Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.
Burudani ya aina yake inategemewa kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu huku makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi kwa timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye.
Wengine katika benchi la ufundi ni meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani. Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.
Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935 kwani historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwaka 1922.
Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinapocheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.
Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.
Habari hizi pia ni simulizi nchini Ghana tembelea:- http://sports.peacefmonline.com/soccer/201111/79235.php
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.