ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 16, 2019

Thursday, November 14, 2019

WANAHABARI WALA SHAVU MAANDALIZI SHEREHE ZA MIAKA 58 UHURU WA TANGANYIKA KITAIFA 2019 MWANZA


WANDISHI toka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mwanza wamejumuishwa kwenye moja ya kamati muhimu katika maandalizi ya sherehe za Uhuru 2019.

Wakiongozwa na Ally Nyakia ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kwimba wanahabari waliowekwa kwenye kamati ya Burudani Uhamasishaji Habari na Matangazo  ni pamoja na Mabere Makubi wa ITV, Team yote ya Shirika la Habari na Utangazaji Tanzania (TBC) tawi la Mwanza, Albert G. Sengo wa Jembe Fm na Gsengo Blog pamoja na George Binagi wa MBG Habari.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye ndiye aliyekuwa akiziainisha kamati hizo amesema kuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ameelekeza sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika (Disemba 9) mwaka huu 2019 kufanyika kitaifa mkoani Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo kabla kutatanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii kwa viongozi kushiriki mkono kwa mkono shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile kufungua miradi, utengenezaji matofali, kujenga madarasa, kushiriki shughuli mbalimbali mashambani (hasa ikizingatiwa kwamba huu ni msimu wa kilimo) makongamano na kadhalika. 
WAGANDA 800 WASAINI WARAKA WA KUTAKA KUFIKISHWA ICC RAIS MUSEVENI.


Waganda 800 wasaini waraka wa kutaka kufikishwa ICC Rais Museveni
Zaidi ya wananchi 800 wa Uganda wamesaini waraka wa kushinikiza kufikishwa katika Mahakama ya Kimataia ya Jinai ICC, Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo.
Kampeni hiyo inayokusudia kukusanya kwa akali saini milioni mbili inaongozwa na kinara wa upinzani nchini humo Dakta Kizza Besigye, ambaye alikuwa mkuu wa chama cha  Forum for Democratic Party (FDC).
Iwapo watafanikiwa kukusanya sahihi hizo, watawasilisha waraka huo kwa mwendesha mashitaka wa ICC, ili kuanzisha mchakato wa kufunguliwa faili la jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu dhidi ya Museveni katika mahakama hiyo iliyoko mjini The Hague nchini Uholanzi.
Baadhi ya ushahidi dhidi ya Museveni ambao wapinzani wanategemea kwenye kesi hiyo, ni mauaji ya watu 100 wakati maafisa usalama walipovamia makazi ya mfalme wa kitamaduni, Omusinga Charles Wesley Mumbere katika mji wa Kasese miezi kadhaa iliyopita.
Dkt Besigye akibebwa hobelahobela na maafisa wa polisi Kampala
Wapinzani nchini Uganda wanalalamika na kuituhumu serikali ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kwamba, imekuwa ikiendesha siasa za mkono wa chuma dhidi ya mrengo wa upinzani, hatua ambayo wanaitaja kuwa, inakandamiza na kubinya demokrasia katika nchi hiyo.
Rais Museveni ambaye amekuwa akiongoza Uganda tangu mwaka 1986 anatazamiwa kuwania tena kiti hicho mwaka 2021 na kuendelea hadi mwaka 2026, baada ya bunge la nchi hiyo kufuta kipengee cha sheria juu ya ukomo wa umri wa kugombea urais nchini humo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MPANGO WA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  amesema kuanzia tarehe 17 – 23 Novemba, 2019 litaanza zoezi la kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo ametoa onyo kwa yeyote atakayevuruga zoezi hilo kuwa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Vikundi vya ulinzi wa jadi au vya ulinzi binafsi au vya mashabiki wa vyama vya siasa havitaruhusiwa kutumika kwenye maeneo ya mikutano ya kampeni au maeneo ya uchaguzi.”


Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Alhamisi, Novemba 14, 2019)alipozindua Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasioambukiza sambamba na Mpango wa Taifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza

Waziri Mkuu amesema kuwa vyombo vya Ulinzi na Usalama hususan Jeshi la Polisi, Mgambo wenye sare na Maafisa wanaosimamia ulinzi vitatumika kuhakikisha kunakuwepo na utulivu wakati wa kampeni na uchaguzi.

Kadhalika,Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na Serikali imejipanga vya kutosha kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi.


Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuchukua hatua stahiki za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ikiwa ni pamoja na kubadili tabia na mwenendo wao wa ulaji wa vyakula kwa kuongeza ulaji wa mbogamboga, matunda.

Waziri Mkuu amesema kila mtu ana wajibu wa kudhibiti matumizi ya vilevi kama sigara na pombe; kuhamasisha jamii kushiriki mazoezi au shughuli za nguvu; kuzingatia mlo unaofaa hasa kwa kuondoa au kupunguza chumvi, sukari na mafuta. “Tujipange kukabiliana na madhara mengine yatokanayo na uharibifu wa mazingira na tabianchi.”

Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wajenge utamaduni wa kufanya mazoezi angalau dakika 30 mara tatu kwa wiki. “Katika eneo hili, niweke msisitizo kwa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendeleza utaratibu wa mazoezi uliozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

“Tuendelee kuhamasisha kuanzisha na kujiunga kwenye vikundi vya mazoezi ya pamoja ambavyo husaidia sana kuleta hamasa ya kufanya mazoezi. Tutumie vikundi vya joggingvilivyopo kwenye kata na mitaa au vijiji vyetu ili kupata mwendelezo wa jitihada zao.

Amesema Halmashauri zote zihakikishe zinatenga na kuyaendeleza maeneo ya wazi katika kila kata au mitaa ili pamoja na shughuli nyingine wananchi pia watumie maeneo hayo kwa ajili ya kufanya mazoezi.

“Kwa upande wa wanafunzi kuanzia sasa kabla ya kuingia darasani wawe wanakimbia mchaka mchaka ili waweze kujiimarisha kiafya jambo ambalo litawaepusha na magonjwa yasiyoambukiza.”

Amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa tishio kwenye jamii na ulimwenguni kote, takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2016 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yanachangia zaidi ya vifo milioni 41, sawa na asilimia 71 ya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016.

“Taarifa za mwaka 2013 za Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) zinaonesha kuwa, pamoja na changamoto hizo za kiafya, magonjwa yasiyoambukiza yanaathiri sana nyanja nyingine za maisha. Inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka 20, kuanzia mwaka 2013 gharama zitokanazo na magonjwa haya zitafikia Dola za Marekani trilioni 47.”

Waziri Mkuu amesema fedha hizo zingeweza kutumika kupunguza umaskini kwa watu bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka 50. Kwa nchi za uchumi wa kati na chini, magonjwa hayo yatagharimu mataifa hayo Dola za Marekani, trilioni saba katika kipindi cha 2011 hadi 2025.

Amesema gharama hizo zinatokana na kuongezeka kwa gharama za huduma za matibabu na upotevu wa nguvukazi unaosababishwa na maradhi hayo, mfano, makadirio yanaonesha kuwa gharama za huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza itafikia asilimia 75 ya mzigo wote wa bajeti ya afya. Ugonjwa wa kisukari pekee utagharimu zaidi ya Dola za Marekani bilioni 465 sawa na asilimia 11 ya bajeti yote ya afya duniani.

Awali,Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema magonjwa yasiyoambukiza yanajumuisha magonjwa ambayo hayawezi kusambazwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pumu, shinikizo la juu la damu, kisukari, saratani, siko seli, magonjwa ya akili, ajali, magonjwa mengi ya macho, kinywa, masikio, pua na koo. “Magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote na kuathiri nyanja zote za kimaisha.”

Waziri Ummy alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Tanzania ilishuhudia ongezeko la idadi ya watu waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukiza kutoka wagonjwa milioni 3.4 kwaka 2016 hadi wagonjwa milioni 4.2 mwaka 2018, ilkiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24.

Kwa upande wao, wadau wa masuala ya afya wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza kiwango cha bajeti ya dawa kutoka sh. bilioni 31 hadi sh. bilioni 270.

KATIBU MKUU MLAWI: ONGEZENI JUHUDI ZA KUTANGAZA UMUHIMU WA SEKTA ZA WIZARA.


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Bibi.Susan Mlawi akizungumza uongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaaga baada ya kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019 kwa mujibu wa sheria.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Bibi.Susan Mlawi (kushoto) akimkabidhi taarifa mbalimbali za majukumu ya Wizara hiyo Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi (kulia)ambaye atakaimu kuanzia kesho mpaka atakapoteuliwa mtu wa kushika nafasi hiyo, mara baada ya kuagana na Menejimenti ya wizara hiyo leo jijini Dodoma, kufuatia kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (mwenye gauni nyekundu) ambaye amekabidhi rasmi ofisi yake leo kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi jijini Dodoma, baada ya kufikia ukomo  wa utumishi wa umma ambapo anatarajia kustaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.

Wednesday, November 13, 2019

RC MONGELLA AGEUKA KUWA MUHUBIRI ASHUSHA INJILI KWA WANAHABARI 'WAPONA'


Mathayo 7: 5 Inasema 'Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako'

Ni kama yalikuwa mahubiri lakini pia twaweza kulifananisha na darasa lenye manufaa kwa maendeleo ya Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla, hapa nauzungumzia Mkutano wa Wasaa wa Marafiki wa Habari uliofanyika Novemba 09, 2019 ukiwa na lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kuchochea ajenda ya maendeleo mkoani hapa.

Katika kusanyiko hilo mbali na Wanahabari pia lililojumuisha viongozi wa Madhehebu ya dini, mashirika ya utetezi na usimamiaji haki katika jamii wadau wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Asasi za Kiraia kama vile benki ya TPB, NIDA, TCRA, EWURA, Mifuko ya hifadhi ya Jamii NSSF na NHIF, Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA), ALPHA PRESS, makampuni ya utengenezaji vinywaji kama vile Coca Cola,  ANCHLAP WINE na kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaasa waandishi wa habari na wadau waliojitokeza kujikita zaidi katika ukosoaji ujengao. 

MVUA KUBWA YAATHIRI ITALIA.

Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa nchini Italia.

Hali ya hewa mbaya imeonekana nchini humo na kusababisha janga la asili huko Venice.

Katika mji maarufu kwa mifereji yake, kiwango cha maji kilifikia sentimita 187 , kiwango hicho kikiwa cha juu zaidi baada ya sentimita 194 katika janga la mafuriko la 1966.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa maji, boti na vivuko vimesababisha watu kuzama.

Meya wa Venice Luigi Brugnaro, amesema kuwa jiji linakabiliwa na janga la kihistoria na kuihimiza serikali kuchukua hatua muhimu hara iwezekanavyo.

Brugnaro ametoa mfano kwamba mji umejisalimisha kwa maji ya bahari na haujapata kuona kitu kama hicho tangu mwaka 1966 na pia ametoa wito katika ukurasa wake wa akaunti ya Twitter kwa WaVeneti kupiga picha za uharibifu huo.

Luca Zaia, mkuu wa Tawala wa Mkoa wa Veneto, ambayo iko Venice, ameeleza kuongezeka kwa maji kama uharibifu

"Sitazidishi maneno yangu, lakini asilimia 80 ya jiji limejaa maji. Uharibifu hautabiriki, unatisha." alisema.

Kituo cha kihistoria cha mji wa Venice, pamoja na mazingira yanayozunguka yameathiriwa na janga hilo.

Watu wawili wameuawa kwa sababu ya kuongezeka kwa maji kwenye kisiwa cha Pellestrina katika dimbwi la Venetian.

Kulingana na Rainews24, mmoja wa waliokufa alikuwa na umri wa miaka 78 na kupoteza maisha baada  ya kurushwa na umeme pale nyumba ilipofurika.

Mtu mwingine pia amekufa kwa sababu ya nyumba kujaa maji.

Kwa upande mwingine, kuna moto mwingi mdogo unaosababishwa na umeme wa sasa huko Venice na maeneo ya karibu yake kwa sababu ya mafuriko.

UNO YA HARMONIZE WITH @DEEJAYKFLIPUNO IMESHIKA HATAMU KILA KONA .......

VINCENT KOMPANY HAKUBALIANI NA KAULI KWAMBA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU YA UINGEREZA ZIMEFIKIA TAMATI


Jose Mourinho and Roy Keane believe that the title race is 'done' as Liverpool now have a eight point advantage on title rivals Man City, however Vincent Kompany believes there is still more drama to come.

Chama cha CUF nacho chajitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania

Habari kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania zinasema kuwa Chama cha Wananchi (CUF)  hatimaye kimejitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.
Kimesema kuwa  kimejitoa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato huo ikiwa ni pamoja na kuenguliwa asilimia 90 ya wagombea wake. 
Msimamo huo umetangazwa leo Jumanne na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati akitoa maazimio ya kikao cha baraza kuu la uongozi la CUF. CUF kinakuwa chama cha siasa cha sita kujitoa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini Tanzania baada ya Chadema, ACT- Wazalendo, NCCR –Mageuzi, UPDP na Chauma.
Katika maelezo yake Profesa Lipumba amesema kuwa baraza hilo limetafakari kwa kina na kuona hakuna umuhimu kushiriki uchaguzi baada ya hoja zao tatu walizoziwasilisha serikalini kutofanyiwa kazi. "Uchaguzi unatakiwa uwe huru na haki lakini serikali imeshindwa kuonyesha hata chembe ya haki. Asilimia 90 ya wagombea wetu wameondolewa tumebaki na asilimia nne tu", amesisitiza Lipumba. Ameongeza kuwa katika mazingira hayo ni wazi kuwa CUF imeondolewa kwa sababu haiwezi kushiriki bila wagombea.

Tuesday, November 12, 2019

MPC YAWASHUKURU WADAU WALIOFANIKISHA MKUTANO 'MARFIKI WA HABARI'

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club- MPC) inatoa shukurani za dhati kwa wadau wote waliofanikisha mkutano wa Wasaa wa Marafiki wa Habari uliofanyika Novemba 09, 2019 ukiwa na lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kuchochea ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza. 
S

TUJENGE UTAMADUNI WA KUIBUA CHANGAMOTO, KUTOA MAPENDEKEZO NA KUSHIRIKI KUTATUA RC MWANZAMkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye Mkutano wa Wasaa wa Marafiki wa Habari mkoani Mwanza ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) Novemba 09, 2019.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa neno la ufunguzi kwa niaba ya wanahabari mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa salamu za ufunguzi kwenye mkutano huo ambapo alisema chama hicho kinaendelea na mikakati yake ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa ofisi na uanzishaji wa redio pamoja na luninga ya mtandaoni.Mwanahabari Alex Mchomvu akichangia mada kwenye mkutano huo.

 Mwanahabari wa siku nyingi, Shija Malando ambaye kwa sasa ni diwani wilayani Kwimba akitoa uzoefu wake kwenye mkutano huo.
Wanahabari na marafiki wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliahidi milioni 100 kwa MPC ili kuimarisha utendaji wake.


Mwenyekiti Mstaafu wa MPC, Jimmy Luhende ambaye kwa sasa ni  mkurugenzi wa taasisi ya ADLG akisherehesha mkutano huo.
Wanahabari na marafiki wa habari mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano huo.