ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 26, 2011

ELITHA NA WADAU CHUO CHA SAUT WALA NONDOz

Tabasamu mwanana toka kwa mwadada Elitha Kariongo aliyehitimu siku ya leo kwenye maafali ya 50 Chuo Kikuu cha St. Agustino Mwanza (SAUT) yaliyofanyika katika viwanja vya wazi vya Raila Odinga chuoni hapo.

Hongera kwa ma-mates wahitimu Elitha Kariongo na Bridget.

Katika flash ya pamoja Mama Marry Damie, mhitimu Farida Damie na dada yake Grace Yotam.

Wahitimu Kagonji na Elitha.

M-m-m (kigugumizi) "Badaye sanaaaaaaAAAaaaaaaa!!!"

"DAWA YA DENI NI ............"

Hivi kwa mfano unamdai mtu ana kuzungusha kwelikweli, halafu mara mkiwa pamoja njiani na mazungumzo yenu ya deni nawe ukiwa umefura ile kinoma noma, unaokota kiasi kile kile unachomdai.

Jeh! utaendelea kudai ama utamsamehe mdeni wakoooooo?

KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU PSI YAJUMUIKA NA WADAU WAKE UFUKWE WA ZIWA VICTORIA

Timu ya wafanyakazi wa PSI Musoma katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali katika ufukwe wa Tunza, mara baada ya kusanyiko la shirika hilo lililofanyika jijini Mwanza.
Timu ya wafanyakazi wa PSI wilaya ya Bunda wakipata flash ya pamoja.
Mchezo wa kwanza ulikuwa ni soka Musoma v/s Bunda ambapo matokeo timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 2-2.
Mchezaji wa timu ya PSI Bunda (light green bips) akishindana kwa mabavu kuunasua mpira mbele ya beki wa timu ya Musoma (orange bips).
Hadi mwisho timu hizo zilitoka sare ya 2-2
Kona ya wafanyakazi mashabiki.
Katika mchezo wa voleball Musoma waliibuka kidedea.
Kuvuta kamba wanawake Timu ya Bunda iliwashinda mabavu Musoma.
Mkurugenzi wa (PSI) Population Services International Tanzania.
PSI imekuwa ikifanya kazi kuboresha afya ya Watanzania tangu mwaka 1993. Ni shirika linalo tumia mbinu mbalimbali kuhamasisha sekta binafsi kuwa na tabia ya kuupa mwili lishe kwaajili ya afya likitoa misaada ya chakula mashuleni, na kutoa elimu kwa wananchi hasa vijijini kufanya kazi kwa ajili ya masoko ya maskini.

Bunda walitia fora katika dancing competation ya Kwaito na kiduku ambapo ni moja kato ya michezo mitatu ya muziki iliyoshirikishwa mahadhi mengine yaliyohusishwa ni muziki wa Sebene.
Mambo ya twisti
Anicet ambaye alikuwa mratibu wa Tamasha hilo lililofanyika Tunza beach mkoani Mwanza, akishiriki timu ya PSI Bunda hapa alikuwa akimwaga shukurani zake kwa wadau wenzake kwa lugha ya Kihindi.

PSI ni shirika linalofanya kazi katika nchi zaidi ya 60, na makao yake makuu ni mjini Washington DC.

BENDI YA TWANGA PEPETA YAWASILI LONDON KWA MAKAMUZI LEO

Bendi ya Twanga Pepeta imewasili leo mjini london tayari kwa makamuzi katika ukumbi wa Silver Spoon London kwa ajili ya Kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa wa Tanganyika. Usikose show hii ya Ukweli JUMAMOSI HII.

KUPIMANA IMANI...teh teeh teEh!

Maafisa usalama wakiwa wanaulinda mti wa krismas wenye urefuwa mita 2.4 uliotengenezwa kwa kutumia madini halisi ya dhahabu na kuonyeshwa katika duka la vito vya thamani la Ginza Tanaka Kikinzoku lililopo jijini Tokyo.

Mti huo umetengezwa kwa vipande vya dhabu na majani yake , wote ukiwa na kilo 12.

Mti huo hauuzwi lakini thamani yake inafikia Yeni Millioni 150 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zinazofikia Trillioni 3.1. Duh watu bwana!...

Meri Krismasi.

Chanzo: Mrindimo

Friday, November 25, 2011

TWANGA PEPETA WAKWEA PIPA 2 LONDON UK.

Twanga Pepeta ''KISIMA CHA BURUDANI'' wameondoka leo asubuhi kutoka uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea kuvinjari katika Jiji la London ili kusugua kisigino na wapenzi wao walioko nchini Uingereza na nchi jirani ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Bendi ya Twanga Pepeta wakijiandaa kuingia kwenye Pipa

Chalz baba akiwa tayari kuingia kwenye Pipa

Full Mzuka

kikosi cha Twanga kikijiaandaa kuingia Katika Uwanja wa Julius Nyerere

Kutoka Kulia Amigolous akiwapa Mikoba Jojoo, Jumanne, Baby Tall na Luiza

kutoka kushoto Shalapova, Charles Baba na Shakashia

Victor Mkambi mpiga kinanda wa Twanga akiwa na Maria Soloma ambae ni dancer wa twanga

MPANGO MZIMA:-
Kundi hilo lililokamilika katika safu zake za waimbaji, wapiga vyombo na wacheza show linatarajiwa kuwasha moto wa burudani yao siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 katika Ukumbi wa Club 2000 Savoir Banqueting Suite, Popin Building Southway, Wembley HA9 0HB kuanzia saa Tatu Kamili Usiku mpaka alfajiri (9pm til late).

Mheshimiwa Balozi Peter Kalaghe atakuwa mgeni rasmi. CD za album mpya na za zamani zitauzwa na vinywaji pamoja na vyakula vya kitanzania vitakuwepo vya kumwaga. Viingilio vitakuwa £20 (singles) na £35 (couples) kabla ya saa sita (mid night) na £25 (singles) na £40 (couples) baada ya saa sita usiku.

Njoo tujumuike, njoo usugue kisigino, njoo usherehekee uhuru wa nchi yako, njoo ule na kunywa kitanzania. Burudani ni watu na watu ni pamoja na wewe. Tanzania itajengwa na watu wenye moyo kama wewe. Karibuni sana.

Shughuli hii imeandaliwa na Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog, chini ya maelekezo thabiti ya Ubalozi wa Tanzania, London.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga Mbele

JOSE CHAMELEONE AWARUSHA WAKAZI WA DMV

Ilikuwa ni Jumatano Nov23, 2011 katika sherehe za Thanksgiving nchini Marekani ambapo muimbaji Jose Chameleone toka nchini Uganda alikamua.

Mamia ya watu walifurika kuja kumuangali Msanii huyo toka Nchini Uganda kwa jina maarufu la Jose Chameleone, ana nyimbo zake, ikiwemo Mama roda, Jamila analia, na nyingi nyingi.

Muziki unaponoga warembo mikono juuuu!!!

Wakati mwingine warembo hupandwa na jazba ya maraha na kwa wale wanaoshindwa kujizuia hukinasa kinasa ili wapate chombeza, hapa ni mdafada akichombeza kwenye songi la 'kipepeo'.

Mambo ya utamuZz hayo cheza ni kuchezee ndani ya Rendezvous Hall nchini marekani.

Wanasema muziki wako ukikubalika kwa warembo baaaasi umewini! chekshia mahudhurio.

Aj Ubao alikuwa ni mwimbaji wa pili kuimba katika onyesho hapa ni nyuma ya jukwaa akipata flash ya pamoja na mdhamini wake wapendo.

Muimbaji Ana Lov akipata flash ya pamoja na rafiki yake kwenye onesho hilo la Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone.

WadadaZzzz.warembo.com ndani ya ukumbi wa Rendezvous mitaa ya Parklawn Dr, Rockville Maryland U.S

Nyuma ya jukwaa mwanadada Luren akipata flash.

Cheza ni kuchezee na flash!!!

Mwana muziki wa kizazi kimpya ndani ya Washington DC, AJ Ubao wa kwanza (kushoto) pamoja mzee wa kuwachanganya Dmk global Dickson Mkama, wa kwanza( kulia) wakiwa nyuma ya jukwaa na Jose chameleone aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wake.

Picha zote na http://swahilivilla.blogspot.com

WATANZANIA WAWILI KUKIPUTA SWEDEN

Joseph Kaniki.
William John.

Wachezaji wawili wa kitanzania, Joseph Kaniki (Golota) na William John wamefanikiwa kujiunga na timu ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF) nchini Sweden, baada ya kufanikiwa kupita katika majaribio( Trials). Majaribio hayo yalijumuisha wachezaji zaidi ya thelathini ambapo wachezaji watano walichaguliwa kujiunga na klabu hiyo ya ligi daraja la pili KonyaSpor (KIF)

Habari hii imeletwa kwenu na
http://www.africa4life.com/

BIASHARA YA SENENE INAPOFUNGA BARABARA.

Biashara inayokuwa kwa kasi mkoani Kagera ya Senene, katikati ya wiki hii imesababisha moja kati ya barabara muhimu mjini Bukoba kufungwa kwa muda ili wadau waweze kujipatia bidhaa hiyo kwa nafasi. Senene wakiwekwa kwenye chombo kama hiki chenye matundu ya hewa (chandarua) wanadumu kwa muda mrefu zaidi kwani hata kesho yake waweza kuwarejesha sokoni wakiwa 'fresh'

Ni biashara iliyotokea kuwa na mvuto wa kipekee mkoani Kagera kiasi cha kuwafanya wageni kuinunua pindi zinapokaangwa vizuri na kuhifadhiwa kwenye vyombo maalum, nyingine zikisafirishwa kwa njia ya ndege kwenda sehemu mbalimbali nchini.

Siyo soko bali mtaa umefungwa kupisha biashara hiyo adimu ya senene.

Bidhaa hii ni tani na tani kiasi kwamba wauzaji senene kujaa mfuko huu mweusi huuzwa shilingi 1000/= tu.

Haya siyo magunia ya maharage au mahindi bali ni magunia ya senene.

Soko lenyewe.

Vitu zaidi www.bukobawadau.blogspot.com

Thursday, November 24, 2011

SIMBA NA YANGA KUUNGANA DESEMBA 11

TIMU ya soka ya Kumasi Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa. Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.

Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.

Burudani ya aina yake inategemewa kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu huku makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi kwa timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye.

Wengine katika benchi la ufundi ni meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani. Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.

Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935 kwani historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwaka 1922.

Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinapocheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.

Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.


Habari hizi pia ni simulizi nchini Ghana tembelea:- http://sports.peacefmonline.com/soccer/201111/79235.php

NINI CHANZO CHA KUKITHIRI KWA WIZI VYUMA CHAKAVU?

Miaka ya nyuma Zoezi la ukusanyaji vyuma chakavu vilivyokusanywa na kuuzwa viwandani ili kuyeyushwa na kutengeneza bidhaa nyingine za chuma, zoezi lilianza vizuri tu kwa watu wakukusanya vyuma vidogo vidogo majalalani, vyuma visivyokuwa na kazi kwenye magereji, vilivyotupwa njiani kiufupi ilikuwa ni vyuma ambavyo ni takataka.
Lakini leo hii ngoma imegeuka!! Thamani ya bidhaa ya chuma imekuwa kama madini, wasio na uungwana wanangoa hadi mifuniko ya mashimo ya maji taka, mabomba ya maji, vyuma vya reli, madaraja, mita za maji, miundombinu ya alama za barabarani na sasa wameyageukia mabango....mmmmmh!.. Naskia uswazi wanapitia majiko, wanangoa hadi mageti..