NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametembelea na kukaguwa eneo la mradi wa upanuzi wa Daraja la Mabatini na barabara unganishi yenye urefu wa meta 590, wilayani Nyamagana, jijini Mwanza na kukuta mradi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 93 hivyo kuanza kupitika. Waziri Ulega pia amempongeza mkandarasi kwa kazi anayofanya. “Wananchi wameridhika. Msongamano wa magari nao umepungua kwa kiwango kikubwa,” alisema Ulega na kuongeza kuwa upanuzi wa barabara mbili kwenda na kurudi umeongeza ufanisi wa usafiri katika eneo hilo. Zaidi fuatilia video hii........Friday, December 12, 2025
WAZIRI ULEGA "SITOONGEZA HATA SEKUNDE UJENZI BARABARA NA DARAJA LA MKUYUNI" - MKANDARASI ATOBOA SIRI
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Mnamo Disemba 5, mwaka huu 2025 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt, Mwigulu Nchemba alifanya ziara jijiji Mwanza kuzitembelea familia zilizopata madhara ya vurugu za uchaguzi Mkuu wa Oct 29/2025. Pamoja na kuzungumza na wakazi wa jiji hili la miamba, pia Waziri Mkuu alipokea kero sugu ya kutokamilika kwa barabara na madaraja kadhaa likiwemo lile la eneo muhimu la Mkuyuni. Katika sehemu ya majibu yake Mhe. Waziri mkuu alitoa agizo kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdalah Ulega kuja na kulikagua daraja hilo haraka iwezekanavyo na kutoka na suluhisho. Mwanahabari wetu Albert G. Sengo anakuja hapa na taarifa kamili. Lakini kwanza hebu tujikumbushe kauli ya Waziri Mkuu aliyoitoa mnamo Disemba 5 2025.Wednesday, December 10, 2025
USALAMA UMEENDELEA KUIMARIKA NCHINI- POLISI
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime amesema hali ya usalama ni shwari kote nchini Tanzania na shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kama kawaida nchi nzima baada ya mapumziko ya sherehe za sikukuu ya Uhuru wa Tanzania bara jana Jumanne Disemba 09, 2025.
Kulingana na taarifa yake kwa Vyombo vya habari, Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha amani na usalama unaendelea kuimarika nchini ili hata wale wachache wenye hofu waweze kutoka na kuendelea na shughuli zao za kila siku za kujitafutia riziki na kupata huduma za kijamii wanazo hitaji.
"Aidha tunawashukuru na kuwapongeza wananchi wote kwa nafasi zao kwa namna wanavyoendelea kuwakataa na kuwapuuza wale wanaohamasisha na kuchochea vurugu na ukiukwaji wa Sheria za nchi kupitia mitandao ya kijamii na njia zingine." Amesema Misime.
CHELSEA YAKUNG'UTWA, BARCELONA YAPINDUA MEZA, LIVERPOOL YANG'ARA ULAYA.
Usiku wa jana umeshuhudia matokeo tofauti katika michezo ya Ulaya, huku Chelsea ikipoteza ugenini, Liverpool ikiwahi dakika za mwisho, na Barcelona ikitoa burudani ya kupindua meza.
Atalanta 2-1 Chelsea
Chelsea imekubali kipigo cha 2-1 dhidi ya Atalanta kwenye mchezo uliochezwa ugenini.
Matokeo:
55’ Gianluca Scamacca (Atalanta)
83’ Charles De Ketelaere (Atalanta)
26’ Pedro (Chelsea)
The Blues walitangulia kupata bao mapema kupitia Pedro, lakini Atalanta walionyesha uimara kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kisha kuongeza bao la ushindi dakika za lala salama.
Inter Milan
0-1
Liverpool
Liverpool imeondoka San Siro na ushindi mwembamba wa 1-0, bao pekee likifungwa dakika ya 88 na Dominik Szoboszlai.
88’ Szoboszlai
The Reds walionyesha uthabiti mkubwa na subira iliyowalipa mwishoni mwa mchezo.
Barcelona
2-1
Eintracht Frankfurt
Barcelona imepindua matokeo kutoka 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.
50’ Kounde
53’ Kounde
21’ Knauff (Frankfurt)
Bao mbili mfululizo za Jules Kounde ndani ya dakika tatu ziliipa Barca ushindi muhimu baada ya hiviwana kuanza nyuma.
GAMONDI ATEMA MAJINA MAKUBWA STARS KUELEKEA AFCON 2025.


Tuesday, December 9, 2025
MECHI ZA LEO UEFA NI PRESHA TUPU....
Italia kutakuwa na mechi ya kukata Inter Milan vs Liverpool ambao hivi karibuni wamekuwa na matokeo ambayo hayaridhishi kabisa kwani kwenye mechi 13 amabzo amecheza ameshinda 3 pekee. Mara nyingi hawa wawili kukutana ilikuwa kwenye fainali na Jogoo wa Anfield alipoteza.
Vijana wa Diego Simeone, Atletico Madrid watakuwa ugenini kukiwasha dhidi ya PSV kutoka kule Uholanzi lakini pia imeweza kupata matokeo dhidi ya timu kubwa kwenye michuano hii.
AS Monaco atakuwa nyumbani kupepetana dhidi ya Galatasaray ambao walipoteza mechi yao iliyopita wakiwa nyumbani. Mwenyeji yeye alitoa sare, hivyo pointi 3 ni muhimu kwa timu zote siku ya leo.
Marseille yeye atakuwa kibaruani kumenyana vikali dhidi ya Union St.Gilloise ambao wanahitaji ushindi siku ya leo ili wasogee mbele kwenye michuano hii. Tofauti ya pointi kati yao hadi sasa ni hakuna kwani wote wana pointi sawa.
Bayern Munich yeye atakipiga dhidi ya Sporting CP ambapo mpaka sasa kwenye mechi 8 ambazo amecheza amekusanya pointi 10 huku vijana wa Kompany wao wakichukua pointi 12. Mwenyeji ametoka kupoteza huku mgeni yeye akishinda.
Kwa upande wa Chelsea wao watakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Atalanta baada ya mechi iliyopita kushinda, halikadhalika kwa wenyeji nao walishinda.
Vijana wa Hans Flick, FC Barcelona watakuwa nyumbani kusaka ushindi dhidi ya Eintracht Frankfurt ambao wana pointi 4 pekee hadi sasa huku Wacatalunya wao wakiwa na pointi 7. Barca wanahitaji ushindi kwa namna yoyote ile ili wajiweke kwenye nafasi nzuri ya michuano hii.
Tottenham Spurs atakuwa kibaruani kukipiga dhidi ya Slavia Prague ambao kwenye mechi 5 wameambulia pointi 3 pekee. Huku wenyeji wao wakiwa na pointi 8 hadi sasa.
"MSIWE NA HOFU MWANZA HALI NI SHWARI CLIP INAYOSAMBAA NI YA TAREHE 31 OCTOBA 2025" RC MTANDA
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
🛑Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, ametoa taarifa rasmi kuhusu hali ya usalama mkoani Mwanza, huku akikanusha vikali uvumi unaoenezwa mitandaoni kuhusu kuwepo kwa maandamano katika jiji hilo. Katika taarifa hiyo, Mhe. Mtanda ameeleza kwa uwazi kuwa video inayosambazwa mtandaoni si ya leo, bali ni tukio la zamani linalotumiwa kupotosha umma. 👉 Fuatilia video kamili kupitia #youtube chanel yetu hapa ujue alichokisema kwa kina Mkuu wa Mkoa juu ya usalama, uzushi wa maandamano, na msimamo wa serikali mkoani humo.Hakuna huduma, hakuna pilikapilika kama ilivyozoeleka, vituo vingi vya wauzaji wa mafuta na gesi jijini Mwanza, vimesitisha huduma kwa siku ya leo.
Ni tofauti na ilivyozoeleka, leo magari ni ya kuhesabu katika barabara hii yenye pilika pilika hapa jijini Mwanza.
Muonekano wa barabara ya kuelekea Kirumba.
Muonekano wa barabara ya Makongoro uelekeo wa uwanja wa ndege jijini Mwanza.
Muonekano kutoka barabara ya Nyerere hii ni barabara ya kuelekea mitaa iliyozoeleka kwa pilikapilika nyingi ya Rufiji na Uhuru, lakini leo watu wachache na magari ya kuhesabu.
Hakuna huduma kwa siku ya leo.
Muonekano.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)






.png)
.png)
.png)
.png)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)