ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 4, 2023

KENYA NA CHINA ZAVUTIWA NA FURSA ZA UWEKEZAJI KWENYE MIFUGO NCHINI

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Ranchi ya Mbogo Bw. Naweed Mullah (kulia) akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi (kushoto) na timu ya washiriki wa  Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula  (AGRF) waliofika shambani kwake Chalinze, Septemba 03,2023 kwa ajili ya kuona namna anavyofanya shughuli zake.
Meneja Uendelezaji biashara kutoka kiwanda cha kusindika nyama cha "TANCHOICE" Bw. Luwungo Hassan (aliyesimama mbele) akielezea kwa ufupi historia ya kiwanda hicho kwa washiriki wa Mkutano wa Jukwa la mifumo ya Chakula (AGRF) waliofika kiwandani hapo Septemba 03, 2023.
Sehemu ya aina ya Ng'ombe waliopo kwenye ranchi ya Mbogo iliyopo Chalinze mkoani Pwani.


 ◾Ni mara baada ya kuwatembelea wadau wa Sekta hiyo..


Nchi za China na Kenya zimeonekana kuvutiwa na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya Mifugo mara baada ya kuwatembelea wawekezaji wa ndani ambao ni Ranchi ya Mbogo na Kiwanda cha kuchakata nyama cha “Tanchoice” vilivyopo mkoani Pwani Septemba 03, 2023.

Ziara hiyo ambayo ni miongoni mwa shughuli za utangulizi zinazofanyika kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula barani  Afrika (AGRF) iliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ambapo alibainisha kuwa Wizara yake imejiandaa kikamilifu kutumia fursa zitakazojitokeza katika pindi chote cha mkutano huo kuiimarisha sekta ya Mifugo nchini.

“Sisi kwa sasa kama nchi tunasema  “flagship” ya wizara yetu ni nyama na samaki ambazo tunazipeleka nje ya nchi na kwa mwaka jana tulifanikiwa kusafirisha tani elfu 14 na malengo yetu ni kuvuka tani elfu 16 kwa mwaka huu wa fedha na hilo tunaweza kufanikiwa kwa kuleta wadau wengi zaidi kama mbogo ranchi” Amesema Dkt. Mushi.

Aidha Dkt. Mushi ameongeza kuwa lengo la mkutano huo ni kupata wawekezaji na masoko mapya ili nyama inayozalishwa nchini iweze kuuzwa kwa wingi nje ya nchi hatua ambayo anaamini itachangia ongezeko la fedha za kigeni kwa kiwango kikubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ranchi ya Mbogo Bw. Naweed Mullah amesema kuwa anatarajia kutumia mkutano huo wa kimataifa wa jukwaa la Mifumo ya chakula kuhakikisha anatoa elimu ya kutosha kwa washiriki wa ndani na nje ya nchi kuhusu njia bora za uongezaji thamani wa ng;ombe wa asili waliopo hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla.

“Tunajua ulimwengu mzima unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula hasa nyama na hali ya upatikanaji wa zao hilo imeendelea kushuka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo tunaamini jukwaa hili limelenga kujadili namna bora ya kukabiliana na changamoto hiyo” Ameongeza Bw. Mulllah.

Naye mmoja wa washiriki wa ziara hiyo Bi. Wangari Kurya kutoka nchini Kenya mbali na kukoshwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta ya Mifugo nchini amevutiwa zaidi na namna Serikali inavyohamasisha aina zote za kilimo ikiwa ni tofauti na kwao ambako kilimo mazao ndio kimekuwa kikisisitizwa zaidi.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya “FAMSUN” kutoka nchini China Bw. Joy Lee amevutiwa na namna Tanzania ilivyobarikiwa kuwa na ardhi kubwa na nzuri kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji tofauti na hali ilivyo nchini kwao ambako wanalazimika kutumia kiwango kikubwa cha teknolojia ili kutekeleza shughuli hizo kwenye maeneo madogo waliyonayo.

“Ninatoa wito kwa wawekezaji wote kuja Tanzania kuna fursa nyingi sana za uwekezaji kwa upande wa sekta ya Mifugo” Amehitimisha Bw. Lee.

Mkutano wa Jukwaa la kujadili Mifumo ya chakula barani Afrika unatarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia Septemba 05-08, 2023 ambapo takribani 6000 wa ndani na nje ya nchi  wanatarajia kushiriki kwenye mkutano huo.

TANGA UWASA YATUMIA MILIONI 20 KUKARABATI MTANDAO WA MAJI TAKA USAGARA

 

Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Meneja wa Mazingira Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani akikagua mtandao wa maji taka katika eneo la Usagara Jijini Tanga ambao wameufanyia ukarabati mkubwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa
Muonekano wa chemba zilizokarabatiwa

Na Oscar Assenga, TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) imetumia milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao wa maji taka wa zamani katika eneo la Usagara maarufu kama Bandari Chafu.

Akizungumza Meneja wa Mazingira wa Tanga Uwasa Nasibu Ramadhani alisema uamuzi wa kuukarabati mtandao huo wa maji taka waliufanya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa wa eneo hilo tokea 2018.

Alisema malalamiko hayo yalikuwa yanahusiana na miuondombiu ya maji taka eneo hilo kuwa chakavu na hivyo kuhatarisha afya zao na hivyo kuomba mtandao huo uliojengwa na TPA miaka ya nyuma na hivyo baada ya kubinafishwa nyumba hizo.

Alisema hivyo wanawaomba Tanga Uwasa iwarebishie mfumo huo ambapo awali ulikuwa baada ya kuona changamoto hizo waliamua watenge fedha Milioni 20 kwa ajili ya kuukarabati mtandao huo.

Alisema katika ukarabati wa mtandao huo ulihusisha ukarabati wa chemba kubwa ambazo zinapokea maji taka kutoka kwenye maeneo hayo na ukarabati wa chemba ndogo ndogo ambazo zinaunganisha bomba na bomba na maeneo yenye bomba chakavu .

“Hayo ndio maeneo tuliyoyakarabati na tunatarajia kukarabati na mwaka huu tutakamilisha mpango huo wa ukarabati kukamilisha mfumo hiyo ili kuuwezesha kuishi muda mrefu hiyo itasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza”Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuhakikisha miundombinu ya maji taka kuhakikisha hawaweki taka ngumu na wanaitunza ili iweze kukaa muda mrefu

NACHINGWEA WATUMIA MATOFALI YA PILIPILI KUDHIBITI TEMBO

 

Afisa Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Kanda ya Kusini Mashariki Linus Ezekiel Chuwa akitoa maelezo namna ambavyo mbinu za tofari la pilipili linavyoweza kufanya kazi ya kuwafukuza Tembo
Afisa Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Kanda ya Kusini Mashariki Linus Ezekiel Chuwa akitoa maelezo namna ambavyo mbinu za tofari la pilipili linavyoweza kufanya kazi ya kuwafukuza Tembo
Afisa Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Kanda ya Kusini Mashariki Linus Ezekiel Chuwa akitoa maelezo namna ambavyo mbinu za tofari la pilipili linavyoweza kufanya kazi ya kuwafukuza Tembo


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


Serikali kupitia Taasisi ya TAWA imeendelea na jitihada za kutokomeza changamoto ya Tembo wanaovamia makazi na mashamba ya wananchi katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi ili kuisadia jamii kufanya shughuli za kiuchumi bila usumbufu wowote.


Akizungumza wakati wa mafunzo ya namna ya kukabiliana na Tembo kijijini Mkoka Ruponda wilaya ya Nachingwea, Afisa Mhifadhi Mkuu Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania Kanda ya Kusini Mashariki Linus Ezekiel Chuwa alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa elimu kwa kila uchwao namna ya kukabiliana na Tembo.

Chuwa alisema kuwa serikali imekuwa ikutumia mikakati ya muda mrefu katika kukabiliana na Tembo,TAWA kwa kushirikiaha na PAMC Foundation imetoa mafunzo ya namna yakukabiliana na wanyama hao kwa kwa kuweka uzio wenye mchanganyiko pilipili na mafuta machafu pamoja na matumizi ya ndege Nyuki, matumizi ya gari Maalum na tofali la pilipili.

Alisema kuwa kuwafundisha mbinu hizo zitasaidia wananchi kuwafukuza Tembo na kuepukana na madhara ambayo yamekuwa yanatokana na mnyama huyo.

Chuwa alisema kuwa mbinu ya kuchoma tofari lilitengenezwa na kwa kinyesi cha mnyama pamoja na pilipili kutasiadia kuwafukuza Tembo Kwa kuwa mnyama huyo hapendi harufu ya pilipili.


kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wanaishukuru serikali kwa jitihada na mikakati inayoendelea kuchukuliwa namna ya kudhibiti mnyama Tembo ili asilete madhara kwa jamii husika.


Sunday, September 3, 2023

NI WAPI JIJINI MWANZA NAWEZAPATA BIDHAA YOYOTE ZA AINA ZOTE NDANI YA DUKA MOJA?

 

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

ONE MORE & DISCOUNT CENTRE One of the best places to find home amenities, carpets, curtains.,towels, furniture and all your need to furnish your home.