Timu ya soka ya mashabiki wa Real madrid ya jijini Dar es salaam ndiyo imeibuka kuwa mshindi katika ligi ya Tamasha la Fiesta Soka Bonanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Leaders jana hivyo kunyakuwa kombe na zawadi ya Fedha taslimu shilingi milioni moja.Timu hiyo imepata ushindi huo mara baada ya kuingia fainali na hatimaye kuishinda timu ya mashabiki wa Chelsea ambao nao wametoka na zawadi kama washindi wa pili ya shilingi laki tano.
RABSHA NAZO SEHEMU YA MICHEZO.'Siunajuwa hawa ni mashabiki wa timu gani na gani?'Katika hatua ya nusu fainali Chelsea waliwaondosha Manchester United nao Real wakawagagadua Ac milan.
Mashindano hayo yataendelea tena katika mikoa mbalimbali hapa nchini yakishirikisha mashabiki wa mikoa husika kwa timu tajwa katika mashindano ambazo ni Man United, Liverpool, Chelsea, Real madrid, Bacelona, Inter Milan, Ac Milan na Alsenal.
Masanja mkandamizaji wa Ze Orijino Komedi katika pozi naye Babuu wa Kitaa toka Ze-supa Brand Clouds Media viwanjani hapo kama mashuhuda kwa yaliyojiri.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.