ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 16, 2018

VICHWA VYABAKI NA MASWALI KIFO CHA MFANYABIASHARA WA MABASI JIJINI MWANZA


HATIMAYE mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa mabasi jijini Mwanza Samson Josiah ambaye alikuwa mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya abiria ya Super Sami, umezikwa leo katika makaburi ya kikristo yaliyoko wilayani Magu mkoani Mwanza.

Majira ya saa 9:30 alasili mwili wa mfanyabiashara huyo ulishushwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele ikiwa ni mara baada ya ibada ya mazishi iliyotangulia ikiongozwa na Mchungaji Jackson Meza kutoka Kanisa la African Inland Church of Tanzania (AICT) kufanyika nyumbani kwake alikokuwa akiishi mtaa wa Majengo Mapya wilayani Magu.

Kwaya ya kanisa ambayo marehemu alikuwa mfadhili wake iliimba nyimbo za maombolezo zenye hisia na hata kusababisha maelfu ya wa waombolezaji wamemiminika kutoka sehemu mbalimbali kuangua kilio kwenye ibada hiyo.

Hata hivyo mwili wa marehemu Josiah haukuweza kufunguliwa katika jeneza lake na kuagwa kwa njia za kawaida kama zilivyo taratibu za imani ya kikristu kutokana na taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu kusema kuwa mwili wa ndugu yao ulikuwa umeharibika sana. 

Jembe Fm kupitia mwanahabari wake Albert G. Sengo imefanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafar Mohamed:- (FUATILIA SAUTI YA VIDEO HAPO JUU)


Mwili wa mfanyabiashara huyo uliokutwa ukiwa umefungwa kwenye viroba ukielea ndani ya Mto Ndabaka mpakani mwa wilaya za Bunda mkoa wa Mara na Busega mkoani Simiyu umewasili asubuhi ya leo Machi 16 ukitokea Hospitali ya Rufaa Mara ulikohifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi tangu juzi.

Marehemu Josia aliyezaliwa mwaka 1968 alipotea tangu Februari 27 kabla ya gari lake kukutwa likiwa limeteketezwa kwa moto ndani ya eneo  la hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara Machi 9.

MFANYABIASHARA SUPER SAMI KUZIKWA MAGU LEO

Na Mwandishi Wetu
Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu Super Sami, atazikwa leo Alhamisi Machi 16, nyumbani kwao wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza saa tisa alasiri baada ya uchunguzi wa kitatibu kukamilika.
Kaka wa marehemu Amini Sambo amesema atazikwa leo Magu Mjini baada ya kusafirishwa kutoka Musoma ambako mwili wake ulipelekwa kwa ajili ya uchunguzi.
Mfanyabishara huyo anadaiwa kutoweka Februari 27, mwaka huu nyumbani kwake eneo la Mwananchi-Buzuruga Kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza na gari lake kupatikana Machi 9, mwaka huu likiwa limeteketea kwa moto kando ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kisha mwili wake kupatikana Machi 14, mwaka huu ukiwa umefungwa kwenye viroba ndani ya Mto Rubana.
Ilielezwa kuwa siku aliyotoweka Super Sami alikuwa katika harakati za ununuzi wa nyumba katika Mji Mdogo wa Ramadi Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu eneo ambalo ni njia kuu ya kwenda mkoani Mara na jirani na lango la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limetangaza kuwashikilia watu watano ambao majina yao hayajatajwa kwa uchunguzi wa kifo cha Super Sami, huku habari za ndani ya zikieleza kuwa wanaoshikiliwa ni pamoja na watu waliohusika na kuwasiliana naye siku ya tukio ikiwa ni pamoja na kutaka kuuziana naye nyumba hiyo.

WAISLAMU NCHINI RWANDA WAPINGA VIKALI HATUA YA SERIKALI KUPIGA MARUFUKU ADHANA, WASEMA NI NJAMA ZA KUFUNGA MISIKITI.



Kwa mara nyingine tena Rwanda imepiga marufuku ya matumizi ya dhana kwenye misikiti ya Waislamu nchini humo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa zimepita wiki mbili tu tangu mamlaka jijini la Kigali kuyafunga makanisa zaidi ya 700 kwa madai ya kuzuia kelele zilizotokana na vipaza sauti wakati wa ibada.

Moja ya misikiti mjini Kigali, Rwanda ambayo inatishiwa kufungwa

Kuzuiliwa kwa adhana nchini Rwanda kumepokelewa kwa hisia tofauti na jamii ya Waislamu nchini humo, ambapo wafuasi wa dini hiyo mbali na kushtushwa na hatua hiyo wameitaja kuwa ni mbinu ya kutaka pia kufunga misikiti nchini.

MAMLAKA YA KUSIMAMIA MADAWA UGANDA YAENDELEA KUNASA DAWA BANDIA KATIKA HOSPITALI NA MADUKA

Huduma za uuzaji madawa zilivyo nchini Uganda.
Taasisi ya kudhibiti madawa nchini Uganda imeendelea kukamata madawa ambayo yamekuwa yakiuzwa katika vituo mbalimbali vya afya nchini humo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu mamlaka kuu ya kutathmini madawa nchini Uganda UNDA, kunasa madawa ya aina hiyo ambayo baadhi yalikutwa katika hospitali za serikali suala ambalo lilileta mshuko mkubwa kati ya wananchi.

Kwa mujibu wa mamlaka hayo, madawa mengi yanayouzwa na kutolewa katika vituo mbalimbali vya afya nchini humo yamepitwa na wakati, au ni madawa bandia ambayo kwa njia mmoja ama nyingine yamesababisha vifo vya watu wengi hadi sasa.

Thursday, March 15, 2018

RAIS TRUMP AMTEUA MTANGAZAJI WA TELEVISHENI KUWA MSHAURI MKUU WA UCHUMI.


Trump amteua Kudlow kuwa mshauri mkuu wa masuala ya uchumi. Mchambuzi wa masuala ya fedha katika televisheni nchini Marekani, Larry Kudlow sasa atakuwa mshauri mkuu mpya wa masuala ya uchumi katika Ikulu ya Marekani ya White house.

Kudlow amelieleza shirika la habari la AP kuwa amekubaliana na uteuzi huo wa rais Donald Trump kuhudumu kama mshauri wa masuala ya uchumi. Kudlow atachukua nafasi ya Gary Cohn ambaye alitangaza wiki iliyopita kuwa atajiuzulu nafasi hiyo baada ya kupinga mipango ya rais Donald Trump inayohusiana na viwango vipya vya kodi kibiashara. Kudlow mwenye umri wa miaka 70 ni mchambuzi mwandamizi katika kituo cha Televisheni cha CNBC.

MASAUNI AZINDUA VITUO MWENDO SITA VYA POLISI,AWAASA WANANCHI KUJIKITA KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituohivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo ikiwa vitumike katika maeneo ya mkoahuo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar esSalaam,  Lazaro  Mambosasa.  Tukio   hilo   limefanyika   leo,  jijini  Dar  es  Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni,akizungumza   wakati   wa   Uzinduzi   wa   Vituo   Mwendo   sita   vya   polisi   ambavyovimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambanana uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Tukiohilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi 

Kamishna   wa   Operesheni   na   Mafunzo   wa   Jeshi   la   Polisi,Nsato   Marijaniakizungumza   wakati   wa   Uzinduzi   wa   Vituo   Mwendo   sita   vya   polisi   ambavyovimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambanana uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi

Kamanda   wa   Kanda   Maalumu   ya   Polisi   Dar   es   Salaam,   Lazaro   Mambosasa,akizungumza   wakati   wa   Uzinduzi   wa   Vituo   Mwendo   sita   vya   polisi   ambavyovimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambanana uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.

Askari   wa   Kikundi   cha   Ulinzi   Shirikishi   kutoka   Mkoa   wa   Polisi   Kinondoni,wakimsikiliza  Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   HamadMasauni (hayupo pichani), wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisiambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia nakupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha naWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Moja   ya   Vituo   Mwendo   vya   Polisi   vilivyozinduliwa   leo   na  Naibu   Waziri   waMambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ambavyovitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia nakupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YASERIKALI -WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

VIDEO:- AFANDE SELE ATOA YA MOYONI MBELE YA MAGUFULI.


VIDEO: KWAHISANI YA AZAM TV.
Msanii wa Hip Hop Bongo, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ leo ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM mbele ya Rais Magufuli ambaye ndiye mwenyeki wa chama hicho. Afande Sele alikuwa ni kada wa chama cha ACT Wazalendo alikuwa mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro Mjini katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kabla ya kujivua uanachama wa chama hicho mwaka jana. Tukio hili limetokea katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha sigara cha Philip Morris International Limited, mkoani Morogoro.
Tazama ilivyokuwa.

DIAMOND AFANYA KUFURU UZINDUZI WA ALBUM YAKE NCHINI KENYA.

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezindua rasmi albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ jijini Nairobi na kufanya bonge la shoo akiwa na timu nzima ya WCB.
Nani tena huyu mbele ya jicho la kifisadi la Diamond Platnumz?
Albamu mpya ya Diamond imesheheni ngoma 20 kali zikiwemo alizowahi kuzitoa kipindi cha nyuma na nyingine mpya.
Mbali na WCB, wasanii wengine waliopada jukwaani na kutikisa katika shoo hiyo, ni msanii wa Marekani, Omario.



LIVE: RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA SIGARA, MOROGORO



LIVE: Rais Magufuli Azindua Kiwanda cha Sigara, Morogoro Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo machi 15 amezindua kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro. Katika uzinduzi huo ulioambatana na burudani kutoka kwa mwanamuziki Afande Sele, ambaye awali alikuwa mwanachama wa ACT- Wazalendo, kabla ya kujivua uanachama na kuhamia CCM, tukio ambalo alilifanya mbele ya Rais Magufuli katika hafla hiyo.

VIDEO:- BARCA ILIVYOIADHABISHA VIBAYA CHELSEA



Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema alihisi kwamba kichapo cha 3-0 ambacho klabu yake ilipokezwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano "hakikuwa cha haki".
Lionel Messi alifunga mabao mawili naye Ousmane Dembele akafunga moja - bao lake la kwanza akichezea Barca - na kuwasaidia miamba hao wa Uhispania kuondoka na ushindi wa jumla wa 4-1.
Mechi ya kwanza uwanjani Stamford Bridge ilikuwa imemalizika 1-1.
Matokeo hayo yaliwaondoa Chelsea kutoka kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu na msimu ujao wanakabiliwa na kibarua cha kufuzu kutokana na ushindani mkali kwenye nafasi nne za kwanza Ligi ya Premia.
"Hatuna majuto," alisema Conte.
"Ukiitazama mechi hiyo, utaona kwamba matokeo hayo hayakuwa ya haki."

Wednesday, March 14, 2018

MAGUFULI ASIMIKA JIWE LA MSINGI KWA AWAMU YA PILI UJENZI WA RELI YA KATI.








*RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UZINDUZI WA AWAMU YA II YA UJENZI WA RELI MOROGORO-DODOMA - MAKUTUPORA, AAHIDI KUJENGA LAMI IHUMWA-MANISPAA YA DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Joseph Magufuli leo ameweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa awamu ya II ya Reli ya Treni ya Umeme kutoka Morogoro-Dodoma-Makutupora katika eneo la Ihumwa,Manispaa ya Dodoma kwa kumtaka Mkandarasi **Yapi Merzeki **kutoka Uturuki kukamilisha ujenzi wa Reli hii ndani ya muda ili watanzania waanze kuona manufaa ya Reli hii ambayo itasaidia katika kukuza Uchumi wa Nchi na kurahisisha sekta ya Usafirishaji nchini Tanzania.

Mh Rais Magufuli ameongeza kuwa Reli hii yenye gharama ya zaidi ya Tsh Trilioni 4 inajengwa kwa fedha za walipa kodi bila kupata ufadhili wowote na hivyo kutoa rai kwa Watanzania kulipa Kodi ili itumike kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.Wakati huo huo Rais Magufuli ameahidi ujenzi wa barabara ya lami kutoka barabara kuu ya Dar es salaam kuingia ndani eneo la Ihumwa.

Akimkaribisha Mh Rais,Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa Majaliwa amemuhakikishia Mh Rais kwamba atasimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi CCM ili kuwaletea Watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali na kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na ujenzi wa Reli hii ya Kati. 

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa TRC Ndg Massanja Kadogosa,kwa nyakati tofauti,wameelezea mradi huu wa Reli kama kati ya miradi michache inayotekelezwa Afrika na hivyo kuiweka Tanzania katika nchi zilizopiga hatua kubwa katika sekta ya Usafirishaji.
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amempongeza Mh Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya maendeleo ambayo yanaigusa Dodoma kwa kiwango kikubwa na kuwataka wanaDodoma wachangamkie fursa za ujenzi wa Reli na maendeleo makubwa yanayotokana na Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.!

WATU NANE (08) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI WILAYANI NYAMAGANA.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 14.03.2018



¨       WATU NANE (08) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI WILAYANI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 13.03.2018 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA MABATINI KUSINI KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU NANE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.DEUS LUCAS, MIAKA 52, DIWANI WA KATA YA MABATINI - CHADEMA, 2. DANIEL MONGO, MIAKA 46, MWENYEKITI CHADEMA TAWI LA KILOLELI B”, 3. LAURENCE CHILO, MIAKA 21, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI, 4.LAMECK KAUNDA, MIAKA 38, MKAZI WA KILOLELI B, 5.JACKSON MADEBE, MIAKA 44, MKAZI WA MTAA WA MWANANCHI, 6.BI SECILIA BUTUKO, MIAKA 4O, MKAZI WA MTAA BUGARIKA, 7.MWITA SAGALI, MIAKA 38, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA NA 8.SELEMAN GABRIEL, MIAKA 45, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU LIPO KUNDI LA WATU KATI YA 200 NA 500, WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WAMEKUSANYIKA KATIKA NYUMBA ALIPOPANGA BWANA LAURENCE CHILO, HUKU WAKIWA WAMEFUNGA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA SPIKA ZA MATANGAZO. HUKU WANACHAMA  HAO WA CHADEMA WAKIDAI KUWA WAMEKWENDA KUMUHANI MWANACHAMA MWENZAO BWANA LAURENCE CHILO ALIYEPATWA NA MSIBA WA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI MIEZI SITA ILIYOPITA KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KISHA KWENDA KUZIKA NYUMBANI KWAO UTEGI WILAYANI TARIME MKOANI MARA MWAKA JANA.

AIDHA BADAE ILIDAIWA KUWA JAMBO LILILOKUWA LIKIENDELEA KATIKA KIKAO HICHO NI UGAWAJI WA KADI ZA CHAMA, KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA NA KUTOA HOTUBA. 

ASKARI WALIFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO KISHA KUWAITA VIONGOZI NA  KUONGEA NAO ILI KUWEZA KUFAHAMU UHALALI WA KIKAO HICHO NDIPO GHAFLA WALIANZA KURUSHA MAWE KWA ASKARI. ASKARI WALIWEZA KUJIHAMI VIZURI KISHA WALIFYATUA MABOMU YA MACHOZI HEWANI KUWATAWANYA NA BAADAE WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WAFUASI NANE TAJWA HAPO JUU  WA CHAMA HICHO.

KATIKA ENEO LA TUKIO KUMEPATIKANA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, KADI ZA CHADEMA ZILIZOANDIKWA MAJINA NUSU, KADI ZA CHADEMA AMBAZO HAZIJAANDIKWA MAJINA NA KADI ZILIZOANDIKWA MAJINA, MIHURI MIWILI, KARATASI TATU ZENYE MAJINA YA MAHUDHURIO NA T-SHIRT ZENYE NEMBO YA CHADEMA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMNI. UFATILIAJI WA KUHAKIKISHA MJI UNAKUWA SHWARI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA VIONGOZI WA SIASA NA WANACHAMA WAO KWA UJUMLA AKIWATAKA KUACHA TABIA  ZA HOVYO AMBAZO ZIPO KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI ZENYE LENGO LA KUONDOA UTULIVU KATIKA MKOA WETU. KWANI SUALA HILO HALIKUBALIKI NA TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. 

PIA EMEOMBA WANANCHI WAELEWE KUWA AMANI NA UTULIVU NA USALAMA MKOANI KWENTU NA NCHI YETU KWA UJUMLA NI JAMBO LA MSINGI. BILA UTULIVU, AMANI NA USALAMA HAKUTAKUWEPO NA SHUGHULI YEYOTE YA MAENDELEO ITAKAYOFANYIKA KWA HIYO TUEPUKE WALE WOTE WANAOSHAWISHI VURUGU/FUJO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU WA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

KWAHERI MWANAFIZIKIA STEPHEN HAWKING.

Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole', Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."



  • Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England
  • Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge
  • Kufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.
  • Alieleza nadharia yake kwamba 'black hole' kutoa "Miali ya Hawking" mwaka 1974
  • Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.
  • Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo

Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.

DR. HASSAN ABASS AZINDUA TOVUTI YA MISA TANZANIA, JIJINI ARUSHA


 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto) wakizindua rasmi Tovuti ya MISA Tanzania inayopatikana hapa www.tanzania.misa.org
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto)pamoja na wadau mbalimbali ambao hawapo pichani wakipata maelezo kuhusiana na Tovuti ya MISA Tanzania kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa
Sengiyumva ambaye hayupo pichani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva(kulia) kulia akiendelea kutoa maelezo mbali mbali na vitu ambavyo vinapatikana katika Tovuti ya MISA Tanzania 
 Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Tovuti ya MISA Tanzania Jijini Arusha.

Tuesday, March 13, 2018

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 8 KWA KOSA LA KUFANYA KUSANYIKO WAKIDAI KUHANI MSIBA



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi ameongea na Jembe Fm kupitia mwanahabari wake Albert G Sengo na kuthibitisha kuwa:- Ni kweli tumewasambaratisha na tutaendelea kuwasambaratisha wale wote wanaokwenda kinyume na utaratibu wa sheria"

"Ni kweli hapo mabatini leo kuna watu kama 500 hivi walikuwa wamekusanyika wakifanya shughuli za siasa, siyo kuhani msiba"

"Kuhani msiba ni sababu tu............"

"Ukiuliza wanasema Oooh Mama yangu alikufa mwaka jana hivyo wamekuja kuhani, hizi ni mbinu tu kwa hawa jamaa kufanya mikutano yao isiyo rasmi na humo ndani hawazungumzi msiba bali wanazungumza siasa tupu......."

ZAIDI SIKILIZA SAUTI HAPO JUU.

POLISI WAFURUSHA MABOMU KWENYE MSIBA JIJINI MWANZA.



NI tukio linalodaiwa kutokea leo majira ya saa kumi na nusu jioni katika mtaa wa mabatini Kusini Kata ya Mabatini Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, kwa mujibu wa wasimuliaji toka eneo la tukio wamedaiwa kuwa Polisi hao walifika nyumbani kwa marehemu Magreth Daniel na kukuta baadhi ya vijana wanaotajwa kuwa ni makada wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuanza kuwatembezea kichapo.

Pia inadaiwa kuwa baada ya kichapo hicho kutoka kwa Polisi, waombolezaji hao walianza kutimua mbio na kutokomea kusikojulikana kila mmoja.

Aidha inadaiwa kuwa katika tukio hilo, Polisi waliofika msiba hapo, wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi milioni 2.5 za rambirambi kitendo ambacho ni cha kushangaza.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka wilaya ya Nyamagana, Khalid Suleiman amesema kuwa katika tukio hilo Diwani wa Mabatini kupitia Chadema Deus Mbehe ametiwa mbaroni na viongozi wengine wanane wa Chama Cha Wafanyabiashara Wadogowadogo maarufu kama wamachinga.

"Mpaka sasa kuna Diwani wa Mabatini amekamatwa na viongozi wengine nane na mwenye msiba wamekamatwa na Polisi na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi.

"Wale (machinga) walikuja kumpa sapoti mwenzao ( Raulenci Chilo ) kwa kuwa wao wana ule mfumo wa kutoa rambirambi pale mwenzao anapopata tatizo," ameongeza Suleiman.

Diwani wa Kata ya Butiba kupitia Chadema, John Pambalu, amesikitishwa na kitendo cha Polisi kuvamia msiba huo na kuanza kupiga mabomu ya machozi jambo ambalo amedai ni mwendelezo wa uonevu unaofanywa na Polisi kwa Chadema na watanzania kwa ujumla. (tizama video hapo juu)

JEH NI KIPI ALICHOZUNGUMZA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA AHMED MSANGI FUATILIA HABARI INAYOFUATA.....

SEHEMU YA MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA NCHINI



Watu 5 wanasadikika kufa maji baada ya mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani lushoto katika kijiji cha lukozi jimbo la mlalo.

Aidha mvua hiyo kubwa iliyonyesha kaitika kijiji hicho imesababisha madhara makubwa nyumba kuanguka huku mawasiliano ya yakikosekana miundombinu ya barabara madaraja kuharibika na mabasi yanayoto dar,arusha,kilimanjoro tanga yakiekea lukozi,makose,mtae na mlalo yakishindwa kwenda safari hizo kutoka na mvua hizo.

Miundombinu mingine nguzo za umeme miundo mbinu ya maji. kutokana na mvua hizo.

MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUZI

 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo Wilayani Shinyanga (hawapo pichani) kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) akizungumza kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum akizungumza na wananchi wake wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akijadiliana jambo na mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum wakati wa mkutano na wananchi wa Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wa kujadili mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Mkuu wa Wilaya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hauypo pichani).
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum (anayemfuatia) wakisikiliza kero za wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.

MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUZI

Wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga wametakiwa kufanya subira wakati mgogoro wao wa fidia na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan Afro Asian Engineering ukitafutiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa wito huo Machi 12, 2018 kwenye mkutano na wananchi hao uliofanyikia kwenye Kitongoji cha Mahiga na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Serikali.

Mkutano huo unafuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alilolitoa Machi 11, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kahama ambapo alielezwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum kuwa wananchi wa Mahiga wana mgogoro wa muda mrefu na mwekezaji hususan kuhusiana na suala la ulipaji fidia ili kupisha mradi.

Kufuatia maelezo hayo ya Mbunge, Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Naibu Waziri Biteko kuhakikisha anafika kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi. 

Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni wakati sasa Watanzania waanze kunufaika na rasilimali zao ikiwemo madini. "Tunataka madini yawanufaishe Watanzania," alisema Rais Magufuli.

Alisema wawekezaji wakifika nchini ni lazima wahakikishe Watanzania wananufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira, kodi na tozo.

"Jukumu langu nimeamua kusimamia suala hili; Nawahakikishia Serikali iko imara kwa ajili ya kuwatetea wanyonge," alisema Rais Dkt. Magufuli.

Aliagiza mwekezaji atakayehitaji kuchimba kwenye maeneo yenye wachimbaji wadogo ni lazima kwanza akubaliane nao ikiwemo suala la ulipaji wa fidia na sio kuwafukuza.

"Suala la wachimbaji lizingatiwe kwa mujibu wa sheria. Tuwalee ndio maana tumeanzisha vituo vya mfano maeneo mbalimbali ili wajifunze," alisema.

Aidha, kwa mujibu wa Mbunge huyo ni kwamba mgogoro huo ulianza tangu Julai 2017 baada ya mwekezaji huyo kuanza shughuli zake za kuandaa mazingira ya kuchimba bila kuwa na makubaliano maalum na wananchi hao.

Akiwa katika mkutano na wananchi hao, Biteko alielezwa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kutoridhishwa na kiasi cha fidia kilicholipwa ili kupisha maeneo yao kwa ajili ya mwekezaji, wengine kutohitaji kabisa fidia na maombi ya baadhi yao kuruhusiwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uchimbaji kwenye maeneo husika.

Biteko aliwataka kufanya subira wakati Serikali inatazama namna bora ya utatuzi wa hoja zao kwa mujibu wa sheria ili manufaa yapatikane bila kumuonea yoyote.

Alisema Rais Dkt. John Magufuli anataka kuona Watanzania wanyonge wananufaika na rasilimali zao ikiwemo rasilimali madini.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ni Serikali inayowaangalia wanyonge. Nimesikiliza kero zenu nitazifikisha na hatua itachukuliwa kwa mujibu wa sheria. Mfanye subira," alisema Biteko

Aliongeza kuwa Serikali haipo tayari kuona Watanzania wanyonge wanateseka na kwamba wakati umefika wa wao kunufaika.

Alifafanua kuwa suala lao litashughulikiwa kwa wakati na kwa kuzingatia Sheria ili haki itendeke pasipo kumuumiza yoyote.

Hata hivyo aliwakumbusha wananchi hao kuhakikisha wanafuata utaratibu na sheria ili manufaa yapatikane bila kuleta madhara yoyote.

Aidha, kwa mujibu wa Mthamini wa Wilaya ya Shinyanga, Devotha Njella ni kwamba wananchi waliofanyiwa tathmini ni 500 na kwamba bado mwananchi mmoja mwenye heka 25 na nyumba 6 ambaye alikataa.

Alifafanua kwamba malipo hayo ya fidia yalifanyika kwa awamu mbili na kwamba katika awamu ya kwanza Shilingi 953,194,050.75 zililipwa na awamu ya pili kiasi kilicholipwa ni Shilingi 472,413,686.32 na kwamba bado kiasi cha Shilingi 208,886,951.01 ambacho taratibu za kulipa zinaendelea.