VICTOR MASANGU,KIBAHA
WANAWAKE wa kampuni ya SF group ya Jijini Dar es Salaam wameadhimisha kilele cha siku ya mwanamke duniani kwa kufanya matendo ya huruma kwa kutoa msaada katika maeneo mbali mbali ya Jimbo la Kibaha mjini.
Wanawake hao wa SF group wameweza kutembelea katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu,afya pamoja ya mambo kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalumu.
Katika maadhimisho hayo wanawake wa SF Group ambayo ndani yake kuna makampuni mbali mbali ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kusaidiana na jamii.
Mkurugenzi wa Rasirimali watu wa SF Group Maria Faustine ambaye aliongoza jopo la wanawake hao walikwenda kutoa msaada wa vifaa mbali mbali katika shule ya sekondari Koka.
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba wameamua kwenda kutoa vifaa katika shule hiyo ya Koka ikiwa ni katika kuwasaidia wanafunzi7 kupata mahitaji yao hususan kwa upande wa wanawake.
"Tumeungana wanawake wote wa SF Group katika kuadhimisha kilele cha siku ya wanawake duniani kwa kutembelea maeneo matatu ikiwemo shule ya Koka,watoto yatima pamoja na hospitali ya Lulanzi,"alisema Mkurugenzi Goleti.
Kadhalika aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu wameamua kutoa zawadi kwa msichana mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake.
Pamoja na hayo walikwenda kutembelea kituo cha watoto yatima cha Buloma kilichopo kata ya Picha ya ndege na kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali ya msingi ikiwemo vyakula mbali mbali kama sukari,unga pamoja na sabuni,madaftari na mambo mengine ya msingi.
Kadhalika sambamba na hayo waliweza kutembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Lulanzi ambapo pia waliweza kutoa msaada wa vitu mbali mbali kwenye wodi ya wazazi.
Mkurugenzi Faustine alibainisha kuwa lengo kubwa la kwenda kutoa msaada katika maeneo matatu ni kwa ajili kuonyesha ushirikiano wa dhati kati ya wanawake wa SF Group pamoja na jamii.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya Koka Sekondari Magreth William aliwashukuru kwa dhati wanawake hao wa SF Group kwa msaada huo pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Silvestry Koka kwa sapoti katika mambo mbali mbali.
Kadhalika nao baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo hicho cha Buloma walitoa shukrani zao za dhati kwa msaada huo kutoka kwa wanawake wa SF Group.
Nao badhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao walishiriki katika zoezi hilo la ugawaji hawakusita kutoa shukrani zao za dhati kwa wanawake hao wa SF group.
SF Group imetumia kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kufanya matendo ya Huruma katika sehemu tatu.shule ya Sekondari Koka.kituo cha watoto yatima Buloma na wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya Lulanzi.