ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 11, 2011

WIKIENDI HIYOOOOoooooooo.......!!!!

jAmANi WIkiEnDi sI nDO hII HApA nA stONe cLUb nDIYo kIWANja cHETuUUUU TUKUTANE PARE-PARE ....... CHUKUWA HIYO!

TSUNAMI YATOKEA JAPANI BADAA YA TETEMEKO KUBWA

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kaskazini-mashariki mwa Japan, na kuibua mawimbi ya tsunami ambayo yamesababisha hasara kubwa. Televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.

Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.

Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya maeneo ya biashara na makazi ya watu eneo la pwani ambapo kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 yamezuka na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi.

Kwa hisani ya mitandao.

TAREHE 8MACHI MWANZA ILIVYO ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Pamoja na kwamba tumeadhimisha miaka 100 ya siku ya wanawake duniani ikiwa ni nia ya kukomesha na kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa dada zetu na mama zetu.Mama huyu mwenye watoto watatu sikio lake hili pamoja na sikio la upande wa pili yamekatwa na mumewe katika ugomvi wa kifamilia na kumwachia ulemavu wa kudumu, mume anadai kuwa 'Ni mke wake amemtolea mahali hivyo atamfanya anavyotaka'.

Wakati hadhira ikiendelea kutafakari kuhusu kilichompata mwanamke huyo kwa kula burudani kutoka kundi la Bwela Masonga toka kata ya Kisesa binti wa miaka 13 ambaye sasa ni mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Isangijo, anasimulia kisa cha kuhuzunisha kilichompata kabla ya kupata msamalia mwema anayemsomesha sasa.Amekaa katika familia hiyo kwa muda wa miezi mi4, watoto wa familia hiyo wakiwa na kawaida ya kukojoa kitandani, Ikatokea siku moja naye akajikuta kakojoa kitandani, mwajiri wake akamwambia atamwonyesha gharama za ukojozi wake. Mwajiri huyo alichemsha kisu kwenye moto na kumchoma nacho sehemu za siri huku akimwonya ole wake akimwambia mtu.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Diwani wa viti maalum Hilda Komanya akipitia kipengere baada ya kipengere risala iliyosomwa.

Kwaya ya mazuzule ikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kijiji cha Isangijo wilayani Magu.

Kama ilivyo jamii nyingine kukusanyika katika maeneo mbalimbali duniani kuadhimisha siku hii na sasa maadhimisho yanatimiza miaka 100, kwa style hii jamii isipo badilika tutegemee kusherehekea miaka mingine 100 tukisimuliana mabaya zaidi ya haya tuyaonayo. 'Ukombozi lazima uanze na jamii'.

MJI WA MAGU NA MAZINGIRA.

Hata wakazi wa town senta ya mji wa magu hutumia kuni kupikia na kuchemshia maji, ukosefu wa nishati mbadala sababu kubwa ya ukataji miti hovyo ndani ya hifadhi ya msitu wa Sakaya hali ambayo inatishia kukauka kabisa kwa mto Simiyu unaotiririsha maji yake ndani ya ziwa Victoria.

Bei ya kuku soko la Magu ni shilingi 4,000/= hadi 5,000/=

Ni asubuhi tuliiiiivu! pozi la kugombania magari barabarani 'Gari langu hilooo!' kutoka kushoto ni viongozi wetu wa kesho Simon, Jose, Charles na Jane.

Ni mwendo kulishwa kondoo kwa wanaoagiza supu hasa ya mbuzi. (limenitokea)

Mjini hapa ukiuliza daladala, basi utaelekezwa hapa. Nauli maelewano ni kati ya 100, 200 au 300 kutokana na umbali wa eneo hadi eneo, wala hazipandi kama zile za Sumatra.

Licha ya kuwa karibu na ziwa upatikanaji wa maji wilayani Geita bado Inshu'

Kanisa la Kakobe (full gospel) la mjini geita na utunzaji wa mazingira.

Thursday, March 10, 2011

ELIMU.....

Kuoga humo humo, kufua humo humo, kujisaidia humo humo, kunyweshea mifugo humo humo, kuoshea vyombo humo humo na hata maji kwa matumizi ya nyumbani, kisha maji hayo yatiririka kuelekea ziwa victoria.

Kimya cha siku hizi mbili ni kutokana na semina ya waandishi wa habari kuzuia uchafuzi wa mazingira wa ziwa Victoria inayoendelea wilayani magu mkoa wa Mwanza hususani eneo la dakio la bonde la mto Simiyu, huku neti inasumbua kweli, naahidi soon kukudondoshea yaliyomo.

Mwandishi wa habari Clara Matomo wa gazeti la habari leo, ambaye ni mmoja kati ya washiriki wa semina hiyo akichukuwa data toka kwa mwezeshaji wa semina hiyo mama Anna Mdamo

Brother Makongo (aliyesimama) akimwaga dit' kwa wanahabari wenzake... Nia ya semina hii ni kuisaidia jamii ifunguke macho kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa nia ya kuokoa raslimali zilizopo ndani ya ziwa.

Tuesday, March 8, 2011

MSINICHUKIE NIMEOTESHWA WAJAMENI!!!!

LEO USIKU....Na Zzzzzz! yangu ya mchana huu:-Barca will hold the ball possession, Arsenal will do the finishing-->
1 - 0. It has been written, Barca will not see the back of the net. Go Gunners!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MIUNDO MBINU ISIPOBORESHWA YA KUMUONA BABU MLIPUKO WA MARADHI WAWEZA TOKEA.

Kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa kunatokana na kusambaa kwa taarifa za watu waliopata tiba hiyo na kupona maradhi hayo sugu, kumeibua hofu ya kutokea kwa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii. Eneo hilo hivi sasa linakabiliwa na tatizo kubwa la huduma muhimu kama vile majisafi, vyoo, nyumba za kulala na vyakula hivyo wageni hao wengi wakiwa wanakabiliwa na maradhi sugu yakiwemo kansa, kisukari, shinikizo la damu, kifua kikuu na Ukimwi.

KUHUSU TIBA:Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa tangu alipokunywa dawa hiyo, tatizo la sukari ambalo lilikuwa likimsumbua limekwisha."Sijui kama nimepona kabisa au la, lakini sasa najisikia vizuri tofauti na mwanzo," alisema kiongozi huyo. Baadhi ya watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU), ambao wamepewa dawa hiyo, licha ya kudai kuwa sasa wana hali nzuri, bado hawajapima kwani wengi waliohojiwa walikuwa hawajatimiza sharti la kukaa siku saba kabla ya kupima ili wajue kama virusi vimekwisha au la.

MZIZI WA TIBA:Mchungaji Masapila alisema dawa hiyo ambayo alioteshwa na Mungu tangu mwaka 1991 na kukumbushwa mwaka 2009, inatokana na maombi na mti wa mgariga ambao ni chakula cha twiga, unaopatikana katika viunga vya Milima ya Sonjo na kupona kwa mgonjwa haraka pia kutokana na imani yake juu ya dawa hiyo ambayo dozi yake ni kikombe kimoja tu kinachonywewa hapo hapo inakotolewa.

TAMKO LA WIZARA:Blandina nyoni ambaye ni Katibu wizara ya afya amesema tayari Wizara ya Afya, imekwishatuma wataalam wake kwenda huko kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa hiyo.

Monday, March 7, 2011

MIX TAPE YA BONTA HII HAPA.....

Bonta na Mix Tape yake inayoitwa Kila Kitu Nyerere.

Mwanaharakati huyu kasema nami leo hii na kunisikilizisha ngoma zinazopatikana ndani ya mix tape hiyo, 'Eh bana eeee! IN SHORT IKO FULL!' Na mie Ninaipa baraka zote kwako Mzalendo mwenzangu isake uimiliki kisha uisikilize. Kama vipi any time ndani ya XXL ya clouds fm itasikika kwenye 'album review'='Just kwa muonjo tu kabla haijatua sokoni rasmi'

@g.sengo

UNITED YAANGUKIA PUA, TENA

Liverpool jana imeichapa Manchester United kwa mabao 3-1, katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Anfiled.Dirk Kuyt alifunga mabao yote hayo matatu katika mchezo uliotwaliwa zaidi na Liverpool. Mabao yalifungwa katika dakika za 34, 39, na 65. Bao pekee na la kufutia machozi lilifungwa na Havier Hernandez katika dakika ya 90.

Mkali wa Liverpool ambaye bado hajaimarika vizuri kutokana na majeraha yanayo mkabiri Andy carroll (c)akichuana na beki mahiri wa man u, mfaransa Patrice Evra.

Wachezaji wa pande zote mbili katika malumbano baada ya mlinzi wa mashetani wekundu mbrazili Rafael Da Silva's kumchezea faulo mchezaji wa Liverpool ambaye pia ni mbrazili Lucas Leiva.

Mchezaji wa Manchester United Nani akiondoshwa kwa machela dimbani hapo mara baada ya kuumia kupitia kuchezewa vibaya na Jamie Carragher.

Liverpool's Dutch forward Dirk Kuyt (L) akisherehekea baada ya kutupia goli la tatu katika mchezo huo. United wanasalia kileleni wakiwa na pointi 60, huku Liverpool wakiisogelea Tottenham kwa kufikisha pointi 42, huku Spurs wakiwa na 47.

10 BORA YA MAGARI YA KIFAHARI KWA 2011

Check out this list of the 10 Best Concept Cars of 2011. Cars include the Audi e-tron, GMC Granite and other car show favorites.Audi e-tron

Citroen Survolt

Deltawing Concept

GMC Granite Concept
Jaguar C-X75

Lancia Stratos

Peugeot SR1

Pininfarina Alfa Romeo 2uettottanta

Porsche 918 Spyder

Renault Dezir