ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 28, 2013

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA YAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA

 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina,sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa. 
  Mmoja wa wasanii wa bongofleva,Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi Washiriki wakifuatilia.
Mmoja wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael akijulikana zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo,ambayo itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba,Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada wengine mbalimbali. 

Mkurugenzi  Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha alipokuwa akiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba.

Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye  semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii. 
 Sehemu ya meza kuu.

MASHABIKI CHELSEA WANYAKUA UBINGWA KOMBE LA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MWANZA

HII LEO KATIKA VIWANJA VYA POLISI MABATINI MWANZA, TIMU YA MASHABIKI WA CHELSEA WAMEIBUKA KUWA MABINGWA WA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MWANZA 2013 BAADA YA KUIFUNGA BARCELONA KWA MIKWAJU YA PENATI.

NI KATIKA MASHINDANO YA SOKA YALIYO VUNJA REKODI KWA KUPATA MAHUDHURIO MAKUBWA KWA MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA MIAMBA (MWANZA) KUJITOKEZA KWA WINGI.

 ZAIDI KUTOKA MWANZA SHAFFI DAUDA NA G. SENGO WALIKUWA MASHUHUDA KAMA JICHO LA SPORTS XTRA WANATIRIRIKA... (BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOJIRI) 

Friday, September 27, 2013

OBAMA AZUNGUMZA NA ROUHANI

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30, viongozi wa Marekani na Iran wamezungumza moja kwa moja.
Rais Barack Obama na mwenzake wa Iran, Hassan Rouhani, wamezungumza kwa simu kwa muda wa robo saa; na kwa mujibu wa Bwana Obama walieleza azma yao ya kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu mradi wa nuklia wa Iran.
Ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kutoka ofisi ya Bwana Rouhani ulionesha hisia kama hizo.
Taarifa kutoka Iran zinaonesha kuwa tukio hilo limefurahiwa nchini humo, hasa kati ya washauri wakuu wa Bwana Rouhani.
CHANZO: bbc Swahili.

HIVI NDIVYO AJALA MBAYA ILIVYOTOKEA LEO ASUBUHI BARABARA YA MAJITA KARIBU NA MAKAZI YA MKUU WA MKOA, KUMRADHI KWA PICHA


4
Askari wa usalama barabarani wakitoa msaada.

                         
NA: BINDA NEWS
Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya mjini musoma kuelekea kamnyonge.

Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.

Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya blog hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa pikipiki Wambura Matiku aliyekuwa nyuma ya pikipiki iliyopata ajali aliiambia blog hii dereva wa pikipiki mara  baada ya kulipita gari hilo aliwahi kuingia upande wa gari na kutokea kwa ajali hiyo.

Hata hivyo jeshi la polisi mara baada ya kumuwahisha majeruhi huyo hospitalini walirejea eneo la tukio na kupima ili kubaini chanjo cha ajali hiyo huku Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui akiahidi kuhitolea taarifa mara baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo

VODACOM YAENDELEA KUTOA MAFUNZO MAONESHO YA WIKI ZA HUDUMA YA KIFEDHA YANAYOENDELEA

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu kushoto akifuatilia kwa umakini jinsi Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude, anavyomuelekeza Bw. Mweusi Mohamed Mweusi, namna ya kifaa cha kuchajia simu kwa kutumia umeme wa Jua (Readset Solar Charger)kinavyounganishwa na kuanza kufanya kazi  leo  Katika banda la kampuni ya Vodacom lililoko katika  maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. 
Mmoja wa maofisa wa Vodacom akitoa maelezo kwa baadhi ya wajasiriamali wanaopata mafunzo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Vodacom imetoa mafunzo kwa wajasiriamali hao ya namna ya kujiunga na kunufaika na fursa ya mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kwa wanawake wajasiriamali  wadogowadogo MWEI.

Thursday, September 26, 2013

KUNDI LA Cash Money, LATOA MSAAA KWA WAGOJWA HOSPITALI YA TEMEKE

Wana kikundi cha Cash Money wakiwa tayali kwa kutoa msaada katika hospitali ya Temeke

Mlezi wa Kikundi cha Cash Money ,Ratifa Masasi kulia akimkabibi muhuguzi wa wodi ya watoto bi, Nuswe Ambokile zawai mbalimbali walizoleta kwa ajili ya watoto waliolaza katika hospital ya Temeke

Baadhi ya wana kikundi cha Cash Money wakiwa katika picha ya pamoja na wahuguzi wa word ya watoto Hospitali ya temeke baada ya kukabidhi msaada

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda  jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za heshima.
Gurumo atatoa  burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki, ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money, la Tandika mjini Dar es Salaam.
"Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na nyimbo zake.
Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi mlezi wa kundi hilo.
Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu zikiwemo Coast na G Five.
Kundi la Cash Money ambalo lilianzishwa mwaka 2011, pia limetoa vitu mbalimbali kwa wodi ya watoto, na vituo vya watoto yatima jana, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo


Mlezi wa kikundi cha Cash Money akimfaliji mama Samir Nassoro, Naomi Ramadhani walipokutana wakati kundi hilo likitoa msaada kwa wagojwa katika hod ya watoto

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Cash Money wakimfariji Bi Naomi Ramadhani

Msanii wa bendi ya Msondo ngoma Saddy Ally katikati akisalimiana na wanakikundi cha cash money walipokutana katika hospitali ya Temeke wakitokea kutoa msaada

Wana kikundi wa chass money kushoto Amina Uredi 'Mmanyema ' na Zulfa Kasongo

Mlezi wa kikundi cha cash money bi, Ratifa Masasa akimfariji mtoto Salimu Ally wakati walipokwenda kutoa msaada katika hospitali ya temeke dar es salaam mwingine ni mama mtoto Tabu Salumu mkadhi wa Tandika

MCHUJO KUPATA WATAKAO WAKILISHA TANZANIA FAINALI ZA POOL TABLE AFRIKA MALAWI WAENDELEA KAMBINI MOROGORO


Kocha wa Timu ya Taifa, Denis Lungu (kulia) akiwaelekeza jambo wachezji wa timu ya Taifa mchezo wa Pool (Safari National Pool Team) wakati wa mazoezi katika kambi inayoendelea mkoani Morogoro ya mchujo wa kuwapata wachezaji 8 kati ya 15, watakaowakilisha Tanzania katika fainali zitakazo fanyika nchini Malawi hivi karibuni.
Picha ya pamoja ya kambi inayoendelea mkoani Morogoro ya mchujo wa kuwapata wachezaji 8 kati ya 15, watakaowakilisha Tanzania katika fainali zitakazo fanyika nchini Malawi hivi karibuni.

Kocha wa Timu ya Taifa, Denis Lungu (kulia) akiwaelekeza jambo wachezji wa timu ya Taifa mchezo wa Pool (Safari National Pool Team) wakati wa mazoezi katika kambi inayoendelea mkoani Morogoro ya mchujo wa kuwapata wachezaji 8 kati ya 15, watakaowakilisha Tanzania katika fainali zitakazo fanyika nchini Malawi hivi karibuni.BLOG MPYA MAALUM KWA VIDEO A BONGO TU - ONLY FOR BONGO VIDEO'S

KUTOKA KAPITALI ONLINE MARKETING & ADVERTISING COMPANY INAWALETEA BLOG HII MAALUM KWA AJILI YA MUSIC WA BONGO TU ,LIVE SHOW ZA WASANII WA BONGO NA INTERVIEW ZAO.

UKITEMBELEA BLOG HII UTAWEZA KUPATA VIDEO ZOTE KALI ZA BONGO
NA MATUKIO YANAYOHUSU WASANII KWA VIDEO.
...KWA WASANII WANAOHITAJI VIDEO ZAO ZIWEKWE KWENYE HII BLOG WANAWEZA WASILIANA NASI KWA
EMAIL: videozabongo@gmail.com
PIA TUNAFANYA VIDEO PROMOTION

KUTOKA:
FOUNDER ,ERICK KISAI
KAPITALI ONLINE MARKETING & PROMOTION COMPANY
DAR ES SALAAM.
 

Wednesday, September 25, 2013

SERIKALI YAIPONGEZA TIMU YA WASICHANA AITEL RISING STARS

Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza timu akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria.  halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt
Wachezaji waliozawadia kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars  pamoja na captain wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi  Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Naodha wa timu ya wasicha ya Airtel Rising Stars chini ya umri wa miaka 17 Stumai Abdalah akimkabidhi kombe la ubingwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.

Kaptain ya timu ya wasichana Stumai ……. Akikabithi cheti cha kushinda kwa Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo baada yakuwa mabingwa katika mashindano yaliofanyika nchini Nigeria jumapili. Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Mchezaji wa timu ya wasichana Neema Paul pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo wakionyesha mfano wa hundi ya dolla 10,000 iliyokabithiwa kwa timu ya washichana na Airtel baada ya kuibuka washindi wa michuano ya Airtel Rising stars Afrika Kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi na katikati ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.
Wachezaji wa timu ya wavulana wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya halfa ya kuwapongeza iliyofanyika katika hotelya Hyatti jijini Dar es salaam, pichani kutoka kushoto Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo, wakurugenzi wa Airtel , mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah pamaoja na Salim Madadi wa TFF

Serikali yaipongeza timu ya wasichana ARS

·         Yashauri sekta binafsi kusaidi katika michezo.
Mkurugenzi wa maendeleo wa michezo nchini bw Leonard Thadeo ameipongeza timu ya wasichana ya Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars yaliomalizika juzi nchini Nigeria.

Tanzania waliibuka mabingwa baada ya kuwafunga Kenya katika fainali, pia amewapongeza wavulana baada ya kufikia hatua ya nusu fainali. Mabingwa wamezawadiwa kombe pamoja na kitita cha dola za marekani 10,000.

Katika pongezi zake pia amewapongeza wafungaji kwa upande wa wasichna ni Shelda Boniface na  mvulana  ni Athanas Mdamu na pia amempongeza mchezaji bora kutoka timu ya wasichana ambae ni Tatu Iddi .

Katika mashindano haya Tanzania imetoa rekodi tatu , mfungaji bora kwa upande wa wasichana  magoli matano, mfungaji bora wa kiume magoli manne , mchezaji bora kwa upande wa wasichana na pia wachezaji watatu upande wa wavulana wamefunga magoli matatu katika mechi moja (hat-trik) na kuondoka na mpira kila mmoja.

Kabla ya kukabidhiwa kombe na mabingwa hao , Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini bw Leonard Thadeo amesema kuwa serikali kupitia wizara ya michezo itaendelea kusaidi mpira wa vijana wenye umri mdogo ili kuifikisha mbali Tanzania katika medani ya soka.

Akiongea kwa niaba ya msafara wa timu kocha Rogacian Kaijage amesema kua mashindano yalikua magumu ila wamefanikiwa kuchukua ubingwa , amewapongeza vijana wake , kocha mwenzie wa timu ya wavulana Abel Mtweve na pia ameishukuru Serikali , Airtel , TFF, pamoja na  DRFA

Mkurugenzi wa masoko wa Airtel bw Levi Nyakundi ameahidi kuwa Airtel itaendelea kudhamini mpira hasa wenye umri mdogo na pia kuongeza mikoa ya ushiriki  wa mashindano ya Airtel Rising Stars 

Tuesday, September 24, 2013

WIKI YA UTALII KITAIFA YAZINDULIWA JIJINI MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akizungumza na wananchi waliojitokeza leo kwenye uzinduzi wa wiki ya utalii ambapo kitaifa maonesho yanafanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa kamati ya kukuza utalii mkoa wa Mwanza naye alipata fursa kuzungumza na wananchi nia na madhumuni ya kulitangaza jiji la Mwanza lifahamike katika sekta ya Utalii.
Mila na tamaduni nazo ni sehemu ya utalii..Ngoma za watu kabila la Wasukuma bila nyoka au fisi haijakamilika.
Nyoka surualini...tobaaaaa...
Mkuu wa mkoa katika pitapita kukagua shughuli mbalimbali za mabanda ya wajasiliamali hakutoka kapa, alizawadiwa.


Moja kati ya bidhaa ambazo ni utalii.


Mavazi na mapambo.
Umeona.


Wou...!!

Wanyama...
Haujaonaaaa...!!


Masai.
Banda la Wizara ya Maji.


Afrika kabisa.
Mkuu wa mkoa Evarist Ndikilo alipotembelea banda la Ofisi za jiji la Mwanza.


Tuzo mbalimbali iliyopata mkoa wa Mwanza
Maelezo zaidi.