Shindano la kumsaka mnyange wa Kilimanjaro 2011 linategemewa kuanza hivi karibuni baada ya waandaji wa shindano hilo kudai kuwa sehemu kubwa ya maandalizi imeanza kukamilika ikiwa na pamoja kuwakusanya warembo kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya mazoezi (catwalk).
Msemaji wa shindano hilo Bw.Methuselah Magese amesema kuwa yeye na mundaji mkuu wa shindano hilo Jaquekline Chuwa tayari wako katika mchakato mnene kuhakikisha miss Tanzania wa mwaka huu anatokea mkoani Kilimanjaro.
Shindano la miss Kilimanjaro litafanyika june 11 juni katika hoteli nya Salsanero iliyoko Shant town mjini Moshi ambapo mchekeshaji masanja toka kundi la Ze Komedi Orijino atakuwa ndiye mc wa siku hiyo wakati msanii 20% na wengine wengi wataburudisha vya kutosha.
Miss kilimanjaro 2011 imedhaminiwa na Vodacom, Redds, Africa sana pub,Rafiki min super market, Excutive solution, Bamm solution na www.uniqueentertz.blogspot.com.
"Tunawaomba warembo wanaojiamini kuwa wao ni warembo na wenye ari ya kuwa vinara wa sanaa ya urembo wajitokeze kuwania taji hilo ambalo litakuwa na ushabiki wa aina yake kwani tunategemea kutoa warembo bomba ambao watatoa changamoto kwa vitongoji na kanda zingine" alisema magese.
Thursday, April 07, 2011
HABARI
Thursday, April 07, 2011
BANGO
*******************KUMBUKUMBU YA MASUBO********************
Familia ya marehemu Fidelis Michael Masubo inapenda kuwakaribisha ndugu, Jamaa na Marafiki wote kwenye misa fupi ya kumbukumbu ya kutimiza miaka miwili Tangu atutoke Baba yetu mpendwa Fidelis Michael Masubo.
Misa itafanyika Nyumbani kwake Myakato Buzuruga siku ya ijumaa (kesho) Tarehe 08/04/2011 kuanzia saa 1:00 usiku, Hii ikiwa na lengo la kuwapa nafasi waumini wa Kanisa Katiliki kuhudhuria kwanza misa ya njia ya msalaba.
ENYI NDUGU NA MARAFIKI Njooni tujumuike PAMOJA katika sala.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
*****************************AMEN******************************
Thursday, April 07, 2011
FIESTA
Thursday, April 07, 2011
HABARI
Tuesday, April 05, 2011
HABARI
SHARIF SHEIKH AHMED.
Ziara iliyokuwa ifanywe na Rais wa Somalia SHARIF SHEIKH AHMED, nchini Tanzania kuanzia tarehe 6 hadi tarehe 7, 04,2011 Imeahirishwa mpaka pale itakapotangazwa tena.
IMETOLEWA NA ISHENGOMA
AFISA HABARI MWANDAMIZI.