Wananchi waathirika wa mgogoro wa maeneo ya Nyandoto wamemwagia sifa Naibu waziri nyumba maendeleo na makazi,Angelina Mabula kwa kuingila kati mgogoro wao baina ya halmashauri ya mji wa Tarime.Mgogoro huo umeendelea kufukuta licha ya kuwa Naibu huyo aliutolea majibu pindi wananchi hao walipofika Mjini Musoma Agost mwaka 2020 akiwa katika ziara ya kikazi na kumtaka kuwasaidia ambapo alisema nimesikiliza pande zote mbili nimegundua kuwa halmashauri ilipima maeneo hayo bila kuwashirikisha walengwa.
Katika mazungumzo hayo na Wananchi hao Mabula aliongeza kuwa baada ya kuwasikiliza,natoa maelekezo halmashauri irudi ipime maeneo hayo upya kwa upimaji shirikishi kwa kutumia wataalamu wa serikali na wananchi wa maeneo hayo wapewe kipaumbele kulipia gharama za upimaji na atakaye shindwa kulipia hatua zaidi zitachukuliwa.
Mmoja wa wananchi hao,Anna Nguru alisema kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha watu wa halmadshauri na Polisi kuwa wahanga hao walienda Musoma kumuona Naibu waziri akiwa katika ziara ya kikazi walipofika na kutoa kilio chao,Mabula aliwasikiliza na kutoa majibu,baya hapo akawaahidi kwenda kuongea na watu wahalmashauri ya Mji wa Tarime na kuwapa maelekezo hayo aliyoyatoa cha ajabu agizo halikutekelezwa ambapo watu wa halmashauri walidai kuwa Naibu huyo kama aliwarudishia maeneo yao ingebidi awape barua kama sivyo wanaendelea na mchakato wao wa awali wa kugawa viwanja kwa atakaye hitaji kununua.
Neema Timothy aliuliza swali la kutaka kujua kama kweli halmashauri inadai maeneo niyao kwasababu gani wanakuja na dola kwa maana ya polisi wakiwa na silaha wakati wa zoezi la kugawa viwanja na kwenye mikutano ya wananchi wanahofu gani na mali niyao.
Pia Neema aliongeza kuwa kama halmashauri inadai Naibu waziri aliwapa barua ya maelekezo tofauti na walioambiwa mkutanoni Musoma halmashauri ingepaswa kutoa barua hiyo na kuwasomea hadharani wananchi ili kujiridhisha lakini wanasema kwa maneno matupu kuwa Mabula aliwabariki kuendelea na zoezi ila wawape kipaumbele wananchi wapale kwa kuwagawia kiwanja kwanza.
Naye Butebi Moya awali alisema kuwa wananchi hao wanania nzuri na halmashauri yao cha msingi wanaomba kupimiwa na viwanja vitakavyo patikana wagawane kwa kufuata uwiano na pia walitoa mda mrefu tangu mwaka 2014 mgogoro ulipoanza na wamefika kila Ofisi ya serikali wakilalamika bila kusaidiwa mdipo wakaamua kwenda kwa Naibu Waziri nyumba maendeleo na makazi ambapo aliwasaidia lakini cha ajabu halmashauri inakaidi ambapo sasa tayari wameweka zuio la kutaarifu halmashauri Tarime mji kuwa wanataka kwenda kuishitaki mahakamani.
Samo Nyang’anyi ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Nyagesese alisema kwenye kikao hicho kuwa mgogoro huo umedumu kwa mda mrefu na halmashauri wakati inafanya mchakato wote hawajawahi kumshirikisha kama mwenyekiti wa eneo husika ambapo jana alitangaza kutoshiriki katika zoezi lolote la halmashauri katika mgogoro huo na kuwa halmashauri wafanye wenyewe.
Mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kushukuru serikali iliyopo madarakani chini ya Mama Samia Suluhu Hassani ambapo alitumia nafasi hiyo kumwambia kaimu mkuu wa kituo cha polisi Tarime Mjini aliyefika katoka kikao hicho kuwa ni bora amefika katika kikao hicho amejionea hali halisi baina ya halmashauri na wananchi wa mgogoro wa Nyandoto.
Mwenyekiti huyo alitupia halmashauri lawama ya kuto mshirikisha na kutokuwa karibu na wananchi wanaokaa na kumiliki maeneo hayo ambapo alisema kama halmashauri ina ushahidi kuwa wanawashirikisha kila zoezi je nilini walikuja na kuwatangazia wananchi kuwa viwanja vilivyopimwa ni vingapi na atakaye kuwa anahitaji kununua au kumilikishwa anatakiwa kufuata taratibu gani hilo halijawahi kutokea alisema.
Kwa upande wake mwanasheria wa halmashauri hiyo,Haruna Matata alisema kuwa halmashauri imeandaa utaratibu wa kugawa viwanja kwa watakao hitaji kununua huku kipaumbele kikiwa cha watu 33 waliokutwa na ramani na kuwa watu hao watapewa bure kiwanja bila kutozwa hata shilingi moja,
Mwanasheria huyo aliongeza kuwa halmashauri imepanga Desemba 14,2021 itaenda kuwaonyesha viwanja waliokwisha lipia na kuwaonyesha wenye uhitaji wa kununua kwa hali hiyo wanaomba ushirikiano.
ASP Maskamo Petro alisema kuwa wananchi hao hawana vielelezo vinavyoonyesha kuwa maeneo wanayoyalalamikia niyao badala yake wanavielelezo vya magazeti na TV na kuwa hivyo havitambuliki.
ASP Maskamo aliongeza kuwa katika mkutano huo police hawakujan kuwatisha badala yake wamekuja kwa swala la kisheria kulinda Raia na mali zake na kuwa wapo kisheria na mtu yeyote akiwahitaji kisheria wanaenda bila kujali ambao aliwaomba kutii sharia bila shuruti.