ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 12, 2014

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAIZAWADIA TIMU MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA VIJANA WA MITAANI ZAWADI YA ENEO LA ARDHI KWA KIWANJA CHA MICHEZO.

Mabingwa wa dunia Timu ya vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy wakiwasili katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa MOIL Aritaf Mansoor aka Dogo ambaye pia ni Rais wa TSC Academy akiwa amelinyanyua juu kombe la Dunia kwa vijana wa mitaani lililotwaliwa na TSC Academy ya Mwanza Tanzania wakati wakuingia katika himaya ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo ameongoza maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza katika mapokezi ya Timu ya Watoto wa mitaani TSC Academy ambao ni mabingwa wa dunia iliyowasili leo nyumbani jijini hapa ikiwa ni majira ya saa nane mchana ikitokea mjini Dodoma ambako pia ilipata fursa ya kutembelea Bunge la Katiba linaloendelea sanjari na kulionyesha kombe hilo kwa waheshimiwa.
Licha ya Ofisi yake kuwazawadia wachezaji hao pamoja na benchi lake la ufundi kiasi cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu kumi (kila mmoja akipata sh 110,000/=) Ndikilo ameyanyooshea kidole makampuni yanayosita kuwekeza kwenye michezo akisema kuwa hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa, licha ya hayo bado suala la Mwanza kukosa timu ligi kuu soka Tanzania Bara linamuumiza kichwa mkuu huyo..(MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY HAPA CHINI)

Katika mapokezi ndani ya uwanja wa michezo Nyamagana, Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia mkurugenzi wake Hassan Hida aliyekuwa ameambatana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Stanslaus Mabula, imeahidi kutenga eneo la ardhi kama zawadi kwaajili ya kujengwa kiwanja cha soka kwa kituo cha TSC.


Kampuni ya MOIL kupitia Mkurugenzi wake Aritaf Mansoor imetoa kiasi cha dola elfu moja kwa kila mchezaji. Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo amewazawadia kila mchezaji na viongozi full set ya kingamuzi bora cha Continental. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo akinyanyua juu kombe la dunia lililo twaliwa na Vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy cha jijini Mwanza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Brazil.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akinyanyua juu kombe la dunia lililo twaliwa na Vijana wa mitaani wa kituo cha TSC Academy cha jijini Mwanza kwenye mashindano hayo yaliyofanyika nchini Brazil.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evaristi Ndikilo akimvisha taji mwenyekiti wa vilabu mkoa wa Mwanza John Kadutu aliye ambatana na timu hiyo nchini Brazil na hatimaye kuibuka mabingwa wa dunia kombe la vijana wa mitaani. 
Mataji kwa wachezaji walio iletea sifa Tanzania.
Mambo kadhaa yamejitokeza leo wakati wa hitimisho la mapokezi ya Mabingwa hao jijini Mwanza moja kati ya yale yaliyowavutia wengi ni simulizi ya changamoto walizokutana nazo kuanzia uongozi wa timu hiyo na hadi wachezaji Mutani Yangwe ni Mkurugenzi wa TSC Academy na hapa anasimulia (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA ALICHOSEMA).


Kushoto huyu ndiye kijana aliye pachika mabao matatu ya ushindi yaliyoipatia ubingwa TSC. 
Kocha wa timu hiyo mabingwa wa dunia Suleiman Jabir kutoka Zanzibar amewashukuru uongozi wa TSC kwa kumwamini na kumkabidhi timu licha ya mkoa kuwa na makocha wengi wenye ubora lakini anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia uwezo akili na maarifa kuwaongoza vijana wenye vipaji na hatimaye kuliletea taifa la Tanzania sifa alimaliza na kusema "Muungano Oyeeeeee!!!" kauli ambayo ilishangiliwa kwa nguvu na maelfu ya wahudhuriaji.
Ngoma wa muziki wa ngoma asili kutoka kwa wataalamu wa muziki wa asili kutoka Bujora Mwanza Tanzania.
Bango lajieleza.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Antony Diallo amewazawadia kila mchezaji na viongozi full set ya kingamuzi cha Continental na hapa mkuu wa mkoa alikuwa akikabidhi ikiwa ni zamu ya kocha wa timu hiyo mabingwa wa dunia Suleiman Jabir kutoka Zanzibar.
Moja ya engo ya mahudhurio ndani ya Nyamagana stadium Mwanza.
Picha ya Pamoja.

HONGERA FAMILIA YA BW & BI DAVID SIMBA KWA MTOTO.

Familia ya Bw & Bi David Simba wa Mwanza Tanzania wakiwa na furaha kubwa wanamshukuru Mungu kwa mtoto wao kipenzi aitwaye Rainha kwa kutimiza umri wa mwezi mmoja na nusu, wakiwa na matumaini kuwa Mwenyezi Mungu ataendelea kuwalinda na kuwapigania katika malezi hatimaye kuwa na mwana bora wa familia na jamii kwa ujumla.

Wanasema aksante kwa wale wote majirani, ndugu na marafiki wa kweli wanao wakumbuka kwa sala na maombi. Wakihitimisha kwa kusema Mungu awabariki.....
Amen. 

Friday, April 11, 2014

PICHA ZA AJALI YA BASI LA SMART ENEO LA LUGOBA AMBAPO WATU 2 WAMEFARIKI DUNIA.

Basi la smart likiwa limepinduka eneo la Lugoba
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata mshtuko
Watu wawili Wamefariki Dunia Kutokana na Ajali ya Basi la Smart Asubuhi Ya leo.
Basi Hilo Lililokuwa likitokea Jijini dar es salaam Kuelekea Mombasa Nchini Kenya Limeacha Njia Na Kupinduka na Kusababisha Vifo vya watu Wawili pamoja na Kujeruhi abiria wanaokadiriwa kufika 20. Ajali hiyo imetokea katika Eneo la Mkata na Lugoba  Barabara Kuu ya Chalinze Segera.
PICHA NA HABARI: DJ SEK BLOG

MABONDIA MIYEYUSHO, CHEKA, KING CLASS MAWE WAPIMA UZITO KUPAMBANA JUMAMO.

Bondia Mustafa Dotto kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'KIng class Mawe' kabla ya kuzipiga katika ukumbi wa PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi katikati ni Promota Jay Msangi. 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Mustafa Doto utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam.
Bondia Sukkasem Kietyongyuth kushoto akiwa na kocha wake Win Panyaparichot wakati wa upimaji uzito
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi. 
Bondia Sukkasem kietyongyuth kutoka Tahiland akituishiana misuli na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika PTA Sabasaba April 12 siku ya jumamosi. 
Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba kushoto ni bondia Gavad Zohrehvand wa Iran.

Baadhi ya waandishi wa habari na taswira yao kikazi zaidi.

Na Mwandishi Wetu
 Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi' Mawe naBondia SukkasemKietyongyuth  kutoka Thailand wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya April 12 katika ukumbi wa PTA Sabasaba

Mpambano huo wa raundi kumi utasindikizwa na mabondia Fransic Cheka na bondia Gavad Zohrehvand wa Iran atakayecheza raundi 8, mbali na mapambano hayo kutakuwa na mpambano mwingine utakao wakutanisha mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atakaye pambana na Mustafa Doto mpambano wa Raundi sita.


Pia kutakuwa na mapambano mengi ya utangulizi yatakayo sindikiza mchezo huo katika ukumbi wa PAT Sabasaba Dar es salaam ambapo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile:- Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Chachu zaidi ni kwamba kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha.

KUELEKEA LISBON UEFA 2014 REAL MADRID, CHELSEA ZACHENGANA: CHAMPIONS LEAGUE SEMI-FINALS DRAW.

UEFA-Champions League-Semi-Final-Draw-12

Atletico Madrid vs Chelsea Real Madrid vs Bayern Nusu fainali ya kwanza kupigwa April 22 and 23, ya pili kufanyika April 29 and 30. Jiandae kuona kandanda la nguvu lenye ushindani.

Chelsea’s dramatic victory over Paris St Germain and Real’s narrow aggregate win over Borussia Dortmund in the quarter-finals earned both a place in the last four of Europe’s premier club competition, where they are joined by Barcelona’s conquerors Atletico Madrid and holders Bayern Munich, who beat Manchester United.
Mourinho, 51, left Madrid in acrimonious circumstances in the summer – having led them to the 2011/12 La Liga title during his three-year reign – to rejoin Chelsea, who he led to two Premier League titles and an FA Cup victory during a successful spell from 2004 to 2007.
The Portuguese has faced Real four times in Europe as a manager, all during his time as Porto boss, and has never beaten them, losing three of the matches and drawing the other.
Diego Simeone’s men, despite the absence of star striker – and Chelsea’s main summer target – Diego Costa, ended Barcelona’s six-year run of semi-final appearances with a thoroughly-merited 2-1 agreate triumph on Wednesday.
Like Chelsea, Atletico are still on course for the dream Double of domestic crown and the Champions League, although the two-legged tie will represent their first semi-final appearance in the main European competition since 1974.
Jose Mourinho’s side, chasing a third final in seven seasons, are away at the Vicente Calderon in the first leg.
Atletico have a one point lead at the top of La Liga and defeated Spanish rivals Barcelona in the quarter-finals.
Nine-time winners Real are at home to holders Bayern in the first leg, to be played April 22-23.
The clash has extra spice as on-loan Chelsea goalkeeper Thibaut Courtois could line up against his parent club for Atletico, despite suggestions that Mourinho would try to block the Belgian from playing – unless Atletico paid hefty compensation.
In the other semi-final draw, Bayern Munich will face Real Madrid, meaning Chelsea could face the winner of either of those two in the final in Lisbon.

BILIONEA WARREN BUFFET AMWAGA MABILIONI KUPAMBANA NA UJANGILI TANZANIA.

BILIONEA namba tatu duniani Warren Buffet, ametoa misaada mbalimbali kwa Wizara ya Maliasili na Utalii yenye thamani ya bilioni nane kwa ajili ya kupambana na ujangili katika mbuga pamoja na mapori ya akiba.
Bilionea Buffet ametangaza ufadhili wake huo wakati akizungumza katika hafla maalumu iliyofanyika katika Chuo cha Taaluma cha Wanyamapori cha Pasiansi, kilichopo Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.
  
Msaada wa  bilionea huyo kupitia taasisi yake ya Warren G Buffet ni pamoja na ununuzi wa Helkopta mbili aina ya R44,ambazo zitakamilika katika kipindi cha miezi sita pamoja na mafunzo kwa marubani wanne,kugharimia wataalamu elekezi,magari matano aina ya Landcruiser.

Tajiri huyo raia wa Marekani pia amegharimia ukodishaji wa Helkopta ambayo tayari imeanza kazi katika pori la Selou,wakati ikisubiri kukamilika kwa utengenezaji wa Helkopta mpya mbili ambazo zimeaagizwa toka nchini Marekani.

Bilionea Buffet pia amegharimia uhifadhi na utafiti wa duma katika hifadhi ya Serengeti na kutoa kiasi cha shilingi bilioni 2.2.

Taasisi nyingine ambayo imenufaika na ufadhili wa bilionea huyo ni Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi ambao watajengewa mabweni sita yenye thamani ya shilingi bilioni 2,282,000/= kwa ajili ya wanachuo 300.

Chuo hicho pia kitanufaika kwa kununuliwa mabasi mawili yenye thamani ya shilingi milioni  490,960,000/=,malori mawili aina ya Scania yenye thamani ya shilingi milioni 240,590,000/=,darubini 24 zenye thamani ya shilingi milioni 24.

Naye Waziri Nyalandu alisema kuwa Wizara yake imejipanga kikamilifu kupambana na ujangili kw adhati na kawme haitaweza kurudi nyuma kwa suala lolote lile hadi pale itakapotokomeza ujangili.

AIRTEL "Smart Phone" OFA PATA SAMSUG S5 LEO

Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akionyesha simu ya Aina ya Samsung S5 mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu hityo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

Airtel "Smart Phone" Ofa Pata Samsung S5 Leo
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na  kupata dakika 1500 bure , SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”

Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu  za smart phones yaliyoko nchi nzima.

Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde.

AMREF HEALTH AFRICA LAUNCH ITS NEW IDENTITY.

Country Director, AMREF, Dr. Festus Illako cutting the ribbon during the AMREF Health Africa launch new identity. The frame Ceremony held yesterday April 10, 2014 AMREF office in Dar es Salaam, Tanzania.
Country Director, AMREF, Dr. Festus Illako with Amref Health Africa staff during the new identity launch
---
AMREF, the leading international African organisation in health today rebranded to Amref Health Africa after 57 years as the African Medical and Research Foundation.
A key reason for the rebrand is to ensure that our name more accurately reflects the nature and scope of our work, which has grown beyond research and provision of basic medical services to strengthening of health systems through training and capacity building and strategic programming in areas such as maternal and child health, HIV, Water and Sanitation, TB and Malaria, and clinical and diagnostics services.

“Our new name exemplifies our commitment to improving health in Africa through a wide a range of critical programmes and services so that we can achieve lasting health change for the people of Kenya and Africa in general,” said Director General Dr Teguest Guerma.

Although we are rebranding, our focus remains the same: communities continue to be the primary beneficiaries of our work. Our rebrand will in effect put us in a more strategic position to continue working with our partners and aligning ourselves as an African-led and Africa-based health organisation seeking to meet the needs of the most vulnerable populations on the continent.

Since 1957, Amref Health Africa has been providing health services to the most vulnerable communities, working in partnership with a cross-section of stakeholders including governments. With seven offices in Africa and 10 in Europe and North America, Amref Health Africa reaches over 30 countries with its work and has impacted the lives of millions of people living in hard-to-reach parts of Africa.

Thursday, April 10, 2014

MKUTANO WA 32 WA SEKTA YA FEDHA,SOKO LAMITAJI NA MIFUKO YA JAMII (CISNA) WAFUNGULIWA JIJINI DAR.

Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Mkutnao huo umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka (kushoto) akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama Masinda akieleza jambo wakati Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA),Oaitse Ramasedi (wa tatu kushoto) akiongoma Mkutano huo unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

MWANZA KUWA NA KIWANDA CHA KWANZA CHA DAWA ZA BINADAMU.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akizungumza na kusanyiko la uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akiweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Pamoja na kuelezea mikakati ya jinsi uongozi na wafanyakazi walivyo jipanga kwaajili ya kufanya kazi kwa ufanisi ili kufikia malengo, Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical, Bwana Prince Hetal Vithlani alimaliza maelezo ya mipango yake kwa kutoa mchango wa Mifuko 100 ya Sementi kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara za Sekondari wilayani Nyamagana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo pamoja na msafara wake uliojumuisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga pamoja na madiwani na viongozi wengine ulipata nafasi ya kutembelea idara mbalimbali za uzalishaji kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Phamaceutical.
Hatua kwa hatua wakipata maelezo ya mashine za utengenezaji dawa.
Moja ya mashine zilizosimikwa kiwandani hapa kwaajili ya uzalishaji dawa.
Ufafanuzi kwa kina.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alivutiwa na uwekezaji huu wa kwanza kufanyika jijini Mwanza.

Anaonekana kikamilifu (katikati mwenye suti nyeusi) ni mshereheshaji Maarufu jijini Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Ma-Mc wa Mwanza Mc Baba Paroko.
Mitambo.
Uzalishaji kwa majaribio tayari umekwishaanza na hii ni moja kati ya sample zitakazo oneshwa kwa wakaguzi wa Viwanda, Chakula na Madawa watakao dhuru kiwandani hapa hivi karibuni kwa ajili ya ukaguzi ili uzalishaji upate kuchukuwa nafasi.
Korido ndani ya kiwanda hicho chamadawa.
Meza kuu ikijadili ya msingi, wa pili kutoka  kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, akitete na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Prince Hetal Vithlani na mwisho anaonekana Kaimu meneja wa TFDA Moses Mbambe.


MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wamiliki wa viwanda katika mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya viwanda kabla yakufikiria watu kutoka mbali.

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana.
Ndikilo amesema haiwezekani hata ajira kama za kukata majani badala yakuwapa wananchi wanaozunguka maeneo haya mkaenda kutafuta mtu kutoka mbali, kwani kwa kufanya hivyo mtawafanya wananchi hawa wasiwe rafiki wa kiwanda na wakati mwingine wanaweza kufanya uhujumu.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze  kukifungua kiwanda hicho mapema na  shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja. " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu  wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" Huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.
Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho Prince Hetal Vithlani, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,
Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali  kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.
Prince Phamaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.