Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa pamoja na mke wake Selina Koka nyumbani kwao mtaa wa Vigaeni Wilayani Kibaha na Kalani wa sensa na mjumbe wa shina la Mkoani 'A'Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha .mjini Silvestry Koka leo mapema akiwa na mke wake Selina Koka wameshiriki kikamilifu zoezi la Kuhesabiwa huku akiwasisitiza wananchi wa Jimbo lake kutoa ushirikiano kwa mawakala wa Sensa ambao wanapita kwa lengo la kujua taarifa mbali mbali ambazo zinawahusu wananchi.
Koka ameshiriki kuhesabiwa zoezi hilo la sensa ya watu na makazi akiwa na mke wake nyumbani kwao katika mtaa wa Vigaeni kata ya Tumbi Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani Sambamba akiwa na familia yake.
Mbunge huyo baada ya kuhesabiwa alisema kwamba zoezi hilo limefanyika salama na kubainisha kuwa taarifa zote ambazo ameulizwa ameweza kuzijibu ipasavyo kwa kalani wa sensa ambaye alifika nyumbani kwake kwa lengo la kufanya zoezi hilo.
"Tunashukuru zoezi hili limefanyika vizuri na mm nimeweza kupata fursa ya kuweza kuhesabiwa nikiwa pamoja na mke wangu na familia yangu na kikubwa naweza kusema zoezi kimemalizika salama na tumetoa ushirikiano wa kutosha katika zoezi hili,"alisema Koka.
Pia Mbunge huyo alibainisha kuwa umuhimu wa zoezi hilo la kuhesabiwa kutaweza kuisaidia serikali kupata takwimu halisi ya wananchi wake lengo ikiwa ni kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Kadhalika Koka alimpomgeza Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta chachu ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo Sambamba na kuwahimiza wananchi kujitokeza katika suala zima la kuhesabiwa.
Naye mmoja wa makalani wa zoezi hilo la sensa Mariam Mohamed amesema kuwa zoezi hilo limeanza tangu asubuhi japo kulikuwa na changamoto ya mvua lakini wananchi wamekuwa na hamasa katika kuhesabiwa.
"Zoezi la sensa ya watu na makazi tumelianz mapema ya asubuhi na tumepita katika maeneo mbali mbali ikiwemo kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini ambaye tumemkuta nyumbani kwaki mtaa wa Vigaeni akiwa pamoja na mke wake na ametupa ushirikiano wa kutosha,"alisema Kalani huyo.
Katika hatua nyingine mke wa Mbunge huyo Selina Koka ameeleza kuwa ameshiriki kikamilifu katika kuhesabiwa na kwamba zoezi hilo limekwenda vizuri na wamehesabiwa yeye pamoja na familia yake.
Pia mama Koka alisema kwamba matarajio yake makubwa katika zoezi hilo la sensa ni kuwa litaweza kusaidia katika kufahamu idadi ya wananchi ili serikali iweze kupanga mambo yake ya kimaendeleo
Mjumbe wa shina namba tatu kutoka mkoani 'A' Jestina Lewis alisema kwamba wananchi wa Jimbo la Kibaha wameonekana kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makalani ambao wamekuwa wakipita katika maeneo mbali mbali.
Kadhalika amemshukuru Mbunge wa Jimbo kwa kuweza kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo Sambamba wa kuwahimiza wananchi wake kuweza kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
Katika Jimbo la Kibaha mjini pamoja na maeneo mengine ya Wilayani Kibaha wananchi wake tangu asubuhi wameonekana kuhamasika katika kushiriki katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi.