NA ALBERT GSENGO/MWANZA
SERIKALI ilikuwa namuono wa kupunguza utumiaji wa mkaa na kuni kwa wananchi mijini na vijijini, Jeh katika bidhaa zenu zimekuja na mlengo gani kuisaidia Serikali wananchi wapate nishati mbadala au majiko yenye kumumia umeme rafiki, yaani usio na gharama kubwa tofauti na utumiaji wa majiko ya kizamani? Ni moja kati ya maswali yaliyoulizwa mwishoni mwa wiki wakati Mabingwa wa vifaa vya kielectronic ‘Haier’ wakizindua tawi lao lauuzaji bidhaa zao, linalopatina Rock City Mall Gorofa ya kwanza Mkoani Mwanza. Sasa Kwa wakazi waishio maeneo ya jirani Mkoani hapa wakifika kwenye Mall hiyo wataweza kujipatia bidhaa mbalimbali za kieletronic ikiwemo TV, Friji, Majiko na Jezi mpya za Young Africans Msimu wa 2024/25. Kampuni ya Haier iliingia rasmi ubia na kampuni ya GSM GROUP mnamo mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa kipindi hiki chote, kampuni ya Haier ikishirikiana na GSM GROUP imekuwa ikihakikisha inaleta bidhaa ambazo zina tija sokoni. ‘Tangu uanzishwaji wa kampuni ya Haier, Tanzania, tumekuwa tukijitahidi kuangalia matakwa ya soko na kuhakikisha tunaboresha huduma na ufanisi wa bidhaa zetu kwa watumiaji’ Alisema haya meneja biashara, Bw. Ibrahim Kiongozi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.