ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 20, 2025

MWENYEKITI CCM BAGAMOYO AONYA KUFANYA SIASA ZA KUCHAFUANA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

 


NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

Mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi  (CCM) Wilaya Bagamoyo Ndugu Aboubakary Mlawa amewataka wana CCM kuachana na tabia ya kuwa na siasa za  fitina na kuchafuana kwenye mitandao ikiwemo kwamba kitahakikisha kwamba  hakitoteua wagombea kwa mihemko ya mitaani hama  kupitia mitandao ya simu.

Mlawa ameyasema hayo  wakati wa kikao cha  mkutano wa Halmashauri kuu ya  Kata ya  Mapinga  juu kuhusiana na  utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa 2020 hadi 2025 na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama, viongozi wa serikali, pamoja na viongozi wa dini.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kwa sasa chama kimejipanga kwa ajili ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 na kuwahimiza wanachama wa ccm kuhakikisha wanawachagaua wagombea  wenye sifa ambao wataweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

"Kitu kikubwa ninawaomba wanachama na viongozi kuachana na vitendo vya kufanyiana siasa za kuchafuana na fitina na kuhakikisha wanaachana kabisa na siasa za kwenye mitandao na lengo letu kubwa ni khakikisha kwamba katika uchaguzi mkuu kuna kuwa na hali ya amani na utulivu,"amebainisha Mwenyekiti Mlawa.

Aidha Mlawa amesema kwamba  kumekuwepo  na  tabia kwa baadhi ya wana ccm kutumia  makundi ya mitandao ya kijamii kwa kuanza kulazimisha wagombea wao ndio waweze kuteuliwa  katika nafasi mbali mbali kitu ambacho amekemea vikali kwani wanapaswa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

"Kitu kikubwa ninachowaomba wana  ccm kuhakikisha kwamba msiwateuwe kabisa  watu kwa  kupitia njia za  magroup ya mitandao ya kijamii kwani pamoja na kuachana kabisa na kuwa na siasa za kuchafuana na badala yake ni kuweka mikakati madhubuti ya kumpa kura nyingi Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan aweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,"amesema Mlawa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mapinga Dismas Dismas  amesema kwamba katika kipindi  miaka mitano ameweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ambayo imeweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi kuweza kupata huduma za maji,afya, elimu pamoja na miundombinu ya barabara.

RASMI SAMIA AFUNGUWA DARAJA LA JPM KIGONGO BUSISI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisogeza kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo la Kigongo, Misungwi mkoani Mwanza tarehe 19 Juni, 2025. Daraja hilo ambalo ni sehemu ya barabara ya Usagara-Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Sirari hadi Mtukula na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipepeza bendera ya taifa kuruhusu mabasi na magari kupita kwenye daraja hilo rasmi badala ya kutumia vivuko.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipungia mkono abiria wa gari la kwanza (basi) lililopata idhini ya kufungua safari rasmi kupitia daraja hilo.

              

DIWANI KATA YA MAPINGA BAGAMOYO AACHA GUMZO YA AINA YAKE UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA KISHINDO 2020/2025

 

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO.

Zaidi ya shilingi  bilioni 3.2 zimeweza kutumika katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Kata ya Mapinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni katika  kutekeleza  ilani ya chama cha mapinduzi  CCM)  kwa kipindi cha  kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Mapinga Chandika Chandika  wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo ambayo imeweza kugusa katika  maeneo mbali mbali ikiwemo sekta  ya  afya,elimu,umeme ,maji, miundombinu ya barabara  pamoja na huduma za kijamii.

Chandika amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano kumefanyika mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi  wa mradi wa shule ya msingi ya Kiembeni iliyojengwa manamo mwaka wa 2023 katika kitongoji cha kiharaha lengo ikiwa ni kupunguza kero ya wanafunzi kusoma katika mlundikano mkubwa ambayo imegharimu kiasi cha shilingi zaidi ya  milioni 475.

Aidha Chandika amebainisha kwamba katika kipindi hicho cha miaka mitano wamezidi kuboresha sekta ya elimu ambapo mradi wa shule ya sekondari Shushila Ladwa iliyopo katika kitongoji cha Udindivu ambayo ilijengwa tangu mwaka 2022 kwa lengo la kuweza kupunguza umbari kwa watoto ambao wanatokea katika vitongoji vya udindivu, Tungutungu, Kiharaka, kiembeni pamoja na Changwahela lengo ikiwa ni kupata elimu.

"Tumeweza kupiga hatua kubwa sana katika kipindi hiki kwani tumeweza kufanya ukarabati wa vyoo vya wanafunzi pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu katika shule ya msingi kimele,pamoja na kutoa meza na madawati ya wanafunzi katika shule ya msingi kiembeni ikiwa sambamba na kuboresha mazingira kwa ajili ya kufundishia kwa walimu,"amesema Diwani Chandika.

Kadhalika amesema katika utekelezaji wa miradi ya afya katika kumefanyika mageuzi makubwa ambapo mradi wa ujenzi wa zahanati iliyopo katika kitongoji cha Tungutungu ambapo imeweza kumalizika na kwamba wananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine kuweza kupata huduma ya matibabu ikiwa sambamab na kusafanya ukarabati wa zahanati ya Mapinga.

Pia katika kipindi hicho cha miaka mitano kumefanyika upatikanaji wa dawa za kutosha pamoja na vifaa tiba, pamoja na kufanya  ukarabati  wa ujenzi wa miundombinu ya kisasa kwa ajili ya kutolea huduma katika zahanati hiyo.

Akizungumzia maendeleo makubwa ambayo yamefanyika katika miundombinu ya barabara ambapo katika eneo la barabara mbali mbali zimeweza kukarabatiwa ikiwemo ya kutokea eneo la kwa Joyful kuelekea  katika shule ya sekondari  Mapinga  kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi na wanafunzi kusafiri kwa urahisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa amempongeza kwa dhati Diwani wa kata hiyo ya Mapinga kwa kuweza kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika suala zima la kuchochea na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aidha aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kuachana na siasa za fitina na kuchafuana bila sababu yoyote na badala yake wanapaswa wanatakiwa kubadilika kwa kushikamana na pamoja hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 na kuhakikisha kwamba wanaondoa tofauti zao na kumpa kura nyingi za kishindo Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kadhalika Mwenykiti huyo amekemea vikali uwepo wa viongozi wa chama kuondoa na kumalizika kabisa migogoro mbali mbali iliyopo na kwamba kwa  kipindi hiki wanapaswa kujipanga kuanzia ngazi za chini na kushikamano kwa umoja lengo likiwa ni kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu.

Naye Diwani wa Kata ya Kiromo  Salum Mikugo amempongeza Diwani Chandika kwa kuweza kuchapa kazi kwa bidii katika suala zima la kutekeelza ilani ya chama kwa kioindi cha mwaka wa 2020 hadi 2025 na kuwahiza kuachana na mambo ya chuki na kuwahimiza waweze  kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuendeleo kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Taarifa ya utekelezaji wa chama cha mapnduzi (CCM) Kata ya Mapinga katika kipindi cha mwaka 2020hadi 2025  imeweza kusomwa na kuwasilishwa na Diwani wa Kata ya mapinda Chandika Chandika ambayo imeweza kueleza kazi na miradi mbali mbali ambayo imefanyika na kuweza kupokelewa na kukubaliwa kwa mikono miwili na viongozi na wanachama wake.

Thursday, June 19, 2025

ROOM TO READ MKOMBOZI KWA WATOTO WA KIKE MKOA WA PWANI KATIKA STADI ZA MAISHA MASHULENI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

SHIRIKA lisilokuwa la kiseriki  la Room to Read katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu limewafikia na kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha na malezi wanafunzi  wa kike wapatao 679  kutoka Mkoa wa Pwani.

Aidha shirika hilo  limeishukuru kwa dhati  serikali  kwa ushirikiano ambao umefanikisha mradi wa Usomaji na Maktaba kwa baadhi ya Shule za Msingi  na kuwezesha kupunguza changamoto ya wahitimu kumaliza wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Hayo yabebainishwa na Mratibu wa Mradi Usomaji na Maktaba kutoka Room to Read  Dickson Msuva kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Halmashauri ya Mji Kibaha.

Msuva alisema kuwa mradi huo ambao uko kwenye baadhi ya mikoa kwenye shule hizo umewarahisishia wanafunzi kujua kusoma na kuandika kwa haraka kutokana na uanzishwaji wa maktaba mashuleni.

"Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano ambapo anzishwaji wa maktaba mashuleni kumesaidia kukabili changamoto ya wanafunzi kuchelewa kujua kusoma na kuandika kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili,"alisema Msuva.

Naye Mhamasishaji Jamii kutoka Room to Read Rogathe Matulo amesema  kwamba katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora wamekuwa wakiwafundisha stadi za maisha ili kuwaongezea kujiamini.

Matulo amebainisha kwamba  wanawafundisha stadi za maisha ili wawe na maamuzi sahihi akiwa shuleni na aweze kupata elimu kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne na siyo kuishia njiani.

Shirika hilo la Room To Read linatekeza mradi huo wa kuwasaidia watoto wa kike katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam,Tanga pamoja na Mkoa wa Pwani inatekeleza katika shule nne zilizopo katika Halmashauri ya mji Kibaha.

ZAIDI YA BILIONI 4.3 ZATOLEWA KUWEZESHA MRADI WA UMEME LUPALI NJOMBE

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu (kulia) akiwasili kwenye bwawa la kuzalisha umeme mradi wa Lupali na kupokelewa na Mratibu wa mradi, Sista Imakulata Mlowe katika Kata ya Matola Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA na wadau wengine wa maendeleo Juni 18, 2025

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu (kulia) akipokea maelezo ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa Lupali kutoka kwa Mhandisi Ujenzi wa mradi, Mha. Zacharia Dandu alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA na wadau wengine wa maendeleo Juni 18, 2025

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu (kulia) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Lupali alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA na wadau wengine wa maendeleo Juni 18, 2025. Kushoto ni Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage.

   

WAENDELEZAJI WA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA LUPALI MKOANI NJOMBE WAELEKEZWA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA MRADI

 

·       Waishukuru REA kwa uwezeshaji wa zaidi ya shilingi bilioni 4.3

·       Utekelezwaji wake wafikia 97.5%


Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameelekeza waendelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa kilowati 317 kwa kutumia maporomoko ya Mto Lupali kuimarisha ulinzi na usalama wa mradi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Ameelekeza hayo Juni 18, 2025 katika Kata ya Matola Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA.

"Mradi huu hadi kufikia hatua hii umetumia gharama kubwa, na ni mradi utakaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na Taifa kwa ujumla, tuna kila sababu ya kuhakikisha unalindwa," alielekeza Balozi Kingu.


Alielekeza kujengwa kwa uzio utakaozunguka bwawa la kuzalishia umeme sambamba na kusimika mifumo ya taa na kamera maalum za ulinzi maarufu kama CCTV Camera maeneo yote muhimu ya mradi.


Sambamba na hilo, Balozi Kingu aliwapongeza kwa hatua waliyofikia na aliwaelekeza waendelezaji wa mradi huo kushirikiana kwa karibu na waendelezaji wa miradi mingine ili kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa miradi.

"Hapa mmezungukwa na waendelezaji wa miradi ya namna hii wenye uzoefu, ni vyema mkajenga utaratibu wa kuwa mnabadilishana uzoefu ili kuimarisha uendeshaji wa mradi," alisisitiza Balozi Kingu.


Akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu wa Mradi, Sista Imakulata Mlowe alitoa shukrani kwa uwezeshwaji unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na aliahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Balozi Kingu.

"Tangu kuanza kwa mradi mwaka 2011, REA imetuwezesha sehemu kubwa katika hatua zote; tunaahidi kutimiza maelekezo yote yaliyotolewa," alisema Sista Mlowe.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema hadi sasa REA imewezesha zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.


"REA imetoa ruzuku kwa awamu tofauti kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo wakiwemo benki ya Dunia na Serikali ya Sweden ili kuwezesha mradi huu tangu hatua za mwanzo za utafiti wa awali, ujenzi wa njia kuu za kusafirisha na kusambaza umeme kwa watumiaji takriban 600.


Mhandisi Advera alibainisha maeneo mengine yaliyowezeshwa na REA kuwa ni pamoja na ruzuku iliyotolewa kukamilisha mradi ikihusisha ujenzi wa sehemu ya kupokelea maji, nyumba ya mtambo, uwekaji wa mabomba pamoja na shughuli nyingine za Mradi.


Alisema kukamilika kwa mradi kutazalisha kiasi cha kilowati 317 ambazo kiasi zitatumiwa na mwendelezaji na kiasi kitakachobaki zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.


Alisema kuwa REA imeendelea kufadhili miradi ambayo itaongeza wigo wa Gridi ya Taifa ili kukuza uchumi wa Taifa kwa kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.


"REA imefadhili miradi ya uzalishaji na usambazaji nishati vijijini inayotekelezwa na taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta Binafsi kwa kutoa ruzuku pamoja na kuwezesha mikopo ya masharti nafuu sambamba na kuwajengea uwezo waendelezaji wa miradi," alisisitiza Mha. Mwijage.

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu yupo Mkoani Njombe kwa ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme inayowezeshwa na REA.

 

JUKWAA LA NNE LA UTEKELEZAJI WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI LILETE MABADILIKO -OLLAL

 

MWANZA

Wadau wa madini nchini wametakiwa kutumia Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini kama kichocheo cha mabadiliko katika Sekta ya Madini hasa kwenye eneo la ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini  katika eneo la ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini kama vile  usambazaji wa vifaa na  vyakula.

Hayo yamesemwa jijini Mwanza leo Juni 18, 2025 na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo wakati akifunga Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta la Madini.


Jukwaa hilo lililoanza mapema Juni 16, 2025 limekutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na  Wizara ya Madini na Taasisi zake, Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Taasisi za Fedha, Kampuni za Uchimbaji wa Madini na Watoa Huduma kwenye Migodi ya Madini.


Sehemu ya viongozi vinara wa mkutano.

Amesema kufanyika kwa jukwaa hilo ni mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Madini kuhamasisha ushiriki wa watanzania katika shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini na usambazaji wa bidhaa na huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ili wananchi waendelee kunufaika na rasilimali madini na kukuza uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, amezitaka kampuni za madini kuendelea kutoa kipaumbele kwa watanzania kwenye  ajira na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini.

Wakati huo huo amempongeza Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde kwa kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini hali iliyopelekea mchango wake katika Pato la Taifa kufikia asilimia 10.1.

 Jukwaa hilo lenye kaulimbiu inayosema Ongezeko la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ni chachu ya Ukuaji wa Uchumi limeambatana na maonesho yenye lengo la kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini.



Sunday, June 15, 2025

CCM KUPITISHA WAGOMBEA WENYE UWEZO UCHAGUZI MKUU- GAVU

 Na Mwandishi Wetu


KATIBU wa NEC Oganizesheni na Mafunzo CCM Issa Haji Usi maarufu Gavu amesisitiza Watanzania kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kinaendelea na mipango yake ya kuwaletea Wananchi Maendeleo.

Akizungumza wakati Kongamano la Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM Wilaya ya Temeke kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM, Gavu amesema kupitia mabadiliko ya Katiba ya chama hicho, yataiwezesha kuisimamia ipasavyo serikali kutekeleza miradi ya kijamii na ile ya kimkakati lengo likiwa ni kuharakisha maendeleo.


Kwa upande wao UVCCM Temeke imekiri kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CMM 2020/25 huku ukieleza namna Bilioni 900 zilizotolewa ndani ya kipindi cha Serikali ya awamu ya sita ambavyo zimetekeleza changamoto ya madarasa katika vyuo na vyuo vikuu nchini.

Kwa upande wake Zena Mgaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Temeke amekemea tabia ya baadhi ya vyama vya upinzani kutweza utu na kufanya vitendo ambavyo vina ashiria uvunjifu wa amani.


Wakati huo huo Ofisa Mipango kutoka Manispaa ya Temeke pamoja na Dk.Siriel Mchembe mlezi wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi vyuo vikuu vya Dar es Salaam wamesema katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, vyuo vikuu vimenufaika kwa kupata miradi ya ujenzi wa madarasa pamoja na mikopo huku Manispaa ya Temeke ikieleza kupokea zaidi ya Sh.Bilioni 268 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

MAANDALIZI KABAMBE YA JUKWAA LA 4 LA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katika kuelekea Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, CPA. Venance Kasiki, amefafanua umuhimu, malengo na matarajio ya jukwaa hilo litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni, 2025.
CPA. Kasiki amesema lengo kuu la jukwaa hilo ni kutoa fursa kwa Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini kupitia huduma na bidhaa wanazoweza kutoa kwenye mnyororo wa thamani ya madini. Ameeleza kuwa, jukwaa hilo pia litaweka mkazo kwenye ushirikiano kati ya serikali, wawekezaji na watoa huduma wa ndani, huku likipambanua fursa mpya zinazopatikana ndani ya sekta hiyo.

Jukwaa hilo litahusisha maonyesho, mijadala ya kitaalamu, mikutano ya kibiashara na majadiliano ya sera ili kuhakikisha Watanzania wanajumuishwa ipasavyo na kunufaika zaidi na utajiri wa rasilimali za madini nchini.