ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 10, 2014

MWANZA KUWA NA KIWANDA CHA KWANZA CHA DAWA ZA BINADAMU.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akizungumza na kusanyiko la uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akiweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Pamoja na kuelezea mikakati ya jinsi uongozi na wafanyakazi walivyo jipanga kwaajili ya kufanya kazi kwa ufanisi ili kufikia malengo, Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical, Bwana Prince Hetal Vithlani alimaliza maelezo ya mipango yake kwa kutoa mchango wa Mifuko 100 ya Sementi kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara za Sekondari wilayani Nyamagana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo pamoja na msafara wake uliojumuisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga pamoja na madiwani na viongozi wengine ulipata nafasi ya kutembelea idara mbalimbali za uzalishaji kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Phamaceutical.
Hatua kwa hatua wakipata maelezo ya mashine za utengenezaji dawa.
Moja ya mashine zilizosimikwa kiwandani hapa kwaajili ya uzalishaji dawa.
Ufafanuzi kwa kina.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alivutiwa na uwekezaji huu wa kwanza kufanyika jijini Mwanza.

Anaonekana kikamilifu (katikati mwenye suti nyeusi) ni mshereheshaji Maarufu jijini Mwanza ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Ma-Mc wa Mwanza Mc Baba Paroko.
Mitambo.
Uzalishaji kwa majaribio tayari umekwishaanza na hii ni moja kati ya sample zitakazo oneshwa kwa wakaguzi wa Viwanda, Chakula na Madawa watakao dhuru kiwandani hapa hivi karibuni kwa ajili ya ukaguzi ili uzalishaji upate kuchukuwa nafasi.
Korido ndani ya kiwanda hicho chamadawa.
Meza kuu ikijadili ya msingi, wa pili kutoka  kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, akitete na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Prince Hetal Vithlani na mwisho anaonekana Kaimu meneja wa TFDA Moses Mbambe.


MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wamiliki wa viwanda katika mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya viwanda kabla yakufikiria watu kutoka mbali.

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana.
Ndikilo amesema haiwezekani hata ajira kama za kukata majani badala yakuwapa wananchi wanaozunguka maeneo haya mkaenda kutafuta mtu kutoka mbali, kwani kwa kufanya hivyo mtawafanya wananchi hawa wasiwe rafiki wa kiwanda na wakati mwingine wanaweza kufanya uhujumu.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze  kukifungua kiwanda hicho mapema na  shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja. " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu  wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" Huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.
Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho Prince Hetal Vithlani, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,
Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali  kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.
Prince Phamaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.