ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 20, 2025

DIWANI KATA YA MAPINGA BAGAMOYO AACHA GUMZO YA AINA YAKE UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KWA KISHINDO 2020/2025

 

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO.

Zaidi ya shilingi  bilioni 3.2 zimeweza kutumika katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Kata ya Mapinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni katika  kutekeleza  ilani ya chama cha mapinduzi  CCM)  kwa kipindi cha  kuanzia mwaka 2020 hadi 2025.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Mapinga Chandika Chandika  wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo ambayo imeweza kugusa katika  maeneo mbali mbali ikiwemo sekta  ya  afya,elimu,umeme ,maji, miundombinu ya barabara  pamoja na huduma za kijamii.

Chandika amesema kwamba katika kipindi cha miaka mitano kumefanyika mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi  wa mradi wa shule ya msingi ya Kiembeni iliyojengwa manamo mwaka wa 2023 katika kitongoji cha kiharaha lengo ikiwa ni kupunguza kero ya wanafunzi kusoma katika mlundikano mkubwa ambayo imegharimu kiasi cha shilingi zaidi ya  milioni 475.

Aidha Chandika amebainisha kwamba katika kipindi hicho cha miaka mitano wamezidi kuboresha sekta ya elimu ambapo mradi wa shule ya sekondari Shushila Ladwa iliyopo katika kitongoji cha Udindivu ambayo ilijengwa tangu mwaka 2022 kwa lengo la kuweza kupunguza umbari kwa watoto ambao wanatokea katika vitongoji vya udindivu, Tungutungu, Kiharaka, kiembeni pamoja na Changwahela lengo ikiwa ni kupata elimu.

"Tumeweza kupiga hatua kubwa sana katika kipindi hiki kwani tumeweza kufanya ukarabati wa vyoo vya wanafunzi pamoja na ujenzi wa vyoo vya walimu katika shule ya msingi kimele,pamoja na kutoa meza na madawati ya wanafunzi katika shule ya msingi kiembeni ikiwa sambamba na kuboresha mazingira kwa ajili ya kufundishia kwa walimu,"amesema Diwani Chandika.

Kadhalika amesema katika utekelezaji wa miradi ya afya katika kumefanyika mageuzi makubwa ambapo mradi wa ujenzi wa zahanati iliyopo katika kitongoji cha Tungutungu ambapo imeweza kumalizika na kwamba wananchi wa maeneo hayo pamoja na maeneo mengine kuweza kupata huduma ya matibabu ikiwa sambamab na kusafanya ukarabati wa zahanati ya Mapinga.

Pia katika kipindi hicho cha miaka mitano kumefanyika upatikanaji wa dawa za kutosha pamoja na vifaa tiba, pamoja na kufanya  ukarabati  wa ujenzi wa miundombinu ya kisasa kwa ajili ya kutolea huduma katika zahanati hiyo.

Akizungumzia maendeleo makubwa ambayo yamefanyika katika miundombinu ya barabara ambapo katika eneo la barabara mbali mbali zimeweza kukarabatiwa ikiwemo ya kutokea eneo la kwa Joyful kuelekea  katika shule ya sekondari  Mapinga  kwa lengo la kuweza kuwasaidia wananchi na wanafunzi kusafiri kwa urahisi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Aboubakary Mlawa amempongeza kwa dhati Diwani wa kata hiyo ya Mapinga kwa kuweza kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kushirikiana bega kwa bega na wananchi katika suala zima la kuchochea na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aidha aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kuachana na siasa za fitina na kuchafuana bila sababu yoyote na badala yake wanapaswa wanatakiwa kubadilika kwa kushikamana na pamoja hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 na kuhakikisha kwamba wanaondoa tofauti zao na kumpa kura nyingi za kishindo Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kadhalika Mwenykiti huyo amekemea vikali uwepo wa viongozi wa chama kuondoa na kumalizika kabisa migogoro mbali mbali iliyopo na kwamba kwa  kipindi hiki wanapaswa kujipanga kuanzia ngazi za chini na kushikamano kwa umoja lengo likiwa ni kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa mwaka huu.

Naye Diwani wa Kata ya Kiromo  Salum Mikugo amempongeza Diwani Chandika kwa kuweza kuchapa kazi kwa bidii katika suala zima la kutekeelza ilani ya chama kwa kioindi cha mwaka wa 2020 hadi 2025 na kuwahiza kuachana na mambo ya chuki na kuwahimiza waweze  kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuendeleo kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

Taarifa ya utekelezaji wa chama cha mapnduzi (CCM) Kata ya Mapinga katika kipindi cha mwaka 2020hadi 2025  imeweza kusomwa na kuwasilishwa na Diwani wa Kata ya mapinda Chandika Chandika ambayo imeweza kueleza kazi na miradi mbali mbali ambayo imefanyika na kuweza kupokelewa na kukubaliwa kwa mikono miwili na viongozi na wanachama wake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment