NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametembelea na kukaguwa eneo la mradi wa upanuzi wa Daraja la Mabatini na barabara unganishi yenye urefu wa meta 590, wilayani Nyamagana, jijini Mwanza na kukuta mradi huo ukiwa umekamilika kwa asilimia 93 hivyo kuanza kupitika. Waziri Ulega pia amempongeza mkandarasi kwa kazi anayofanya. “Wananchi wameridhika. Msongamano wa magari nao umepungua kwa kiwango kikubwa,” alisema Ulega na kuongeza kuwa upanuzi wa barabara mbili kwenda na kurudi umeongeza ufanisi wa usafiri katika eneo hilo. Zaidi fuatilia video hii........ #jembefmtz #samiasuluhuhassan #mwanza #waziriWaUjenzi #WaziriUlegaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment