa.

Kufuatia hali hiyo raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliandamana wakitaka askari hao wachukuliwe hatua kwa kushitakiwa na mahakama za nchi hiyo, ingawa serikali ya Paris iliwarejesha askari hao na kuahidi kuwashitaki katika mahakama zake, kitendo ambacho kilitafsiriwa kama mchezo wa kisiasa. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko mwaka 2013 kufuatia uingiliaji wa madola ya Magharibi yakiongozwa na Ufaransa.

MAGUFULI USO KWA USO NA NDALICHAKO NA JAFO KUJADILI MICHANGO MASHULENI.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani S. Jafo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce L. Ndalichako Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 17, 2018. Mhe. Rais amepiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali za msingi na sekondari na amewaagiza mawaziri hao kusimamia hilo. Taarifa kamili inakuja.






Tuesday, January 16, 2018

ZANTEL YAZINDUA KAMPENI YA ‘JERO YAKO TU' KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary na kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapo ongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja na eni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El Barbary akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa na Zantel jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Zantel, Wane Ngambi (kushoto) na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) (kulia).

Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherif El-Barbary (kulia) na Mkuu wa Zantel, Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Baucha) (kushoto) kwa pamoja wakifungua pazia kuonyesha baadhi ya zawadi zitakazo shindaniwa kwenye Kampeni ya Zantel ya ‘JERO YAKO TU’ iliyozinduliwa jana mjini Zanzibar. Kampeni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapo ongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
Zanzibar. 
Kampuni ya Mawasiliano ya ZANTEL, leo imezindua kampeni yake kabambe inayoitwa 'JERO YAKO TU', promosheni ambayo imelenga kuwashukuru wateja kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
Kampeni hiyo ambayo imeanza rasmi siku ya leo, itadumu kwa muda wa miezi mitatu huku takribani washindi 235 wakitarajiwa kuibuka na zawadi kabambe kutoka Zantel.
Zawadi kubwa katika promosheni hii itakuwa ni pamoja na magari matatu aina ya Suzuki Carry kwa washindi watatu, ambazo zitakabidhiwa mwishoni mwa kampeni hii mwezi Machi.
Zawadi za kila wiki ni pamoja na pikipiki 1, na baiskeli 4 huku zawadi za kila siku zikiwa ni simu aina ya smartphone 4G pamoja na fedha taslimu kiasi cha Sh. 50,000/= kila siku.
Kwa mujibu wa Zantel, Promosheni ya ‘JERO YAKO TU' ni mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja na kuthamini uvumilivu wao wakati ambapo mtandao huo ulikuwa kwenye hatua za maboresho na hatimaye kuzindua mfumo wa 4G katika mikoa 22 nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mjini Zanzibar, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Sherrif El- Barbary  alisema, "Sisi Zantel tunathamini mchango wa wateja wetu ambao wametuonyesha kwa miaka mingi, na wanastahili kupongezwa kwa kuendelea kuwa nasi hususani kutufanya kuendeliea kuwa mtandao wa simu unaoongoza Zanzibar pamoja na kuongoza kwenye utoaji wa huduma ya data nchini Tanzania.
El Barbary Alisema, Ili kushiriki kwenye droo hiyo, cha kwanza anayeshiriki atapaswa kuwa na laini ya Zantel na kuweka salio la kuanzia shillingi 500 na moja kwa moja atakuwa ameingia kwenye droo. Aliongeza kuwa ili kujiwekea nafasi ya kushinda zawadi nono, mtumiaji atapaswa kuweka vocha mara nyingi kadri anavyoweza.
Aliongeza kuwa, "Ushindani kwenye soko umekuwa mkubwa na Zantel haina mpango wa kupunguza kasi na tunavyozungumza hivi sasa, tumeshamaliza zoezi la kuboresha vituo vyetu kwenda mfumo wa 3G na 4G kitu kinachoifanya Zantel kuwa kampuni ya mawasiliano iliyoonea nchi nzima.
Zantel imedhamiria kuwaweka mbele wateja wake kwa kuwaletea teknolojia mpya na ya kisasa pamoja na kuwa mtandao bora zaidi unaotoa suluhisho la huduma bora za data nchini Tanzania.

MHE BITEKO AITAKA STAMICO KUITHIBITISHIA SERIKALI KWANINI IENDELEE KUWEPO

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya  pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umetakiwa kutoa maelezo kwa serikali katika kipindi cha muda mfupi kueleza sababu za kuendelea kusalia kuwepo kwa shirika hilo kutokana na kukosa umakini katika utendaji.

Kauli ya kuchukizwa na utendaji wa Shirika hilo imetolewa Leo 16 Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko Wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika hilo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam.

Mhe Biteko alisema kuwa serikali ilikuwa na makusudi mazuri kufuatia mabadiliko ya Sera za kiuchumi katika miaka ya 1980 kwa STAMICO kuwekwa kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa na hatimaye kubinafsishwa rasmi mwaka 1996 lakini katika kipindi chote cha utendaji hakuna msaada wowote ambao Shirika hilo limeipatia serikali zaidi ya kuingiza hasara maradufu.

Alisema kuwa pamoja na STAMICO kuwa na jukumu la kuendeleza migodi ya Madini na kufanya biashara za Madini ikiwemo mradi wa dhahabu wa STAMIGOLD uliopo Biharamlo Mkoani Kagera na Mgodi wa Makaa ya Mawe KABULO uliopo Mkoani Ruvuma lakini Taasisi hiyo imeshindwa kuendeleza migodi kwa ufanisi huku wachimbaji wadogo wakisalia kuwa katika uduni wa mbinu rafiki na tija katika utendaji kazi wao.

Alisema kuwa Shirika hilo linapaswa kutafakari kwa umakini utendaji wake kwani limeongeza hasara kwa serikali ya deni la shilingi Bilioni 1.77 hivyo serikali haiwezi kuendelea kusalia kuwa na Shirika linalozalisha madeni kuliko matokeo makubwa na faida.

Aliongeza kuwa wataalamu wote katika sekta ya Madini wanapaswa kutambua kuwa biashara ya Madini ni zaidi ya kutoa leseni hivyo watambue kuwa kuna kila sababu ya kuwa na matumizi bora ya mapato na kutazama namna bora ya kuifanya sekta ya Madini kuchangia asilimia 10% ya pato la Taifa.

Mhe Biteko alisema kuwa imani bila matendo ni uduni wa fikra hivyo kuwa na cheo kikubwa serikalini halafu uzalishaji ni mdogo ni kipimo halisi cha utendaji wa mazoea walionao watumishi wengi ambao wamekosa uzalendo na bidii katika utendaji kazi.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kusimamia vyema rasilimali za wananchi hivyo watendaji katika sekta mbalimbali wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Rais Magufuli katika kuteleleza adhma ya serikali.

MWISHO

MNEC SALIM ASAS AMWAGA MAMILIONI YA FEDHA KATA YA KIHESA KWA AJILI YA MAENDELEO

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa wakifurahia kukabidhiwa kwa hati kwa diwani wa chama hicho tukio hilo lilifanika katika ofisi ya kata ya kihesa likihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani wakizungumza na wananchi waliohudhulia tukio hilo
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani wakiwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa kata ya kihesa 
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiongea na wananchi walijitokeza kushudia tukia na kupewa cheti diwani wa kata hiyo Jully Sawani

Na Fredy Mgunda,Iringa.


KATA ya kihesa manispaa ya Iringa imeanza kupata neema ya mamilioni ya fedha za kimaendeleo mara baada ya kumpata diwani mpya kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya kupita bila kupigwa kutoka na vyama vingine vya siasa kutoweka wagombea.

Akikabidhiwa hati ya utambulisho wa kuwa ndio diwani halali wa kata ya kihesa,Jully Sawani alielezea mikakati ya kimaendeleo ya kata hiyo ambayo ataanza nayo ni kukarabati miundombinu ya barabara kwenye baadhi ya mitaa ya kata hiyo.

“Ukipita kwenye mitaa yetu utagundua kuwa mtaa kama mtaa wa mafifi miundombinu ya barabara sio nzuri kabisho akahidi kuwa ndani ya wiki hii atapeleka kata pila lianze kazi ya kuzikarabati bara bara hizo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wake kwa kuwa wamemtuma kufanya kazi” alisema Sawani

Sawani aliongeza kwa kusema kuwa amejianda kuhakikisha anatatua kero za wananchi kwa kushirikiana na serikali ya manispaa ya Iringa ambayo inatekeleza sera za chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 huku ikiwa na kauli mbiu inayosema kuwa hapa kazi tu.

“Naomba niseme ukweli wananchi wangu wote wa kata ya Kihesa sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio mchezo mchezo mliokuwa mnaufanya nimeomba kuwa diwani kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi wa kata hii anafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa familia yake haiwi masikini,ninasema kuwa kila ukilala hakikisha unaukataa umasikini kwa kuutamka wakati unalala tena kwa zaidi ya mara tisa hapo ndio utafanya kazi” alisema Sawani

Aidha Sawani alitoa kilio chake cha kwa kuomba msaada wa kimaendeleo kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ambapo alimwambia kuwa wananshida ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na kusaidiwa kumalizia ujenzi wa jingo la kibiashara ambalo lipo jirani na ofisi za kata ya hiyo.

“Mheshimiwa MNEC Salim Asas nipo hapa naomba utusidie msaada wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na jingo hili ambalo lipo mbele yetu unaliona linahitaji kumaliziwa ili kuweza kuongeza ajira kwa wananchi wa kata yangu hivyo naomba sana msaada wako kukamilisha hivi vyote kwa awamu hii ya kwanza” alisema Sawani

Akihutubia mamia ya wananchi walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa kata hiyo Jully Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya saruji kwa ajili ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto nyingine.

“Leo naanza kwa kutoa mifuko miambili ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za shule hiyo ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa uhuru kwa lengo la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa katika kuleta maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo hivyo nitasaidia sana kwenye elimu” alisema Asas

Asas aliwakata viongozi wa kata hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na kuacha kuishi kimazoea.

“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas


Asas alisema vijembe na malumbano ya kisiasa katika kata hiyo yanatosha na akawataka vijana hao kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakavyowawezesha kufikiwa kirahisi na mipango mbalimbali ya maendeleo 

MBUNGE RITTA KABATI ATOA MSAADA WA MAFUTA MAALUM YA KUPAKA KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI MKOA WA IRINGA

Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi box la mafuta hayo katibu wa Tas mkoa wa Iringa bwana Leo Sambala katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa  
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi  la mafuta hayo katibu wa Mufindi bwana Andrea Kihwelo
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi  mafuta hayo moja ya walemavu wa ngozi
 Mbunge wa viti maalum Ritta Kabati akimkabidhi boxi la mafuta hayo mwenyekiti wa wilaya ya Kilolo ndugu Anna Masasi 


Na Fredy Mgunda,Iringa

JAMII imetakiwa kuwalea, kuwatunza na kuwajali watu wenye ulemavu wa ngozi albino kwa kuhakikisha kwamba wanaishi katika mazingira mazuri, yenye usalama na sio kuwanyanyapaa pale wanapohitaji mahitaji yao ya msingi.

Aidha Chama cha walemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Iringa kimeshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali, ili walemavu hao pia waweze kupata elimu juu ya afya ya usalama wa ngozi pamoja na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika maisha yao.


Hayo yalisemwa na mbunge wa viti maalum Ritta Kabati wakati alipokuwa akitoa msaada wa mafuta maalum ya kupaka watu wenye ulemavu wa ngozi albino katika hafla fupi iliyohudhuriwa na walemavu hao ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa


“Nampongeza Mwenyekiti wa TAS mkao wa Iringa kwa jitihada zake alizozifanya juu ya namna ya kupata mafuta haya, kama chama endeleeni kuwa wabunifu namna ya kulisaidia kundi hili tete la walemavu kwa kuwalea na kuwatunza katika mazingira mazuri”, alisisitiza mbunge Kabati 

Vilevile Kabati  aliongeza kwa kuwataka viongozi wa chama hicho kutumia fursa waliyopewa na wanachama wao, kuhakikisha kwamba wana ainisha matatizo waliyonayo walemavu wa mkoa wa Iringa na kuyafikisha katika ofisi za serikali ili yaweze kufanyiwa kazi.

Kabati alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inahakikisha kuwa inafakiwa kutatua matatizo ya wananchi wa ikisha maisha yao yanaboreshwa.

“Hata haya mafuta yamenunuliwa na serikali kupitia wizara ya afya ,maendeleo ya jamii ,jinsia ,wazee na watoto na yanasambazwa nchi nzima hivyo sisi viongozi kazi yetu ni kwasaidia usafiri walememavu hawa” alisema Kabati


Awali akitoa maelezo mafupi juu ya changamoto zinazowakabili albino katika mkoa wa Iringa huo, Mwenyekiti wao Hellen Machibya  alisema kuwa wanashindwa kuwafikia wanachama wake kwa urahisi kutokana na kukosa usafiri na rasilimali fedha, kwa ajili ya kuwatimizia mahitaji yao ya msingi. 

Machibya alifafanua kuwa kukosekana kwa fedha kunakwamisha utendaji kazi na uendeshaji wa shughuli husika, hivyo wanaiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kutatua kero zinazowakabili ili kundi hilo tete liweze kusonga mbele kimaendeleo.

Machibya alisema kuwa kazi aliyoifanya mbunge huyo ni kuokoa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuwa watakuwa wanajikinga na mionzi ya jua.

Machibya alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwaathirika wakubwa wa ugonjwa wa kasa kutokana na ngozi zao kushambuliwa na jua na kusababisha kuiathiri ngozi hivyo msaada uliotolewa na serikali umeokoa sana maisha.

“Jamani sisi watu wenye ulemavu tunapenda sana kufanya kazi tatizo mionzi ya jua inatuathiri sana na kusababisha kushindwa kufanya kazi zetu kwa uwezo wetu hivyo tunaomba serikali na wadau kama mbunge Ritta Kabati waendelee kutusaidia maana mafuta haya dukani ni gharama sana hivyo watu wenye ulemavu wa ngozi hatuzimudu” Machibya

Lakini Chama cha walemavu wa ngozi (TAS) mkoa wa Iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati kwa kuwasidia kuwafikishia mafuta ya kujipaka mwilini kwa ajili ya kujikinga na mionzi ya jua ambayo imekuwa ikiwasababishia kupata ugonjwa wa kansa.