ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 1, 2024

HAIER WATUA RASMI MWANZA KWA KUFUNGUWA BONGE LA DUKA NDANI YA ROCK CITY MALL

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

SERIKALI ilikuwa namuono wa kupunguza utumiaji wa mkaa na kuni kwa wananchi mijini na vijijini, Jeh katika bidhaa zenu zimekuja na mlengo gani kuisaidia Serikali wananchi wapate nishati mbadala au majiko yenye kumumia umeme rafiki, yaani usio na gharama kubwa tofauti na utumiaji wa majiko ya kizamani? Ni moja kati ya maswali yaliyoulizwa mwishoni mwa wiki wakati Mabingwa wa vifaa vya kielectronic ‘Haier’ wakizindua tawi lao lauuzaji bidhaa zao, linalopatina Rock City Mall Gorofa ya kwanza Mkoani Mwanza. Sasa Kwa wakazi waishio maeneo ya jirani Mkoani hapa wakifika kwenye Mall hiyo wataweza kujipatia bidhaa mbalimbali za kieletronic ikiwemo TV, Friji, Majiko na Jezi mpya za Young Africans Msimu wa 2024/25. Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni. ‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.

Tuesday, July 30, 2024

MBUNGE MTEMVU AFANYA KWELI ASHUSHA NEEMA UJENZI WA ZAHANATI GOGONI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAMBA 

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu ameingilia kati na  kumaliza sakata la mvutano na mgogoro wa mradi wa ujenzi wa zahanati katika mtaa wa gogoni kata ya Kibamba ambao umedumu kwa pindi kirefu bila ya kuanza kujengwa.

Kukwama kwa mradi huo umeleta hali ya sintofahamu kwa wananchi,viongozi wa serikali,na wa chama cha mapinduzi  kutokana na kusuasua kwa kwa kipindi cha muda mrefu  licha ya kuwepo kwa eneo lililotolewa na serikali.



Kutokana na hali hiyo imemlazimu  Mhe.Mtemvu kuamua kufanya ziara yake ya kikazi   yenye lengo la kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo  inayoendelea  kutekelezwa  na ile iliyokwama ili kuweza kuitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Mtemvu alibainisha kwamba lengo la Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuboresha huduma ya afya ili wananchi waweze kuondokana na changamoto za matibabu.

"Nipo katika ziara yangu ya kikazi lakini lengo lake kubwa ni kutembelea na kukagua miradi mbali mbali ambayo imekwama na ile ambayo inaendelea kutekelezwa,"alibainisha Mhe.Mtemvu.

Aliwaomba viongozi wa chama na serikali kukaa kwa pamoja na kuondoa kabisa tofauti zao kati ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gogoni pamoja na diwani wa kata ya Kibamba na atopenda kuona mradi huo unakwama tena na badala yake umalizike.


Katika hatua nyingine aliwaomba viongozi wa chama pamoja na serikali kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa sambamba na kuhudhuria vikao vya maamuzi ya pamoja ili kuondoa hali ya  kuwepo kwa vikwazo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Gogoni Ally Mohamed alisema wananchi walipatiwa eneo hilo na serikali kwa lengo la mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ili kuwasaidia wananchi kupata huduma.

Naye Diwani wa Kata ya Kibamba Peter Kilango amesema kwamba hapo awali kulikuwepo na  changamoto kutokana na kutokubaliana na baadhi ya viongozi lakini ujio wa Mbunge umeweza kuwa mkombozi ya kuliweka sawa jambo hilo.

Katika hatua nyingine Mbunge Mtemvu ametembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara ambapo amejionea ujenzi wa Makalavati mapya na madaraja  katika kata za Kwembe na Msigani.

Nao baadhi ya wananchi wamepongeza juhudi za Mbunge huyo katika kuleta chachu ya maendeleo na kumuomba aongeze nguvu katika kuwasaidia kumaliza changamoto ya maji na miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo.

Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe.Issa Mtemvu amefanya ziara yake ya kikazi katika kata tatu za Kibamba,Kwembe,na Msigani ambapo amekagua miradi na kusikiliza kero na changamoto za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.

Monday, July 29, 2024

UVCCM YAUNGANA NA OFISI YA MKUU WA WILAYA KUCHANGIA DAMU KITUO CHA AFYA MKOANI

VICTOR MASANGU/PWANI SAUTI BY GSENGO Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu wa tano Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuokoa vifo vya mama na mtoto Ofisi ya Wilaya ya Kibaha kwa kushirikiana na Umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mjini imemua kuendesha kampeni maalumu kwa ajili ya uchangiaji wa damu katika katika kituo cha afya Mkoani kwa lengo la kuweza kuokoa maisha ya mama na mtoto. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha Moses Magogwa amesema kwamba wameamua kwenda kuchangia damu katika kituo hicho kutokana na kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa ambao wanakwenda kupatiwa matibabu hususan kwa wakinamama wajawazito.

ZAIDI YA BILIONI 23 KUTUMIKA KUSAMBAZA UMEME KILIMANJARO VIJIJINI

 

✔️VIJIJI 506 VIMEUNGANISHWA NA UMEME KATI YA VIJIJI 519 SAWA NA 97.49%

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 23.7 ili kuhakikisha miradi yote ya kusambaza umeme vijijini Mkoani Kilimanjaro inakamilika na kuwapatia wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amebainisha hayo mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa Julai 29 Mkoani Kilimanjaro wakati wa utambulisho wa Wakandarasi walioshinda tenda ya kusambaza umeme katika vijiji 13 vilivyokuwa vimesalia. 

"Hadi sasa tumeunganisha umeme katika vijiji 506 kati ya vijiji 519 ambayo ni sawa na asilimia 97.49 Mkoani hapa; na leo hii tupo hapa kutambulisha Wakandarasi watakaotekeleza miradi katika vijiji hivi vilivyosalia," amebainisha Mhandisi Olotu.

Mhandisi Olutu amebainisha kuwa kwa Mkoa wa Kilimanjaro REA inatekeleza jumla ya miradi mikubwa mitatu ambayo ni mradi wa shilingi bilioni 13.1 wa kusambaza umeme vijijini, mradi wa bilioni 8.8 wa kusambaza umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na mradi wa bilioni 1. 7 wa kusambaza umeme katika vituo vya afya na visima vya maji. 

"Tumefika hapa kwa lengo la kutambulisha Wakandarasi watakokamilisha kazi iliyobaki Mkoani hapa sambamba na kutambulisha wasimamizi wake kwa upande wa REA ambao miongoni mwa majukumu walionayo ni kuwasilisha kwako taarifa za mara kwa mara za maendedeleo na hatua za utekelezaji," amefafanua Mhandisi Olotu. 

Akizungumza wakati wa utambulisho wa wakandarasi hao; Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa ameipongeza REA kwa kuendelea kufanikisha dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wake kupitia umeme. 

"Umeme ni injini ya uchumi wa taifa lolote duniani na kwakutambua hilo, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi katika Sekta ya Nishati na kwa bahati nzuri REA mmetambua vyema dhamira ya Mhe. Rais na mnatekeleza kwa vitendo," amepongeza Nzowa. 

Aidha, amewataka Wakandarasi waliopewa jukumu hilo la kufikisha umeme katika vijiji vilivyosalia kufanya kazi kwa weledi na kwa kasi ili kukamilisha na kukabidhi mradi ndani ya muda uliopangwa. 

"Wote mliopewa jukumu ni wazawa; hatutarajii kuona kazi ikikwama; kukitokea changamoto yoyote Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo wazi kuwasikiliza na kusonga mbele," amesisitiza Nzowa. 


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wakandarasi hao waliahidi kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kasi ili kutimiza dhamira ya Serikali. 

"Serikali imetuamini kwa kutupa kazi, nasi tunaahidi kuhakikisha hatufanyi makosa; tutatekeleza kazi hii kwa uzalendo ili sote kwa pamoja tutimize dhamira ya Rais wetu," amesema Mhandisi Cuthbert Shirima, Mkandarasi kutoka Kampuni ya Transpower Limited. 

Kampuni zilizopewa jukumu la kukamilisha vijiji 13 vilivyosalia Mkoani humo ni Northern Engineering works Ltd (Wilaya ya Hai), Radi Services Ltd (Wilaya ya Hai na Moshi), Transpower Ltd (Wilaya ya Same) na Octupus Engineering Ltd (Wilaya ya Mwanga).