Saturday, August 10, 2024
Friday, August 9, 2024
KILA ABIRIA ATAKAYEPANDA NDEGE UTAPANDWA MTI JIJINI MWANZA NA VIA AVIATION
NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Utafiti umebaini kuwa viumbehai wa kuvutia kama ndege, mimea na wanyama siku moja wanaweza kufutika katika uso wa dunia kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na binadamu ambao hivi sasa umeleta mabadiliko ya tabia nchi. Wataalam wanasema mabadiliko ya tabianchi yanatokana na tabia ya watu kukata miti hovyo na kuiacha ardhi ikiwa uchi hivyo kuongeza hewa chafu ya ukaa angani ambayo uzalishwa na viwanda, vyombo vya usafiri nchi kavu, majini na angani pamoja na uchomaji taka hivyo kuleta athari kubwa kwa viumbehai wote ambao wanakuwa katika hatari ya kutoweka katika uso wa Dunia. Kwa kuliona hilo wadau wa maendeleo taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa huduma mbalimbali za ndege VIA AVIATION Mwanza inakuja na kampeni ya 'MTI MMOJA KWA KILA HUDUMA' yaani kila mteja atakaye kata tiketi ya ndege kupitia wakala ya kampuni hiyo basi utapandwa mti kwaajili ya kutunza mazingiraWAPIGA KURA WAPYA LAKI NNE KUANDIKISHWA SHINYANGA NA MWANZA
Uoreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mwanza na Shinyanga utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 21 hadi 27 Agosti, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura wapya 400,082 wanatarajiwa kuandikishwa.
Hayo yamesemwa leo tarehe 09 Agosti, 2024 kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi iliyofanyika mkoani Mwanza na Shinyanga.
Mkoani Mwanza mkutano wa wadau umefunguliwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na mkoani Shinyanga mkutano umefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk.
Viongozi hao wa Tume wamewataka wadau hao wa uchaguzi kuhamasisha wananchi na wapiga kura kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili zoezi lifanyike kwa ufanisi.
Katika mikutano hiyo mada ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani imebainisha kuwa mkoani Shinyanga wapiga kura wapya 209,951 wataandikishwa na mkoani Mwanza wapiga kura wapya 190,131 wataandikishwa na kufanya jumla ya wanaotarajiwa kuandikishwa kuwa 400,082.
“Kwa mkoa wa Mwanza Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 190,131. Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.3 ya wapiga kura 1,845,816 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Hivyo, Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Mwanza utakuwa na wapiga kura 2,035,947,” amesema Bw. Kailima.
“Kwa mkoa wa Shinyanga Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 209,951. Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ya wapiga kura 995,918 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Hivyo, Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869,” amesema Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Seleman Mtibora ambaye amewasilisha mada kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoani Shinyanga.
Bw. Kailima amefafanua kuwa idadi hiyo inatokana na makisio yaliyofanywa kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na kwamba inaweza kuongezeka.
Uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulifanyika mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 ambapo ulienda sambamba na kuanza kwa mzunguko wa kwanza wa uboreshaji kwenye mikoa mitatu ya Kigoma, Tabora na Katavi na kufuatiwa na mzunguko wa pili umejumuisha mikoa ya Geita na Kagera.
Kwa sasa, uboreshaji wa Daftari unaendelea kwenye mikoa hiyo ya Kagera na Geita hadi tarehe 11 Agosti, 2024 ambapo vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.Viongozi na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa wakishiriki katika mkutano huo
NISHATI SAFI YA KUPIKIA AJENDA YA KITAIFA
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akielezea ufanisi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi waliotembelea Banda la Wakala, Nzuguni Jijini Dodoma. |
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewaasa wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia ili kuokoa gharama na muda, kulinda mazingira na afya zao hasa ikizingatiwa kuwa teknolojia sasa imeboreshwa na gharama yake ni nafuu ikilinganishwa na nishati zingine.
Mhandisi Saidy ametoa rai hiyo Agosti 8, 2024 mbele ya wananchi waliotembelea Banda la REA katika Maonesho ya Siku Kuu ya Wakulima (Nane Nane), Nzuguni Jijini Dodoma.
"Tunaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia kwani ni salama, rafiki na gharama yake ni nafuu kwani teknolojia sasa imeboreshwa," amesema Mhandisi Saidy.Mhandisi Saidy amesema ipo dhana ambayo imejengeka katika jamii kuwa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ni ghali na si salama na pia chakula kinachopikwa kutokana nayo hakina ladha suala ambalo alisisitiza halina kweli.
"Ninawathibitishia Nishati Safi ya Kupikia ni salama kuliko nishati zingine tulizozizoea, niwatoe wasiwasi katika hili na tunaendelea kutoa elimu kuhusu usalama na umuhimu wa nishati hii bora," amesema Mhandisi Saidy.
Akizungumzia upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia kwa wote, amesema Serikali imetoa ruzuku katika usambazaji wa Mitungi ya Gesi (LPG) na Majiko Banifu ili kuvutia wawekezaji wengi na pia kumuwezesha kila mwananchi aweze kumudu gharama zake."Serikali imekuja na mfumo wa kumrahisishia kila mwananchi hususan yule mwenye kipato cha chini kumudu gharama ya Nishati Safi ya Kupikia kokote aliko ili aachane na matumizi ya nishati nyingine," amefafanua Mhandisi Saidy.
Amesema Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipatia REA jukumu la kuhakikisha inasimamia vyema utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ili kufikia 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia.
"Tunamshukuru Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini na kutupatia jukumu hilo kubwa na tayari kwa kushirikiana na wadau tumeanza utekelezaji wake na tunakwenda vizuri," amefafanua Mhandisi Saidy.Amesema hatua inayoendelea sasa ni kuibua na kuwawezesha wazalishaji wengi wa vifaa vya Nishati Safi ya Kupikia ili kuongeza umahiri sambamba na kuwawezesha kutengeneza bidhaa nyingi kwa gharama nafuu na kwa ubora wa kimataifa," amesema.
Amesema kwa kufanya hivyo kutakuwa na ongezeko la matumizi ya nishati safi ya kupikia, ongezeko la ajira na hivyo kukuwa kwa uchumi.
Monday, August 5, 2024
VIDEO;- CHADEMA KIMEWAKA WENJE ATANGAZA KUMNG'OA TUNDU LISSU NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI
NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Joto la uchaguzi ndani ya CHADEMA limeanza kupamba moto, baada ya Ezekia Wenje kutangaza nia ya kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho Bara. Wenje ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria CHADEMA yenye mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita, anakusudia kujitosa kuomba ridhaa ya nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Tundu Lissu. Mbunge huyo wa zamani wa Nyamagama, Mkoa wa Mwanza amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari juu ya kusudio lake hilo, akisisitiza ameamua kuwania nafasi hiyo, ili kuongeza ufanisi wa kazi na uwajibikaji.
CRDB Bank Marathon Congo yakusanya Dola 50,000 kusaidia wodi ya watoto Hospitali ya Jason Sendwe DRC
PROFESA ASSAD ATAKA USHIRIKIANO UJENZI WA HOSPITALI YA KIISLAMU TANGA
Sunday, August 4, 2024
WAZIRI MKENDA AZINDUA BODI YA USHAURI CHUO CHA ADEM BAGAMOYO
NA VICTOR MASANGU/BAGAMOYO