ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 8, 2021

ZAIDI YA 100 WAUAWA KATIKA MAPIGANO YA DARFUR MAGHARIBI MWA SUDAN.

 

Zaidi ya watu 100 wameuawa kufuatia mapigano ya kikabila katika jimbo la Dafur Magharibi nchini Sudan.


Mapigano kati ya Waarabu na wapiganaji wa Kiafrika kutoka jamii ya Masalit inayoungwa mkono na waasi wa zamano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa sasa.


Mapigano katika eneo la Kreinik yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao, wengine wakivuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Chad, Umoja wa Mataifa unasema.


Mmoja wa manusura wa ghasia hizo anasema wanaume waliyojihami walishambulia vijiji vyao magharibi mwa Kreinik, na kuanza kupiga risasi kabla ya kuchoma moto nyumba zao.


Pia waliweka vizuizi katika barabara kuu kuwazuia watu kutoroka.


Waliyojeruhiwa hawana njia ya kupata matibabu ya dharura.


Mapigano mapya ya kikabila yalianza Jumapili kati ya jamii hizo mbili, karibu watu 55 wameuawa.


Miili zaidi ilipatikana msituni na kuongeza idadi ya vifo hadi zaidi ya 100. Makumi ya wengine hawajulikani waliko.


Mwezi uliopita, watu 43 waliuawa katika sehemu tofauti ya Darfur Magharibi.


Mapigano ya kikabila pia yameripotiwa kusini mwa eneo hilo lenye machafuko.


Serikali imetuma kikosi cha pamoja cha vitengo vya kijeshi, jeshi na polisi huko Darfur Magharibi na Kusini ili kujaribu kuzuia ghasia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.