ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 19, 2013

BOMBA FM YATOA AJIRA MOJA VIGEZO HIVI HAPA...


Kituo cha Bomba Fm Mbeya kimetangza ajira moja katika kituo hicho, ambapo mmoja kati ya watu watakao kuwa wakiwania nafasi hiyo ya ajira watashindana moja kwa moja kupitia vipindi viwili.
Akitangaza nafasi hiyo wakati wa kipindi cha Kali za Bomba kinachorushwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7 ya mchana hadi saa 10 ya jioni, Meneja Mkuu wa Kituo hicho FREDY HELBERT amesema licha ya ajira hiyo kutolewa kupitia mashindano bado vigezo na taratibu za kazi zitazingatiwa.
Mshindi wa mashindano atapatikana kwa ushirikiano mkubwa kati yake na wasilikilizaji ambao ndio watakuwa majaji wakuu……

VIGEZO vya mshiriki:-
1. Awe na umri wa kuanzia miaka 18.
2. Awe raia wa Tanzania.
3. Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha nne.
4. Awe hana mkataba wowote na kampuni yoyote ile.
5. Awe hajawahi kufungwa jela au kushitakiwa na kosa lolote.
6. Awe na akili timamu.
Fomu ya ushiriki ni shilingi 10,000/= tu ya Kitanzania.
Kwa Waliopo nje ya Mbeya maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu ya mkononi.+255764 240 440

Thursday, April 18, 2013

CHEREKO CHEREKO LA HARUSI YA MARTIN WILLIAM NA JOYCE KABAGO LAFANA JIJINI MWANZA.

Hongera kwa Martin na Joyce kwa kufunga ndoa.

Bwana Martin William akimvisha pete Bi. Joyce Kabago kamaishara ya uaminifu kwa ndoa takatifu.

Bibi harusi Joyce Kabago akimvisha pete ya harusi Bw. Martin huku akila kiapo mbele ya kanisa.

Vyeti vya ndoa takatifu ya Bw. Martin na Bi. Joyce, iliyofungwa katika kanisa la Roman Catholic Buswelu jijini Mwanza.

Maharusi wakijiandaa kwaajili ya msafara.

Msafara kutoka kanisani mara baada ya ndoa takatifu ya Bw. Martin na Bi. Joyce, kufungwa katika kanisa la Roman Catholic Buswelu jijini Mwanza.

Wow....!!!

Nice.

Safi.......!!!!

Meza kuu ya bwana harusi.

Ndugu toka familia zote nao walijumuika katika picha za ufukweni.

Smile za maharusi katika siku hii muhimu.

Bwana harusi anaitwa Martin naye mshenga anaitwa Martin.

Wakipongezana kushoto ni Baba wa Bibi harusi  Mr. Kabago na kulia ni Baba wa Bwana harusi Mr. William.

Nilishe nikulishe ya keki ya harusi ya Bw. Martin William na Bi. Joyce Kabago.

Mambo ya maakuli.

Wafanyakazi wenzake na bwana harusi katika picha ya pamoja na maharusi.

H. BABA AINGIZA SOKONI PIPI ZENYE JINA LAKE


H. Baba akionesha pipi zake.

Katika kuonyesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inakuwa na kuvuma mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi wa kikazi, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini H. Baba ameamua kujikita katika biashara kwa style ya kiutofauti kwa kuingiza sokoni bidhaa aina ya pipi zenye jina, picha na chata zake, pipi zinazojulikana kwa jina la 'H. BABA & FLORA MAPENZI KWA WATOTO'.

Muonekano wa mbele.
Pipi hizo zilizapambwa kwa picha ya H. Baba katika karatasi ya kuishika pipi, zikipambwa na mfuko wa nylon wenye uzito wa gram 250 uliona picha ya mwanamuziki H. Baba na mwigizaji wa Bongo movie Flora Mvungi, zinazo tengenezwa na kampuni ya TANFRIK LIMITED ya Nairobi nchini Kenya, tayari zimeanza kuuzwa kwenye baadhi ya maduka na vibanda mbalimbali vya biashara kanda ya ziwa.
Muonekano wa nyuma.

Blogu hii imekutana naye uso kwa uso jijini Mwanza akiwa na mzigo wa pipi hizo na swali la kwanza kwake lilikuwa kipi kimepelekea kwa msanii H. Baba kuja na ubunifu huo ambao ni wa kwanza kabisa nchini Tanzania?..... (BOFYA PLAY KUSIKIA JIBU )


Msanii Lady Jay Dee miaka michache liyopita alikuja na bidhaa za maji zenye jina lake, mzigo ukaingia sokoni kisha baada ya muda mzigo ukatoweka sokoni, unawathibitishia vipi wateja kuwa pipi za H. Baba zitadumu sokoni? ......(BOFYA PLAY KUSIKIA JIBU)

"Lete mzigo tuonje!!" Hivi ndivyo wanavyoonekana kusema kutoka kushoto ni mtangazaji wa Passion Fm ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mwanza Kwanza Philbert kabago, H. Baba (mgawa pipi), Samadu Abdul wa Clouds Fm 88.1 Mwanza na Tecnix Muheshimiwa.
Sasa ni zamu ya wadau wa Metro Fm kufurahia utamu Loyce Nhaluke, Sefroza Joseph, Smith King Presenter and Amina Rashidi.

Kwa uwekezaji huu kwenye pipi za H. Baba ndiyo tuseme kuwa hili sasa ni hitimisho kwako kujishughulisha na sanaa ya muziki?.... (BOFYA PLAY KUSIKIA JIBU)

Wednesday, April 17, 2013

BONDIA FADHILI MAJIHA ARUDI NA UBINGWA KUTOKA INDONESIA.

Bondia Fadili Majia akiwa na kombe la ubintaifa wa wa ngumi kimaifa alililinyakua nchini Indonesia wiki iliyopita alipo mpiga bondia Heri Amol  hapa alipo rakiwa baada ya kurudi dar es salaam jana kutoka kushoto ni Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini wengine ni mabondia Japhet Kaseba, Kanda Kabongo na Pendo Njau.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuraia na bondia pendo Njau baada ya kumpokea bondia Fadhili Majiha katikati aliyerudi na kombe la ubingwa aliouchukua Indonesia wiki iliyopita  baada ya kumtwanga bondia Heri Amol Heri Amol wa pili ni Japhet Kaseba mwingine ni Kanda Kabongo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MASUFURIA YALITUMIKA KUFICHA MABOMU YA MILIPUKO YA BOSTON.


Mabomu yaliyolenga Mbio za Marathon huko Boston Marekani huenda yalifichwa ndani ya sufuria za kupikia. Hii ni kwa mujibu wa majasusi.
This image from a Federal Bureau of Investigation and Department of Homeland Security joint bulletin issued to law enforcement and obtained by The Associated Press, shows the remains of a pressure ... more 

Baadhi ya picha zilizochapishwa kwenye taarifa ya shirika la ujasusi-FBI zinaonyesha vipande vipande vya chuma. Shambulio hilo la Jumatatu wiki hii liliwaua watu saba na kuwajeruhi wengine zaidi ya 170. Miongoni mwa walipoteza maisha ni pamoja na mvulana wa miaka minane na mwammke wa miaka 29, pamoja na mwanafunzi raia wa China.
Mwandishi wa BBC mjini Boston anasema mkesha wa maombi kwa waathirka ulifanyika hapo Jumanne, huku wenyeji wakitafakari sababu za kutaka kulenga mbio hizo ambazo huwa kivutio cha wengi.
Huku haya yakiarifiwa Rais Barack Obama anatarajiwa kuzuru Boston hapo Alhamisi kwa maombi maalum ya kuomboleza vifo hivyo.
Obama pia atawahutubia waathiriwa na jamaa zao. Madaktari wanaowahudumia majeruhi wamesema bomu hilo lilikua na vyuma, na vipande vya makombora. Majeruhi kadhaa wamekatwa miguu na mikono.
CHANZO: BBC SWA/PICHA NA FBI

LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA MGAMBO YAIDINDIA YANGA, KAGERA YAIPIGA MSUMARI TOTO AFRICANS

Mgambo yatia Nuksi Ubingwa
Mgambo Fc V/s Yanga 


Ligi kuu Tanzania bara iliendelea leo, huku vita kubwa ikiwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijjini Tanga ilipoikutanisha Yanga na Mgambo Fc.

Wakicheza kwa presha kubwa kuhitaji pointi muhimu sana ili kukaribia kutangaza Ubingwa mapema, Yanga walijikuta wakipata sare ya goli moja kwa moja.

Mgambo ndio walikua wa kwanza kupata bao kabla ya Msuva kusawazisha dakika ya 87 na kuisaidia timu yake kuepuka kipigo kabisa, kwa matokeo hayo sasa Yanga wanahitaji pointi nne tu ili kutangaza ubingwa kwani watafikia pointi 57 ambazo wapinzani wao wakubwa msimu huu Azam Fc hawawezi kizifikia.

Matokeo ya mechi nyingine Mtibwa waliifunga JKT Oljoro goli moja bila majibu pia Kagera Sugar imewashindilia bila huruma msumari mmoja bila majibu majirani zao Toto Afrikans inayopigana kutoshuka daraja.

KWA HERI BI KIDUDE.

Mwimbaji mkongwe wa taarab asilia na muziki mahadhi ya pwani ya Zanzibar nchini Tanzania Fatma Bin Baraka maarufu kama Bi Kidude amefariki dunia.

Akiongea kutoka Zanzibar mjukuu wa marehemu ambaye naye anaitwa Fatma Kidude amesema kuwa bibi yake amefariki akiwa nyumbani kwa mtoto wa kaka yake maeneo ya Bububu mjini Zanzibar.

Fatma ambaye naye pia ni mwimbaji wa kundi la Gusa Gusa la jijini Dar es salaam amesema kuwa bado taratibu zote za mazishi zinaendelea kufanyika lakini mwili wa marehemu utahamishwa kuelekea nyumbani kwake Raha leo.

Mara kadhaa kulitokea uzushi wa Bi Kidude kufariki na baadaye kukanushwa, lakini safari hii taarifa hizi ni sahisi kwani zimethibitishwa.

Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu.

Tuesday, April 16, 2013

KESI YA KUPINGA UCHAGUZI TFF YARINDIMA LEO JIJINI MWANZA. JE UCHAGUZI WA TFF KUCHELEWESHWA HADI JULY 2013?


NA ALBERT G. SENGO:MWANZA

Mahakama kuu kanda ya Mwanza leo imetupilia mbali shauri lililowasilishwa na Richard Rukambula kuitaka mahakama hiyo kusimamisha uchaguzi mkuu wa TFF mpaka kesi yake ya madai ya msingi itakapo sikilizwa na kutolewa uamuzi.

Rukambula aliyefungua kesi dhidi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) mnamo tarehe 25 mwezi February mwaka huu kupinga kuenguliwa kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya uongozi TFF kwa madai kuwa TFF katika masharti nane yaliyoorodheshwa kwenye tangazo la uchaguzi kipengele cha kuwataka wagombea kuomba nafasi moja tu hakikuwepo na hivyo wagombea wote waliomba kulingana na jinsi nafasi hizo zilivyokuwa.
BOFYA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA TAARIFA KAMILI. 

MKIMBIAJI MKENYA ASIMULIA HOFU MILIPUKO BOSTON


Korir alishinda mbio za Boston Marathon mwaka 2012.


Mshindi wa mbio za mwaka 2012 za Boston Marathon, Wesley Korir, aliyemaliza wa tano mwaka huu, ameambia BBC kuhusu hofu yake pindi aliposikia milipuko miwili iliyotokea Boston Marekani.
Milipuko hiyo ilitokea karibu na msitari wa mwisho wa kumalizia mbio hizo na kuwajeruhi takriban watu 140 takriban saa mbili baada ya mshindi kumaliza mbio hizo.

Alikuwa akisherehekea ushindi wa mkenya Rita Jeptoo katika mbio za wanawake.''Ikiwa shambulio hilo lingetokea saa mbili kabla ya mbio kumalizika labda ningekuwa miongoni mwa waliojeruhiwa,'' alisema bwana Korir.
"furaha yetu ni kuwa tulikuwa tayari tumeondoka katika eneo hilo,'' Korir aliambia BBC.
Bi Jeptoo anatoka katika eneo bunge la Cherangany, ambalo bwana Korir ni mbunge wake baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwezi jana.
Licha ya milipuko hiyo pamoja na jukumu lake la kisiasa, Korir amesema kuwa ataendelea kushindana katika mbio za marathon hata ikiwa Boston itaandaa mbio zengine mwaka ujao.
Rais Barack Obama emesema wahusika lazima
watasakwa na kuchukuliwa hatua kali
.

Korir alisema kuwa aliogopa sana aliposikia kuhusu habari ya milipuko.
Alisema kuwa punde tu baada ya kusikia habari hiyo aliwapigia simu wakwe zake kuwajulia hali kwani walikuwa wamemtembelea pamoja na kocha wake.
Balozi wa Kenya nchini Marekani amesema kuwa hana taarifa zozote kuhusu wakenya waliojeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.
Raia wawili wa Afrika Kusini walitibiwa baada ya kupata majeraha
Lelisa Desisa, wa Ethiopia alishinda mbio za wanaume mbele ya mshindani wake Micah Kogo.
Mbio hizo mwaka huu zilikuwa na wanariadha 23,000 na zilitazamwa na mamia ya mashabiki.

AIBU YETU AIBU YAO? (YETU = WANANCHI, YAO = WABUNGE)


TABIA ya wabunge kurushiana matusi wakati wa mjadala wa Bunge, imezidi kushika kasi, baada ya tabia hiyo kuendelea tena jana wakati wa mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Pamoja na tabia hiyo kuendelea tena jana, wiki iliyopita Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu (CHADEMA), alisema Baraza la Mawaziri linaundwa na mawaziri wapumbavu.
Kwa siku ya jana, tabia hiyo ilianzia kwa Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kisha ikasisitizwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM).

Wakati Nkamia akichangia bajeti hiyo na kueleza jinsi asivyokubaliana na vitendo vya udini vinavyodaiwa kuwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Sugu aliingilia kati bila kuruhusiwa na kusema, je Lwakatare.

Baada ya Sugu kusema neno hilo, Nkamia alikatisha kuchangia na akasema:

“Sugu naomba unyamaze mimi ndiye nazungumza, mimi siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa,” alisikika Nkamia.
Chanzo; Gazeti la Mtanzania

AIRTEL NA NOKIA WAZINDUA OFFER KABAMBE YA NOKIA LUMIA 620



Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Batuli Chombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju

Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa  simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu

Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Jimy Tara mwandishi wa habari wa ITV kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa  Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia  utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju

Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha simu za rangi tofauti za Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa  Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.

Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa  Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi  wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.


AIRTEL NA NOKIA wazindua Offer Kabambe ya Nokia Lumia 620

*          
Wateja kupata muda wa maongezi wa dakika 275 bure

*          Offa itajumuisha SMS bila kikomo na kifurushi cha internet ya 3.75G cha 3GB


Monday 15 Aprili 2013, Airtel Tanzania imeungana kwa pamoja na kampuni ya Nokia na  kuzindua simu ya Nokia Lumia 620 itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kuunganishwa na huduma ya technologia ya juu kwa
kupitia simu za kisasa na kupata ofa kabambe za bure za muda wa mongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet kwa muda wa mienzi mitatu

Nokia Lumia 620 pamoja na simkadi ya Airtel itatoa uwezo tofauti ikiwemo kuunganishwa na internet na mtandao na kuangalia mitandao mbalimbali yakijamii pamoja na tovuti mbalimbali. Nokia Lumia inamuonekano mzuri na wa kisasa wenye rangi za kipekee ambapo kutokana
na ubunifu `wetu wa kutengeneza simu zenye rangi tofauti mteja ataweza kujichagulia simu yenye mvuto na rangi aitakayo

Vitu vingine vilivyopo kwenye simu hii ya Nokia Lumia ni pamoja na kamera yenye lensi ya kisasa, ya mega pixel 5, pamoja na kamera ya mbele, kutokana na kuwa na Lensi bora hii itamuwezesha mteja kupata video au picha yenye muonekano mzuri zaidi

Ndani ya Nokia Lumia 620 unaweza kupata vitu muhimu sana ikiwemo ramani ya Dunia pamoja na maelekezo maalum wa vitu au sehemu maalum mbalimbali,

Akiongea wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema" tumeshirikiana na Nokia katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora na nafuu kwa kupitia vifaa vya Nokia vinavyokuhakikishia kiwango cha juu huku tukiwapa wateja wetu uzoefu wa pekee katika huduma zetu. Kwa kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G tunayoitoa nchi nzima wateja wetu wana hakikishiwa huduma za uhakika wakati wote.

Nokia Lumia itaunganishwa na ofa ya kifurushi cha muda wa maongezi cha dakika 275, sms bila kikomo na intenet ya kifurushi cha 3GB kitakachopatika kwa wiki moja kila mwenzi kwa muda wa mienzi mitatu"

"Kupata offa hii wateja wetu watatakiwa kuweka muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi 1000 mara wanaponunua simu ya Nokia Lumia 620. Na katika kuthibitisha thamira yetu ya kutoa huduma zinazoendana nathamani ya pesa ofa hii itadumu kwa muda wa mienzi mitatu.

Airtel itaendelea kushirikiana na makampuni mbalimbali katika kutoa huduma bora na bei nafuu kwa kupitia mtandao wake mpana wenye huduma muhimu za Airtel Money na huduma yetu kabambe ya Airtel yatosha Aliongeza Mmbando.

Kwa upande wake Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, alisema kampuni ya Nokia inaendelea kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kutoa bidhaa za simu bora zitakazowapatia wateja kile
wanachokihitaji.  Tunafurahia kuleta bidhaa bora na za bei nafuu zenye uwezo tofauti, simu ya Nokia Lumia 620katika soko la Tanzania,.Tunaamini  muundo mzuri wa simu hii, rangi nzuri na uzoefu tofauti pamoja na huduma za Airtel zitawapatia wateja wetu sababu ya kujipatia simu hii ya Nokia Lumia"


"Nokia Lumia 620 zinapatikana kwa gharama ya shilingi 450,000/= tu. Simu inapatikana katika maduka yote ya Airtel, midcom na wakala wa Nokia wa premium. kwa sasa, kinachotakiwa kufanya ni wewe mtanzania kutembelea moja kati ya haya maduka na kujipatia simu hii orijino kutoka Nokia.

Kutokana na ubora wa simu hizi za Nokia Lumia 620 mteja ataweza kufurahia zaidi huduma zote za kimtandao za Airtel zikiwemo zile za kutuma na kupokea pesa, Airtel Yatosha, Jirushe, kutuma na kupokea SMS, huduma bora ya Intaneti ya 3.75G na nyingi nyinginezo.

Monday, April 15, 2013

OPORESHENI YA KUWAONDOSHA WALIOVAMIA HIFADHI ZA BARABARA NA KUFANYA BIASHARA NA UJENZI YAANZA LEO JIJINI MWANZA


Ni moja kati ya eneo linalo ripotiwa mara kwa mara kutokea ajali.

TANROAD Mkoa wa Mwanza  imeanza oporesheni ya kuvunja majengo, vioski na  kuwaondoa watu  waliovamia na kujenga kando ya barabara ikiwemo kufanyabiashara ndani ya hifadhi ya barabara za Jijini Mwanza na zile zilizopo kwenye Wilaya zote za Mkoa huo.

Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonard Kadashi alieleza toka ofisini kwake kwamba muda wa wiki tatu uliokuwa umetolewa tayari umekwisha kwa watu waliovamia hifadhi kuondoka kwa hiari.

“Tulitoa wiki tatu na zimeisha hivyo leo tunaanza rasmi zoezi la kuwaondosha watu wote waliovamia na kufanya ujenzi pamoja na wale ambao wamekuwa wakipanga bidhaa zao kandokando ya barabara kwa lengo la kufanya biashara ikiwemo pia sehemu za kuoshea magari, mashine za kusaga na kukoboa nafaka zoezi ambalo litakuwa maalum kama safisha barabara zinazomilikiwa na wakala wa barabara Mkoani hapa”alisisitiza.

Mhandisi Kadashi alisema kwamba baadhi ya barabara zilizo chini ya TANROAD Mkoani Mwanza zimevamiwa na watu ambao wamekuwa wakivunja sheria na kuamua kufanya ujenzi na biashara holela pia wamekuwa wakikaidi kuondoka ama kuacha kuendelea na ujenzi katika maeneo mbalimbali pamoja na kuwekewa alama za X.

“Tunazingatia sheria kwa hili hivyo naomba wananchi na watu waliovamia barabara hizo kuwa ndani ya hifadhi, watuelewe na maandalizi ya zoezi la kuwaondoa tayari yamekamilika na leo tunaanza rasmi tukienda sanjari na ubomoaji ”alisema Kadashi.

Hatua hiyo ya TANROAD kuwaondosha waliovamia kandokando ya barabara zake ilifuatia hoja iliyowasilishwa na Mhandisi Kadashi Machi 21 mwaka huu wakati wa vikao viwili ngazi ya Mkoa  cha Bodi ya barabara na kile cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Mwanza (RCC) na kukubaliana na hoja hiyo kisha kutoa maazimio ya kutekelezwa haraka zoezi hilo ili kuokoa maisha ya watu pindi magari yanapopata ajali.

Jeh karakana hii ya mashine ya kusaga na kukoboa iliyo pembezoni mwa barabara eneo la Mabatini itasalimika?
“Kufanya biashara kandokando ya barabara ni riski kwa watu hao kwani mara nyingine tumepata taarifa za ajali kwa magari yanayopoteza uelekeo na watu kadhaa kupoteza maisha, mbali na hilo kwa wafanyabiashara hao kupanga bidhaa zao kwenye maeneo hayo husababisha kuzidisha msongamano wa magari hali inayochangia kuchelewesha shughuli za kiuchumi za kila siku"

Alizitaja baadhi ya barabara ambazo ziko Jijini Mwanza zitakazohusika na zoezi hilo ni pamoja na barabara ya Kenyata kwenda Mkoa wa Shinyanga, barabara ya Nyerere hadi Mkoani Mara na Simiyu, barabara ya SAUT Nyegezi na zingine zote zilizo chini ya TANROAD zikiwemo zile za kuunganisha Makao makuu ya Wilaya zote za mkoa wa Mwanza.

Meneja, Mhandisi Kadashi ametoa rai kwa watu waliovamia barabara hizo kutojaribu kufanya mgomo wa kuondoshwa katika maeneo ya hifadhi ambayo ni mita 30 kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na badara yake waanze kuondoka wenyewe kabla ya kukumbwa na zoezi hilo na watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kulipa garama za ubomoaji wa majengo na vioski na hakuta kuwa na fidia yoyote baada ya zoezi hilo kutekelezwa.

MTANDAO WA WASANII TANZANIA WAJA NA MBINU MPYA KUWAKWAMUA WENYE VIPAJI.


                                 PRESS RELEASE

 SHIWATA imeandaa maonesho maalum kila mwezi ili kutoa nafasi kwa wasanii wa fani ya mbalimbali pamoja na wanamichezo kuonesha vipaji vyao.

Peter Mwenda

 Wasanii wengi chipukizi wanakosa mahali pa kuonesha kazi zao, mara nyingi kazi za wasanii wakubwa ndizo ambazo hurushwa katika redio na luninga (TV).

 SHIWATA imeamua kuandaa maonesho haya kwa malengo makuu yafuatayo

(1)   Kukuza vipaji

(2)   Kuwapatia soko (underground) mahali ambapo wanaweza kuonesha vipaji vyao na kuwashawishi mapromota mbalimbali kuwaajiri.

(3)   Kuelimisha jamii kuhusu matatizo mbalimbali kama maadili na magonjwa kama UKIMWI,malaria.

(4)   Kuimarisha umoja kati ya wasanii na wanamichezo

 SHIWATA inawataarifu viongozi mbalimbali na makundi ya sanaa na Michezo pamoja na wasanii binafsi kutakua na mkutano Siku ya Jumatano Aprili 17 mwaka huu saa 8 mchana katika ukumbi wa Splendid,Bungoni Ilala kupanga ratiba na kupata taarifa zaidi.

Onyesho la Kwanza litaoneshwa katika ukumbi wa Star Light Hotel, Mnazi Mmoja Dar es Salaam siku ya Jumamosi Aprili 24.

 Michezo itakayoneshwa ni pamoja na maigizo, sarakasi, ngoma, kwaya, karate, Taekwondo, Taarab, Dansi, Bongo Flava, Mavazi, Gospal na Kasida, mada kuu katika maonesho hayo ni Amani na Utulivu.

 Hii ni nafasi ya pekee kwa wasanii chipukizi (underground) kuonesha vipaji vyao.Watengenezaji wa filamu, mapromota, wamiliki wa bendi, MaDj na wanunuzi wa mbalimbali wa kazi za sanaa wanaalikwa ili waweze kuona vipaji na kununua kazi za wasanii hao chipukizi.

 Wanafunzi wenye vipaji kutoka shule za msingi, Sekondari na vyuo mbalimbali wanaalikwa kuja kuonesha vipaji vyao.

 Mipango iliyofanywa ili maonesho haya yarushwe live kituo kimojawapo cha televisheni.

 Kutokuwa na chakula kwa wasanii na zawadi mbalimbali zinazotolewa kwa wasanii watakaofanya vizuri katika kila onesho.

 Hii itakuwa nafasi nzuri kwa wapenzi wa burudani ya sanaa kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajui wapi wanaweza kupata burudani kama hiyo kiingilio kitakuwa bure.

 

Wote mnakaribishwa

 

Peter Mwenda 0715/0752- 222677

Ofisa Habari wa SHIWATA

Sunday, April 14, 2013

BREAKING NEWS: RCO GEITA AFARIKI KWA AJALI YA GARI


Taarifa zilizotufikia zimesema kuwa Afisa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Geita (RCO) SSP-Magnus Mng'ong'o anadaiwa kupata ajali na kufariki dunia.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya jeshi la polisi vimedokeza kuwa afisa huyo gari alilokuwa akisafiria limegongana na Roli la kubeba Samaki majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo eneo la Chibingo katika barabara ya Geita Bukoba wakati akitoka eneo la Katoro kikazi.

Tutaendelea kuwajuza zaidi kadri taarifa zitakavyo patikana.