Soko la dagaa kwa mwalo wa Kirumba jijini Mwanza linaonekana kudoda mara baada ya mizigo mingi ya bidhaa hiyo kuonekana sokoni hapo bila kuwa na wanunuzi kama ilivyokuwa nyakati za nyuma kwa soko hilo kushamiri wanunuzi na wachuuzi toka pande mbalimbali Afrika Mashariki.
Ni msimu wa mauzo na gunia moja linauzwa shilingi 50,000/= lakini kwa sasa mali yote imedoda sokoni hapa ukilinganisha na mwaka jana ambapo gunia moja liliuzwa shilingi 100,000/= na bidhaa zilikuwa zikitoka kwa kasi licha ya bei hiyo kuwa juu.
wafanyabiashara bado hawaridhishwi na mfumo uliopo sasa ambao umeshindwa kuwabana/kuwazuia wageni kutoka Kenye na kongo kwenda kununua dagaa moja kwa moja kwa wavuvi.
Waandishi wa Habari walio maliza mafunzo ya kuripoti Habari za biashara na uchumi wakifanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara soko la kimataifa Mwaloni kirumba Mwanza.
Wafanyabiashara wakisubiri wanunuzi katika soko la Kimataifa Mwaloni kirumba jijini Mwanza.
Kadri wanavyoendelea kukaa kwenye soko dagaa hushuka thamani hivyo bei nzuri ni kwa wale dagaa wapya.
Mwanahabari Florah Magabe akipata ufafanuzi kuhusu bidhaa za dagaa soko la Kimataifa Mwaloni kirumba jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya uripoti habari za Uchumi na Biashara.
Mwisho wa siku wafanyabiashara hao 'waliungishwa' na waandishi hao kwa kununuliwa bidhaa zao.
Picha ya pamoja kwa washiriki mafunzo ya Uchumi na Biashara pamoja na mwalimu wetu Mr. Mnaku (aliyesimama kulia mwenye begi mgongoni).