Wana kikundi cha Cash Money wakiwa tayali kwa kutoa msaada katika hospitali ya Temeke |
Mlezi wa Kikundi cha Cash Money ,Ratifa Masasi kulia akimkabibi muhuguzi wa wodi ya watoto bi, Nuswe Ambokile zawai mbalimbali walizoleta kwa ajili ya watoto waliolaza katika hospital ya Temeke |
|
Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa dansi aliyestaafu, Muhidini Gurumo, atapanda jukwaani leo kutumbuiza na mkewe, sambamba na kupewa zawadi za heshima.
Gurumo atatoa burudani hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaaga mashabiki, ambapo shughuli hiyo itaambatana na uzinduzi wa kundi la Cash Money, la Tandika mjini Dar es Salaam.
"Tumeandaa zawadi kwa mzee Gurumo kutokana na heshima kubwa aliyonayo katika tasnia ya muziki na kujenga maadili kwa taifa kutokana na nyimbo zake.
Hivyo zawadi zetu zitaenda sambamba na uzinduzi, ambapo tumepanga hivyo, ili lee mwenye chochote ampe mzee wetu,"Aliongeza Latifa Masasi mlezi wa kundi hilo.
Uzinduzi huo unafanyika kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Aziz Ali, Dar es Salaam na utapambwa na bendi mbalimbali za taarabu zikiwemo Coast na G Five.
Kundi la Cash Money ambalo lilianzishwa mwaka 2011, pia limetoa vitu mbalimbali kwa wodi ya watoto, na vituo vya watoto yatima jana, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo
Mlezi wa kikundi cha Cash Money akimfaliji mama Samir Nassoro, Naomi Ramadhani walipokutana wakati kundi hilo likitoa msaada kwa wagojwa katika hod ya watoto |
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Cash Money wakimfariji Bi Naomi Ramadhani |
Msanii wa bendi ya Msondo ngoma Saddy Ally katikati akisalimiana na wanakikundi cha cash money walipokutana katika hospitali ya Temeke wakitokea kutoa msaada |
Wana kikundi wa chass money kushoto Amina Uredi 'Mmanyema ' na Zulfa Kasongo |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.