ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 23, 2013

"YANGA YAICHANA PYAAaaaaa AZAM!!"


 "Mechi hii ilikuwa ngumu sana kwa Yanga kwani walikuwa wakicheza na timu mbili.... naoa hapa uwanjani mashabiki wa Azam na washirika wao wanaanza kuondoka....Na mpiraaa..... UMEKWISHaaaaa!!!! Mpira Umekwisha mpenzi msikilizaji  Yanga wanaondoka kifua mbele kwa bao 1 na Azam 0. naona pale Chuji, Domayo na Didie Kavumbagu wanakwenda moja kwa moja kumpongeza 'Sure Boy' picha hii siielewi... naomba waungwana mnisaidie....tehe tihi-te----!!!!"

KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AZAM
1.Ally Mustafa 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Jerson Tegete

10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Nizar Khalfani
6.Didier Kavumbagu
7.Said BahanuziKIKOSI CHA AZAM FC1: Mwadini Ally, Balou Kipre, Kipre Tchetche, Waziri Salum, Jockins Atudo, David Mwantika, Ibrahim Mwaipopo, Salaum Aboubakar, John Bocco, Humphrey Mieno, Mcha Khamis

KUNDI LA SANAA LA THE GREAT ZONE ENTERTAINMENT LATEMBELEA TBL MWANZA

Kundi la Great Zone lililosheheni vipaji mbalimbali katika picha ya pamoja na Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi ambaye aliwatembeza kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Hapa ni ndani ya eneo la uzalishaji ambapo kundi la sanaa la The Great Zone Entertainment lilipata fursa ya kutembelea kujionea yaliyomo na yanayojiri. 

Dirisha la kuelekea eneo jingine la chemba ya uzalishaji ndani ya kampuni ya Bia TBL Mwanza.

Haya ndiyo yanayosomeka toka dirishani hapo panapo chunguliwa.

Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi akitoa maelekezo juu ya shughuli nzima ya uzalishaji kiwandani hapo kwa wasanii wa kundi la The Great zone Entertainment.

Viambatanisho elekezi vilivyo muhimu kwa ajili ya uzalishaji bora na makini viko kwenye eneo la ufungaji bia.

Umakini unazingatiwa  kuanzia ndani ya kiwanda hivyo ufungaji si wa vizibo pekee bali hata upachikaji lebo makini unapewa kipaumbele. 

Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi akitoa maelekezo katika seksheni ya ugongaji vizibo.

Sasa bia imekamilika na inapakiwa kwenye gari kuelekea kwenye soko.

Wasanii walipata fursa pia kutembelea ghala ya kuhifadhi bia zilizo kamilika kuelekea sokoni.

Wasanii wa The Great Zone wakipata flash eneo la ghala kabla ya kwenda kupata vinywaji na chakula walichoandaliwa..

Wadau wa TBL Mwanza wakiburudika mara baada ya kazi ndani ya bar iliyoko ndani ya kiwanda hicho eneo la Bwiru wilayani Ilemela.

Picha na kinywaji vya TBL.

MAMA SALMA KIKWETE AONGOZA HAFLA YA KUCHANGIA WANAWAKE WANAWAKE MATATIZO YA AFYA, ZAIDI YA MIL 142 ZAPATIKANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda pichani kushoto akizungumza machache mbele ya meza kuu kabla ya kumpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija hiyo maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.Kulia ni  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal.

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.


Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar. 

Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal pichani kulia akizungumza machache,ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi Milioni mbili katika hafla hiyo.
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake.

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa pongezi na kumkabidhi cheti cha heshima Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal kwa kuchangia kwake

Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa.

Makofi  ya pongezi na shukurani kwa Bonge Barabarani yakipigwa.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi mmoja wa Wakilishi wa Kampuni ya ndege ya Flight Link cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshima Meneja mahusiano wa PPF,Lulu Mengele ,mara baada ya kuchangia kiasi cha fedha kwenye hafla hiyo,kulia kwake akishuhudia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal..Mgeni Rasmi,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) mara baada ya kuifanikisha hafla hiyo kwa kiasi kikubwa.

Mmoja wa Waratibu wa hafla ya  Montage Charity Ball,Barbra  Hassan akiwakaribisha baadhi ya viongozi mbalimbali wa kiserikali,mabalozi na wageni waalikwa wengine waliofika kwenye hafla hiyo ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

 
Pichani juu ni wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete.

Kalunde Band wakitumbuiza jukwaani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akipewa kampani na baadhi ya wanamuziki wenzake jukwaani,wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),ndani ya hotel ya Serena jijini Dar.

Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiongozwa na MKurugenzi wao Mtendani (wa tatu kulia),Steve Gannon wakiwa katika picha ya pamoja,aidha kampuni hiyo pamoja na kudhamini hafla hiyo pia ilichangia kiasi cha shilingi milioni tano 

Baadhi ya magauni yakinadiwa kwa staili ya kipekee kabisa,kwa ajili ya kuchangia mfuko huo wa kuwasiadia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball.
PICHA ZOTE NA Michuzijr Blog.

MZUNGU KICHAA ANNOUNCES ”unplugged” SPRING TOUR IN APRIL & MAY 2013


Mzungu Kichaa announces ”unplugged” spring tour in April & May 2013
Mzungu Kichaa has been selected to perform at the Danish showcase festival SPOT (www.spotfestival.dk) in May 2013. The tour also includes performances in Tanzania, Germany and the UK. Concerts will be announced on www.facebook.com/mzungukichaa.
During the “unplugged” tour Mzungu Kichaa will launch a new performance setup, which will be ”raw” and “intimate” than before. ”I realised that when I try to enter a new territory with my music, the main problem I face is mobility. My band is from Tanzania and I feel a band from Europe cannot replace them.  Therefore I decided to reinvent my music and create an ”unplugged” setup, which is just me and my guitar and just a few accompanying musicians. However, in August and November I will be touring Europe again with my full Tanzanian band. I am very excited about standing on my own two feet during this next tour and getting close and personal with my audience through my ”unplugged” concerts this spring”. – Mzungu Kichaa

Friday, February 22, 2013

HATIMAYE MWANARIADHA MLEMAVU ANAYETUHUMUWA KWA MAUAJI YA MPENZI WAKE NCHINI AFRIKA YA KUSINI AACHIWA KWA DHAMANA


Jaji nchini Afrika Kusini hii leo wametoa dhamana mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mchumba wake. 
Mwanariadha huyo alikanusha kosa la mauaji akisema kuwa alimpiga risasi Reeva Steenkamp akidhania kuwa alikuwa jambazi.
Pistorius amesema kuwa hakuua 
mchumba wake kwa maksudi. 
Pamoja na kwamba upande wa mashtaka awali ulikuwa na hofu kuwa huenda Pistorius angekosa kufika mahakamani kwa siku ya leo, Pistorius amejitokeza leo na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana.Upande wa utetezi ulisema kuwa ushahidi huo wenye utata na uliotolewa na mmoja wa polisi umeweza kuhujumu upande wa mashtaka.
Mara baada ya kupewa dhamana Pistorius anatarajiwa kurejea katika mazoezi wiki ijayo.
Kocha wake aliyasema hayo alipowasili mahakamani kwa siku ya nne ya kusikiliza kesi ya dhamana dhidi ya Pistorius.
Mnamo Alhamisi polisi walimbadilisha jasusi aliyekuwa anachunguza kesi hiyo na kuweka polisi mwingine baada ya taarifa kujitokeza kuwa polisi huyo mwenyewe alikuwa anakabiliwa na kesi ya jaribio la mauaji.
Carl ambaye ni kaka wa Oscar pistorius akikumbatiana na
 baba yake mzazi mara baada ya maamuzi ya dhamana kwa 
mdogo wake. (Reuters)
Jasusi mkuu wa Afrika Kusini Luteni, Vineshkumar Moonoo, ndiye anachunguza kesi hiyo sasa.
Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa Pistorius alifyatua risasi nne katika bafu yake iliyokuwa imefungwa huku marehemu Steenkamp akiwa ndani. Aligongwa kichwani , kwenye paja na mkononi.

HAPA NA PALE NDANI YA ROCK CITY

Nani kati ya hawa abiria yuko salama? 

Akinamama Mwanza mmejiandaandaaje?

Masupa staa wa kesho na michezo yao.

Katangazo ka Miti dawa.

KONGAMANO LA NANE LA WANAHABARI NA WADAU WA NHIF LAMALIZIKA LEO MKOANI MTWARA

Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa ufafanuzi wa Wizara juu ya maswala ya afya hapa nchini wakati wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote hapa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro akizungumza wakati akifunga Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote hapa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro kwa ajili ya kufunga Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania,Dkt. Mildred Kinyawa akiwasilisha mada yake ya kuuhusiana na Usajili wa Maduka ya Dawa Baridi Vijijini wakati wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevile Meena akiwasilisha ya kuhusu Mchango wa Vyombo vya Habari katika Sekta ya Afya,katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Meneja Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango Kazi na Mpango Mkakati kutoka Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD),Cosmas Nalimi akiwasilisha Mada ya Kuhusu Upatikanaji wa Dawa Vijijini,katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Wakali wa Uchoraji wa Vibonzo hapa nchini,toka kulia ni Masoud Ally Kipanya,King Kinya pamoja na Nathan Mpangala a.k.a Kijast Bikozzz wakifatilia kwa makini Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Wadau Stephen Wang'anyi (Muwakilishi wa ITV na Radio One,Shinyanga),Augustine Nigendi wa Channel Ten,Mara) pamoja na George Maratu wa ITV Mara wakipitia Libeneke la Glogu ya Jamii.
Mdau wa Globu ya Jamii kutoka Mkoani Lindi,Abdulaziz Video akiendeleza libeneke wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.