Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kaskazini-mashariki mwa Japan, na kuibua mawimbi ya tsunami ambayo yamesababisha hasara kubwa.Televisheni nchini Japan, imeonesha magari, meli na hata majengo makubwa yakizolewa na mawimbi makubwa ya maji ya bahari baada ya tetemeko lenye ukubwa wa 8.9 kupiga.
Katika mji mkuu Tokyo, usafiri wa umma umesimamishwa, lifti katika majengo mengi zimezimwa na maelfu ya watu wamekusanyika katika bustani za wazi na vituo vya treni.
Mawimbi makubwa yalipiga katika miji ya Miyagi na Fukushima, na kuharibu vibaya sehemu kubwa ya maeneo ya biashara na makazi ya watu eneo la pwani ambapo kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo limesema mawimbi yaliyofikia urefu wa mita 10 yamezuka na kupiga bandari ya Sendai huko Miyagi.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.