ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 21, 2025

PWANI YAWAONYA VIKALI BAADHI YA WAFANYABIASHARA WANAOTUMIA NJIA ZA MAGENDO

HABARI IMEANDIKWA NA VICTOR MASANGU, PWANI NA KUSOMWA NA ALBERT GSENGO

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imesema kwamba kwa sasa bado kuna changamoto sugu kwa baadhi ya wafanyabiashara kuamua kuvunja sheria na taratibu za nchi kutokana na kupitisha biashara zao kinyemela kwa njia za magendo kupitia maeneo ya uknda wa bahari ya hindi hali ambayo inasababisha upotevu mkubwa wa mapato kwa serikali. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA) Mkoa wa Pwani ,Masawa Masatu wakati wa hafla ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi kwa mwaka 2023/2024 ambapo pia amebainisha bado kuna udang'anyifu mkubwa unaofanya kwa wafanyabiashara kutumia stempu katika bidhaa ambazo ni bandia.

SIMBA SC NA AL MASRY ROBO FAINALI, IKIVUKA INA ZAMALEK

 

KLABU ya Simba itamenyana na Al Masry ya Misri katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mechi ya kwanza ikichezwa Aprili 3 Jijini Cairo na marudiano Aprili Aprili 10 Jijini Dar es Salaam.

Ikifanikiwa kuvuka hapo na kwenda Nusu Fainali itakutana na mshindi kati ya Stellenbosch ya Afrika Kusini na mabingwa, watetezi, Zamalek ya Misri.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, mabingwa watetezi, Al Ahly watamenyana na Al Hilal ya Sudan, wakati MC Alger ya Algeria itamenyana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

TRA PWANI YAPAMBANA VIKALI YAFANIKIWA KUKUSANYA BILIONI 60.69 KWA WALIPA KODI WAO


 NA  VICTOR MASANGU, PWANI

Mamlaka ya mapato Tanzania  (TRA) Mkoa wa Pwani imepata mafanikio makubwa   kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2023 /2024 baada ya kufanikiwa  kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 60.69 ikiwa ni sawa na kiwango cha utendaji wa asilimi 99.13 ambazo zimetokana na juhudi za kuwaelimisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiari bila shuruti.

Hayo yamebanishwa na Meneja wa  TRA  Mkoa wa Pwani  Masawa Masatu wakati wa hafla ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi kwa mwaka 2023/2024  ambapo amesema kwamba matokeo hayo ya mafaniko yamekuja kutokana na watanzania wengi kuwa wazalendo na wamehamasika  kwa kiasi kikubwa katika suala zima la ulipaji wa kodi.

"Sisi kama Mamlaka ya Mapato Tanznaia (TRA) tumejitahidi sana katika kutoa elimu kwa wafanyabiashara wetu juu ya umuhimu wa kulipa kodi ndio maana tumeweza kufanikiwa  kwa kiasi kikubwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 60 na kwamba watanzania wengi kwa sasa wamekuwa wazalendo kwani wanatambua umuhimu wa kulipa kodi ambayo inakwenda kuchangia kuleta maendeleo,"alisema Masatu.
Kadhalika ameongeza  kwamba  anatambua umuhimu mkubwa na mchango  ambao unafanywa na  baadhi ya wafanyabiashara katika suala la kulipa kodi  kwani ndio wamekuwa ni muhimili mkubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo na kutekeleza miradi mbali mbali  katika nchi ya Tanzania.


"Tunatambua umuhimu mkubwa wa mchango wa walipakodi wetu na kwamba wamekuwa mstari wa mbele katika kulipa kodi zao kwa hiari na ndio maana  tumeamua kutambua umuhimu wao na kuwapatia vyeti ikiwa kama ni moja ya kuwapa motisha pamoja na kuweza kuwahimiza kuendelea kulipa kodi kwa wakati wakati  bila shuruti yoyote kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania,"alisema Masatu.

Pia Masatu amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwa mzalendo na kutambua mchango wake mkubwa ambao anaufanya katika suala zima la kuhimiza ulipaji wa kodi kwa maslahi mapana kwa wananchi wa Tanzania ikiwemo pamoja na kuleta maendeleo katika nyanja mbali mbali.

Naye Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa Kodi (TRA) Tanzania  Richard Kayombo amebainisha kwamba katika kipindi cha  mwaka wa fedha 2023/2024  wameweza kukusanya  ujumla trioni 27.64  ikiwa ni ukuaji wa wa asilimia 14.45% ukilinganisha na mwaka uliopita.

Kwa  upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo  ya mlipa kodi ameitaka TRA kuhakikisha kwamba wanakuwa wabunifu na kusimamia vizuri suala zima la ukusanyaji wa mapato ikiwa sambamba na kuweka mikakati ya kuwa na vyanzo vipya.

Naye Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wafanya biashara Mkoa wa Pwani  Bundala Ndauka ameipongeza  Mamlaka ya TRA kwa  kuweza kuwapatia elimu mbali mbali juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi sambamaba na kuwawekea mazingira rafiki katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao.

Kauli mbiu  ya mwaka huu  katika  kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa  mlipa kodi kwa kipindi cha mwaka 2023 /2024  inasema kwamba kodi yetu maendeleo yetu

Wednesday, February 19, 2025

TRA PWANI YATUMIA MIL. 15 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA NA ELIMU KWA KUTOA MSAADA KWA JAMII

 


NA VICTOR  MASANGU, PWANI

Mamlaka ya mapato  Tanzania  (TRA) Mkoa wa Pwani imetumia kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kununua  vifaa na mahitaji mbali mbali  kwa ajili ya kutoa msaada kwa jamii pamoja na maeneo mbali mbali ikiwemo sekta ya afya pamoja na sekta ya elimu ikiwa ni moja ya kurudisha kwa jamii kwa kile ambacho wanakikusanya katika suala zima la  ukusanyaji wa mapato.


Meneja  wa TRA Mkoa wa Pwani  Masawa Masatu  ameyabainisha hayo wakati wa ziara maalumu ya  kwenda kutoa misaada mbali mbali kwa jamii ikiwa ni moja ya utekelezaji   wa Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kwamba wanaendelea kudumisha mahusiano mazuri  kwa jamii inayowazunguka  pamoja na walipa kodi.

"Kama tunavyofahamu serikali ya awamu ya sita kupitia kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa na kampeni maalumu kwa lengo la kuhakikisha kwamba TRA inakuwa na mahusiano mazuri na walipa kodi mbali  mbali na kwamba katika Mkoa wa Pwani tunatekeleza kampeni hiyo kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali.

Aidha Meneja huyo amebainisha kwamba wanatambua mchango mkubwa ambao unafanya na walipa kodi ambao wameweza kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka wa 2023 na mwaka 2024 ikiwa sambamba na kuwashukuru kwa dhati wale walipa kodi wote ambao wamekuwa mstari wa mbele katika suala zima la ulipaji wa kodi.

  Pia amesema kwamba katika kampeni hiyo wameweza kutoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo mifuko ya saruji katika zahanati ya misugusugu kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa wodi ya mama na mtoto, vifaa tiba mbali mbali katika kituo cha afya Mkoani, viti mwendo,taulo za watoto, kitanda katika Hospitali ya Kisarawe sambamba na kusaidia mipira  ya kuchezea katika shule msingi Mkoani kitengo cha elimu maalumu.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mkoani Abdulkadir Sultan ameishukuru kwa dhati TRA Mkoa wa Pwani kwa kuweza kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kutoa misaada na mahitaji mbali mbali ambayo yataweza kuwa ni  mkombozi mkubwa katika suala zima la kuwahudumia wagonjwa.

Naye Mganga mfawidhi katika  Hospital ya Kisarawe Dkt. Yona Kabata  amesema kwamba msaada ambao wamepatiwa  na TRA ikiwemo kitanda maalumu  kwa ajili ya kujifungulia wakinamama utakuwa ni mkombozi mkubwa kwani hospitali hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitanda.

Afisa Elimu kata  ya Tumbi Inocensia Mfuru  amesema msaada ambao wamepatiwa  wa viti maalumu ni moja ya hatua kubwa katika  kuwasaidia watoto hao ambao walikuwa wanapata shida  katika kutembea hivyo kutaweza kuleta mabadiliko chanya katika kuboresha sekta ya elimu hasa kwa watoto wadogo.

Mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Pwani imetekeleza kwa vitendo maelekezo ya serikali ya awamu ya sita na kufanikiwa kutembelea katika Wilaya za Kibaha, Kisarawe, na Wilaya ya Kibiti na kukabidhi misaada mbali mbali ikiwemo, vitanda kwa ajili ya kujifungulia,  mifuko ya Saruji,vifaa tiba Vitimwendo , taulo za watoto  na mipira  ya kuchezea  vyote vikiwa na thamani ya kiasi cha shilingi milioni 15.


WAFANYABIASHARA KIGOMA WAIPONGEZA TRA KWA UTOAJI WA ELIMU YA MLIPA KODI

 

Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa kwanza Kasulu Motel Co LTD kwa kuwa mlipa kodi mzuri
Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa pili,Malagalasi Enterprises & Contractors Co. LTD
Katibu tawala wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele akimkabidhi Tuzo ya Walipakodi Bora kwa Wilaya ya Kasulu kwa mwaka wa fedha 2023/2024,Mshindi wa tatu,Zabron Nashon Baroshigwa Co. LTD


Na Fredy Mgunda, Kigoma.

Wafanyabishara wa Mkoa wa Kigoma wameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kutoa elimu ya mlipa Kodi iliyopelekea  wafanyabishara kulipa kodi kwa wakati na kwa haki na kupunguza utitiri wa Kodi.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo Walipa Kodi wazuri kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Kirahumba Kivumu  mfanyabiashara aliyenyakua tuzo Bora ya mlipa Kodi Mkoa wa Kigoma alisema kuwa kwa sasa kulipa kodi limekuwa suala la kukaa mezani na kujadiliana sio vita tena kama inavyodhaniwa hapo awali na kuwaomba wafanyabishara kutunza kumbukumbu pamoja na kutoa lisiti wanapouza bidhaa na wateja kudai risiti wanaponunua bidhaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabishara Mkoa wa Kigoma Bw. Juma Chaulembo alipongeza mfumo mzima wa ulipaji kodi kuwa umesaidia kuondoa utiti wa kodi na kuwa rafiki kwa wafanyabishara wa Mkoa huo na kupongeza juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukuza uchumi wa Wafanyabishara wa Mkoa wa Kigoma.

Beatus Nchota ni Meneja wa TRA Mkoa wa Kigoma aliwapongeza wafanyabishara wote kwa kuendelea kulipa kodi kwa wakati na haki na kuiunga  mkono Serikali ya awamu ya Sita  inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la ukusanyaji wa mapato uliopelekea kukusanya bilioni 15.48 kwa mwaka wa fedha 2023/2024

Naye Bi. Julieth Nyomolelo mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa TRA alisema kuwa tuzo hizo zinalengo la kuwaongezea morali wafanyabishara kulipa kodi kwa wakati na haki ili kuchochea maendeleo ya Watanzania.


Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Kigoma Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye aliyewakilishwa na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, ambaye alisema kuwa kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kunakofanywa na TRA kumesaidia Serikali kutekeleza miradi mikubwa kwenda kwa wananchi na kuwataka wafanyabiashara kutojihusisha na biashara za magendo kwani licha ya kuinyima mapato Serikali lakini pia inasababisha kuingiza bidhaa ambazo hazina viwango na hatari kwa afya.

Dkt. Chuachua alisema kuwa Serikali ya Mkoa wa Kigoma inaipongeza Mamlaka ya TRA mkoa wa Kigoma kwa kazi kubwa ya kukusanya kodi na kufikia malengo ya ukusanyaji yaliyowekwa jambo ambalo linaifanya serikali kuweka mazingira wezeshi ya kuifanya Mamlaka hiyo kutimiza malengo yake kwa ufanisi.

Tuesday, February 18, 2025

NCAA: TUTAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU MAPANGO YA AMBONI

 


Na Oscar Assenga, TANGA

MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kwamba inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya Mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga ili yaendelee kuwavutia watalii wengi zaidi.

Hayo yalibainishwa February 14 mwaka huu na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko NCAA Mariam Kobelo wakati wa kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani katika eneo la Mapango hayo kampeni hiyo iliambatana na Mashindano ya Mapishi.

Alisema kwa sasa wana mpango wa utekelezaji wa mikakati ya kuboresha miundombinu ikiwemo mfumo wa ukusanyaji wa mapato,kujenga maeneo ya kupumzikia pamoja na uwekwaji wa kambi za wageni ambao wanakwenda kutalii na kupenda kulala hapo hapo.

“Labda niwaambie kwamba kuhitimishwa kwa kampeni hii leo itatusaidia kufungua fursa ya kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo wa ndani ya wilaya ya Tanga “Alisema Mariam.

Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha aliupongeza uongozi wa NCAA kwa kuja na ubunifu ambao kupitia kampeni hiyo imeongeza hamasa kubwa ya utalii wa ndani katika mkoa huo na hivyo kukuza utalii.

Mkuu huyo wa wilaya aliwahaidi mamlaka hiyo kwamba Serikali ya wilaya hiyo itaendelea kushirikiana nao kuendeleza na kutunza mapango hayo ya pekee .

“Lakini niwapongeze uongozi wa NCAA kwa kuweza kuinua hadhi ya Mapango ya Amboni ambayo ni kuvutia kikubwa kwa watalii kutoka nje na ndani kutembelea hivyo kutokana na hamasa hii tutaweza kuongeza pato la nchini”Alisema

WASANII WA FILAMU,WANAHABARI WAZAWA WA MKOA WA TANGA WATUA KUHAMASISHA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA

 




Na Oscar Assenga, TANGA

MABALOZI 23 wa Mkoa wa Tanga unaoundwa na Wasanii wa Filamu,Waandishi pamoja na watangazaji wametua Jijini Tanga kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Kupiga kura .

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari leo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga Ramadhani Omary alisema wameamua kujikusanya kwa pampoja kuja mkoani kwao kuleta hamasa kwenye dafrati la kudumu la wapiga kura.

Alisema kwamba watu wanapozungumzia mkoa wa Tanga hawawezi kuacha kuitaja Bandari,Zao la Mkonge ,Reli na Viwada na ukiangalia Bandari,Reli ndio ina hudumia viwanda na Rais Dkt Samia Suluhu ameweka fedha nyingi kwa ajili ya upanuzi kwenye Bandari ya Tanga .

Aidha alisema pia mkakati wa kuiboresha reli kuelekea mkoa wa Arusha na ambao itaifungua mkoa wa Tanga na serikali ina mkakati baada ya ubinafsishaji wale watu ambao hawakuviendelea viwanda vitarudi chini ya Serikali.

“Waliposikia Rais Dkt Samia Suluhu anatarajiwa kuja Tanga nao wakaamua kuja nyumbani kumpokea tutashiriki kwenye maandalizi na tutakuwepo Tanga muda wote mpaka Rais atakapowasili na leo tumeona tuhabarisha umma kupitia nyie wanahabari”Alisema

Awali akizungum za Chuchu Hans alisema kwamba wameungana na mabalozi wa Tanga na wao ni watu wa kujituma wana vipaji vingi ikiwemo ukarimu na wao wanawakilisha wenzao.

“Tumeona ni muda sahihi na umefika wakati wa kujiandikisha na tukaona tutumia nafasi hii kuhamasisha wananachi na sisi kuja kujiandikisha kwenye Daftari lakini pia Rais anakuja”Alisema

Hata hivyo aliwaomba wananchi amba bado hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupigia kura wakajiandikishe vituo vyote vipo wazi hivyo watumie haki yao ya msingi kwa ajili ya baadae kuwachagua viongozi wao.

Awali akizungumza katika mkutano huo na wanahabari Salim Awadhi “Gabo”- alisema wao wamekuja kuwakilisha wenzao kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema kwasababu mkoa wa Tanga ni watu wa ukarimu wao wameliona wabebe jukumu hilo kumsaidia Mkuu wa Mkoa huo Balozi Batilda Burian ambaye amekuwa kinara wa maendeleo kwenye mkoa huo.

Hata hivyo kwa upande wake Maliki Bandawe ambaye ni Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la TNG alisema wameamua kurudia Tanga ili kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lakini pia kutoa hamasa na kuwakumbusha vijana kujiandikisha kwenye daftari hilo.

“Wana Tanga tujitokezeni kwenye mapokezi ya Rais Dkt Samia Suluhu anakuja kwa mara ya kwanza baada ya kupitishwa na CCM kuwa Mgombea Urais kwenye uchaguzi Mwaka huu 2025”Alisema

Akielezea malengo ya ziara hiyo, Kiongozi wa Msafara Khalidi Swalehe alisema msafara huo mabalozi 23 kutoka mikoa tofauti wote ni wazawa wa mkoa wa Tanga ambao wanaitumia kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na mapokea ya kumlaki Rais Dkt Samia Suluhu.

“Naombeni wakazi wa Tanga waunge mkono na tulichokuja kukifanya ni kuhamasisha watu kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la kupiga kura na kuhakikisha tunaunga mkono jitihada za maendeleo kwa mkoa wa Tanga zinaofanywa na Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda akimuwakilisha Rais Dkt Samia”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba mkoa huo umeendelea kuamka kwa maana Tangu Tanzania ipate uhuru ilikuwa inasifika na kuna miradi mingi ya maendeleo imefanywa na Rais Dkt Samia Suluhu na wao wanahamasisha yale yanayopaswa kwenda masikioni mwa watu.

HAMOUD JUMA AWAHIMIZA CCM KUCHANGAMKIA FURSA ZA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 
Mjumbe wa Halmashauri kuu  ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Taifa Hamoud Juma (MNEC) kupitia wazazi katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025  amezihimiza jumuiya zote za wazazi pamoja na wananchi kuhakikisha wanatumia siku zilizobaki kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ambalo linatarajiwa kufikia tamati  Februari 19 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na  mwenendo mzima wa zoezi linaloendelea la uboreshaji wa daftari hilo amebainisha kwamba jumuiya za wazazi  pamoja na wanachama wote wa CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujitokeza kwa wingi  ikiwa pamoja na kuwahimiza wananchi wengine ambao walikuwa bado awajakwenda kujiandikisha kutokana na sababu mbali mbali.

Juma  amesema  kwamba kuna umuhimu mkubwa sana katika kushiriki kikamilifu katika daftari hilo ikiwa linakwenda sambamab na kuboresha taarifa za muhusika pamoja na kuwaandikisha watu wapya wengine ambao wameweza kutimiza umri wa miaka 18 na kuendeleoa amabpo hapo awali hawakuwemo kabisa katika daftari hilo.

"Nipende kuchukua fursa hii ya kuziimiza jumuiya zote za wazazi katika Mkoa wa Pwani  pamoja na wanachama na viongozi wa kutumia fursa katika siku ambazo zimesalia katika kujiandikisha katika daftari hilo la kudmu kwani ni muhimu sana hasa kaatika kuelekea katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupataa viongozi wa nafasi mbali mbali ikiwemo Urais,wabunge pamoja na nafasi za wabunge mbali mbali,"alisema Mnec Juma.

Katika hatua nyingine amemewakata  viongozi wa jumuiya mbali mbali hususan wazazi pamoja naa wanachama wote wa chama cha mapinduzi (CCM) kutofanya makosa hata kidogo na badala yake wanatakiwa wajipange mapema na kuwa na umoja na mshikamano wa kutosha katika kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,wabunge  pamoja na madiwani wote wa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Monday, February 17, 2025

SEKTA YA UTANGAZAJI INAZIDI KUKUWA MKUTANO WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI NCHINI 2025 WABAINI

 NA ALBERT G. SENGO/DODOMA

Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na Jembe Fm mara baada ya kumalizika Mkutano wa mwaka wa vyombo vya Utangazaji, uliofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.