Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi akizungumza uongozi wa Menejimenti ya Wizara hiyo leo Jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaaga baada ya kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019 kwa mujibu wa sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi (kushoto) akimkabidhi taarifa mbalimbali za majukumu ya Wizara hiyo Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi (kulia)ambaye atakaimu kuanzia kesho mpaka atakapoteuliwa mtu wa kushika nafasi hiyo, mara baada ya kuagana na Menejimenti ya wizara hiyo leo jijini Dodoma, kufuatia kufikia ukomo wa utumishi wa umma ambapo anastaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.
Baadhi ya
watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya
pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi (mwenye gauni nyekundu)
ambaye amekabidhi rasmi ofisi yake leo kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt.Ally Possi
jijini Dodoma, baada ya kufikia ukomo wa
utumishi wa umma ambapo anatarajia kustaafu rasmi kuanzia Novemba 15,2019.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.