Thursday, January 07, 2010
MWANZA
Wednesday, January 06, 2010
MWANZA
Wednesday, January 06, 2010
MWANZA
WAKATI JIJI LA MWANZA LIKIWA KTK MCHAKATO WA KUJITANGAZA ZAIDI KATIKA SUALA ZIMA LA UTALII, NAMI PIA KAMA MDAU WA SEKTA YA KUBLOGISHA SIKU SI NYINGI NITAKULETEA VIVUTIO VINAVYO PATIKANA KTK JIJI HILI LA MIAMBA. ENDELEA KUCHUNGULIA BLOG HII YAWEZEKANA IKAWA KESHO, NANI AJUAYE? TOKA JUU MJENGONI MAHALA NILIPO PIGA PICHA HII NI USIKU WA JANA MAJIRA YA SAA 22:13 KEEP LEFT KIELELEZO CHA MWANZA.
Monday, January 04, 2010
MWANZA
PICHANI WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI WAKISAKA NEWS BILA MAFANIKIO KATIKA OFISI ZA MAOFISA WA KAMPUNI YA MARINE SERVICE MWANZA WANAOMILIKI MELI HIYO.
MELI YA MV.BUTIAMA IMEKWAMA LEO ZIWANI VICTORIA MARA BAADA YA KUPIGWA NA DHORUBA KALI NA KUZIMIKA INJINI.TUKIO HILI LIMETOKEA KARIBU NA KISIWA CHA MAKOBE MWENDO WA SAA TANO NA DAKIKA 18 ASUBUHI IKIWA NI SAA MOJA MARA BAADA YA KUANZA SAFARI KUTOKA WILAYA YA UKEREWE KUELEKEA JIJINI MWANZA. MELI HIYO IKIWA INASUKUMWA NA UPEPO HUKU IKIKABIRIANA NA MAWIMBI MAZITO YA MAJI IMEKOKOTWA HADI ENEO LA KARIBU NA MWAMBAO WA IGOMBE. MARA BAADA YA HALI HIYO KUTOKEA HUKU MVUA KUBWA IKINYESHA NA UPEPO MKALI UKIVUMA ZIWANI HUMO ABIRIA WALICHANGANYIKIWA WASIFAHAMU KINACHOFUATA KWANI ILICHUKUA MASAA MATATU TANGU TUKIO HILO KUTOKEA NA KUSIWE NA MSAADA WOWOTE WALA JITIHADA ZOZOTE TOKA KWA VYOMBO HUSIKA (INASIKITISHA). SABABU ZA MISUKOSUKO HIYO ZINATAJWA KUWA NI MELI HIYO KUBEBA ABIRIA NA MIZIGO ZAIDI YA UWEZO WAKE, KIASI CHA ABIRIA WENGI KUSIMAMA. JANA MELI HIYO ILISHINDWA KUFANYA SAFARI ZAKE KUTOKANA NA KUWA NA HITILAFU HALI NA HAIJAFAHAMIKA KAMA KWELI MELI HIYO MARA BAADA YA MATENGENEZO KAMA ILIKAGULIWA NA WADAU WA CHOMBO CHA KUDHIBITI USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI MAJINI NA NCHI KAVU (SUMATRA). KIASI CHA SAA NANE NA DAKIKA 30 MELI YA CLARIAS NA BOTI ZA JESHI LA POLISI MAJINI TAYARI ZIMEFIKA ENEO LA TUKIO KUFANYA UOKOAJI. Tukio hili na lile la MV.Bukoba karibu kuwa dugu moja. HATARI LAKINI SALAMA
Monday, January 04, 2010
MWANZA