Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameshiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa akiwa katika makazi yake ikungi singida
Zoezi la kuhesabiwa limeongozwa na karani wa sensa ya watu na makazi Bi. Scovia mkempia deus akiwa pamoja na mwenyekiti wa kitongoji cha gairo kijiji cha ikungi Bw. Justin juma mghwai
Dc Muro pia amewapongeza sana waratibu na wasimamizi wa zoezi hilo wakiwemo karani na mwenyekiti kwakufanya kazi yao kwa uadilifu na umakini mkubwa uku wakiwa wakarimu na waungwana katika uulizaji wa maswali
Dc Muro ametoa rai kwa wananchi wote wa ikungi kuendelea kuwapokea na kuwapa ushirikiano wa kutosha makarani wetu wa sensa ili waweze kuifanya kazi hii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa katika zoezi hili la sensa ya watu na makazi 2022
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.