![]() |
| Watoto na ndugu wa marehemu katika picha ya pamoja nje ya kanisa la Menonite jimbo la Musoma mjini ambapo ibada ya kuuaga mwili wa marehemu mchungaji mstaafu Olimo ilifanyika. |
![]() |
| Wachungaji wakiwakilisha kanda mbalimbali nchini wamehudhuria ibada hii takatifu. |
![]() |
| Huzuni na majonzi vilitawala ndani ya kanisa la Menonite Musoma Mjini pale watoto wa marehemu walipokaribia mwili wa mpendwa baba yao kwaajili ya kutoa heshima za mwisho. |
![]() |
| Waumini ndani ya Kanisa la Menonite Musoma mkoani Mara wakishiriki ibada hiyo. |
![]() |
| Wachungaji na Maaskofu zaidi ya 50 toka makanisa mbalimbali nchini wameshiriki ibada hiyo hii leo. |
![]() |
| Wachungaji na Maaskofu wakiwa wameubebe mwili wa mpendwa wao kutoka kanisani tayari kwa safari kuelekea Nyumbani kwa ukoo wa marehemu eneo la Kiabakari kwa ajili ya maziko. |
![]() |
| Mwili wa marehemu Mchungaji Mstaafu Olimo, uliwasili kijiji cha Kiabakari majira ya saa nane hivi na kukutana na Ummati mkubwa wa waombolezaji. |
![]() |
| Marafiki na wazee wa kaya mbalimbali eneo la Kiabakari. |
![]() |
| Mwili wa marehemu Mchungaji Mstaafu James Kwaka Olimo ukishushwa kaburini kwa heshima na taratibu za kanisa wahusika wakiwa ni wachungaji waliohudhuria toka makanisa mbalimbali. |
![]() |
| Marafiki wakishuhudia yanayojiri kwa safari ya mpendwa wao. |
![]() |
| Kamera yako haikupata jukwaa kuonyesha picha kamili ya Umma ulioshiriki maziko hayo lakini ilipenya na kuona japo engo hii. |
![]() |
| Kamera yako iliwasihi Mabinti hawa wa marehemu 'japo watabasamu' kwani baba yao waliyempenda katwaliwa na yule aliyemleta mara baada ya kumaliza kazi yake duniani, nao wakatabasamu kujifariji. |
![]() |
| Picha ya pamoja na mzee mkongwe wa ukoo. |
![]() |
| Wakufunzi wa Chuo Cha Ualimu Bunda ambao ni mashabiki namba moja wa www.gsengo.blogspot.com nao walihudhuria mazishi hayo, kutoka kulia Alex Mwingira, Emmanuel Mandango, Jublet Shuma, Hilary Majimbe na Tumaini Mnale. |
![]() |
| Kutoka kushoto ni Edgar Mapande, G. Sengo na Mr Ben. |
Tupe maoni yako
















0 comments:
Post a Comment