Saturday, August 31, 2024
CCM KIBAHA MJI YATEMA CHECHE ZAKE KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini kimewataka viongozi wa CCM kuanzia katika ngazi za Kata, Wilaya na Mkoa kutoingilia kabisa maamuzi ya wana ccm pamoja na wananchi katika suala zima la kuwachagua viongozi wanaowapenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu kwani wao ndio wanawafahamu vizuri uwezo wao wa kuchapa kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) mwalimu Mwajuma Nyamka wakati wa kikao cha Halmashauri kuu CCM Wilaya ya Kibaha mji ambacho kimefanyika kwa lengo la kuweza kupitisha utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chma.
Nyamka amebaainisha kwamba lengo kubwa la chama cha mapinduzi ni kuhakikisha inaweza kushinda kwa kishindo katika mitaa yote hivyo ni wajibu wa viongozi wote wa CCM kuanzia ngazi za mashina na matawi kushikama kwa pamoja na kwamba kutokana na kazi nzuri ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika miradi mbali mbali ya maendeleo watatembea kifua mbele katika kuomba kura kwa wananchi.
Kadhalika Mwenyekiti huyo aliwapongeza madiwani wa Halmashauri ya mji Kibaha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega katika suala zima la utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwa sambamba na kutatua kero na changamoto za wananchi.
"Pamoja na juhudi kubwa ambazo zinafanywa na CCM kusimamia utekelezaji wa Ilani lakini bado kuna baadhi ya watendaji wa mitaa,na kata wamekuwa ni kama tatizo kubwa kwa wananchi kiasi cha kupelekea kuwakwaza kwa kiasi kikubwa kutokana na kutoa lugha zisizokuwa na staha kabisa na kwamba hawataweza kuwawafumbia macho hata kidogo watendaji wa namna hiyo kwani watatupunguzia kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa,"alisema Nyamka.
Pia katika Katika kikao hicho Mwenyekiti Nyamka amesema kwamba wameiagiza Halmashauri ya mji Kibaha kuhakikisha kwamba wanaitunza miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo imemalizika hususan katika miundombinu ya barabara.
"Tumepitisha utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu wa 2024, lakini kitu kikubwa tumeagiza halmashauri yetu ya mji kuitunza miundombinu ya barabara hasa katika maeneo yenye lami kwani kumukuwa na changamoto ya kutozitunza maana utakuta maeneo mengine nusu kifusi cha mchanga na nusu lami,"alibainisha Nyamka.
Aidha Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kuna baadhi ya halmashauri nyingine wameweka mikakati ya kuzitunza barabara zao kwa kuzifanyia usafi na kuzifagia lakini kwa upande wa Halmashauri ya kibaha mjini jambo hilo linakuwa ni vigumu hivyo linapaswa kufanyiwa utekelezaji.
Pia Mwalimu Nyamka amesema kwamba kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara ambao unafanywa na baadhi ya madereva kupitisha magari ya mchanga yenye uziti mkubwa ambayo ndio yamekuwa ni moja ya chanzo cha kufanya barabara ziweze kuharibika kwa haraka.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Issack Kalleiya ametumia kikao hicho kutoa pongezi kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya mji Kibaha kwa kuweza kubuni vyanzo vipya amabvyo vimepelekea kuongeza zaidi ukusanyaji wa kasi ya kuongeza mapato.
Kadhalika Katibu kalleiya amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, madiwani,pamoja na Mbunge kwa kuweza kushikamana kwa pamoja katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amemshukuru na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika Halmasshauri ya mji wa Kibaha ambazo zimeweza kuleta matokeo chanya katika suala zima la kuwasaidia wananchi katika miradi mbali mbali za maendeleo.
Aidha Mkuu huyo alisema kwamba kwa ushirikiano mkubwa ambao anaupata kutoka kwa viongiozi wa chama cha mapinduzi (CCM) Madiwani wote pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini,mkurugenzi wameweza kutekeleza Ilani ya chama kwa kiwango kikubwa ikiwemo kumsaidia Rais katika utekelezaji wa majukumu yake.
DIWANI KAMBI AFANYA KWELI ATOA MSAADA WA PHOTOCOPY MASHINE SHULE YA MSINGI VISIGA
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Kambi amesema kwamba amesema kwamba ameamua kutoa msaada huo kutokana na kubaini katika shule hiyo kuna uhitaji mkumbwa kupeleka mashine hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia walimu na wanafunzi ambao wamekuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo kutumia gharama kubwa hivyo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao.
"Mimi kama Diwani wa kata ya Visiga nimebaini kuna changamoto kubwa na wazazi na walezi kuchanga michango mbali mbali kwa ajili ya kutoa nakala za mitihani hivyo kunatumika gharama nyingi sana kwa hivyo nikaona kuna umuhimu mkubwa kupitia mahafali haya niweze kutoa mashine hii ya Photocopy ambayo nina amini itaweza kuleta mageuzi makubwa katika shule hii ya msingi Visiga,"alisema Mhe. Kambi
Pia aliongeza kwamba lengo lake kubwa ni kuweza kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo hivyo ameahidi kuendelea kutoa sapoti katika shule nyingine zilizobaki ili kuweza kukuza na kuboresha sekta ya elimu kwa ngazi ya msingi na Sekondari katika Kata ya Visiga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya shule ya Visiga Kasmir Komba amempongeza kwa dhati Diwani huyo kwa kuweza kutoa mashine hiyo ambayo itaweza kwenda kupunguza changamoto ya siku nyingi ambayo ilikuwa inawakabili katika suala zima la kutoa nakala mbali mbali hasa katika kipindi cha kutolea mitihani na mambo mengine ya muhimu.
Mwenyekiti huyo aliongeza kwamba shule hiyo ambayo imeaanzishwa mnamo mwaka 1992 imekuwa ikifanya vizuri kwa wanafunzi wake katika mitihani mbali mbali japo inakabiliwa na baadhi ya changamoto mbali mbali zikiwemo uhaba wa madawati, pamoja na uchakavu wa madirisha kwa baadhi ya madarasa.
Nao baadhi ya wazazi ambo wamehudhuria katika mafali hayo akiwemo Zainabu Abdalah hawakusita kutoa pongezi zai za dhati kwa Diwani wa kata ya Visiga ambaye ameweza kuondoa kero ya michango mbali mbali ambayo walikuwa wakichangishwa na walimu kwa ajili ya kutoa nakala za mitihani hivyo mashine hiyo itawaondolea kabisa baadhi ya michango.
Alifafanua kwamba kabla ya kutolewa kwa mashine hiyo hapo awali wazazi na walezi walikuwa wanachangia kiais cha shilingi elfu 1200 ili mtoto aweze kupata huduma ya kufanya mitihani jambo amabalo lilikuwa ni usumbufu mkubwa kutokana na hali ya kipato na uchumi waliyonayo lakini kwa kitendo alichokifanya diwani huyo kinafaa kuigwa kwa viongozi wengine.
MKE WA MBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI KULETA MAGEUZI YA ELIMU SHULE YA MSINGI MKUZA
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
PEPFAR YAUPONGEZA MKOA WA TANGA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA VVU
Na Oscar Assenga, KOROGWE
Friday, August 30, 2024
RUMBA YA UKWELI KUTOKA KWA WANAMUZIKI WA ZAMANI WALIOTOKA KWA WERRASON
DC ARUMERU ASISITIZA UHAKIKI KUKAMILISHWA KATIKA HALMASHAURI ZOTE ZA WILAYA HIYO
Thursday, August 29, 2024
UWT KIBAHA MJI YATEMA CHECHE KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo imeamua kufanya kongamano kubwa la kumpongeza kwa dhati kutokana na kutenga fedha ambazo zimekwenda kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza katika kongamano hilo ambalo limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama na serikali pamoja na jumuiya zake Mwenyekiti wa UW T Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amebainisha kwamba lengo lubwa ni kumpongeza Rais kwa kazi nzuri ambazo amekuwa akizifanya za kuwasaidia wananchi hususan kumtua mama ndoo kichwani.
"Sisi kama umoja wa wanawake UWT Kibaha mjini tumeungana kwa pamoja na kuandaa kongamano hili kwa lengo kubwa la kumpongeza Rais wetu Mama Samia kwani ameweza kufanya mambo makubwa katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuboresha huduma ya afya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, elimu sambamba na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama ambayo imepelekea kumtua mama ndoo kichwani,"alisema Mgonja.
Mgonja alisema kwamba Rais Samia kwa kipindi chake cha miaka mitatu na nusu tangu alipoingia madarakani ameweza kuendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Jimbo la Kibaha pamoja na Mkoa mzima wa Pwani ambayo baadhi yake imeanza kufanya kazi na kuwasaidia wananchi katika maeneo tofauti sambamba na kuongeza kasi ya kuleta uchumi.
Katika hatua nyingine hakusita kumshukuru kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mkurugenzi wa Kibaha mjini, Mlezi wa UWT Selina Koka,Mke wa mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mariam Ulega , pamoja na madiwani wote kwa kushirikiana bega kwa bega katika kuhakikisha kongamano hilo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Selina Koka ambaye pia mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini amesema kwamba amemshukuru Rais Samia kwa kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa vitendo katika Jimbo la Kibaha mjini ambayo imeweza kuleta chachu ya kuwasaidia wananchi katika nyanja tofauti tofauti.
Mama Koka amesema kwamba katika Jimbo la Kibaha mjini Rais Samia ameweza kuleta mageuzi makubwa katika nyanja mbali mbali kwenye kata zipatazo 14 ikiwemo sekta afya, katika kuboresha miundombinu ya zahanati, vituo vya afya, Hospitali, elimu, huduma ya maji safi na salama,nishati ya umeme pamoja na miundombinu ya barabara.
Naye mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mariamu Ulega ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga amewapongeza wanawake wa UWT kwa kuweza kuandaa kongamano hilo kwa lengo la kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwasaidia wananchi katika mambo mbali mbali ikiwemo kuwasogezea huduma za kijamii ikiwemo vituo vya afya, elimu, maji pamoja na mahitaji mengine.
Aliongeza kwamba wanawake wa UWT wameweza kufanya kitendo cha kiugwana kutokana na kutambua umuhimu na mchango mkubwa ambao ameufanya na Rais Samia katika kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo kwa kushirikiana bega kwa bega na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Umoja wa wanawake wa UWT Kibaha mjini katika kongamano hilo limeweza kugusia mambo muhimu ambayo yamefanywa na Rais ikiwemo utoaji wa vifaa vya Tehama,utoaji wa elimu bila malipo,kuboresha fursa za watoto wa kike katika elimu,stahiki za walimu,uboreshaji wa afya, huduma ya maji, pamoja na miundombinu ya barabara.
Wednesday, August 28, 2024
DAWA ZA ASILI ZILIZO HAKIKIWA KUTIBU NGUVU ZA KIUME ZAPAMBA MAONESHO YA TIBA ASILI JIJINI MWANZA
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Aneth Chambo ni Meneja Masoko wa Kampuni ya IPhytos Tanzania Co. LTD kutoka jijini Arusha, kampuni inayojihusisha na Utafiti, Uchunguzi wa mimea tiba ambayo ni sahihi kwa utengenezaji wa dawa asili za binadamu ambazo zinatengenezwa kwa njia ya teknolojia ya Sayansi ya Computer. #nguvuzakiume #tibaasili #FurahishaMwanza #mwanza #samiasuluhuhassanTuesday, August 27, 2024
Benki ya CRDB, Visa kutoa punguzo la asilimia 22 kwa abiria wa Qatar Airways wanaolipa kwa Tembocard Visa
REA YAMTAKA MWENDELEZAJI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MAGUTA MKOANI IRINGA KUONGEZA KASI
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lung'ali Natural Resources Co. Ltd alipotembelea Mradi wa kufua umeme wa Maguta kwa kutumia maporomoko ya maji
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage akielekeza jambo alipotembelea Mradi wa kufua umeme wa Maguta kwa kutumia maporomoko ya maji.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lung'ali Natural Resources Co. Ltd alipotembelea Mradi wa kufua umeme wa Maguta kwa kutumia maporomoko ya maji
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage (kushoto) akikagua miundombinu ya Bwawa la mradi wa kufua umeme wa Maguta.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage akielekeza jambo alipotembelea Mradi wa kufua umeme wa Maguta kwa kutumia maporomoko ya maji.
Na Mohamed Saif- Iringa
Serikali imemtaka Mwendelezaji wa Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji wa Maguta uliopo katika Kijiji cha Masisiwe Wilayani Kilolo Mkoani Iringa kuukamilisha kwa wakati.
Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage ametoa maelekezo hayo Agosti 26, 2024 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao umefikia asilimia 95.
Mradi unatekelezwa na Mkandarasi ZECO ambaye Makao Makuu yake yapo Nchini Italia. Mwendelezaji ametakiwa kuhakikisha makubaliano ya utekelezaji wa mradi kati yake na ZECO yanatekelezwa kwa wakati ili mradi ukamike ifikapo Desemba 2024.
"Hatua iliyofikiwa inaridhisha; hakuna kikwazo kinachosababisha mradi uchelewe, Mkandarasi anapaswa kuhakikisha ifikapo Desemba mwaka huu awe amekamilisha na umeme umeingia kwenye Gridi ya Taifa," ameelekeza Mhandisi Advera.
Mhandisi Advera amefafanua kuwa mradi umesanifiwa kuzalisha Megawati 2.4 na kwamba unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza inayoendelea hivi sasa itazalisha megawati 1.2.
Amesema licha ya kuongeza umeme kwenye Gridi ya Taifa, mradi utazalisha ajira kwa wananchi wa eneo la mradi, utapunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, ni rafiki kwa mazingira, utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme kwenye maeneo mengi na hivyo kuleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Kilolo na maeneo mengine.
"Kukamilika kwa mradi huu kutakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na maeneo mengine pia; umeme ni injini ya uchumi hivyo tunatarajia kuona maendeleo makubwa baada ya kuanza uzalishaji wa umeme," amesema.
Mhandisi Advera amebainisha kuwa mradi unatumia Nishati Safi na Salama kutokana na maporomoko ya maji hivyo ili uwe endelevu ametoa wito kwa kila mwananchi kulinda na kutunza mazingira ya maeneo ya vyanzo vya maji.
"Umeme unaokwenda kuzalishwa hapa ni wa maporomoko ya maji, sasa tusipolinda mazingira yanayozunguka hivi vyanzo vya maji yaani hii Mito tutasababisha mradi ushindwe kutupa matokeo tunayoyatarajia," amesisitiza Mhandisi Advera.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi kwa ujumla, msimamizi wa mradi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lung'ali Natural Resources Co. Ltd inayosimamia mradi huo kwa niaba ya Kanisa Katoliki-Parokia ya Jimbo la Iringa, Padri Luciano Mpoma ameishukuru Serikali kwa mchango wake katika kuhakikisha mradi unakamilika.
Amesema mradi unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Mitaji kwa ajili ya Maendeleo (UNCDF).
"REA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mradi unafanikiwa na unaleta manufaa yanayokusudiwa. Mara zote wamefika hapa kukagua na kutushauri tunawashukuru sana," amepongeza.
Miongoni mwa majukumu ya msingi ya REA ni pamoja na kuwezesha ujenzi wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati Jadidifu ambayo ni Nishati Safi na Salama.