ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 8, 2017

ZAIDI YA WATU 70 WAOKOLEWA LEO KUTOKANA NA MAFURIKO YALIYOTOKANA NA MVUA KUBWA


Faustine Ruta, Bukoba
 ZAIDI ya watu 70 wameokolewa na Serikali baada ya kukumbwa na mafuliko yaliyotokana na mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 9 usiku. 

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo wakati alipo hojiwa na waandishi wa habari katika Kata ya Bakoba mtaa wa nyakanyasi. 


Kinawilo alisema kuwa nyumba zote zilizoko kandokando ya mto kanoni zote zimeathiliwa na maji kiasi kwamba tumetumia mitumbwi ya uvuvi kuvusha watu.

“Niseme tu mpaka sasa hakuna kifo chochote kile Zaidi ya vitu kuhalibika kwa kulowa maji”alisema kinawilo.


Aidha mkuu wawilaya alisema kuwa kuwa wananchi wachukue tahadhali pindi mvua zinapo nyesha tu watoke nje ya nyumba kwa usalama Zaidi. 


Naye Josefati Bonge mkazi wa Omukigusha alisema kuwa katika nyumba yake hakuna kilichobakia kikiwa kizima kwani nimetoka mimi kama nilivyo na ninamshukuru mungu familia yangu haikuwepo. 


“Kiukweli kuna kila sababu ya kuhama maeneo kama haya maana nihatali kwa binadamu mfano’ waliokuwa wamelala fofo wanahali gani hivyo kunatakiwa kuchua hatua mapema ili kuhamia sehemu stahiki”alisema Bonge 


Anitha Mziba mkazi wa Nyakanyasi alisema kuwa yeye katika familia yake hakuna alie umia Zaidi ya vitu vyote vyandani hakuna kilichotoka.

“Yani nimewabeba watoto wangu begani mmoja baada ya mwingine wakati huo mimi maji yakiwa yamenifikia kwenye shingo kwakweli nihatali”alisema Mziba







Wakaazi wa hapa Tangu usiku saa 9 waliondoka!
Mkazi wa Omukigusha akisaidiwa kuvutwa juu baada ya kuanguka shimoni asubuhi leo kwenye mufda wa saa nne. Picha na habari na Faustine Ruta



Prince Motel


Crane Lodge and Tours



Hii ni nyumba ya Wageni...lakini inasemekana Usiku hawakupata usingizi kabisa!
Hivi ndivyo ilivyokuwa Asubuhi ya leo
Eneo la Ziwa Victoria...Ufukweni

Ufukweni Ziwa Victora

Patashika wakazi wakiokoa Nyasi kwa ajili ya Mifugo yao

Mkazi wa Nyakanyasi akivuka huku akiwa hana matumaini Aendako


Katikati ya Makazi ya watu Eneo la Nyakanyasi Mitumbwi imefanya kazi



Okoa okoa ikiendelea eneo la Nyakanyasi Mjini Bukoba leo hii



TAARIFA:- ROMA MKATOLIKI NA WENZAKE WAPATIKANA.

CHANZO: Global Publisher 
Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar.

Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

Friday, April 7, 2017

Burundi: WAPIGANAJI WA KAGAME NDIYO WALIOTUNGUA NDEGE ALIYOKUWA AMEPANDA CYPRIEN NTARYAMIRA, RAIS WA ZAMANI WA BURUNDI.

Mabaki ya ndege aliyokuwa ameipanda rais huyo wa zamani wa Burundi aliyeongoza kwa miezi miwili pekee.
Serikali ya Burundi imeadhimisha hapo jana mwaka wa 23 tangu kuuawa kwa Cyprien Ntaryamira, rais wa zamani wa nchi hiyo. 

Ntaryamira alipoteza maisha katika ajali ya ndege kwenye anga ya mji wa Kigali, Rwanda ambayo hata hivyo serikali ya Bujumbura imeitaja kuwa ilifanywa na wapiganaji wa Rais Poul Kagame wa Rwanda.
  
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Bujumbura kuituhumu moja kwa moja serikali ya Kigali kuhusika katika tukio hilo.

AFUNGWA MIKONO NA MIGUU KWENYE BAISKELI KISHA ATOSWA ZIWA VICTORIA.

Wakati familia kadhaa za watanzania zikiendelea kupoteza ndugu zao bila kujulikana walipo, leo huko mkoani Mara katika ufukwe wa ziwa Victoria imeokotwa maiti ya mtu mmoja asiyefahamika ikiwa imetupwa ziwani.

Mazingira ya kifo chake yanaonesha mtu huyo mwanaume aliuawa, akafungwa kama kifurushi kwenye baiskeli, kisha yeye na baiskeli yake wakatoswa ziwani. Hapa ndipo tulipofika kama taifa.! TAHADHARI: Picha zinaweza kusababisha usumbufu kisaikolojia maana ni za kuogofya.


MBELE YA BEN POL, JOH MAKINI NA JUX, HUYU NI MMOJA YA MA-DJ WATAKAO ONGOZA SHOW YA MKESHA WA PASAKA MWANZA

Mnaouliza nani aketie on wheels za chuma nowadays ndani ya lile likipindi lako unalolizimikia la mida ya 5 HADI 7 mchana #KAZINANGOMA = Ladies and gentlemen let me introduce to you moja kati ya ma-Dj watakao kibengisHa tarehe 15 April 2017 #MkeshaWApasaka eneo la tukio #Unyamwezini @chrissthedj @chrissthedj @chrissthedj @chrissthedj CC:- @mansourjumanne @gsengo @jembenijembe

VIDEO:- WASANII WAUNGANA KUMSAKA ROMA.

East Africans love Tanzania's Hip Hop star @roma2030. How can he and his friends disappear without a trace?

What crime did he commit? Alikamatwa na majambazi au polisi? Kama ni polisi, kosa lake ni lipi? Kama ni majambazi hatua gani imechukuliwa kuwatafuta? Ni maswali ambayo yanaumiza vichwa watu na bado hayajapata majibu mpaka sasa............ 


Lets join hands kusupport wasanii wengine na kusikitika na Familia ya Roma, J Rider na Monii katika kipindi hiki kigumu. Tuiombee nchi yetu Amani na Utulivu. Mungu awalinde popote walipo na warejee wakiwa salama #WakinaRomaWakoWapi


BREAKING NEWS: Mkewa Roma ashindwa kujizuia, aangau kilio mbele ya wandishi wa habari, ashindwa kuendelea kuongea, atolewa huku akilia. Wasanii Waungana Kumsaka ROMA, Wakutana COCO Beach wakiwa na nyuso za huzuni!

WAPINZANI WAILAUMU SERIKALI YA RWANDA KWA KUSEMA KUWA MSAMAHA WA PAPA FRANCIS KUHUSU MAUAJI YA ALAIKI RWANDA, UNATOSHA.

Mauaji ya Rwanda.
Serikali ya Rwanda imetupilia mbali baadhi ya madai ya wakereketwa ambao awali walisema kuwa, Papa Francis hajaomba msamahama ipasavyo kuhusu ya namna Kanisa Katoliki duniani lilivyohusika katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda. 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema kuwa, hatua aliyoichukua kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki ni ya hekima kubwa.
 
 Papa Francis
Hii ni baada ya kiongozi huyo wa kidini kuliomba taifa la Rwanda msamaha kwa kuhusika kwake katika mauaji hayo ya mwaka 1994 ambayo zaidi ya watu milioni moja waliuawa nchini humo.

FARU FAUSTA ALITIKISA BUNGE.

WAKATI kishindo cha faru dume aitwaye John kikitulia baada ya kubainika kuwa alifariki na serikali kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na chanzo cha kifo chake, faru mwingine jike aitwaye Fausta alitwaa nafasi ya mjadala bungeni mjini Dodoma jana kuhusiana na gharama za kumtunza kwa mwezi.

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa kuhusiana na faru huyo ambaye pia yupo katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha kama ilivyokuwa kwa faru John, ni kwamba gharama za kumtunza kwa mwezi ni Sh. milioni 64 na hivyo kushtua baadhi ya wabunge kiasi cha kuibua maswali.

Kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe, mshahara wa mbunge mmoja kwa mwezi kabla ya makato ni takribani Sh. milioni 3.6, hivyo gharama hizo za kumtunza Faru Fausta ni sawa na wastani wa mishahara ya wabunge 17 kabla ya makato.

Aliyeibua suala hilo la Faru Fausta ni Mbunge wa Babati Mjini(Chadema),Pauline Gekul, ambaye alidai kushtushwa na kitendo cha Hifadhi ya Ngorongoro kutumia kiasi cha Sh. Milioni 64 kwa mwezi sawa na Sh.Milioni 768 kwa mwaka kumlisha na kumtunza faru huyo.

Akiuliza swali la nyongeza kwa Waziri wa Maliasili na Utalii bungeni jana, Gekul alisema faru huyo amekuwa akigharimiwa fedha nyingi na kuhoji serikali ina mpango gani kuhusiana naye.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, alikiri faru huyo kutunzwa kwa gharama kubwa kwa ajili ya kumlisha kwa sababu ni mzee.

Alisema mbali na hilo, mnyama huyo pia huandamwa na magonjwa mbalimbali na ndiyo maana ana gharimiwa kwa fedha zinazoonekana kuwa ni gharama kubwa.

Aidha, Prof. Maghembe alisema wanafanya hivyo pia kwa sababu wanyama wa aina hiyo ni wachache katika hifadhi nchini.

“Hivi sasa utafiti unafanyika kwa kumtumia faru Fausta juu ya namna ya kuishi na wanyama wa aina hiyo ili waweze kuishi maisha marefu… ni kweli kufanya hivi ni gharama kubwa lakini takwimu zinazopatikana zina thamani halisi,”alisema.

Pamoja na majibu hayo, Waziri Maghembe aliendelea kubanwa kuhusiana na gharama za faru huyo. Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka, aliomba mwongozo baada ya kipindi cha maswali na majibu kuhusu majibu ya waziri huyo juu ya faru Fausta kutunzwa kwa fedha hizo huku ikielezwa kuwa ni mzee ilhali ikifahamika kuwa kwa hali yake, kamwe mnyama huyo hawezi kuingiza faida yoyote.

Akijibu muongozo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema katika hifadhi hiyo yupo pia Faru Ndugai na kumwambia waziri kwa kutania kuwa siku faru huyo (Ndugai) akitoweka patachimbika bungeni.

Hata hivyo, kuhusiana na swali kuhusu faru Fausta, Ndugai alisema suala hilo analiachia wizara ili wakalifanyie kazi.

TAARIFA ZAIDI KUHUSU FARU FAUSTA
Kwa mujibu wa Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro, Dk Freddy Manongi, ambaye alizungumza na Nipashe hivi karibuni, ni kwamba faru Fausta ni mzee mwenye miaka 54 na kwamba, alipokuwa porini alikuwa akishambuliwa na fisi na kupata vidonda vingi.

Alisema baada ya kumwona fausta akiwa katika hali mbaya kiafya na pia kuwa katika hatari kubwa ya kuuawa na fisi kutokana na uzee wake, askari wa uhifadhi walimchukua na kumtengea eneo maalum huku wakilazimika kimnunulia chakula kama miwa kutoka wilayani Babati na pia kumpatia huduma nyingine muhimu.

Alisema kutokana na jitihada zinazofanyika katika kumtunza, hivi sasa vidonda aliyokuwa navyo vimepona na anaendelea vizuri.

Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka kwenye hifadhi hiyo jana zilidai kuwa kutokana na umri wake mkubwa, faru huyo hivi sasa ana tatizo la kutoona na jambo hilo linamuweka katika wakati mgumu kimaisha ikiwa ataachiwa aishi porini bila ya uangalizi maalumu.

*Taarifa ya ziada na John Ngunge (Arusha) na Salome Kitomari (Dar)

FARU FAUSTA ATAFUNA MILIONI 768, MBUNGE AGONGWA NA PIKIPIKI DODOMA, BOSI WA FREEMASON TZ AFARIKI, HALIMA MDEE ANASA MTEGONI.

Spika: Halma Mdee atiwe pingu, Mbunge agongwa na pikipiki Dodoma, bosi wa Freemason Tanzania afariki. 
 
Dk.Shein awaonya wapenyeza rushwa, Roma Mkatoliki alivyotekwa nyara studio, Halima Mdee anasa mtegoni, Faru Fausta atafuna milioni 768. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.

Thursday, April 6, 2017

VYAMA VYA SIASA VYARUHUSIWA KUJIHESABIA KURA KENYA.

CHANZO:- BBC
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kuruhusu vyama vya kisiasa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Hata hivyo tume hiyo ilisema kuwa ndiyo ina ruhusa ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa Nasa, utabuni kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Viongozi wa upinzani wanasema kuwa kuwepo kituo hicho itasaidia kuzuia udanganyifu kwenye uchaguzi.

Rais Uhuru Kenyatta anawania uchaguzi kwenye muhula wa pili na anatarajia kuukabili mungano wa vyama vikuu vya upinzani.

TANZANIA YANG'ARA VIWANGO VYA FIFA, YAPANDA NAFASI 22 JUU.

TANZANIA imepanda Kwa nafasi 22 kwenye viwango vya FIFA duniani kutoka nafasi ya 157 kwa mwezi wa pili na sasa imeshika namba135. Hii inatokana na Stars kufanya vizuri kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya Botswana waliyoshida kwa magoli 2-0 na Burundi iliyoshinda kwa magoli 2-1.

Pia Brazil imeipiku Argentina kwenye nafasi ya kwanza kwa mwezi wa tatu Argentina ilikuwa nafasi ya kwanza kwa mwezi wa pili huku Brazil wakiwa nafasi ya pili. Haya ndio mataifa kumi yanayoongoza kwenye viwango vya soka Duniani 1. Brazil 2. Argentina 3. Germany 4. Chile 5. Colombia 6. Ufaransa 7. Ubeligiji 8. Ureno 9. Uswisi na 10. Hispania.

Mataifa 10 yanayongoza Afrika, kwenye mabano ni nafasi zao za viwango vya ubora duniani.

1. Misri (19) 2. Senegal (30) 3.C ameroon (33) 4. Burkinafaso (35) 5. Nigeria (40) 6. DR Congo (41) 7. Tunisia (42) 8. Ghana (45) 9. Ivory Coast (48) 10. Morocco (53)

Kwa Afrika Mashariki Uganda inaendelea kuongoza ikiwa nafasi 72 ikiwa imepanda nafasi 3 kutoka 75 ya mwezi wa Pili, Kenya nafasi 78 nayo ikiwa imepanda Kwa nafasi 10 kutoka 88 ya Mwezi uliopita wakati Rwanda yenyewe inakamata nafasi ya 117 ikiwa imeshuka kwa nafasi 17 kutoka nafasi ya 100 ya mwezi uliopita na Burundi ambao ilifungwa na Tanzania ipo katika nafasi ya 141 nayo ikiwa imeporomoka kwa nafasi 3 kutoka nafasi ya 138 ya mwezi wa pili.

TANESCO YAKABIDHI MRADI WA UMEME KWENYE SHULE YA MSINGI GARAGAZA HUKO KIBAHA

 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akipena mikono na Afisa Elimu, (Taaluma), mkoawa Pwani, Bw.Shirley Membi Swai, wakati wa makabidhiano ya mradi wa uwekaji umeme katika shule ya Msingi Galagaza, kata ya Msangeni, Kibaha kwa Mfipamkoani Pwani, Aprili 7, 2017. Mradi huo una thamani ya Shilingi Milioni 10. Anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw.Shaaban Langweni

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi mradi wa umeme kwenye majengo ya shule ya msingi Galagaza iliyoko, kata ya Msangani wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Akikabidhi mradi huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 10, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo leo Aprili 7, 2017, Meneja wa TANESCO, Mkoani Pwani, Mhandisi Martin Madulu, alisema “mradi ulihusisha utandazaji nyaya za umeme (wiring installation),  ufungaji wa power circuit- breaker, taa, pamona na ufundi kwenye majengo yote ya shule ikiwemo ofisi ya walimu”. Alifafanua meneja huyo.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Madulu alisema, “tumeona tuwaunge mkono shule kwenye level ya msingi kwani ni maandalizi mazuri kwa wataalamu wa baadaye kwani sasa mazingira yatakuwa mazuri kwa kusoma, pia mazingira yatakuwa mazuri kwa walimu kuandaa masomo yao na tunaamini italeta matokeo chanya.” Alisema.
Alisema, TANESCO imeamua kusaidia shule hiyo katika harakati za shirika kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi, lakini pia kuhamasisha umma kutumia umeme.
“Ni fursa kwenu kutumia vizuri umeme huu, ili muweze kufanya vizuri zaidi katika masomo yenu, tunategemea kiwango cha ufaulu kitaongezeka kwani hivi sasa mnaweza kutumia fursa mbalimbali za kupata elimu kama matumizi ya kompyuta, ambazo zinahitaji uwepo wa umeme.” Alifafanua.
Akipokea mradi huo, Afisa Elimu (Taaluma) wa Mkoa wa Pwaniambaye alimwakilisha Afisa Elimu wa Mkoa huo, Bw.Shirley Membi Swai, aliishukuru TANESCO kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi na walimu kutumia vizuri uwepo wa umeme shuleni hapo kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwani sasa mazingira ya kusoma ni mazuri zaidi.
“ Huu ni mchango mkubwa sana katika maendeleo ya elimu nchini, msaada huu umekuja kwa muda muafaka kwani hivi sasa, serikali tayari imeanza kufundisha TEHEMA katika shule na kufundisha kwa kutumia mtandao (digital learning na tayari umeshaanza hapa nchini, ambapo wanafunzi na walimu wameanza kutumia kompyuta ndogo (tablets).” Alisema.
Pia nawashukuru TANESCO kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwapatia wanafunzi elimu bure, msaada huu unaongeza chachu ya kufanikisha azma hiyo ya serikali.

Mhandisi Martin Madulu, akitoa hotuba yake
 Bw.Shirley Membi Swai, akitoa hotuba yake
 Afisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Salama akizungumza wakati wa utangulizi wa hafla hiyo
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Galagaza
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Galagaza, Bw. Shaaban Lagweni, akiwatambulisha walimu wenzake
 Sehemu ya majengo yaliyowekewa umeme na TANESCO kama msaada
 Wanafunzi wakipiga makofi kushangilia hotuba
 Mwalimu Echi Mkopi, akisoma risala
 Kwaya ya shule ikiburudisha
 Mgeni rasmina uongoziwa TANESCO wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananfunzi
  Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Pwani, Mhandisi Martin Madulu, (kushoto), akimuonyesha Afisa Elimu (Taaluma), Bw.Shirley Membi Swai,moja ya vifaa vilivyofungwa na TANESCO katika mradi huo

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani waliohudhuria hafla hiyo wakibadilishana mawazo