Mathayo 7: 5 Inasema 'Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako'
Ni kama yalikuwa mahubiri lakini pia twaweza kulifananisha na darasa lenye manufaa kwa maendeleo ya Mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla, hapa nauzungumzia Mkutano wa Wasaa wa Marafiki wa Habari uliofanyika Novemba 09, 2019 ukiwa na lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika kuchochea ajenda ya maendeleo mkoani hapa.
Katika kusanyiko hilo mbali na Wanahabari pia lililojumuisha viongozi wa Madhehebu ya dini, mashirika ya utetezi na usimamiaji haki katika jamii wadau wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Asasi za Kiraia kama vile benki ya TPB, NIDA, TCRA, EWURA, Mifuko ya hifadhi ya Jamii NSSF na NHIF, Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA), ALPHA PRESS, makampuni ya utengenezaji vinywaji kama vile Coca Cola, ANCHLAP WINE na kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaasa waandishi wa habari na wadau waliojitokeza kujikita zaidi katika ukosoaji ujengao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.