Nje ya lango kuu la Bandari ya Kaskazini jijini Mwanza ambapo lango hilo lilifungwa kwasababu za usalama. |
Sakata hilo lilitokea jana kuanzia majira ya saa12:30 na kudumu hadi saa 7:00 mchana baada ya Meli ya Mv Victoria kuweka Nanga kwenye Bandari ya Mwanza Kaskazini kufatia Mamlaka ya Bandari nchini( TPA) kutoa maelekezo kwa uongozi wa TPA Mwanza kuwa muda wa mzabuni aliyekuwa akifanya kazi za kupakia, kupakua na kutoza ushuru wa mizigo kumaliza muda wake na kazi hiyo kufanywa na Mamlaka hiyo.
Askari wamezingira lango kuu la Bandari ya Kaskazini jijini Mwanza ambapo lango hilo lilifungwa kwasababu za usalama. |
Askari akilinda lango kuu kuzuia watu wasitinge bandarini ambapo shughuli zote za huduma na biashara zimesimama. |
Akizungumza wakati wa kutekeleza mgomo huo Mwenyekiti wa Ushirika wa Wahudumu wa Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini Rajabu Said alisema kuwa wao waliokuwa wazabuni wa kufanya shughuli za kupakia, kupakua na kutoza ushuru wa mizigo Bandarini hapo kugomea na TPA kuendelea na kazi hizo kutokana na muda wa miaka miwili waliokuwa wamepewa kumalizika na kutakiwa kutjishughulisha tena.
Mwenyekiti Said alieleza kuwa kutokana na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kutoa mwongozo wa ukusanyaji mapato na ushuru baada ya kumalizika kwa muda wa USHIRIKA wa miaka miwili uliokuwa umetolewa kwa zabuni ambayo walishinda mwaka 2011 hadi kumalizika Agosti 30 mwaka huu aligubikwa na mizengwe na kuwa na usiri na kutowekwa bayana na viongozi wa TPA Mwanza.
Mwenyekiti Said akizungumza na chombo cha habari. |
Baada ya Kikao hicho kumalizika kwa makubaliano yaliyoafikiwa jambo la kushangaza asubuhi ya leo Agosti 31 mwaka huu wakati tulipofika Bandarini Mwanza Kaskazini tulikuta utaratibu mpya kwa walinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SUPREM na kuteleleza kuwa haturuhusiwi kufanya shughuli za kutoza ushuru, kutoza mizigo tutakayo pakua leo Jumamosi (Jana) na kupakia Jumapili na kazi hiyo iko chini ya TPA kuanzia sasa.
Said alisema baada ya taarifa hiyo tulipinga na kuwataka wafanyabiashara wa kutoka Mjini Bukoba kuacha kushusha mizigo hiyo hadi muafaka upatikane na wao waliafiki kwa kutuunga mkono kutokubaliana na uongozi wa TPA kwa vile ulilenga kuwatoza fedha zaidi kwa kulipia VAT mala tano kwa mizigo yao ikiwa ni kupakia kulipa VAT asilimia 18 kwa Marine na TPA ikiwa na kushusha na tozo la fedha za Makuli hao.
“Hatukubaliani na kabisa na kilichofanywa na uongozi wa TPA kwani zabuni haijatangazwa nasi tukapata kutuma maombi yetu lakini imedaiwa kuwa kuna Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo (TPA) Mwanza (DOWUTA) wamekisajili ili kuchukua nafasi ya Ushirika kufanya kazi hiyo na ndiyo maana Tenda hawajaitangaza na tumeelezwa na uongozi kuna mzabuni tayari nasi tumepinga na kugomea kukubaliana na utaratibu huo hivyo Bandari zote Makuli tumeomba uwazi uwepo na tenda zitangazwe” alisisitiza.
Ushirika huo wenye jumla ya wanachama 3000 na ulisajiliwa na kufanya kazi hizo Bandari za Mwanza Kaskazini na Kusini baada ya kushinda zabuni hiyo mwaka 2011 ulipunguza tatizo la ajira na kuwafanya wanachama hao ambao ni wafanyakazi wa kubeba mizigo wamekuwa na utaratibu wa kukopeshana, kuchaniana kwa matatizo ya ugonjwa na kutoa fedha kwa mwanachama anayefariki na wanaositaafu kubeba mizigo hulipwa milioni 1.5 ikiwa na hisa yake ya uanachama hivyo kutopewa kazi hiyo imedaiwa kuongeza watu kujihusisha na uhalifu mitaani na kuweka mashaka kwa wasafiri na mizigo yao kuanza kuibiwa na watu kwa kukabwa nakati za usiku na asubuhi.
Mizigo imedoda melini hakuna wapakuaji. |
Ile hali meli ikiwa imejaa mizigo na bidhaa za ndizi baadhi ya wafanyabiashara waliamua wenyewe kupakua mizigo. |
Vuta nikuvute nje ya lango la Mamlaka ya Bandari. |
Baada ya vuta ni kuvute kutoka kwa wafanyabiashara na uongozi wa
TPA Mwanza na Makao Makuu iliyotuma wawakilishi wake kujadiliana na kuona jinsi
ya kumaliza mvutano huo na kumaliza mgomo wa Makuli hao na kupelekea kuibuka
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Huduma wa TPA Clementi Kiloyavaha na kueleza kuwa
utaratibu uendelee kwa leo kama ilivyokuwa wakati wakianda Kikao cha pamoja.
Kiloyavaha alisema kwamba kutokana na maelekezo kutoka kwa Waziri
wa Uchukuzi Dr.Harison Mwakyembe kwa Mamlaka hiyo ya TPA wamepewa utaratibu na
hivyo utaanza kutekelezwa kuanzia Septemba mosi na kunachotakiwa kufanyika ni
kikao cha pamoja baina ya wadau wa TPA na Wafayabiashara wanaotumia Bandari za
Mwanza Kaskazini na Kusini kuwapa utaratibu mpya.
Kwa upande wa wafanyabiashara baadhi yao waliozungumizia sakata
hilo na kukataa kutajwa majina yao walisema kuwa wao wanapinga kutozwa VAT
asilimia 18 kwa kila tani moja na vifurushi wakati wa kupakia na kupakua mala
mbili ikiwa ni kwa Kampuni ya Meli ya Marine na Mamlaka ya Babdari TPA pamoja
na kutozwa VAT ya fedha za vibarua wa kupakia na kupakuwa wanayolipia kuwa ni
kero kubwa kwao.
“Hili litatufanya kuacha kupitisha mizigo yetu katika Bandari hizi
za TPA kwa vile utaratibu huu umelenga kuturudisha nyuma na kutukamua zaidi na
kukosa faida kabisa na leo tumepoteza wateja na tutauza ndizi,mihogo na matunda
kwa bei ya hasara na hili limetukera sana nibora wangetuarifu kwa matangazo
badala ya kukurupuka na kuamua hata kama ni maagizo ya Waziri Mwakyembe” walisema
.
Hali ililejea majira ya saa 7:00 mchana makuli na wafanyabiashara
kuendelea na utoaji wa bidhaa zao na kupakia baada ya kuishusha ili iliyotoka
Mji wa Bukoba na kusababisha mgomo wa masaa 7 na kuasilika kwa makundi ya
wafanyabiashara wa ndizi mbivu na mbichi, matunda na mihogo katika masoka
mbalimbali ya Jiji la Mwanza kama ilivyozoeleka Meli ya Mv Victoria inapofika
Jijini Mwanza toka Mjini Bukoba.