NI tukio linalodaiwa kutokea leo majira ya saa kumi na nusu jioni katika mtaa wa mabatini Kusini Kata ya Mabatini Wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, kwa mujibu wa wasimuliaji toka eneo la tukio wamedaiwa kuwa Polisi hao walifika nyumbani kwa marehemu Magreth Daniel na kukuta baadhi ya vijana wanaotajwa kuwa ni makada wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuanza kuwatembezea kichapo.
Pia inadaiwa kuwa baada ya kichapo hicho kutoka kwa Polisi, waombolezaji hao walianza kutimua mbio na kutokomea kusikojulikana kila mmoja.
Aidha inadaiwa kuwa katika tukio hilo, Polisi waliofika msiba hapo, wanadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi milioni 2.5 za rambirambi kitendo ambacho ni cha kushangaza.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka wilaya ya Nyamagana, Khalid Suleiman amesema kuwa katika tukio hilo Diwani wa Mabatini kupitia Chadema Deus Mbehe ametiwa mbaroni na viongozi wengine wanane wa Chama Cha Wafanyabiashara Wadogowadogo maarufu kama wamachinga.
"Mpaka sasa kuna Diwani wa Mabatini amekamatwa na viongozi wengine nane na mwenye msiba wamekamatwa na Polisi na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi.
"Wale (machinga) walikuja kumpa sapoti mwenzao ( Raulenci Chilo ) kwa kuwa wao wana ule mfumo wa kutoa rambirambi pale mwenzao anapopata tatizo," ameongeza Suleiman.
Diwani wa Kata ya Butiba kupitia Chadema, John Pambalu, amesikitishwa na kitendo cha Polisi kuvamia msiba huo na kuanza kupiga mabomu ya machozi jambo ambalo amedai ni mwendelezo wa uonevu unaofanywa na Polisi kwa Chadema na watanzania kwa ujumla. (tizama video hapo juu)
JEH NI KIPI ALICHOZUNGUMZA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA AHMED MSANGI FUATILIA HABARI INAYOFUATA.....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.